- Ni kutangaza (kutoa ushuhuda) kuhusu mambo yale ambayo uliyoyaona na kuyasikia au hata kuyaonja au kuyagusa – kuhusu Mungu. [1Yohana 1: 1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; 2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.]
- Siyo maana yake kumueleza mtu kuwa yeye ni mwenye dhambi na wewe ni mwenye haki mbele za Mungu, eti kwa sababu wewe umeokoka nayeye hajaokoka, na kwamba wewe unakwenda mbinguni; na kwa sababu yeye hajaokoka anakwenda motoni(jehanamu) hapana!
- Siyo kujisifu mbele za watu au kujivunia wokovu!
- Ni kutumika mbele za Mungu kwa ajili ya wenye dhambi(ulimwengu) ili nao walijue Neno, waamue kumuamini BWANA Yesu Kristo na waepukane na dhambi, shetani na matui; bali wapate Wokovu na uzima wa milele.
- Wapate kumjua BWANA YESU KRISTO, upendo wake, uweza wake, huruma zake, na wokovu mkuu sana wa Mungu kwa mwanadamu.
- Ni kuwashirikisha wengine habari njema yaa mema uliyoyapata kutoka kwa Mungu, ambayo Mungu anapenda nao wayapate.
Kwa nini tunashuhudia watu? Kwa nini tuwashuhudie watu?
- BWANA Yesu Kristo alitumwa kwa sababu hii ya kuhubiri ufalme wa Mungu Luka 4:43 Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa. 44 Basi, alikuwa akihubiri katika masinagogi ya Galilaya.
- Kuifikisha ujumbe wa Wokovu na upendo wa Mungu kwa wenye dhambi na wasiomjia Mungu; yaani, kuutangaza mwaka wa BWNA uliokubalika.
- Kuzivunja kazi za Ibilisi
- Kuwafungua waliofungwa na Ibilisi
- Watu wanakufa dhambini na kwenda motoni
- Utahukumiwa kwa sababu ya hao wanaopotea
- Ushuhuda wa ndani Kanisani kwa waaminio
- Umeachwa siku hizi haupo sana?
- Kujengana kwa maneno ya Mungu.
- USHUHUDA WA NJE KWA WASIOAMINI – UINJILISTI.
- MWENENDO WA MWAMINI AU MAISHA YAKO. Waebrania 3:6 bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho. Wafilipi 1:21 Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. 22 Ila ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui. 23 Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana; 24 bali kudumu katika mwili kwahitajiwa zaidi kwa ajili yenu. 25 Nami nikitumaini hayo, najua ya kuwa nitakaa na kudumu pamoja nanyi, ili mpate kuendelea na kufurahi katika imani; 26 hata mzidi kuona fahari katika Kristo Yesu juu yangu kwa sababu ya kuwapo kwangu pamoja nanyi tena. 27 Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili; 28 wala hamwaogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara mathubuti ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokovu, huo utokao kwa Mungu. 29 Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; 30 mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, na kusikia kwamba ninayo hata sasa.
- USHUHUDIAJI WA KIRAFIKI
- Kufanya urafiki na mtu asiyeamini ili kumfahamu kabla haujaanza kumweleza habari za BWANA Yesu Kristo. Mfano: unapotaka kumshuhudia mtu mwenye imani nyingine tofauti na ukristo, ni lazima kwanza upate kibali cha kuzungumza naye kwanza, ili akuone kweli unamaanisha kile unacho kiamini na kusema.
- Ni ushuhudiaji wa upole / ushuhudiaji wa rehema na mazungumzo ya kirafiki.
- Ni kumuombea pia mahitaji yake.
- USHUHUDIAJI WA KUTEMBELEA (MTAANI, BARABARANI, SOKONI, STENDI, NYUMBA KWA NYUMBA, HOSPITALINI, …)
- Kutembelea sehemu mbali mbali na kuongea na wale unaowakuta na kuongea nao kuhusu Wokovu.
- Ibada za ushemasi(nyumba kwa nyumba) ni njia ya kuabudu na kuwashuhudia ndugu za wapendwa na majirani katika nyumba hizo. Hivyo hudhuria ili ukashuhudie, bila kujali msimamo wa kiroho wa Yule anaye waalika!
- Kuwaombea pia mahitaji yao;
- Mathayo 10: 5 Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. 6 Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. 8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. 9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu; 10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake. 11 Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hata mtakapotoka. 12 Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni. 13 Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi. 14 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu. 15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule.
- Matendo 20:17 Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa. 18 Walipofika kwake, akawaambia, Ninyi wenyewe mnajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu wakati wote, 19 nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na kwa machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi; 20 ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lo lote liwezalo kuwafaa bali naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba, 21 nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.
- MKUTANO WA INJILI
- Ushuhudiaji wa hadharani kwa watu wote.
- VYOMBO VYA HABARI(Mass Media)
- Rediio, kanda, CD, Video, DVD, na TV.
- Mitandao: Face book, SMS, …
- Vipeperushi, magazeti, vitabu …
- Utangazaji kwa kipaza sauti – mfano Kanisa la Biblia.
- MICHEZO NA BURUDANI
- Nyimbo, mahubiri, uigizaji,
- Mpira wa miguu?
- TUKIO LA KUSHITUKIZA / DHARULA / GHAFLA.
- Ni kuituia nafai ya tukio la dharula; mfano, safarini katika basi, treni, ndege, meli, …(Waweza kumuulizaswali uliyekaa naye jirani hivi “Kwa imani uliyo nayo, kaka ukifa leo katika ajali katika safari hii unafikiri utakwenda wapi? Mbinguni au motoni?”)
- Katika ugonjwa au hatari ya kifo au vitani? Pia waweza kuitumia nafasi hiyo.
- MAJANGA, MAAFA NA MISIBA.
- Huu si wakati wa mkristo kufadhaika na kukata tama kama wasioamini, wala si wakati wa kuwatia watu moyo kwa ahadi au maneno mazuri tu! Bali kuwahubiria watu ili waokoke rohoni mwao kwanza. (Mathayo 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.)
- Usiwape tumaini tu kuwa yatakuwa shwari; wala usiwahukumu pia! Bali wakumbushe kujiandaa kukutana na Mungu wao siku ya hukumu, kwani biblia inasema hivi, katika Waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
- MUALIKO KATIKA TUKIO MAALUMU, kuhudhuria:-
- IBADA – SIFA NA KUABUDU
- BURUDANI NA MICHEZO
- Sherehe/Arusi – arusi za waliookoka ni muhimu sana kila kama ikiwezekana, shughuli ikafanywa na waliookoka ili kuweza kikamilifu kuwashuhudia wasioamini ili waokoke.( Kumbuka Arusi ya Kana)
- MPIRA WA MIGUU
- TAFRIJA / KARAMU- chakula cha pamoja; isiwe kawaida yetu kuomba michango tu(chakula cha hisani) bali kama tunavyofanya mikutano ya injili. [BWANA Yesu alihubiri katika MUALIKO WA CHAKULA: Mathayo 7:36 Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani. 37 Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu. 38 Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu. 39 Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi. 40 Yesu akajibu akamwambia, Simoni, nina neno nitakalo kukuambia. Akasema, Mwalimu, nena. 41 Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini. 42 Nao walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili. Katika hao wawili ni yupi atakayempenda zaidi? 43 Simoni akajibu akasema, Nadhani ni yule ambaye alimsamehe nyingi. Akamwambia, Umeamua haki. 44 Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. 45 Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu. 46 Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. 47 Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo. 48 Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako. 49 Ndipo wale walioketi chakulani pamoja naye walianza kusema mioyoni mwao, Ni nani huyu hata asamehe dhambi? 50 Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa amani.
- TAMASHA LA MUZIKI / KWAYA ( DISCO/DANCE)
- MAIGIZO(TAMTHILIA)
- VIKAO VYA CHAMA NA SERIKALI
- Mikutano ya kisiasa, vyama, na kazini.
- Eneo lako ulalofanyia kazi, biashara, housegirl/boy, …
- Ila uwe muangalifu sana, usiwe moja kwa moja…!
- USHUHUDIAJI KUPITIA TENDO LA UKARIMU WA VITU VILIVYOOMBEWA NGUVU ZA MUNGU.
- Kuwapa watu vitu – hasa majirani na marafiki zetu.
- Kumpa kila akuombaye
- Kuwakopesha watu kwa namna nzuri
- Kushirikiana nao na kusaidiana nao katika matatizo yao na kuwaombea.
- Kupaka mafuta yaliyoombewa … Ombea mafuta yako ya kupaka!
- SALIMIA NA UJITAMBULISHA
- Wewe ni nani unatoka wapi, unaishi wapi.
- ELEZA LENGO NA NIA YAKO
- Samahani, ninafahamu una shughuli nyingi, sipendi kukupotezea muda wako.
- Mimi ni mmoja wao wanaopenda kufahamu na kushirikiana kuhusu mambo ya imani kuhusu Mungu hapa nchini Tanzania; bila kujali dini, dhehebu, rangi, wala kabila.
- MUULIZE KUHUSU KUAMINI KWAKE NA UHAKIKA WAKE YEYE BINAFSI KUOPNA KWAKE NA HUKUMU YA MUNGU – EPUKA KUMUHUKUMU.
- Nikikuangalia wewe na kwa jinsi ulivyotukaribisah kwa ukarimu na kutusikiliza, wewe ni mtu wa busara na ninaamini uanamwamini Mungu kupitia dini Fulani; je wewe ni Mkristo, muisilamu, ….?
- Na kaka iliyo, sisi wanadamu wote ni wapitaji, je, kama Mungu akikuchukua leo, una uhakika wa kupona na hukumu ile ya mwisho na kufika kwa Mungu?
- ELEZEA JINSI ULIVYOTENEWA WEWE NA BWANA YESU ANAVYOWEZA KUWATENDEA WOTE WAMWAMINIO.
- Pamoja na imani uliyo nayo, ninaomba nikueleze ili kukushirikisha jinsi unavyowesa kupata uhakika wa kupona na hukumu ya Mungu na kufika salama mbinguni, kwani mwanadamu mwenyewe hawezi; maandiko yanasema hivi: katika Warumi 3:23 “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;” na katika Waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; 28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
- Eleza jinsi, lini, na nani alikuongoza kumpokea BWANA Yesu Kristo kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha yako.
- Elezea tofauti ya maisha yako ya wawali na ya sasa baada ya kumpokea BWANA Yesu Kristo jinsi yalivyo kwa kifupi sana na kwa ufanisi.
- Elezea jinsi uweza wake BWANA Yesu Kristo ulvyo halisi kwa kila amwaminiye.
- Msomee maandiko na mpe kipepeperusi(tract) na umuelezee kwa kifupi.
- Usitumie maneno mengi na ya kuchosha, wala usitumie muda mrefu sana kuongea naye.
- MUULIZE
- Analo swali lolote? Labda hajaelewa?
- Ni tatizo gani linalomsumbua katika maisha yake-kiroho au kimwili analohitaji Mungu amfungue? Je/ pombe, madawa ya kulevya, magonjwa sugu, mapepo, umasikini, familia, uchawi, … anahitaji kazi, mtoto, mume, mke…
- MTIE MOYO KWAMBA BWANA YESU ANAWEZA KUMSAIDIA NA KUMPONYA KABISA
- Huku ukimwonyesha maandiko ya ahadi za Mungu kwake katika Biblia na kumfafanulia
- Mwambie achukue biblia yake na afungue kama anayo – maana wengine hudhania tunatumia kitabu kingine abadala ya biblia.
- MPE MUALIKO WA KUMPOKEA BWANA YESU MOYONI MWAKE
- i. Akikubali, muongoze SARA YA TOBA mara moja.
- Asipokubali mwache ulimlazimisha.
- Muachie vipeperushi (kaka unavyo) au maandiko ajisomee zaidi.
- Unapomshuhudia mtu, hakikisha unatoa nafasi yay eye kukata shauri, usimuachie njiani – ni mateso na ni hatari kwake!
- Zinazomzuia kuelewa
- Zinazomfanya asipende kusikiliza au zinazompa usingizi kwa lengo la kukata mawasiliano.
- Zinazomzuia asiamue kuokoka.
- Kama mpo wawili – basi mmoja tu aongee na mwingine aombe kimoyo moyo huku akisikiliza na kuchangia mara chache pale anaposhirikishwa au pale inapobidi.
- Akihitaji maombi, hata kama hajakubali kuokoka unaweza kuitumia nafsi hii kumuongoza sala ya toba kwanza, kasha umuombee.
- Mpe uhakika wa kuokokga kwake
- Mpe maelekezo au muongozo kuhusu mahali pa kwenda kuabudu, ratiba za ibada; na kama atapenda kushiriki kanisa jingine lolote la waliookoka, usimzuie kamwe.
- Chukua maelezo na uandike taarifa kamila ya kuhusu mahali anapoishi, kazi na ratiba ya jinsi ya kuwasiliana naye.
- Mwandikie barua, ikiwa unaona inahitajika akasaidiwe na watumishi wengine walio jirani naye, au kanisa la jirani na anakoishi.
OMBEA NA KUMSHUKURU MUNGU
- Endelea kuomba kwa waliokushirikisha mambo yao ya kuombea.
- Endelea kuombea wote waliokata shauri na hata ambao hawakukata shauri – wale uliokwisha ongea nao tayari.
- Hakikisha usiwe mtu wa kuropoka ovyo yale watu waliyokushirikisha ili uwaombee, TUNZA SIRI ZAO, TUMIA HEKIMA!
- Mshukuru Mungu kwa ajili ya huduma yote.
- Ana ujasiri wa kukiri ya kuwa sasa ameokoka? – omba pamoja naye na kumtia moyo.
- Amepokewa nyumbani kwake au amefukuzwa? Omba pamoja naye na umsaidie.
- Kumchukua ili aje ibadani, kama hafahamu sehemu au ameamua kuja kuabudu pamoja nawe.
- Msaidie ikiwa kipo kiwazo chochote, mfano, mavazi, kazi, nauli, ….
- MAOMBI – mzoeshe kuomba.
- UJAZO WA ROHO MTAKATIFU
- Mfundishe kuhusu Roho Mtakatifu na umuombee ujazo wa Roho Mtakatifu.
- Mzoeshe kuomba katika Roho Mtakatifu.
- KUSOMA NENO
- Soma neon pamoja naye na pia umpe vifungu vya kujisomea au kukariri.
- Mpe nafasi ya kuuliza maswali
- Muulize maswali ya msingi ili kujenga ufahamu wake katika neno la Mungu katika kweli.
- Mfundishe kumtegemea Roho mtakatifu katika kulielewa na kulitafsiri vizuri neno la Mungu.
- Mfundishe Biblia na faida za Wokovu.
- Awe na ujasiri asiogope, maana ameokoka –Marko 16: 16-18.
- Pamoja na michango mbali mbali kanisani na kwa bidii kuwasaidia wahitaji kwa kuutegemea uongozi wa Roho Mtakatifu na kwa ukarimu bila kumpinga Roho Mtakatifu wala uchoyo.
- KAZI NA HUDUMA ZA KIROHO – Sifa, neno, kwaya, vijana, kinamama/kinababa, watoto, mikutano, semina, maombi na maombezi, …
- KAZI ZA MIKONO – usafi, ujenzi, …
- Kutembelea na kushirikiana na kufahamiana na washirika / waamini / wapendwa mbalimbali, kanisani na hata makanisa mengine.
- Msimulie au mpe ushuhuda wa mambo mbali mbali katika maisha yako ya wokovu ambayo Mungu amekutendea.
- Mfundishe kuhusu majaribu na jinsi ya kukabiliana nayo na kuyashinda.
- Msaidie kuyashughulikia majaribu yoyote aliy nayo; kama inawezekana.
- Mtie moyo wa kusonga mbele huku akisimamia ahadi za ushindi katika Neno la Mungu.
- Kushiriki ibada kanisani
- Kufanya ibda nyumbani kifamilia
- Kufanya ibada hata binafsi
- Ili ajipatie kipato, asewe mvivu wala omba omba, bali awe na bidii pamoja na utaratibu ufaao kwa ushuhuda mzuri.
- MAISHA MATAKATIFU – MWENENDO MZURI
- Kutokutenda dhambi
- Maisha yenye utaratibu – kazi / biashara / kusoma.
- Usafi wa mwili na mavazi
- Nidhamu – kielelezo nyumbani pia.
- MAOMBI
- Kwako – ulinzi, hekima, uwepo wa Roho Mtakatifu pamoja nawe, na utayari.
- Unaowaendea –
- Anga / eneo uendalo -
- KUSOMA NA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU
- UJAZO NA KUMSIKILIZA SANA ROHO MTAKATIFU KILA WAKATI
- NI VIZURI KWENDA WAWILI WAWILI AU ZAIDI, NA UKIZINGATIA JINSIA .
Mambo ya kuangalia kuyaepuka katika kushuhudia:
- Epuka nia / dhamiri mbaya – uwe na nia na dhamiri njema sawa na upendo wa Mungu kwa ajili ya watu na uchungu(mzigo) kwa ajili yao wale waendao motoni.
- Epuka ubaguzi – uwiwabague watu kwa kuangalia sura au hali ya mtu, mfano:-
- i. Jinsia ya mtu
- ii. Utajiri au umasikini
- iii. Kabila au rangi
- iv. Dini au dhehebu
- v. Ukali au upole wa mtu
- vi. Uzima au ugonjwa
- vii. Mlevi au asiye mlevi.Usimshambulie, usikosoe, au usiseme dhehebu, au chama cha siasa, au dini ya mtu au mila na desturi – utumie hekima ya Mungu akupayo!
- Chunga muda na mazingira ya ushuhudiaji – ili kulinda ushuhuda wao.
Mazingira kuhusu ustaarabu – uwe radhi katika mazingira yoyote utakayoyakuta kuhusu mahalo pa kukaa, vyakula, kani, …
Mazingira kuhusu muda:-
- Jali matumizi ya muda, usimgande mtu masaa mengi.
- Jali ratiba yake au mudawake wa kazi
- Kama umepewa muda (appointment), angalia sana jinsi uendavyo –muda na mazingira ya mitego ya kukunasa dhambini – UZINZI, ULEVI, KUBAKWA, ….
- NB:Kumbuka ushuhudiaji ni kuwa vitani, na vita siyo lele mama, ama adui ashindwe au wewe ushindwe!
- Maneno unayotumia – yakolee munyu(ladha ya chumvi)!
- Tambua jinsi ya kuongea na mtu wa rika tofauti na lako – mtoto, kijana, mzee, mwanaume, mwanamke, …?
- Mkristo, muisilamu, au dini nyingine?
- Kukosa ujazo wa Roho Mtakatifu
- Kukosa nguvu za Mungu.
- KUKOSA UJASIRI
- Woga / hofu
- Aibu/haya
- Mashaka/kusitasita
- Kukosa moyo wa kujituma mwenyewe
- Kukosa moyo wa Upendo kwa watu wengine
- Ubinafsi
- Uchoyo wa meme / habari njema
- Kushindwa kujitoa uhai kwa ajili yaw engine.
- Kukosa utakatifu (Maisha ya Safi)
- Dhamiri au nia mbaya
- Mwenendo usio mzuri
- KUTOSOMA NENO LA MUNGU
- Kutojaa neno la Kristo moyoni.
- KUTO KULIFAHAMU NENO VIZURI.
- Anza sasa kushuhudia! Usingoje baadae!
- Fanya kazi ya BWANA kama vile BWANA YESU atarudi leo, au kama vile utakufa leo!
UBARIKIWE NA BWANA KWA UTUMISHI MWEMA WA KAZI YA MUNGU.
Maandishi ya rangi hayasomeki kabisa nimeshindwa kusoma
ReplyDelete