Tuesday, August 4, 2015

Je, ni gani sheria hizi Nne za Kiroho?


Swali: "Je, ni gani sheria hizi Nne za Kiroho?"

Jibu:
Sheria hizi Nne za kiroho ni njia za kushiriki habari njema za wokovu upatikanao kupitia imani ndani ya Yesu Kristo. Ni njia moja rahisi ya kupanga habari muhimu katika injili kwa sehemu Nne.

Ya kwanza kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Mungu anakupenda na ana mpango wa ajabu juu ya maisha yako.” Yohana 3:16 yatwambia, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 10:10 yatupa sababu ya kuja kwake Yesu, “Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” Ni kitu gani kinachotuzuia na upendo wa Mungu? Ni kitu gani kinacho tupinga kupata uzima ulio tele?

Ya pili kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Hali ya Utu wa mwanadamu inachafuliwa na dhambi na hivyo basi kutengwa na Mungu. Kwa matokeo haya basi, hatuwezi kamwe kuufahamu mpango wa ajabu alio nao Mungu juu ya maisha yetu.” Warumi 3:23 inatuhakikishia habari hii, “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Warumi 6:23 inatupatia madhara ya dhambi, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.” Mungu alituumba ili tukaweze kuwa na ushirika naye. Hata hivyo hali ya Utu/Ubinadamu ilileta dhambi katika dunia, na hivyo basi kutengwa na Mungu. Tumeharibu uhusiano pamoja naye ambao Mungu alikusudia tukaupate. Je, suluhisho ni nini?

Ya tatu kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Yesu Kristo ndiye toleo la Mungu pekee kwa ondoleo la dhambi zetu. Kupitia kwa Yesu Kristo, tunaweza kusamehewa dhambi zetu na kurudisha ushirika wa haki na Mungu.” Warumi 5:8 yasema, “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” Wakorintho 15:3-4 inatufahamisha kinachotupasa kujua na kuamini ili tupate kuokoka, “……ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko, yakuwa alizikwa; ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko….” Yesu mwenyewe akiri yakwamba yeye ndiye njia ya pekee ya wokovu katika Yohana 14:6, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Je, ninawezaje kupata kipawa hiki kikuu cha wokovu?

Ya Nne kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Ni sharti tuweke imani yetu ndani ya Yesu Kristo kama mwokozi ili tukaweze kupokea kipawa cha wokovu na kujua mpango wa ajabu wa Mungu juu ya maisha yetu. Yohana 1:12 inatuelezea hivi, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. “Matendo16:31 inazungumzia kwa ufasaha zaidi, “Mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka!” Tunaweza kuokolewa kwa neema peke yake, kwa njia ya imani pekee, ndani ya Yesu Kristo pekee (Waefeso 2:8-9).

Ukiwa unataka kumwamini Yesu Kristo kama mwokozi wako, sema maneno yafuatayo kwa Mungu. Kusema maneno haya haitakuokoa, lakini itawezekana kwa kumwamini Kristo!Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kum shukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, ninajua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha- karama ya uzima wa milele! Amina!”

No comments:

Post a Comment