Katika Waefeso 1:17 Biblia inasema ‘Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi ROHO YA HEKIMA NA YA UFUNUO KATIKA KUMJUA YEYE’. Hili moja ya maombi muhimu ambayo Mtume Paulo alifanya kwa jili ya Kanisa la Efeso. Kila nisomapo mstari huu nimekuwa nikijuliza sana ni kwa nini Mtume Paulo aliomba maombi haya kwa kanisa hili?.
SOMA MAANDIKO
LINDA SANA MOYO WAKO KULIKO YOTE MAANA NDIKO ZOTOKAKO CHEMCHEMI ZA UZIMA
Friday, November 4, 2016
ROHO YA HEKIMA NA UFUNUO
Katika Waefeso 1:17 Biblia inasema ‘Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi ROHO YA HEKIMA NA YA UFUNUO KATIKA KUMJUA YEYE’. Hili moja ya maombi muhimu ambayo Mtume Paulo alifanya kwa jili ya Kanisa la Efeso. Kila nisomapo mstari huu nimekuwa nikijuliza sana ni kwa nini Mtume Paulo aliomba maombi haya kwa kanisa hili?.
Sunday, February 14, 2016
Biblia inasema nini juu ya talaka na kuoa tena?
Biblia inasema nini juu ya talaka na kuoa tena?
Swali: "Biblia inasema nini juu ya talaka na kuoa tena?"
Jibu: Kwanza ni muhimu kukumbuka maneno ya biblia katika malaki 2:16a: “ nachukia talaka, asema Bwana Mungu wa Israeli,” kulengana na biblia,mpango wa Mungu juu ya ndoa ni iwe ushikamano wa siku zote za mwanadamu duniani. “ Hata si wawili tena bali mmoja. Kwa hivyo kile Mungu amekiunganisha mwanadamu asikitenganishe” (mathayo 19:6). Mungu antambua ya kwamba kwa kuwa ndoa ni ya wenye dhambi wawili, talaka haina budi kutokea. Katika agano la kale aliweka shaeria za kulinda haki za watalaka hasa wanawake (kumbukumbu la torati 24:1-4). Yesu akasema sheria hizi zilitolewa kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya wanadamu lakini
Jibu: Kwanza ni muhimu kukumbuka maneno ya biblia katika malaki 2:16a: “ nachukia talaka, asema Bwana Mungu wa Israeli,” kulengana na biblia,mpango wa Mungu juu ya ndoa ni iwe ushikamano wa siku zote za mwanadamu duniani. “ Hata si wawili tena bali mmoja. Kwa hivyo kile Mungu amekiunganisha mwanadamu asikitenganishe” (mathayo 19:6). Mungu antambua ya kwamba kwa kuwa ndoa ni ya wenye dhambi wawili, talaka haina budi kutokea. Katika agano la kale aliweka shaeria za kulinda haki za watalaka hasa wanawake (kumbukumbu la torati 24:1-4). Yesu akasema sheria hizi zilitolewa kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya wanadamu lakini
Matendo ya Mitume
TUJIFUNZE KATIKA MLANGO NA MUNGU ATAWABARIKI SANA.
1 Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi.2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu,
3 akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo.
4 Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache.
5 Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;
6 na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako,
7 na Yasoni amewakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema na kwamba yupo mfalme mwingine, aitwaye Yesu.
8 Wakafadhaisha ule mkutano na wakubwa wa mji walipoyasikia hayo.
9 Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yasoni na wenziwe wakawaacha waende zao.
10 Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi.
11 Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
12 Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache.
13 Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipopata habari ya kwamba neno la Mungu linahubiriwa na Paulo hata katika Beroya, wakaenda huko nako wakawachafua na kuwafadhaisha makutano.
14 Mara hiyo wale ndugu wakampeleka Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo wakasalia huko.
15 Lakini wale waliomsindikiza Paulo wakampeleka mpaka Athene; nao wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kwamba wasikawie kumfuata, wakaenda zao.
16 Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake.
17 Basi katika sinagogi akahojiana na Wayahudi na waliomcha Mungu, na wale waliokutana naye sokoni kila siku.
18 Na baadhi ya Waepikureo na Wastoiko, wenye ujuzi, wakakutana naye. Wengine wakasema, Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza habari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akihubiri habari za Yesu na ufufuo.
19 Wakamshika, wakamchukua Areopago, wakisema, Je! Twaweza kujua maana ya elimu hii mpya unayoinena?
20 Kwa maana unaleta mambo mageni masikioni mwetu, tutapenda kujua, basi, maana ya mambo haya.
21 Kwa maana Waathene na wageni waliokaa huko walikuwa hawana nafasi kwa neno lo lote ila kutoa habari na kusikiliza habari za jambo jipya.
22 Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini.
23 Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.
24 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;
25 wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.
26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;
27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.
28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.
29 Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu.
30 Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.
31 Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.
32 Basi waliposikia habari za ufufuo wa wafu wengine walifanya dhihaka; wengine wakasema, Tutakusikiliza tena katika habari hiyo.
33 Basi hivi Paulo akaondoka akawaacha.
34 Baadhi ya watu wakashikamana naye, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionisio, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao.
Wednesday, September 2, 2015
KUSHUHUDIA[UINJILISTI]
I. MAANA
Kwa nini tunashuhudia watu? Kwa nini tuwashuhudie watu?
- Ni kutangaza (kutoa ushuhuda) kuhusu mambo yale ambayo uliyoyaona na kuyasikia au hata kuyaonja au kuyagusa – kuhusu Mungu. [1Yohana 1: 1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; 2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.]
- Siyo maana yake kumueleza mtu kuwa yeye ni mwenye dhambi na wewe ni mwenye haki mbele za Mungu, eti kwa sababu wewe umeokoka nayeye hajaokoka, na kwamba wewe unakwenda mbinguni; na kwa sababu yeye hajaokoka anakwenda motoni(jehanamu) hapana!
- Siyo kujisifu mbele za watu au kujivunia wokovu!
- Ni kutumika mbele za Mungu kwa ajili ya wenye dhambi(ulimwengu) ili nao walijue Neno, waamue kumuamini BWANA Yesu Kristo na waepukane na dhambi, shetani na matui; bali wapate Wokovu na uzima wa milele.
- Wapate kumjua BWANA YESU KRISTO, upendo wake, uweza wake, huruma zake, na wokovu mkuu sana wa Mungu kwa mwanadamu.
- Ni kuwashirikisha wengine habari njema yaa mema uliyoyapata kutoka kwa Mungu, ambayo Mungu anapenda nao wayapate.
Kwa nini tunashuhudia watu? Kwa nini tuwashuhudie watu?
- BWANA Yesu Kristo alitumwa kwa sababu hii ya kuhubiri ufalme wa Mungu Luka 4:43 Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa. 44 Basi, alikuwa akihubiri katika masinagogi ya Galilaya.
- Kuifikisha ujumbe wa Wokovu na upendo wa Mungu kwa wenye dhambi na wasiomjia Mungu; yaani, kuutangaza mwaka wa BWNA uliokubalika.
- Kuzivunja kazi za Ibilisi
- Kuwafungua waliofungwa na Ibilisi
- Watu wanakufa dhambini na kwenda motoni
- Utahukumiwa kwa sababu ya hao wanaopotea
Kristo pekee awaondoleeni roho ya kukata tamaa inayoisumbua mioyo yenu
Na Sarah Pelaji
Tunapofanya kumbukumbu ya miaka 25 tangu alipotutembelea Mtakatifu Yohane Paulo II (Papa) mwaka 1990, ni vyema tukarejea maneno ya hekima aliyotuletea kama zawadi sisi watoto wa Tanzania.
Ni maneno ambayo ni hai katika maisha yetu ya kila siku hasa pale tunapoelemewa na mizigo ya ulimwengu huu, dhambi zetu na matatizo mbalimbali ya kiroho na kimwili ambayo yanawakatisha wengi wetu tamaa na kuona zawadi ya maisha haina maana tena.
Basi tufarijiwe na maneno haya ya Mtakatifu Yohane Paulo II (Papa) aliyoyatoa katika Kanisa Kuu la Mtaatifu Yosefu Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam
“Ndugu zangu, Amani ya Bwana iwe nanyi.
Tuesday, August 4, 2015
Nina wezaje kupokea msamaha wa dhambi toka kwa Mungu?
Swali: "Nina wezaje kupokea msamaha wa dhambi toka kwa Mungu?"
Jibu: Matendo 13:38 yasema, “Basi naijulikane kwenu, ndugu zangu ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi.”
Msamaha ni nini na kwanini ninauhitaji?
Neno “samehe” linamaanisha kusafisha nia au jambo nakulifanya kutokuwa na mawaa yoyote, ku achilia, kufutilia mbali deni. Tunapo kosea mtu, huuliza msamaha wao ili tukarudishe uhusiano. Msamaha haupeanwi kwa sababu mtu anastahili kusamehewa. Hakuna anaye stahili kusamehewa. Msamaha ni ishara ya upendo, huruma na neema. Msamaha ni uamuzi wa kutoshikilia jambo ndani yako kinyume cha mtu mwengine, haijalishi amekukosea kiasi gani.
Bibilia inatuambia yakwamba sote tunahitaji msamaha toka kwa Mungu. Sote tumefanya dhambi. Mhubiri 7:20 asema, “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.” 1Yohana 1:8 asema, “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” Dhambi zote ni kitendo cha uasi kinyume chake Mungu (Zaburi 51:4). Basi kwa hivyo, tunahitaji kwa vyovyote msamaha wake Mungu. Kama dhambi zetu hazitasamehewa, tutakuwa katika adhabu ya milele tukiteseka kwa ajili ya madhara ya dhambi zetu (Mathayo 25:46;Yohana 3:36).
Msamaha-Je, ni upate vipi?
Kwa shukurani, Mungu ni mwenye upendo na huruma-mwenye ari ya kutusamehe dhambi zetu! 2Petro 3:9 asema, “Yeye hutuvumilia maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” Mungu anatamani kutusamehe, kwa hivyo alitoa kwa ajili ya msamaha wetu.
Adhabu ya haki pekee inayostahili kwa ajili ya dhambi zetu ni mauti. Sehemu ya kwanza ya kitabu cha Warumi 6:23 yasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…..” Mauti ya milele ndiyo ndiyo tuliyopokea kama mshahara wa dhambi zetu. Mungu, kwa mpango wake mahususi, alifanyika kuwa mwanadamu - Yesu Kristo (Yohana 1:1, 14). Yesu alikufa juu ya msalaba kwa kuchukua adhabu tuliyo stahili-mauti. 2Wakorintho 5:21 inatufundisha, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. “Yesu alikufa msalabani, akichukua adhabu tuliyo stahili!Kama Mungu, kifo chake Yesu kilitoa msamaha wa dhambi kwa ulimwengu mzima. 1Yohana 2:2 asema, “Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. “Yesu alifufuka katika wafu, akishuhudia ushindi juu ya dhambi na mauti (1Wakorintho 15:1-28). Mungu apewe sifa kwa kupitia kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo, Sehemu yote ya pili ya kitabu cha Warumi 6:23 ni kweli, “…bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Je, ungetaka dhambi zako zisamehewe? Je, uko na hisia za kuudhi za kila mara zinazo kuhukumu na kuonekana kuwa ngumu ku epukika?Msamaha wa dhambi zako upo ikiwa utamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako. Waefeso1:7 yasema, “katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” Yesu alitulipia deni ili tukapate kusamehewa. Unacho stahili ni kumuuliza Mungu akusamehe kupitia kwake Yesu, ukiamini yakwamba Yesu alikufa ili upate msamaha-naye atakusamehe! Yohana 3:16-17 ina habari hii ya ajab, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”
Msamaha-Je, ni jambo lililo rahisi?
Ndio, ni rahisi! Huwezi kupata msamaha toka kwa Mungu. Huwezi kulipia msamaha wako toka kwa Mungu. Unaweza ku upokea tu, kwa imani, kupitia neema na huruma za Mungu. Kama unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na kupokea msamaha toka kwa Mungu, hapa kuna ombi unalo weza kuomba. Kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haiwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutaleta msamaha wa dhambi. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea msamaha. “Mungu, najua ya kwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu na nina weak imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu/ya ajabu na kwa msamaha! Amina.”
Je umepata uzima wa milele?
Swali: "Je umepata uzima wa milele?"
Jibu: Bibilia inaonyesha njia ya wazi ya uzimani.Mwanzo ni sharti tutambue yakwamba tumetenda dhambi kinyume chake Mungu: “Kwasababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi Mungu,ambayo yanafanya tustahili adhabu.Kwa kuwa dhambi zetu ziko kinyume kabisa na Mungu aliye uzima wa milele,basi ni adhabu ya milele pekee itoshayo. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti,bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).
Hata hivyo Yesu Kristo asiyekuwa na dhambi (1 Petro 2:23), mwana wa Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Yohana 1:1,14) na akafa ili kutulipia adhabu. “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi,kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu,tulipokuwa tungali wenye dhambi” (Warumi 5:8). Yesu Kristo alikufa msalabani (Yohana 19:31-42), kwa kuchukua adhabu ambayo sisi tulistahili (2Wakorintho 5:21). Siku tatu baadaye akafufuka katika wafu (1Wakorintho 15:1-4), kudhihirisha ushindi juu ya dhambi na mauti. “kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu” (1Petro 1:3).
Kwa imani ni sharti tuungame dhambi zetu na tumrejee Kristo kwa ajili ya wokovu (Matendo 3:19). Tukiweka imani yetu kwake, kwa kuamini kifo chake msalabani kama malipo ya dhambi zetu,tutasamehewa na kuahidiwa uzima wa milele mbinguni. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). “Kwa sababu,ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10:9). Imani pekee katika kazi aliyo ikamilisha Kristo pale msalabani ndiyo njia ya kweli ya pekee ya uzimani! “Kwa maana nimeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yoyote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9).
Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako,tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haitakuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo peke yake ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumuelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu,najua yakwamba nimetenda dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Nina ziacha dhambi zangu na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu /ya ajabu na kwa msamaha - karama ya uzima wa milele! Amina!”
INJILI YA YESU KRISTO
INAMHITAJI KILA MWANADAMU.
BWANA YESU asifiwe ndugu.
Karibu tujifunze habari njema za ufalme wa MUNGU.
Injili maana yake ni habari njema za ufalme wa MUNGU.
Kama kuna kitu cha muhimu cha kuhubiri kwa wahubiri basi injili ni jambo
la kwanza.
Injili ndiyo inayohubiri wokovu.
Injili ndiyo inayohubiriwa na watu wanapata ondoleo la dhambi kama
wakimpokea BWANA YESU.
Injili ya BWANA YESU inamuhitaji kila mwanadamu, wanaoipokea injili na
kutubu na kuanza kuishi maisha sahihi ya wokovu hao wataurithi uzima wa
milele.BWANA YESU anatutaka wanadamu wote tutubu na kuiamni injili, Neno
la MUNGU ni injili na shabaha ya Neno la MUNGU ni ili wanadamu wafike
uzima wa milele, YESU anakutaka wewe ndugu uiamini injili, Marko 1:14-15
'' ......... YESU akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya
MUNGU, akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni,
na kuiamini INJILI. ''
Injili Ni Neno La MUNGU, Sehemu Nyingine Biblia Imesema Kwamba Injili Ni
Neno La Msalaba. Wokovu Wetu Unatokana Na Injili, Msingi Wa Wokovu Wetu
Umesimama Juu Ya Yale Yaliyotendeka Msalabani, Juu Ya Ukweli Na Juu Ya
Kazi Ya MUNGU. 1 Kor 15:3 '' Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo
yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa KRISTO alikufa kwa ajili ya
dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; ''
-Kama KRISTO asingelikufa msalabani basi injili isingehubiriwa, lakini
sasa BWANA wetu YESU KRISTO yuu hai, ameshinda kifo na mauti na sasa
yeye ndio sababu ya watu kuupata uzima wa milele, Hakuna Mwokozi
mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO.
Injili Ni Ujumbe Wa MUNGU, Wala Sio Maoni Ya Wakristo Tena Sio Mawazo Ya
Wafuasi Wa Kanisa Lolote. Ndugu Hubiri Injili Ya KRISTO Siku Zote Za
Maisha Yako.
Katika Biblia Kila Jambo Lazima Lithibitishwe Kwa Mashahidi Wawili Au
Watatu. Hata Wokovu Wetu Unathibitishwa Na Mashahidi Wawili NENO LA
MUNGU Na ROHO MTAKATIFU.
1: NENO Linasema Hakuna Hukumu Juu Ya Waliookoka(Warumi
8:1, Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika KRISTO
YESU. )
YESU Ndio Sababu Ya Wokovu Wetu Sisi Tunaomtii(Waebrania 5:9, naye
alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote
wanaomtii; ),
2. ROHO MTAKATIFU Anashuhudia Kwamba Sisi Tu Watoto Wa
MUNGU(Warumi 8:16-17, ROHO mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya
kuwa sisi tu watoto wa MUNGU; na kama tu watoto, basi, tu warithi;
warithi wa MUNGU, warithio pamoja na KRISTO; ......... )
-ROHO MTAKATIFU anashuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi tu watoto wa
MUNGU.
-Wasiookoka na watenda dhambi hata ROHO MTAKATIFU hayumo ndani yao
hivyo hawezi kushuhudia kwao.
-Na Ndio Maana Yeye ROHO Anakaa Ndani Yetu(Warumi 8:9, Lakini ikiwa ROHO
wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata
roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake. )
-Kama huna ROHO MTAKATIFU huwezi kuzishinda dhambi.
-Kama una ROHO MTAKATIFU na ukashindwa kumtii pia huwezi kushinda
dhambi.
-Kama huna ROHO MTAKTIFU huwezi wewe sio wa KRISTO.
-Lakini pia kuna tofauti kati ya kujazwa ROHO na kufurika ROHO. Kuna
kunena kwa lugha na pia wakati mwingine kunena kwa Lugha ni karama kama
Biblia inavyosema.
-Kuna wenye kiwango kidogo cha udhihilisho wa ROHO MTAKATIFU na kuna
wenye kiwango kikubwa.
-Kuna watu ROHO huongea nao kwa sauti kabisa, kuna watu hata akama
anaambiwa jambo lolote iwe ni kwenye simu au kwa njia ya kawaida ROHO
anamwambia ''hilo unaloambiwa ni la uongo''
-ROHO MTAKATIFU ni muhimu sana kwa kila mwenda mbinguni.
-Tamani kufikia kiwango cha juu cha udhihilisho wa ROHO MTAKATIFU.
-ROHO MTAKATIFU ni mtakatifu hivyo hakikisha unaokoka na kuwa mtakatifu.
Injili ya BWANA YESU inaambatana na uponyaji wa roho na mwili.
Ndugu, Usipoteze Uhakika Wa Wokovu Kwa Kukaa Kwenye Mafundisho Ya Kanisa
Linakataa Neno La MUNGU Na Nguvu Ya MUNGU Huku Kanisa Hilo KRISTO Kwao
Akiwa Ni Ziada Tu. Sali Kanisa Ambapo Utapata Injili Kamili, Injili
Ambayo Haijawekewa Chumvi Ya Udhehebu.
Watu Wengi Huishi Kama Wateule Wa MUNGU Lakini Hawajaokoka. Ndugu
Anayeishi Hivyo Huyo Amepungukiwa Na Utukufu Wa Ukombozi Utokao
Mbinguni. Maisha Ya Bila Kuokoka Ni Ya Kujisukuma Kwa Nguvu Zao Wenyewe.
Mteule Ni Yule Aliyepokea Asili Ya MUNGU Kwa Kuzaliwa Mara Ya Pili
Kutoka Juu. BABA Yao Wa Kiroho Yuko Mbinguni.
Hakuna anayetakiwa kuigeuza injili ya BWANA YESU, Kama yupo na alaaniwe
ndivyo Biblia inavyosema, Wagalatia 1:7-9 '' Wala si nyingine; lakini
wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya KRISTO. Lakini
ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote
isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema,
na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote
isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. ''
-Mtu akileta injili tofauti na Wokovu kupitia YESU KRISTO, huyo haijui
injili sahihi.
-Mtu akileta mafundisho yanayomkataa ROHO MTAKATIFU, huyo ni wakala wa
shetani.
-Mtu akileta mafundisho ya kwamba kuna njia nyingine ya uzima wa milele
nje na KRISTO, huyo ni baba wa uongo na ni shetani kabisa.
-Mtu akileta mafundisho yeyote yanayokataa kuokoka, huyo hajitambui na
hamjui MUNGU aliye hai.
-Mtu akihubiri kuabudu sanamu na kuabudu watu wakiwemo watakatifu, huyo,
huyo hayuko upande wa MUNGU.
=Anayeabudiwa ni MUNGU BABA(Ufunuo 19:10, 1 Nyakati 16:29) ,
=MUNGU MWANA(Mathayo 14:33, Mathayo 28:9; Luka 24:52; Yohana 9:38 )
=na MUNGU ROHO MTAKATIFU (Ayubu 33:4,Yohana 4:24) , ukimwabudu mariamu,
Musa au Eliya wewe uko upande wa sheatni hata kama una jina la Kikristo.
Ukitaka Kuwa Mkristo Mwenye Afya Njema Hakikisha Kwanza Unakula Chakula
Kizuri Ambacho Ni Neno La MUNGU. Pili Hakikisha Unakunywa Maji Mengi
Ambayo Ni Ujazo Wa ROHO MTAKATIFU. Tatu Hakikisha Unafanya Mazoezi
Ambayo Ni Kumtumikia MUNGU Na Kutenda Kazi Yake. Nne Pata Hewa Safi
Ambayo Ni Kwenda Kwenye Ibada Kanisani Kila Iitwapo Leo. Na Mwisho
Jiburudishe Kwa Kuwa Na Ushirika Na Wateule Wengine Mkishauriana Na
Kuombeana.
Mafundisho Yeyote Ya Dini Ambayo Yanakuacha Mashakani Juu Ya Wokovu Wa
Roho Yako, Hayo Hayaambatani Kabisa Na Injili Ya KRISTO. BWANA YESU
Anasema Ukimpokea Yeye Kwa Imani Maana Yake Umepita Kutoka Mautini Na
Kuingia Uzimani (Yohana 5:24, Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye
neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala
haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani) . Wokovu
Ni Muhimu Sana Kwa Kila Mwanadamu. YESU KRISTO Anaokoa, Ukiamini Leo
Unaokoka.
Neno La MUNGU Humnyamazisha Mshitaki Wetu ibilisi. Ukitaka
Kumnyamazisha shetani Tumia Neno La MUNGU Kwenye Maombi Yako Na Maisha
Yako Kwa Ujumla, Kiri Neno La MUNGU Na Hakikisha Unaishi Kama Neno
Litakavyo. BWANA YESU Anakupenda Sana.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku
nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio
kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na
utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi
kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Je, ni gani sheria hizi Nne za Kiroho?
Swali: "Je, ni gani sheria hizi Nne za Kiroho?"
Jibu: Sheria hizi Nne za kiroho ni njia za kushiriki habari njema za wokovu upatikanao kupitia imani ndani ya Yesu Kristo. Ni njia moja rahisi ya kupanga habari muhimu katika injili kwa sehemu Nne.
Ya kwanza kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Mungu anakupenda na ana mpango wa ajabu juu ya maisha yako.” Yohana 3:16 yatwambia, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 10:10 yatupa sababu ya kuja kwake Yesu, “Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” Ni kitu gani kinachotuzuia na upendo wa Mungu? Ni kitu gani kinacho tupinga kupata uzima ulio tele?
Ya pili kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Hali ya Utu wa mwanadamu inachafuliwa na dhambi na hivyo basi kutengwa na Mungu. Kwa matokeo haya basi, hatuwezi kamwe kuufahamu mpango wa ajabu alio nao Mungu juu ya maisha yetu.” Warumi 3:23 inatuhakikishia habari hii, “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Warumi 6:23 inatupatia madhara ya dhambi, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.” Mungu alituumba ili tukaweze kuwa na ushirika naye. Hata hivyo hali ya Utu/Ubinadamu ilileta dhambi katika dunia, na hivyo basi kutengwa na Mungu. Tumeharibu uhusiano pamoja naye ambao Mungu alikusudia tukaupate. Je, suluhisho ni nini?
Ya tatu kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Yesu Kristo ndiye toleo la Mungu pekee kwa ondoleo la dhambi zetu. Kupitia kwa Yesu Kristo, tunaweza kusamehewa dhambi zetu na kurudisha ushirika wa haki na Mungu.” Warumi 5:8 yasema, “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” Wakorintho 15:3-4 inatufahamisha kinachotupasa kujua na kuamini ili tupate kuokoka, “……ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko, yakuwa alizikwa; ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko….” Yesu mwenyewe akiri yakwamba yeye ndiye njia ya pekee ya wokovu katika Yohana 14:6, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Je, ninawezaje kupata kipawa hiki kikuu cha wokovu?
Ya Nne kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Ni sharti tuweke imani yetu ndani ya Yesu Kristo kama mwokozi ili tukaweze kupokea kipawa cha wokovu na kujua mpango wa ajabu wa Mungu juu ya maisha yetu. Yohana 1:12 inatuelezea hivi, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. “Matendo16:31 inazungumzia kwa ufasaha zaidi, “Mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka!” Tunaweza kuokolewa kwa neema peke yake, kwa njia ya imani pekee, ndani ya Yesu Kristo pekee (Waefeso 2:8-9).
Ukiwa unataka kumwamini Yesu Kristo kama mwokozi wako, sema maneno yafuatayo kwa Mungu. Kusema maneno haya haitakuokoa, lakini itawezekana kwa kumwamini Kristo!Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kum shukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, ninajua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha- karama ya uzima wa milele! Amina!”
Monday, July 20, 2015
MAMBO YA KUMSAIDIA KIJANA ALIYEOKOKA AISHI MAISHA YENYE USHUHUDA MZURI
Mtume Paulo katika waraka wake kwa Timotheo anamwambia hivi, ‘Mtu awaye yote ASIUDHARAU ujana wako, bali uwe KIELELEZO kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. JITUNZE nafsi yako, na mafundisho yako. DUMU katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo UTAJIOKOA NAFSI YAKO NA WALE WAKUSIKIAO PIA’ (1Timotheo 4:12 & 14).
Sentensi hizi zinatuonyesha kwamba kijana yeyote ambaye amefanya uamuzi wa kuokoka, kwa hakika amefanya maamuzi ambayo yanamtaka amaanishe katika kumfuata kwake Yesu au kuuishi wakovu wake. Pamoja na kumpa Yesu maisha yake ni lazima kijana afanye maamuzi ya kuishi maisha ya kudumu kumpendeza Mungu kwa kuzikubali gharama zinazohusiana na wokovu aliouchagua na si kuishi maisha yenye kupelekea jina la BWANA kutukanwa kama ilivyo kwa baadhi ya vijana wengi leo.Ukisoma mstari huu wa 1Timotheo 4:14 kwenye toleo la kiingereza la ESV unasema ‘Keep a close watch on yourself and on the teaching. Persist in this, for by so doing you will save both yourself and your hearers’. Kwa mujibu wa dictionary ya kigiriki na kiebrania neno ‘save’ lina maana ya kuweka huru (deliver), kulinda (protect), kuponya (heal), kutunza (preserve), kuokoa (save). Jambo muhimu ambalo Mtume Paulo alikuwa akilisisitiza hapa ni hili; jambo muhimu si tu kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wako, bali kila mwamini ana kazi kubwa ya kufanya ili KUULINDA NA KUUTUNZA WOKOVU WAKE.
Moja ya changamoto kubwa sana ambazo zinawakabili vijana wengi waliokoka leo ni kuipenda dunia. Kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana wengi na kwa sababu ya kuipenda dunia; (a) Mahusiano ya vijana wengi na Mungu wao yameharibika (b) Maisha ya vijana wengi yamekosa uelekeo (c) Kutokana na uovu wao jina la Bwana Yesu limekuwa likitukanwa.
Katika kile kitabu cha 1Yohana 2:16 ni dhahiri kwamba dunia imejaa TAMAA YA MWILI, TAMAA YA MACHO NA KISHA KIBURI CHA UZIMA. Tamaa ina nguvu ya kuvuta pamoja na kudanganya, naam inamuingiza mtu kwenye jaribu. Hii ina maana tamaa ni mlango, naam mlango huu unapaswa kufungwa mapema usikupoteze. Hebu tujifunze kutokana na anguko la mfalme Daudi na mke wa Bathssheba (Samweli 11:1-2). Tunaona anguko la Daudi lilisaabishwa na kumpa Ibilisi nafasi kwa kutokwenda vitani. Mkristo akipoa katika kuvipiga vita vya kiroho inakuwa rahisi kwake kuanguka dhambini (Yakobo 1:14-15), naam kumbuka kwamba siku zote tamaa inalenga kumfurahisha mtu binafsi (self-pleasing) bila kujali matokeo yake.
Hivyo katika nyakati tulizonazo sasa suala la kuipenda dunia ni lazima litafutiwe ufumbuzi wa kudumu miongoni mwa vijana wetu. Ujumbe huu mfupi unalenga kueleza kwa namna gani kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana na nini vijana wafanye ili kuikabili na kuishinda changamoto husika.
Pia katika waraka 2Timotheo 2:15 Mtume Paulo anaendelea kumwambia kijana Timotheo ‘Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli’.
Pengine kila mmoja wetu atafakari maisha yake kwa kuhusianisha na maelekezo ya Paulo kwa Timotheo. Naomba jiulize na kujijibu kwa uaminifu kwamba mosi, je, ujana wako wako unaheshimika au unadharauliwa? Pili, je, kwa waamini wenzako umekuwa kielelezo cha kweli kwa habari ya imani, upendo, usafi, usemi na mwenendo au la?
Binafsi nimekuwa nikijiuliza ni kwa namna gani kijana atahakikisha kwamba (a) Ujana wake haudharauliwi (b) Anakuwa kielelezo kwa waamini wenzake (c) Anathibitisha kwamba kweli amekubaliwa na Mungu. Naam katika kusoma na kutafakari neno la Mungu nimejifunza kwamba zifuatazo ni njia ambazo zitatusaidia sisi vijana wa leo kuifikia kweli hii ya neno la Mungu.
- Kijana adumu katika kuomba na kusoma (kutafakari + kulitenda) neno la Mungu
Naam katika Mathayo 26:41 imeandikwa ‘Kesheni, mwombe, MSIJE mkaingia majaribuni; roho I radhi, lakini mwili ni dhaifu’. Yohana 17:17 inasema ‘uwatakase kwa ile kweli ;neno lako ndiyo kweli. Mambo haya mawili yanapaswa kwenda kwa pamoja nakijana akidumu katika kuomba na kusoma neno la Mungu ushindi ni lazima.
- Kijana asimpe Ibilisi nafasi.
Hii ndiyo sababu iliyomfanya Paulo awaambie Waefeso ‘Wala msimpe Ibilisi nafasi’ (Waefeso 4:27) na pia awaambie Warumi “Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili hata kuwasha tamaa zake’. Toleo la KJV linasema ‘But put ye on the Lord Jesus Christ, and MAKE NOT PROVISION for the flesh, to fulfill the lusts thereof’. Na toleo la ESV linasema ‘But put on the Lord Jesus Christ, AND MAKE NO PROVISION FOR THE FLESH, TO GRATIFY ITS DESIRES’ (Warumi 13:14). Je hivi leo ni kwa namna gani vijana wanaungalia mwili na kumpa Ibilisi nafasi? – Mitandao ya kijamii, kuangalia na kusoma vitu vichafu, hasira, mawazo, mazingira.
- Kijana azikimbie tamaa za ujanani
Pamoja na ushawishi aliokutana nao Yusufu alijibu kwamba ‘Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?’ Mwanzo 39:12 inasema ‘huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake akakimbia akatoka nje. Ili kuzikimbia tamaa za ujanani kijana anapswa (a) ajiepushe na mazingira/marafiki wabaya (Mithali 1:10 & 1Wakorinto 15:33) (b) Ajitenge na uovu (Mithali 16:17, Zaburi 1:1).
Ni muhimu ukakumbuka kwamba hukupewa mwili kwa ajili ya zinaa maana miili yenu ni ni viungo vya Kristo na tena hekalu la Roho Mtakatifu (1 Wakorinto 6:15 & 19), tena yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye (1 Wakorinto 6:17) maana tena imeandikwa ‘Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili’ (1Wakorinto 6:13b). Tena imeandikwa ‘Lakini uasherati USITAJWE kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu’ (Waefeso 5:3).
- Kijana ajifunze kuenenda kwa roho na si kwa mwili
Je kuenenda kwa Roho ndio kukoje?
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, ATAWAONGOZA awatie kwenye kweli yote (Yohana 16:13) na pia imeandikwa ‘kwa kuwa wote WANAOONGOZWA na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu’ (Warumi 8:14). Kuenenda kwa Roho ina maana ya kuishi kwa kufuata utaratibu/uongozi wa Roho Mtakatifu kwenye maisha yako (Warumi 8:2).
Naam kadri unavyokuwa mtiifu kufuata utaratibu wake ndivyo unavyokuwa mbali na sheria ya dhambi na mauti ambayo ni mwili. Kumbuka imeandikwa ‘kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waiufuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia mwili ni mauti bali nia ya roho ni uzima na amani (Warumi 8:5-6) na pia Wafilipi 4:8.
Naam imeandikwa ‘Kila mmoja wenu ajue KUUWEZA MWILI wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu. Maana Mungu HAKUTUITIA UCHAFU, bali tuwe katika utakaso’ (1Thesalonike 4:4-5, 7). Ni jambo la ajabu sana kwamba kwamba tumepewa fursa ya kuiweza miili yetu. Ndio tunapaswa kuuweza mwili kwa maana ya kuudhibiti kwa kuuongoza na kuufanya ufuate nia ya roho.
Kijana mwenzangu kama umechagua kumpa Yesu maisha yako kwa njia ya wokovu, nakusihi na kukushauri zingatia haya ili kuwa na maisha yenye kielelezo na ushuhuda mzuri maana imeandikwa ‘Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa’ (2Petro 2:20-21).
Neema ya Kristo iwe nanyi, na tuzidi kuombeana.
Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA.
KWA NINI VIJANA WENGI HAWAJAKA KWENYE NAFASI ZAO KI-MUNGU?
Iyohana 2:14
Kila
kundi katika kanisa, jamii na hata nchi Mungu amelipa nafasi na wajibu
wake maalumu wa kutekeleza. Pia Mungu anao mtazamo wake binafsi na
matarajio yake kwa hayo makundi
mbali
mbali ndani ya nchi. Vijana, watoto, wababa, wazee, wanawake, viongozi
wote / yote yana mtazamo wake mbele za Mungu. Ukimuuliza Mungu nini mtazamo wako kwa vijana, atakujibu soma vizuri IYohana 2:14 maana yake Mungu anawatazama vijana kama watu wenye nguvu, watu ambao neno la Mungu linakaa ndani yao na pia wamemshinda mwovu.
Sasa ukirudi mazingira halisi unaona kwa asilimia kubwa vijana wengi hawako kwenye nafasi ambazo Mungu aliwakusudia. Lengo la somo hili ni :-– Kueleza sababu za kwa nini vijana wengi hawajakaa katika nafasi zao.– Kumweleza kijana mambo ya kujiepusha nayo ili aweze kukaa kwenye nafasi yake.– Kumpa kijana maarifa yatakayomsaidia kurejea kwenye nafasi yake na ili aweze kutekeleza matarajio ya Mungu kwake. Zaidi ujumbe huu umekusudia kulenga na kuelewesha vijana waliokoka, nazungumza na vijana waliookoka maana hawa ndio ambao Mungu amewatamkia maneno haya au kuwa namtazamo huu juu yao. Zipo sababu nyingi
lakini hizi zifuatazo ni za msingi na zimesababisha wengi kuishi maisha
nje ya kusudi la Mungu na kufa bila kutekeleza matarajio ya Mungu kwao sababu hizo ni:-
– Moja vijana wengi hawajajazwa nguvu za Roho Mtakatifu.
Biblia inasema katika matendo ya Mitume 1:8 kwamba “lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika uyahudi wote, na samaria, na hata mwisho wa nchi”. Hivyo vijana wengi hawajakaa katika nafasi zao kwasababu wengi wa vijana leo makanisani hawajajazwa nguvu za Roho Mtakatifu si kwamba Mungu
hataki kuwajaza lakini shida ipo kwa vijana wenyewe wengine kutotaka
kujazwa nguvu hizo, lakini wengine hawajui nini wafanye wajazwe nguvu za Roho Mtakatifu na wengine wanajua lakini hawana kiu ya kujazwa nguvu hizo.
Pili vijana wengi hawajui namna ya kuenenda kwa Roho .Paulo kwa warumi anasema” kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” Warumi 8:14 na pia kwa wagatia anasema” Basi nasema enendeni kwa Roho hamtatimiza kamwe tamaa za mwili “Gal 5:16. Kuna wengi waliojazwa lakini si wote wanaoenenda au wanaoishi wa Roho. Vijana wengi Mungu amewapa vitu vizuri sana ndani yao lakini kwa sababu ya kukosa utiifu na kutoenenda kwa Roho wameshindwa kusimama kwenye nafasi zao.
Tatu vijana wengi wameshindwa kushirikiana na upako wa Mungu uliodhihirishwa kwao.
Hili ni tatizo kubwa kwa kweli, Mara nyingi Mungu amekuwa akiwapa upako, nguvu au uweza wa kufanya mambo mbalimbali vijana. Sasa si vijana wote wanaojua namna ya kushirikiana na huo upako ambao Mungu aliwapa kwa jambo fulani Mfano, Mungu anaweza akampa kijana upako wa kuomba lakini kijana huyo badala ya kuomba yeye anaangalia mpira, au ni mwanafunzi anatakiwa kusoma na Mungu ameleta upako huo sasa yeye anaenda kuomba mambo huwa hayakai hivyo. Upako lazima utumike kwa kusudi lile uliotumiwa. Upako wowote unaokuja kwako unakuja kwa kusudi maalumu.
Nne Kukosa maarifa ya Mungu.
Mungu anasema katika Hosea 4:6 kila kipengele cha kwanza watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa na pia katika Zaburi 119:9 anasema “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii akilifuata neno lake”. Sasa kwa sababu nazungumza na vijana naweza nikaweka mistari huu hivi “Vijana wangu wanaagamizwa kwa kukosa maarifa. Maarifa yanayozungumzia hapa ni mafundisho ya neno la Mungu.
Vijana wengi wako tayari kuangalia mechi mbili mfululizo kuanzia saa nne kasoro usiku hadi saa nane kwa masaa ya Kitanzania, lakini hawako tayari kusoma Biblia kwa saa moja, wako tayari kuangalia “Movie” za kinigeria, au za kizungu hata masaa matatu (3) lakini si kuangalia na kusikiliza mafundisho ya Neno la Mungu. Na Biblia inasema Apendaye mafundisho hupenda maarifa. Sasa kwa vile vijana wengi hawapendi mafundisho ndiyo maana hawako kwenye kusudi la Mungu.
Tano, vijana wengi bado wanaipenda dunia,
Mzee Yohana katika 1Yohana 2:15” Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia, mtu akiipena dunia kumpenda Baba hakupo ndani yake”. Na pia Daudi anasema katika Zaburi 1:1 Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki wala kusimama katika njia ya wakosaji wala hakuketi barazani pa wenye mzaha.Ni vijana wachache sana katika kanisa la leo ambao wako tayari kujikana nafsi zao kwa ajili ya Mungu wengi wanapenda kupoteza muda kwa habari zisizo za Msingi, wengi wanapenda mzaha na utani, ni vijana wachache ambao wanaweza kuacha kuangalia mchezo kwenye TV, au akakataa kwenda kutembea ufukweni kwa lengo la kuomba, au kusoma Neno, ninachojaribu kusema hapa ni hiki, najua kila jambo lina wakati wake, lakini ni vijana wachache sana waliojizuia katika mambo ya mwili kwa ajili ya kufanya yaliyo mapenzi ya Mungu.
Sita, Vijana wengi hawajazivaa silaha za vita.
Waefeso 6:11 Vaeni Silaha zote za Mungu, mpate kuzipinga hila za shetani.Viajana wengi wameshindwa kumshinda mwovu kwa sababu hawazajivaa silaha za vita. Wengine hawajui silaha za vita ni zipi? Lakini wengine wanajua lakini hawajazivaa. Ile sura ya sita ya waefeso 6:10-18 Paulo anazungumzia silaha za vita, ambazo ni kwlei, haki, amani, Imani, wokovu na Neno la Mungu. Sasa hizi ni silaha na kama ni silaha zina namna zinavyovaliwa na namna zinavyotumika. Sasa si vijana wote waliozivaa silaha, wengi hawasomi neno la Mungu, hawatendi haki, wengi wana imani ya maneno isiyo ya Matendo.
Saba, Vijana wengi wanaishi bila kuwa na malengo katika maisha yao / maono.
Mithali 29:18. Inasema “Pasipo maono watu huacha kujizuia bali ana heri mtu yule aishikaye sheria”. Hivi leo ukiwauliza vijana wengi kwamba una maono au hasa malengo gani katika maisha yako? Asilimia kubwa watakujibu sina malengo yeyote yale.Wakati huo huo hakuna aliyeumbwa kwa bahati mbaya Yeremia 29 :12. Kwa kila mtu Mungu analokusudi maalum la kumuumba na pia anayo malengo na mikakati ya kumpa huyu mtu atekeleze katika maisha yake. Sasa kwa sababu vijana wengi hawana na hawajajua hayo malengo ndio maana wanafanya kila kinachotokea mbele yao bila kujua kama ni kusudi la Mungu.
Naamini baada
ya kuwa umesoma ujumbe huu umepata maarifa ya kukusaidia kukaa katika
nafasi yako kama kijana kwa sababu umeshajua sababu za kuktokukaa kwenye
nafasi yako.
Wednesday, July 8, 2015
NGUVU YA DAMU YA YESU
Damu ya Yesu ina nguvu sana! Lakini je unajua ni kwa nini ilimwagika katika maeneo tofauti tofauti ya mwili wake?
Kwa mfano, tunasoma ya kuwa; “Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; …” (Luka 2:21). Tena imeandikwa katika wakolosai 2:11 ya kuwa: “Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo”.
Kwa mfano, tunasoma ya kuwa; “Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; …” (Luka 2:21). Tena imeandikwa katika wakolosai 2:11 ya kuwa: “Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo”.
HASARA ZA KULIPIZA KISASI - MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE
Usilipize Kisasi! Unasikia? Hata ikiwa umefanyiwa ubaya wa namna gani, Biblia inafundisha na inakusihi usilipize kisasi kwa huyo aliyekufanyia ubaya. Biblia inasema hivi:
Tuesday, July 7, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)