Wednesday, July 1, 2015

Maswali ya Biblia toka Injili ya Mathayo


Maswaliambayo huulizwa mara kwa mara kuhusu Injili ya Mathayo na Injili nyingine yanajadiliwa kwenye Mathayo au vinginevyo kwenye sehemu inayohusu Injili kwa ujumla.

S: Kwenye Mathayo, kuna vitu gani vinavyoitofautisha Injili hii na nyingine?
J: Mathayo anasistiza kuhusu Yesu Mfalme aliyeahidiwa, anayeanzisha ufalme wa Mungu na nu ukamilifu wa sheria. Kristo ni utimilifu wa matumaini. Kati ya waandishi wote wa Injili, Mathayo ndiye anayeonyesha vizuri zaidi jinsi ambavyo unabii wa Agano la Kale unvyotimizwa kwa Kristo. Karibu 1/3 ya Mathayo ni mahubiri, na Injili hii imepangiliwa kwa kufuata hotuba kubwa tano.
Kwa mujibu wa lugha, Papias, mwanafunzi wa mtume Yohana, alisema kuwa Injili ya Mathayo awali iliandikwa Kiebrania/ Kiaramu. Yesu ndiye "aina" ya Israeli, na wengine wanamwona Mathayo kuwa anatumia mbinu za Kimidrashi (njia ya kutafafanua Maandiko iliyotumiwa na Wayahudi wa kale yenye kuelezea mafundhisho ya kidini, kisheria na kimaadili kwa namna inayozidi maelezo halisi ya tukio husika) zilizofahamika n Wayahudi wa wakati wake.
Kuhusiana na dini za uongo, Mathayo 20:1-16 I kifungu kizuri cha kuwaeleza Wamomoni na Mashahidi wa Yehova kuhusu neema. Mathayo 18:21-35 pia inafaa kuwaonyesha Wamomoni kuwa hakuna jinsi tunavyoweza hata kuanza kumlipa Yesu kwa ajili ya neema yake kwa kutumia matendo mema.

S: Kwenye Injili ya Mathayo, inawezekanaje baadhi ya nabii zilioelezwa kwenye kitabu hiki zimuhusu Kristo?
J: Kabla ya kujibu swali, natuangalie orodha ya baadhi ya nabii zinazoongelewa kwenye swali hili.
1. Mungu anawaita wana wa Israel kutoka Misri (Hosea 11:1; Mathayo 2:15)
2. Raheli anawalilia watoto wake pale Rama (Yer 31:15; Mat 2:18)
3. Unabii kuhusu Zabuloni na Naftali (Isaya 9:1, 2; Mat 4:15-16)
4. Zakaria analipwa vipande 30 vya fedha na anavitoa kwa mfinyanzi (Zek 11:12-13; Yer 32:6-9, Mat 27:9-10)
Jibu: Mathayo, zaidi ya Injili nyingine, iliandikwa kwa wasomaji wa Kiyahudi ambao walilifahamu Agano la Kale na njia za Kimdrashi. Papias, mwandishi wa kanisa la awali, aliandika kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwa mara ya kwanza katika lugha ya Kiebrania, sio Kigiriki. Mathayo, akiongelea watoto wanaotoka Misri, Raheli anayeomboleza kwa ajili ya watoto wake, n.k. anafanya kitu fulani kwa makusudi kabisa hapa. Anaonyesha jinsi ambavyo maisha ya Masihi wa Israeli yanavyofanana na maisha ya wana wa Israeli. Tunaweza kuuchukulia unabii kuwa ni maelezo tu ya kina ya utabiri yasiyohusiana na nabii za zamani yaliyotokea kutimia, lakini maoni haya ni finyu sana. Mathayo anaonyesha kuwa maisha ya wana wa Israeli, kwa ujumla, yalikuwa ni utabiri kuhusu Yesu.

S: Kwenye Mathayo 1, kuna umuhimu gani wa orodha ya vizazi vya ukoo wa Yusufu kuishia kwa Daudi kwani Mariamu alikuwa bikira wakati Yesu alipozaliwa?
J: Ingawa Yusufu hakuwa baba mzazi wa Yesu, Yusufu alikuwa baba wa Yesu kisheria. Kwa hiyo ahadi alizopewa Daudi zilitimizwa kwa jinsi zote kisheria kupitia kwa baba/mwana wa kisheria na kiuhalisi kupita ukoo wa Mariamu kwenye Injili ya Luka.

S: Kwenye Mat 1:5, kwa kuwa bibi wa Daudi alikuwa Ruth Mmoabu, Daudi angewezaje kuwemo kenye kusanyiko, kwa sababu Kumb 23:3 inasema Mmoabu hawezi kuingia kwenye kusanyiko hadi kizazi cha kumi?
J: Kwanza nitatoa maelezo ambayo hayana uwezekano wa kuwa jibu, ksha maelezo ambayo ni jibu.
Maelezo ambayo huenda si jibu: Hata kama uwepo wa Daudi kwenye kusanyiko ungekuwa kinyume cha Kumb 23:3, Biblia bado inasema kuwa Daudi alikuwa pamoja na watu na aliabudu pamoja na. Watu walikuwa na uwezo wa kufanya makosa kwa kutokujua. Kwa mfano, Yoshua alifanya makubaliano na Wagibeoni wakati jambo hilo lilikuwa kinyume na sheria ya Mungu. Hta hivyo, mara makubaliano hayo yalipofanyika, Mungu aliwataka Waisraeli wayaheshimu. Naam, Mungu kwa majaliwa yake aliwaruhusu kufanya kosa hili na aliwatumia Wagibeoni baadaye.
Maelezo ambayo ni jibu: Panaweza kuwa na hojo kuwa Daudi hakukiuka Kumb 23:3 hapa.
1. Koo zilitambuliwa kupitia upande wa baba sio mama. Hivyo, inawezekana (lakini hakuna uhakika) kuwa Kumb 23:3 ilitarajiwa kutumika kwa wahenga wa kiume.
2. Ruth "alibadilisha watu." Alimwambia Naomi kuwa watu wako watakuwa watu wangu na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. Ingawa watu leo hii wanaweza kubadilisha uraia ikiwa watu wenyewe na nchi inayoombwa watakubali, jambo hili lilikuwa kubwa zaidi; Mungu alimruhusu (Ruth), kama Rahabu, kuwa miongoni mwa taifa teule la Israeli.

S: Kwenye Mat 1:8, je Yoramu alikuwa ndie baba wa Uzia, au babu wa babu yake kwenye 1 Nya 3:11-12?
J: Kwa kweli yote ni kweli, kwa kuzingatia ufahamu sahihi wa maneno yaliyotumika. Wayahudi walichukulia msemo ‘baba wa’ kama pia ‘mhenga wa’ (kama kwenye Mdo 7:19; 1 Fal 15:24; 22:50; 2 Fal 15:38), kama ambavyo ‘mtoto wa’ ilivyomaanisha pia ‘wa uzao wa.’
Mfalme Yoramu alikuwa ni babu wa babu wa Mfalem Uza.

S: Kwenye Mat 1:9, kwa nini Uzia anaitwa baba wa Yoramu wakati 2 Fal 15:1-7 na 1 Nya 3:12 zinasema kuwa Azaria alikuwa baba wa Yoramu?
J: Uza lilikuwa ni jina linguine la Azaria kama 2 Fal 15:32, 34 na 2 Nya 26:1-23; 27:2; Isa 1:1; 6:1 na 7:1 zinavyosema. Wafalme wengi walikuwa na majina yao binafsi na majina ya kifalme waliyoyapata baadaye. Lakini kwa watu wote, wafalme na wasio wafalme, jambo hili lingeweza kudhaniwa kuwa si kawaida kwa: Abram/Abraham, Sarai/Sara, Yakobo/Israeli, Ben-Oni/Benjamin, Zafenathi-Panea/Yusuf, Hoshea/Yoshua, Gideoni/Jerubaali, Ammieli/Eliam, Bathsheba/Bath-shua, Azaria/Uzia, Abijam/Abija, Yehoahaz mwana wa Yosia/Shalum, Eliakim/Yehoiakim, Yehoiakin/Yekonia/Konia, Zedekia/Matania, Hanania/Shadraki, Mishaeli/Meshaki, Azaria/Abednego, Danieli/Belteshaza, Simon/Petro, Yusufu/Barnabas, na Saulo/Paulo.

S: Kwenye Mat 1:11, 16, kwa nini orodha ya vizazi inaonyesha kuwa Yesu alitokea kwenye ukoo uliolaaniwa wa Yekonia/Yehoiakin, kama Yer 22:28-30 na 36:30 zinavyosema? (Tazama pia 1 Nya 3:16). Yekonia (Yehoyakin) na baba yake Yehoyakimu wote walilaaniwa na Mungu mwenyewe, aliyesema kuwa hakuna mtu yeyote kati yao ambaye mzao wake atakalia kiti cha enzi cha Daudi. Iliwezekanaje Yesu kuwa Masihi, aliyepangiwa kutawala milele kwenye kiti cha enzi cha Daudi, ikiwa alitokana na yeyote kati ya watu hawa wawili?
J: Orodha ya vizazi ya Mathayo haionyeshi kuwa Yusufu alitokea kwenye uzao uliolaaniwa. Jambo hili lingekuwa shida kubwa endapo Yusufu angekuwa baba halisi wa Yesu kwa sababu Yeremia alitabiri kuwa Yehoyakin hatakuwa na mzao wake yeyote atakayeketi kwenye kiti cha enzi. Hata hivyo, orodha ya uzao ya Mariamu kwenye Luka inaonyesha kuwa Yesus hakutoka kwenye ukoo wa Yekonia na Yehoyakimu, kwa sababu wazazi wa Mariamu walifuata njia tofauti na ukoo wa kifalme. Tukitazama nyuma tunaweza kuona kuwa Daudi na Suleiman walipewa ahadi tofauti kidogo. Yusufu tu ndiye aliyetokana na Suleiman, na wote Yusufu na Mariamu walitoka kwenye ukoo wa Dauid.
Katika historia, Irenaeus, askofu wa Lyons huko Gaul, alijibu hili pingamizi la Yusufu kuwemo kwenye orodha ya vizazi kwenye Injili ya Mathayo kwenye Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 21.9, uk.453-454, kilichoandikwa miaka ya 182-188 BK.

S: Kwenye Mat 1:17, ni kweli kuwa kulikuwa na vizazi 3 x 14 = 42, au vizazi 41 tu?
J: Kuna seti tatu za majina 14, lakini hazijatokana na kujumlisha vizazi kwa pamoja, kwani setiya kwanza ni kutoka Abraham hadi na kumhusisha Daudi, na seti ya pili ni Daudi hadi uhamisho wa Babeli. Tungeweza kuwa na shida endapo Mathayo angekuwa amesema kuwa kulikuwa na vizazi 42, lakini Mathayo hakusema kuwa jumla ya vizazi vyote ni 42.Mathayo anaelekea kuwa alizisema kwa ufupi hizi seti tatu za majina 14 kama njia mojawapo ya kuzikumbuka.

S: Kwenye Mat 1:1-17 na Luka 1, kwa nini orodha za majina zinaachana baada ya Suleiman, lakini zinakuja tena pamoja kwa Shealtieli?
J: Mat 1:12 inasema Yehonia (Yehoyakini), Shealtieli, na Zerubabeli, wakati ambapo Luka anasema Neri, Shealtieli, na Zerubabeli. Sababu ya moja kwa moja ya tofauti ilitolewa kwenye 1 Nya 3:17-19. Uzao wa kifalme, ambao karibu wakati wote ulipita kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto wa kiume, ulipita, badala yake, kutoka kwa Shealtiel kwenda kwa Zerubbabeli, mtoto wa Pedaya, kaka yake Shealtiel..
Sababu ya kuwa hivyo haitolewi, lakini inaweza kuwa Shealtiel hakuwa na mtoto yeyote, au angalau watotowaliokuwa hai wakati alipokufa. Hivyo, Shealtieli huenda alimuasili mtoto wa kaka yake (yaani alimfanya kuwa mtoto wake). Wanazuoni wanafikiri kuwa ama Pedaya alikufa na Shealtieli alimuasili Zerubabeli akiwa yatima, au vinginevyo Shealtieli alimpa Zerubabeli haki ya uzao wa kifalme kwa sababu tu hakuwa na watoto.

S: Kwenye Mat 1:18-19, kwa nini Yusufu alikusudia kumwacha Mariamu ikiwa walikuwa bado kuoana?
J: Mila zao zilikuwa tofauti na zetu. Mwanaume na mwanamke waliunganishwa pamoja wakati wanapopeana miadi ya kuoana (uchumba), ingawa hawakuruhusiwa kuhusiana kimwlili hadi baada ya harusi. Yusufu alikuwa anapanga kuuvunja uchunba wao rasmi.

S: Kwenye Mat 1:18, je Mariamu alikuwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, au Yesu alikuwa uzao wa viuno vya Daudi kwa mujibu wa Mdo 2:30?
J: Mariamu alikuwa bikira; Biblia inasema Roho Mtakatifu "alimfunika" Mariamu, si kwa jinsi ya kuhusiana kimwili. Yusufu alikuwa baba pekee wa kisheria aliyemuasili Yesu, hakuwa baba halisi. Lakini Yesus alikuwa mzao halisi wa ukoo wa Daudi kupitia Mariamu, kama orodha ya vizazi yenye kupitia kwa Mariamu ya Lk 3:23-37 inavyoonyesha. Aya nyingine zenye kusema kuwa Yesu ni mtoto (mzao wa ukoo) wa Daudi ni Mat 12:23; 15:22; 20:30; 21:9,15; Marko 10:47-48; 12:35; Luka 10:41; 18:38-39; Yoh 7:42; 2 Tim 2:8; Ufu 5:5; 22:16.

S: Kwenye Mat 1:20; 2:12; 2:13; 2:19; 2:22; 27:19, kwa nini Mathayo anataja ndoto na waandishi wengine wa Injili hawafanyi hivyo?
J: Mathayo anataja ndoto nne au tano tu:
Ndoto tatu au nne wakati wa utoto wa Yesu: Mat 1:20 (usihofu kumchukua Mariamu mkeo); 2:12 (wasimrudie Herode); 2:13 (ukimbilie Misri); 2:19 (ushike njia kwenda nchi ya Israeli); 2:22 (aliogopa kwenda huko [Uyahudi]). Mat 2:22 inaweza kuwa ni ndoto tofauti, au ndoto ileile ya Mat 2:19.
Wakati wa Yesu kushtakiwa, mke wa Pilato Mat 27:19.
Marko na Yohana hawaongelei miaka ya utoto wa Yesu, kwa hiyo hawatarajiwi kuandika kuhusu ndoto hizi. Kwa kuwa Luka haongelei kitu chochote kuhusu Mamajusi na (karibu) kitu chochote kuhusu Yusufu, hatarajiwi kuandika kuhusu ndoto hizi.
Mambo haya yanalibakiza tukio la Mathayo (linalomhusu mke wa Pilato) kuwa taarifa ambayo haijaandikwa kwenye Injili nyingine.
Hata hivyo, kwa kutumia ukweli huu, huwezi kusema kuwa waandishi wengine wa Injili walipinga kuandika kuhusu ndoto. Kwenye Mdo 16:9, usiku Paulo aliota ndoto ambapo mtu kutoka Makedonia alimwomba aende na kuwasaidia.

S: Je Mat 1:23 inatafsiri Isa 7:14 kimakosa kwa kutumia jina "bikira?"
J: Hapana. Si tu kwamba neno la Kiebrania lililotumiwa hapa linamaanisha amaa "bikira" ama "msichana", lakini pia Asimov mwenyewe kwenye uk. 780 anatambua kuwa tafsri ya Kigiriki ya Agano la Kale (Septuagint) imelitafsiri neno hili kuwa parthenos, yaani bikira. Ni kweli, Asimov haamini kuwa miujiza ya kwenye Biblia ni ya kweli, kwa hiyo hangeweza kuamini kuwa Isaya alikuwa akimwongelea bikira.

S: Kwenye Mat 1:23, kwa nini kua vizazi 27 kutoka Daudi hadi Yesu, wakati Lk 1:3:23-31 ina vizazi 42?
J: Ingawa inawezekana kusiwe na namba zenye kufanana za vizazi kwenye orodha za vizazi za Yusufu na Mariamu, Mathayo ana mapengo kadhaa bila shaka yoyote. Kwa kuwa "mwana wa" inaweza kumaanisha mzao wa kiume, hakuna shida hapa. Yekonia (Yehoyakini) alitawala karibu mwaka 604 KK, kwa hiyo kuna vizazi 14 kutoka Daudi hadi Yekonia katika kipindi cha karibu miaka 400, au miaka 29 kwa kizazi. Kutoka mwaka 604 KK hadi 4 KK inatarajiwa kuwepo vizazi 20 1/2 , na Mathayo anataarifu vizazi 13, au miaka 46 kwa kizazi.
Huenda Mathayo hakuvitaja vizazi zaidi ya 14 baada ya uhamisho wa Babeli kwa sababu hakuyajua majina mengine, na yeye aliandika mambo yale tu aliyoyajua. Vinginevyo alkuwa anatumia seti tatu za majina kumi na nne kam kitu cha kusaidia kukumbuka.
Haiwezi kuwa bahati tu kwamba tarakimu za herufi za Kimasoretiki za jina ‘Daudi’ (dwd) zikijumlishwa huwa 4 + 6 + 4 = 14.

S: Kwenye Mat 1:23 na Lk 1:26-35, inawezekanaje Yesu aliyezaliwa na bikra awe mzao wa ukoo wa Daudi?
J: Mambo matatu ya kuzingatia kwenye jibu la swali hili.
1. Yesu hakuwa mtoto halisi wa Yusufu. Kama angekuwa, Yer 29:32 ingekuwa ni unabii wa uongo.
2. Yesu alikuwa mtoto wa Yusufu kisheria. Leo hii, mwanaume anayemuoa mwanamke aliye na mtoto anakuwa baba wa mtoto huyo kisheria, ingawa si baba halisi.
3. Yesu alikuwa mtoto halisi wa Mariamu.
Yesu alikuwa wa ukoo wa Daudi kisheria kupitia Yusufu, na Yesu alikwa wa ukoo wa Daudi kuuhalisi kupitia Mariamu.

S: Kwenye Mat 1:25, je Mariamu alikuwa na watoto wengine wowte?
J: Mstari huu hautakuwa na maana yeyote na wenye kupotosha kama Yusufu na Mariamu hawakuwa wamewahi kuwa na uhusiano wa kimwili.
Zaidi ya hapo, Mat 13:55-56; Mak 6:4; Gal 1:19; na Yuda 1 pia zimerekodi kuwa Yesu alikuwa na wadogo wake wa kiume (ndugu). Eusebius, katika kitabu chake kiitwacho Ecclesiastical History (karibu mwaka 360 BK) 2:23 na d 3:20 pia anase,a kuwa wadogo wane wa kiume wa Yesu walikuwa Yakobo aliyeitwa mwenye haki), Yose (au Yusufu), Yuda na Simoni.
Moja ya majibu yatolewayo na kanisa Katoliki ni kuwa Yusufu alikuwa na watoto kupitia ndoa yake ya awali, lakini si kupitia kwa Mariamu. Hata hivyo, hakuna ushahidi toka kwenye historia ya kanisa kuwa Yusufu aliwahi kuwa na ndoa nyingine kabla ya ile na Mariamu, au mdogo wake yoyote wa kiume hakutokana na Yusufu na Mariamu.
Jibu lingine la kanisa Katoliki ni kuwa kwenye jamii za Kimediteranian neno "ndugu" linaweza kumaanisha binamu na ndugu/jamaa wa karibu wenye unri unaofanana, na sit tu kaka au wadogo wa mtu. Hata hivyo, kutumia jambo ambalo linaweza kuwa kweli kwa Wataliano wa miaka ya baadaye na watu wengine zaidi y Waisraeli ni tatizo.
Moja ya watu wa kale zaidi waliohubiri makosa ya kuwa Mariamu hakuwa na watoto wengine alikuwa Ambrose wa Milan (mwaka 340-397 BK) (Letter 63:110-111, uk.473). Hata hivyo, Ambrose alikuwa wazi kuwa Yesu hakuhitaji msaada wowote ili aweze kuwaunganisha watu na Mungu, na Mariamu hakupaswa kusujudiwa (On the Holy Spirit kitabu cha 3 sura ya 11 na.80 mwaka 381 BK). Alisema, "Na mtu yeyote asihamishie jambo hili kwa Bikira Mariamu; Mariamu alikuwa hekalu la Mungu. Na kwa hiyo Yeye (Mungu) pekee ndiye anayepaswa kuaudiwa Yeye afanyaye kazi katika hekalu lake (mwenyewe)."

S: Kwenye Mat 2:1-4,9-12, kulikuwa na mamajusi wangapi hasa?
J: Maandiko hayasemi kitu chochote kuhusiana na jambo hili. Watu mara nyingi hufikiri ni watatu to kwa sababu ya wimbo "We Three Kings of Orient Are (Sisi Wafalme Watatu wa Mashariki)", na kulikuwa na zawadi tatu, lakini idadi yoyote ya mamajusi inawekana.

S: Kwenye Mat 2:6, kwa nini maandishi ya Kimasoretiki (Kiebrania) ya Agano la Kale yanasema "mdogo" kwa kuwa Mik 5:2 inasema "mdogo" kwenye maandishi ya Kimasoretiki na "mdogo sana" kwenye taafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale?
J: Mambo matatu ya kuyazingatia katika jibu la swali hili.
1) Mik 5:2 inasema, "Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli . . ." Jambo kuu hapa ni kuwa ingawa Bethlehemu alikuwa mdogo kwa kipimo eneo, atakuja kuwa mkubwa kwa umuhimu.
2) Jambo hili lilizungumziwa na makuhani na waalimu wa sheria. Huenda walifanya makosa au walinukuu kwa Herode tafsiri ya Kigiriki mbali ya Septuagint. Lakini jambo ambalo lina uwezekano mkubwa zaidi ni kuwa walikuwa wanatafsiri kutoka Kiebrania kwenda Kiaramu au Kigiriki kwa kuzungumza walipokuwa wanatembea.
3) Hata hivyo, makuhani na waalimu wa sheria hawakuwa wanafanya makosa wakati wanawasilisha maana: mji mdogo wa Bethlehemu HAUKUWA na umuhimu mdogo zaidi ya miji mingine yote kwa sababu mtawala atakakuja kutoka humo.

S: Kwenye Mat 2:6, kwa nini inasema "mtawala", wakati Mik 5:2 inasema "maelfu" kwenye maandiko ya Kimasoretiki na Septuagint?
J: Mambo manne ya kuzingatia katika jibu la swali hili.
1) Mik 5:2 inasema, "Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli . . ." Jambo la muhimu hapa ni kuwa Bethlehemu ulikuwa mji mdogo kwa eneo, utakuja kuwa na umuhimu mkubwa.
2) Neno la Kiebrania lenye kumaanisha "maelfu" (uwingi) kwenye Mik 5:2 ni ‘alapim. Neno la Kigiriki lenye maana hiyohiyo ni chiliasin. Neno la Kiebrania lenye kumaanisha watawala (uwingi) ni ‘allupe. Neno linalofanana na hilo kwa Kigiriki ni hegemosin. Ingawa maneno ya Kigiriki ni tofauti kabisa, maneno Kiebrania karibu ni sawa kabisa isipokuwa voweli zake. Mwanzoni kabisa, Agano la Kale liliandikwa bila voweli; voweli ziliongezwa karibu mwaka 700 BK. Jambo hili linaonyesha kuwa hawakuwa wanasoma kwenye Septuagint iliyoandikwa kwa Kigiriki, lakini ama Kiebrania, Kiaramu, au pengine tafsiri nyingine ya Kigiriki.
3) Jambo hili lilisemwa na makuhani na waalimu wa sheria. Huenda walifanya makosa, au walimnukulia Herode tafsiri ya Kigiriki mbali ya Septuagint. Lakini lenye uwezekano mkubwa zaidi ni kuwa walikuwa wanatfsiri kwa kuongea (si kwa maandishi) kutoka Kiebrania au Kigiriki kwenda Kiaramu au Kigiriki walipokuwa wanaendelea na safari.
4) Hata hivyo, makuhani na waalimu wa sheria hawakufanya makosa katika kuwasilisha maana: mji mdogo wa Bethlehemu HAUKUWA na umuhimu mdogo zaidi ya miji mingine yote kwa sababu ya mtawala atakayekuja kutoka humo.

S: Kwenye Mat 2:1-4, 9-12, je mamajusi walikuwa ni watu gani?
J: Mamajusi walikuwa ni wafuasi wa dini za Mashariki ya Kati waliokuwa wakijishugulisha na unajimu. Ingawa Biblia haisemi kwa wazi kabisa kuwa walikuwa mamajusi watatu, kuna maoni matatu kuhusu nani walikuwa "mamajusi wa Krismas."
Awali, kama Walawi walivyokuwa kabila la kikuhani la Waisraeli, mamajusi wa baadaye walikuwa ni kabila la kihuhani la Wamidiani kwa mujibu wa Herodotus. Jambo hili linafanana na Walawi kuwa kabila la kikuhani miongoni mwa Waisraeli. Mamajusi walikuwa wanatoa dhabihu kwenye moto, wanatafsiri ndoto, na walifanya unajimu. Ingawa neno la Kiingereza "magician" (mfanya mazingaombwe/mchawi) linatokana na jina "Magi" (mamajusi), ukiachia kifungu kwenye Herodotus, hakuna ushahidi kuwa mamajusi walifanya mazingaombwe/uchawi. Wamidiani walikuwa wanaamini miungu mingi (siyo Uzoroastrian). Wakati Dan 5:11 inamwongelea mamajusi, inamaanisha mamajusi hawa.
Baadaye, wakati mmajusi mmoja aliyeitwa "Bardiya wa uongo" alipoitwaa utawala wa Uajemi kwa muda wa miezi saba mwaka 522 KK, Mfalme Cambyses aliwaweka mamajusi wa Kiajemi mahala pa mamajusi wa Kimedi. Mamajusi wa Kiajemi walikuwa ni Wazoroastria. Wazoroastria waliamini kuwa kuna mungu wapinganao wenye uwezo sawa, mmoja ni mwema anayewakilishwa na mwanga na mwingine ni mwovu anayewakilishwa na giza. Kwenye karne ya nne Kabla ya Kristo (4 KK) na baada ya hapo, Wazoroastria waliamini kuwa kuna kufufuliwa. Kwa ujumla, Wagiriki waliwaona mamajusi kuwa Wazoroastria. Clement wa Alexandria aliamini kuwa mamaajusi walioenda Bethlehemu walikuwa Wazoroastria.
Wakati wa Kristo, Wagiriki pia waliwaita Wakaldayo waliofanya unajimu ‘mamajusi.’ Wanajimu wengi walisafiri kuelekea upande wa magharibi kufundisha watu mbalimbali ikiwamo Waberosu wa Kibabeli, waliofundisha kwenye kisiwa cha Cos baada ya mwaka 281 KK. Tacitus anasema mamajusi walifanya uchawi, na Pliny anadai kuwa mazingaombwe/uchawi ulianzishwa na Zoroaster. Origen, mwandishi wa kanisa la mwanzo, alimkosoa mzushi Celsus katika vitu vingi ikiwemo kushindwa kwake kutofautisha kati ya mamajusi na Wakaldayo kwenye Origen Against Celsus kitabu cha 1 sura ya 58, uk.422.
Bila kujali maana halisi ya asili ya Mashariki ya Kati ya "mamajusi wa Krismas", mamajusi walifanya unajimu.

S: Kwenye Mat 2:8, 12, je Mungu aliwaamuru mamajusi kutokutimiza ahadi yao kwa Herode, kwa kuwa waliambiwa kutokurudi kwa Herode?
J: Mambo matatu ya kuzingatia kwenye jibu la swali hili.
1. Mathayo 2 inasema kuwa mamajusi walimuahidi Herode kuwa watarusi kwake.
2. Mathayo 2 inasema mamajusi walimwambia Herode kuwa wanakusudia kurudi. Hata kama walifanya hivyo, baada ya ndoto, makusudio yao yalibadilika.
3. Hata kama walikuwa wamemuahidi Herode, ahadi haingekuwa na ulazima wa kuitimiza kama:
3a) Ilitolewa kwenye mazingira ya uongo
3b) Ilipingana na mapenzi ya Mungu
3c) Kutimizwa kwake kungesababisha mauti kwa mtu asuyekuwa na hatia
Kwa mfano, kama mtu atakuambia kuwa umwite baada ya mwanamke fulani kuondoka nyumbani kwake kwa sababu anataka kumwekea maua kwenye mlango wa nyumba yake, na umeahidi kufanya hivyo. Baadaye umetambua kuwa mtu yule amewahi kupora nyumba kadhaa na anakusudia kupora nyumba ya huyo mwanamke. Utakapomwona mwanamke huyo anaondoka, utapaswa kumwita huyo mporaji kwa sababu hivyo ndivyo ulivyoahidi? Hapana!

S: Kwenye Mat 2:11, kwa kuwa unajimu ni mbaya, kwa nini mamajusi waliifuata nyota?
J: Kwanza natujifunze kuhusu mamajusi, kisha tuone jambo hili linasema nini kuhusu Mungu.
Mamajusi walikuwa kabila la kikuhani la Wamidiani, kwa kiasi fulani kama makuhani wa Waiisraeli walivyotoka kwenye kabila la Lawi. Walifahamika kuwa wanafanya unajimu.
Unajimu ni kinyume cha Biblia: Kuna uwezekano mkubwa kuwa mamajusi hawakujua kuwa Agano la Kale linasema kuwa unajimu ni kitu kibaya (Law 19:26; 22:27; Kum 18:11-14; 2 Fal 17:16; 21:3, 5; 2 Nya 33:3-6). Kwa upande mwingine, nyota haikutabiri kuja kwa Yesu bali ilikutangaza.
Hivi ndivyo Tertullian (mwaka 198-220 BK), mwandishi kwenye kanisa la awali alivyoandika kuhusu unajimu kwenye On Idolatry sura ya 9 (juzuu ya 3), uk.66. "Hufahamu kitu, mnajimu, kama hujui kuwa unapaswa kuwa Mkristo. Kama ulijua, ulipaswa kujua jambo hili pia, kwamba hupaswi kujihusisha tena na kazi yako hiyo ambayo, yenyewe, inaongelea vipindi muhimu vya maisha ya kazi nyingine, na inaweza kukuelimisha kuhusu hatari zake yenyewe. Hakuna sehemu wala nafasi yako kwenye mfumo wako. Hawezi kutegemea ufalme wa mbinguni mtu ambaye kidole au kifimbo chake cha kuchezea mazingaombwe kinazikufuru mbingu."
Mungu hajawahi kusema kuwa atatumia njia nzuri tu kuleata watu kwake. Mara nyingine Mungu hutumia njia ambazo ni ovu kabisa, kama vile jeshi la Wababeli (Hab 1:6,13). Mungu anaweza kutumia ugonjwa, watu waovu, na hata dhambi isiyokusudiwa (kama mamajusi) kuwaleta watu kwake.
Kitu cha kushangaza zaidi, ni kwamba Mungu amewahi kutumia dhambi za makusudi za waamini ili kuwakomboa waamini wengine. Unaweza kusoma jambo hili kwenye habari ya Yusufu na kaka zake katika kitabu cha Mwanzo 37 na 50, na hasa Mwa 50:20. Ukweli ni kwamba Mungu anaweza kutenda mambo yote kwa kusudi jema (Rum 8:28) na kwa mapenzi yake (Efe 1:11).
Hitimisho, kama Mungu alivyotumia kutekwa kwa Yusufu kwa makusudi yake, kitendo cha Mungu kutumia unajimu kwa makusudi yake hakiuhalalishi unajimu.

S: Kwenye Mat 2:15 na Hos 11:1, ni vipi "Kutoka Misri nalimwita mwanangu" uwe ni unabii kuhusu Kristo?
J: Hos 11:1 ilitumiwa kwanza na Waisraeli. Mathayo hatumii Hos 11:1 tu bali pia aya nyingine za Agano la Kale kuonyesha kuwa maisha ya Kristo yalikuwa sambamba na yale ya Waisraeli (isipokuwa maisha yake hayakuwa na dhambi.) Mathayo anawaandikia Wayahudi ambao wanalifahamu sana Agano la Kale, na anaonyesha kutumia njia ambayo wanazuoni wa Kiyahudi wa wakati ule wangeitambua kuwa ni Midrashi (yaani njia ya kutafafanua Maandiko iliyotumiwa na yenye kuelezea mafundhisho ya kidini, kisheria na kimaadili kwa namna inayozidi maelezo halisi ya tukio husika). Ufafanuzi wa Kiyahudi wa Kimidrashi hutafuta kwa juhudi na bila kukoma maana na matumizi yaliyo nyuma ya kila neno.

S: Kwenye Mat 2:16, je kuna tukio linguine lolote la Mfalme Herode Mkubwa kuwachinja watoto Bethlehemu?
J: Kuna mambo mengi ambayo tusingeweza kujua kuwa yametokea, au jinsi yalivyotokea, isipokuwa kupitia rekodi ya moja ya kihistoria. Kwa mfano, hatuna rekodi ya Warumi kuitwaa Gaul – isipokuwa kupitia chanzo kimoja, maandiko ya Julius Kaisari. Katika suala hili, mbali ya Biblia, waandishi wengine wanaoelezea Herode kuchinja watoto wadogo kabla ya Nicea ni:
Justin Martyr kwenye Dialogue with Trypho sura ya 78, uk.238 (karibu mwaka 138-165 BK) inaongelea kuhusu mamajusi kutembelea Herode, na Herode kuua watoto wote Bethlehemu.
Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 16.4, uk.442 (mwaka 182-188 BK) anasema kuwa [Mungu] "aliwaondoa watoto wa nyumba ya Daudi, ambao bahati yao njema ilikuwa kumezaliwa wakati ule, aweze kuwatuma kabla kwenye ufakme wake"
Origen (mwaka 225-254 BK) anasema kuwa aliwaua Herode watoto wote wachanga wa Bethlehemu na maeneo ya jirani akitumaini kumuua Mfalme wa Wayahudi. Against Celsus kitabu cha 1 sura ya 61, uk.423.
Cyprian wa Carthage (mwaka 246-258 BK) (alidokeza, hakumtaja Herode) anasema kuwa wakati wa kuzaliwa kwa Kristo watoto wachanga wenye umri usiozidi miaka miwili waliuawa mahali pa Kristo. Letter 55 sura ya 6, uk.349.
Archelaus (mwaka 262-278 BK) anasema kuwa wakati wa Yesu Herode alimuua "kilamtoto [mchanga] mwanaume miongoni mwa Wayahudi." The Disputation with Manes sura ya 44, uk.220.
Petro wa Alexandria (mwaka 306, 285-311 BK) anawaelezea watoto wachanga ambao Herode aliwachinja kwa sababu ya Kristo. Canonical Epistle Orodha ya 13, uk.277.
S: Kwenye Mat 2:16, licha ya kuwaua watoto Bethlehemu, je Herode alikuwa katiri kwa mtu mwingine yeyoye?
J: Ndiyo. Baadhi ya watu walidhani ni vigumu kuamini kuwa ni kweli mauaji ya Herode yalitokea. Hata hivyo, kama karne ya 20 inayodaiwa kuwa ya kistaarabu zaidi imewashuhudia Pol Pot wa Cambodia, Idi Amin wa Uganda, Hitler, Stalin, na Mao Tze-Tung, je si vigumu kuamini kuwa Herode alifanya hivi.
Angalia swali lililopita kuona waandishi sita wa miaka kabla ya baraza la Nikea ambao waliandiaka kuhusu Herode kuchinja watoto wachanga. Angalizo, usiwachanganye Herode (Mkuu) ambaye aliyekuwa anatawala wakati Yesu anazaliwa na Herode (Antipa) ambaye Yesu aliongea naya kabla ya kusulubiwa kwake.
Tabia ya Herode (Mkuu) ilikuwa kwamba aliwaua watu wengi katika miaka 36 ya utawala wake. Herode aliwanyonga au aliamuru kuuliwa kwa mke wake aliyeitwa Mariamne, na waume wawili wa dada yake aliyeitwa Salome. Herode aliamuru shemeji yake azamishwe kwenye mto Yordani, na mama mkwe wake aliyeitwa Alexandra auawe. Alimwua Hyrcanus, mtawala wa mwisho wa Wahasmonia. Aliwaua mafarisayo wengi na familia nyingi za watu mashuhuri. Rabi Jehuda Saripha ben na Mattathias ben Margoloth waliteketezwa kwa moto wakiwa hai. Herode aliamuru watoto wake mwenyewe Alexander na Aristobulo kuuawa. Kwa kuwa Herode, kama Wayahudi walio wengi, hawakuwa anakula nyama ya nguruwe, jambo hili lilimsababisha Mfalme wa Rumi kutania kuwa angependa kuwa nguruwe wa Herode kuliko kuwa mtoto wake wa kiume. Siku tano kabla ya kifo cha Herode, aliamuru mtoto wake Antipater auawe. (Watoto wake wadogo watatu wa kiume, Archelaus, Herode Antipa, na Filipo, walinusurika). Hakuna shaka kwamba Herode alikosa uadilifu hata kuua watoto wachanga, na kulingana na "taarifa" nyingi za mambo ambayo Herode alikuwa anafanya, kuua watoto wachanga katika mji mdogo kulishindwa kuonekana kuwa habari muhimu.
Baada ya Herode kufa mwaka 4 KK, kulikuwa na uasi, na Archelaus ilituma majeshi Yerusalemu na kuua watu 3000 katika siku moja. Wakati Herode Antipa Archelaus ameenda Rumi, Sabinus, wakala wa hazina ya kifalme alikuja kufanya ukaguzi wa kodi. Alichukua talanta 400 toka kwenye hazina ya hekalu. Kulikuwa na uasi mwaka 9 BK, na majeshi ya Siria yakiongozwa na Qunitilius Varus yaliuzimisha.
Kulikuwa na kupatwa kwa mwezi Herode (Mkuu) alipokufa, jambo ambalo linaonyesha kuwa kifo kilitokea March 12/13, 4 KK.

S: Kwenye Mat 2:16, je wafalme wengine walikuwa wabaya kama Herode?
J: Wako waliokuwa bora kuliko wengine, lakini wengine walikuwa wabaya sana. Kwa mfano, Mfalme Phraates IV wa Wapartian alimuua baba yake Orodes II mwaka 37 KK. Warumi walimtumia mjakazi wa Kitaliano aliyeitwa Musa. Phraates alizaa naye mtoto wa kiume, Phraataces (= Phraates V). Musa alimuua Phraates IV kwa sumu mwaka 2 KK. Kisha akaolewa na mtoto wake mwenyewe wa kiume mwaka 2 BK. Phraataces V alipelekwa uhamishoni mwaka 4 BK.

S: Kwenye Mat 2:18, je unabii wa Yeremia kuhusu Raheli ulitimizwa kupitia Yesu?
J: Kwenye Mwa 35:16-19, Raheli alikufa wakati alipokuwa anajifungua Benjamini. Wakati Yeremia alipokuwa anaandika maneno haya kuhusu Rachel mke wa Yakobo, Raheli alikuwa tayari amekufa zaidi ya miaka 1000 iliyokuwa imepita. Maneno haya ya Yeremia hayana maana mbili bali moja tu na utimilifu wake wa namna mbili nay a tatu ni ile inayorudi nyuma kwenye kitabu cha Mwanzo. Maana ya Yeremia ni kwamba kama Raheli alivyokuwa na kwa ajili ya kifo na utumwa ya wazao wake, iwe kwa mkono wa Wamisri au Wababeli, Raheli atakuwa na huzuni kwa ajili ya kifo cha mtoto wake kwa mkono wa Herode. Katika kipindi cha Yeremia, nabii alirudia maneno haya akitabiri hisia zilezile za huzuni itakayotokana na kutokuwepo kwa Wayahudi wataopelekwa uhamishoni Babeli, karibu na kaburi la Raheli.
Vivyo hivyo, Mathayo anatumia maneno hayohayo kuonyesha hasara itakayotokana na vifo vya watoto wa kiume wa Bethlehemu, ambayo ilikuwa karibu na kaburi la Raheli.
Kama mtu mwenye kushuku atakuwa na tatizo na Mathayo kutumia maneno ya Yeremia, ataweza kuwa na tatizo la jinsi hiyohiyo na Yeremia kutumia maneno ya kitabu cha Mwanzo. Kiini cha tatizo ni hiki: kama Wayahudi wa wakati wa Yeremia waliielewa maana kwa kusema kuwa uhamisho utahusiana na huzuni ya Raheli kwenye Mwanzo, Wayahudi wa wakati wa Yesu waliielewa tafsiri hii ya Kimidrashi ambayo Mathayo aliitumia.

S: Kwenye Mat 2:22, kwa kuwa watoto wa kiume wa Herode (Mkuu) walitawala Uyahudi na Galilaya, kwa nini Yusufu aliamua kwenda Galilaya badala ya Uyahudi?
J: Mawazo mawili ya kwanza.
1. Archelaus, ambaye alikuwa mfalme wa Uyahudi, kuanzia mwaka 4 KK, anawezakuwa alisikia kuhusu Yesu, mfalme aliyekuwa mtoto mchanga na alipenda kumwua pia. Herode Antipa, aliyekuwa gavana wa jimbo la Galilaya, anaweza kuwa alikuwa na mawazo tofauti.
2. Asimov anasema kuwa Archelaus alikuwa adui mkubwa sana kiasi kwamba Wayahudi na Wasamaria, waliokuwa maadui, waliungana Rumi imwondoe Archelaus. Baada ya kifo cha Herode, Archelaus alitawala kwa miaka 10 tu. Kwa upande mwingine, Herode Antipa alitawala Galilaya kwa amani kwa zaidi ya miaka 40.
Hatahivyo, kuna sababu iliyo dhahiri zaidi kwenye Lk 2:39. Yusufu alitokea Nazareti, si Bethlehemu. Si tu kwamba Yusufu alikuwa anakwenda kwenye nchi yenye mtawala mpole, lakini pia alikuwa anarudi sehemu aliyokuwa anatoka.

S: Kwenye Mat 2:23, kwa kuzingatia elimukale, je ni kweli kwamba hakuna uthibitisho wa kuwepo kwa mji wa Nazareti, kama wati wasioamin kuwepo kwa Mungu wanavyosema?
J: Hapana. Talmud imeitaja miji mingine 63 ya Galilaya (lakini si Nazareti), na Josephus ametaja miji mingine 45 huko Galilaya (lakini si Nazareti). Nazareti inatajwa mwanzoni mwa karne ya 4 BK, na kwenye maandiko ya Kiyahudi yaliyoandikwa kuanzia karibu karne ya 7 BK.
Hata hivyo, baada ya kuangamizwa kwa Yerusalemu mwaka 70 BK, mtaalamu wa elimukale alipata orodha ya Kiarami ya makuhani waliohamishwa, na mmoja wao aliorodheshwa kuhamia Nazareti. Makaburi ya karne ya kwanza yamegunduliwa nje kidogo ya Nazareti. Mwisho, mabaki yatokayo kipindi kabla ya Ukristo yamepatikana mwaka 1955 chini ya kanisa la Annuciation la Nazareti ya sasa.

S: Kwenye Mat 2:23, kwa mujibu wa wataalamu wa elimukale, Nazareti ilikuwa na ukubwa gani?
J: Nazareti ulikuwa mji usiokuwa na umuhimu. Ulikuwa na ukubwa wa karibu ekari 60, na idadi ya watu isiyozidi 480 wakati Yesu anazaliwa.

S: Kwenye Mat 2:23 ni wapi palipoandikwa ubaii kuwa Yesu ataitwa Mnazareti?
J: Kwanza tutato jibu la Tertullian mwandishi tokea kanisa la awali (ambayo yanaweza yasiwe sahihi) na kisha jibu lenye uwezekano mkubwa wa kuwa sahihi.
Maombolezo 4:7 (Septuagint) Maombolezo 4:07 (Septuagint) Tertullian, mwaka 207 BK, alijibu kwenye kazi yake, Against Marcion, kitabu cha 4 Sura ya 7. Wakati maandishi ya Kimasoretiki (Kiebrania) ya Agano la Kale ya Maombolezo 4:7 yanasema "wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji, Septuagint inasema, "Wanazareti wake walikuwa safi kuliko theluji." Tertullian anataja hii kuwa maana ya "Wanaziri", "wanadhiri" (wale ambao wameweka nadhiri kwa Mungu ya kujiepusha na pombe, maiti, na uchafu mwingine), na "Wanazareti" wale ambao wanakuja kutoka Nazareti.
Tertullian alisema, "Kristo wa Muumba alipaswa kuitwa Mnazareti kulingana na unabii; kwa ajili hiyo Wayahudi wametupa jina lake, Wanazareti. Maana tu wale ambao kwa ajili yetu iliandikwa, ‘Wanaziri wake walikuwa safi kuliko theluji."
Tawi: Masihi aliitwa "tawi" kwenye Isa 11:1, Yer 23:5; 33:5, na pengine hata Zek 3:8; 6:12. Konsonanti za kwenye neno "tawi" zinafanana na zile za kwenye neno "Mnazareti", na Agano la Kale la Kiebrania la awali liliandikwa bila vokali. Pia neno "tawi" lilikuwa na wazo la mwanzo dhaifu, itikio la Mafarisayo lilionyesha kuwa Nazareti ilikuwa na maana hiyohiyo.

S: Je Mat 2:23 ilikosea kwa kusema kuwa kwa vile Yesu alitoka Nazareti alilitimiza Agano la Kale (Isa 11:1; Zek 6:12 na aya nyingine)?
J: Si hivyo kabisa. Agano la Kale linasema Masihi ataitwa "tawi" bila kubainisha sababu yoyote ya kufanya hivyo. Mat 2:22 haimzuii Yesu kuwa "tawi" la Mungu pia ambalo kutoka kwake kanisa lingekua.

S: Kwenye Mat 3:4 na Mak 1:6, je nzige ambao Yohana Mbatizaji alikuwa anakula walikuwa ni chakula kisafi au najisi?
J: Palikuwa na nzige wasafi na nzige najisi pia, na Injili hazisemi jambo hili kwa ubayana. Hata hivyo, tunaweza kuchukulia kuwa Yohana, kwa vile alikuwa Myahudi mtiifu, alikula aina safi ya nzige. Wanyama wasafi walikuwa ni pamoja na "watambaao wenye mbawa" yaliyounganika na miguui ikiwa ni pamoja na nzige na panzi, kwa mujibu wa Law 11:21-22 na Kumb 14:21. Wanyama najisi ni pamoja na "wenye mbawa na waendao kwa miguu minne" kulingana na Hesabu na Kumbukumbu 11:20, 23; 14:19.

S: Kwenye Mat 3:4 na Mak 1:6, je Yohana Mbatizaji alikula wadudu waitwao nzige, au aya hizi zinaonyesha kuwa alikula toka kwenye mti wa nzige?
J: Vifuatavyo ni vyanzo vya zamani and vya siku hizi vinavyosema kuhusu neno la Kigiriki limaanishalo nzige: akrides.
Waebioni (Wakristo wenye asili ya Kiyahudi wa karne za mwanzo za kanisa la awali waliochukuliwa kuwa waasi) walijitahidi kumfanya Yohana Mbatizaji awe mla mboga za majani (vegetarian). Kwa ajili hiyo walisema kuwa zilikuwa keki za asali, egkrides, badala ya nzige.
Tatian alitoa muhtasari wa Injili nne ulioitwa Diatessaron na alisema "maziwa" badala ya "nzige."
Theophylact 173 anaorodhesha idadi ya mambo yanayowezekana, likiwamo mmea ujulikanao kama melagron.
Watawa mbalimbali wa kiume mbalimbali wameuita mti karuba (wenye kuwa na rangi ya kijani wakati wote huko Arabuni unaotoa matunda yanayoweza kuliwa yenye rangi ya kahawia na zambarau) mti wa mkate wa Mtakatifu Yohana, kwa sababu walifikiri kuwa ulikuwa ni "mti wa nzige."
Theodore wa Mopsuestia, Theodore ya Mopsuestia, huenda katika kuwajibu watu waliokuwa wakisema kuwa hiki kilikuwa kitu kingine, alisema hawa walikuwa nzige waliokuwa na mabawa.
Tatizo lililopo kwenye maelezo haya ni kwamba hakuna aya za Biblia zenye kusema kuwa hivi vilikuwa vitu vyovyote vile zaidi ya "nzige." Wakristo wa awali, kama Clement wa Alexandria, waliandika kuhusu Mat 3:4, na hawakuona sababu ya kuona nzige kuwa kitu kingine chochote zaidi ya wadudu.

S: Kwenye Mat 3:9, Mungu angewezaje kumuinulia Ibraham watoto toka kwenye mawe kama angependa kufanya hivyo?
J: Mungu Mwenye enzi yote anaweza kufanya kitu chochote, hata kuyageuza mawe yasiyo na uhai kuwa watoto wenye nakala za jeni (genes) za Ibrahimu.

S: Kwenye Mat 3:10, Je Yohana Mbatizaji alimaanisha nini aliposema kuwa shoka limewekwa kwenye shina la mti?
J: Vitu vingine maishani haviwezi kurudiwa tena, kama kukata mti. Baada ya kuanza kufanya huwezi tengua kile ulichokianza. Vivyo hivyo, hii ilikuwa ni nafasi yao ya mwisho kabla hawajakatwa.

S: Kwenye Mat 3:11, Yesu anabatizaje kwa Roho Mtakatifu na kwa moto?
J: Waamini wanatabatizwa kwa Roho Mtakatifu wakati wanapomwamini Kristo kwa mara ya kwanza. Ingawa msemo wa kisasa wa "ubatizo wa moto" unamaanisha kitu kingine tofauti kabisa, hii siyo maana yake hapa, kwani ni Yesu, si watesi wanaobatiza, na wanafanya hivyo kwa moto.
Kuna maoni ya aina tatu kuhusu maana ya "moto" kwenye kifungu hiki.
(Maana isiyo na uwezekano mkubwa) Ubatizo wa pili kwa Roho Mtakatifu: Kwenye lugha ya asili, kuna kihusishi kimoja tu hapa, yaani, "kwa Roho Mtakatifu na moto" si "kwa Roho Mtakatifu na kwa moto." Msemo huu unaweza kuwa hauelezei tukio la pili.
(Maana nyingine isiyo na uwezekano) Siku ya Pentekoste: Mitume waliona moto ukitokea juu ya vichwa vyao walipokuwa wanahubiri siku ya Pentekoste, na maoni haya yanamaanisha Yohana Mbatizaji alikuwa anatabiri juu ya Pentekoste. Anonymous Treatise on Rebaptism (karibu mwaka 250-258 BK) sura ya 2, uk.668 inafundisha maoni haya. Lakini maneno haya ya Yohana hayaelekei kuongelea Pentekoste kwa sababu ileile ambayo hayakuongelea ubatizo wa mara ya pili. Moto unafananishwa na hukumu kwenye aya inayofuata.
(Maana nyingine isiyo na uwezekano) Kazi ya utakazo ya Roho Mtakatifu: Origen (mwaka 225-254 BK) pia alikuwa na maoni haya kwenye Commentary on John kitabu cha 6 sura ya 16-17, uk.366-367. Hata hivyo, wazo hili halielekei kuwa sahihi kwani makapi yanachomwa na moto usiokwisha kwenye Mat 3:12. Wako watu wanaoona kuwa kuwepo kwa kihusishi kimoja kwenye lugha ya Kigiriki kunaonyesha ubatizo mmoja siyo mawili (kwa Roho kwa waumini na kwa moto kama hukumu kwa wasioamini) lakini ubatizo mmoja tu (kwa Roho na moto utakasao).
(Maana nyingine isiyo na uwezekano) Moto wa hukumu kwa kazi za Mkristo, haya yalikuwa ni maoni ya Basil wa Cappadocia (mwaka 357-378/379 BK) kwenye On the Spirit sura ya15.36, uk.22.
Moto wa Jehanamu kwa watu wanaomkataa Yesu: John Chrysostom (aliyekufa mwaka 407 BK) alitoa maoni haya kwenye Homilies on the Gospel of Matthew, Homily ya 11 sura ya 6-7, uk.71-72, akisisitiza mwendelezo wa maonyo mengine ya moto ya Yohana Mbatizaji. Yohana alikazia mambo matatu: maji, upepo/roho, na moto. Yohana alibatiza kwa maji, Masihi atabatiza waamini kwa Roho, na ubatizo wa moto utawaangamiza kwenye hukumu wale wote ambao hawakuhushiriki kwa maji na Roho. Irenaeus (mwaka 182-188 BK) anatumia aya hii kuongelea hukumu ya Mungu kwa wasioamini kwenye Irenaeus Against Heresies kitabu cha 4 sura ya 4.3, uk.466. Tertullian (mwaka 198-220 BK) anasema kuwa ubatizo wa maji unaleta wokovu, na imani ya unafiki na dhaifu inabatizwa kwa moto na kuleta hukumu (On Baptism sura ya10, uk.674).
Moto wa siku ya mwisho ya hukumu wakati Yesu atakaporudi.
Maana mbalimbali: Wako watu wanaoona maneno haya ya Yohana yanamaanisha kuhukumu na kutakasa kwa waamini. Theodotus ambaye huenda alikuwa Mmonasti (mfuasi wa kundi potofu la Kikristo linalo amini miaka elfu moja ya utawala wa Kristo duniani na lenye kusistiza unabii, lililoanzishwa na Montanus katikati ya karne ya pili), uk.124 (karibu mwaka 240 BK) anasema kuwa moto ni kitu chenye kuharibu, kitakasacho uovu toka kwa waamini, na (anamaanisha) kuwaharibu watu wengine.
Maana isiyobainishwa: Watu wafuatao waliinakiri aya hii lakini hawakutoa maoni maalumu.
Justin Martyr (aliyeishi karibu mwaka 138-165 BK) kwenye Dialogue with Trypho the Jew sura ya 49, uk.219
Hippolytus (mwaka 222-234/5 BK) kwenye The Discourse on the Holy Theophany sura ya 3, uk.235
Cyprian wa Carthage (mwaka 246-258 BK) kwenye The Treatises of Cyprian makala ya 12 sura ya 1.12, uk.511
Augustine wa Hippo (aliyeishi miaka ya 388-430 BK) anaongelea aya hii lakini hatoi maoni maalumu (Harmony of the Gospels kitabu cha 2 sura ya 12.26, uk.117).

S: Kwenye Mat 3:16, kwa nini "Maskini Yesu (amani iwe juu yake) aliishia kusubiri MIAKA THELATHINI baada ya kuzaliwa kwake ndipo apate zawadi ya ROHO MTAKATIFU wakati wa kubatizwa kwake na Yohana Mbatizaji" wakati zawadi ya Roho Mtakatifu "ni nafuu sana kiasi kwamba Wakristo 75,000,000 wa Kimarekani ‘WALIOZALIWA UPYA’ pia wanajivuna kuwa nayo" na kwenye Luk 1:15 Yohana Mbatizaji alijazwa Roho Mtakatifu tokea kuzaliwa kwake. (Muislam Ahmad Deedat alisema jambo hili.)
J: Kwanza, kama jambo la ziada, Muhammad alisubiri miaka AROBAINI kabla ya kudai kuwa ni nabii. Deedat anachanganya maneno/misemo ‘bure’ na ‘yenye bei ndogo’, na anaonekana kuwa amesahau mafundisho ya Biblia ya Uungu wa Kristo. Deedat hajawahi kupokea zawadi ya Roho Mtakatifu, hivyo hajui tofauti ya zawadi ya Roho Mtakatifu na Roho Mtakatifu kutua kwa Yesu kwa jinsi inayoonekana kama hua.
Bure lakini si ya bei nafuu: Bure lakini si yenye bei ndogo: zawadi hii ilikuwa ghali sana, iligharimu uhai wa Yesu. Lakini Mungu anaitoa bure kwa wote wanaoamini injili yake.
Uungu wa Yesu: "Maskini" Yesu hakusubiri miaka thelathini; neema ya Mungu haikuwa juu ya Yesu kama mtoto (Luk 2:40) tu, lakini Yesu ni Mungu mwenyewe, na Baba alikuwa ndani yake. Yesu hakuwa na haja ya kujazwa Roho Mtakatifu kama sisi tunavyohitaji; Mungu Baba na Yesu walimtuma Roho Mtakatifu kwetu.
Kutua kwa Roho Mtakatifu juu ya Yesu si zawadi ya Roho Mtakatifu: Deedat anasoma kimakosa kuwa Yesu alijazwa na Roho Mtakatifu wakati wa kubatizwa kwake; maandiko hayasemi kuwa Yesu alijazwa Roho Mtakatifu wakati wa kubatizwa kwake. Badala yake, Roho Mtakatifu alitua juu ya Yesu katika umbo linaloonekana kama hua. Wakati Wakristo wanajazwa Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu hatui juu yao kama njiwa, hivyo jambo hili ni tofauti.
Mwisho, hebu tutofautishe mambo yaliyompata Yesu na yale yaliyompata Muhammad.
1. Muhammad, ambaye hadithi zinamwelezea kuwa akiwa nabii alipagawa.
1a. Labid bin el-Asim Myahudi alimpagaisha Muhammad. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3435, uk.60-61
1b. Muhammd alipagawa kwa mujibu wa Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5428-5429, uk.1192-1193; Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 4 na.1888, uk.411. Tazama pia Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 sura ya 56 na.89, uk.57 na Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 sura ya 59 na.400, uk.266
2. Muhammad alihofia mateso yake yeye mwenyewe kaburini.
2a. Mwanamke wa Kiyahudi alimwambia Muhammad "Mungu na akulinde na mateso ya kaburi." Baada ya hapo, Muhammad aliomba apate mahali pa kukimbilia toka kwenye mateso ya kaburi. Sunan Nasa’i juzuu ya 2 na.1479, uk.281-282
2b. "’A’isha alitaarifu: Nabii Mtakatifu (amani iwe kwake) aliingia kwenye nyumba yangu wakati mwanamke wa Kiyahudi alipokuwa pamoja nami mimi na alikuwa akisema: Je, unajua kwamba utawekwa kwenye majaribu ya kaburi? Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) wakatetemeka (aliposikia hivi) na akasema: Ni Wayahudi tu ambao wangeweza kushtakiwa. ’A’isha alisema: tulikaa siku kadhaa kisha pita Sisi kupita usiku baadhi na kisha Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake) alisema: je unajua kuwa imefunuliwa kwangu: "Utashtakiwa kaburini? ‘A’isha alisema: Nimemsikia Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake) akitafuta mahali pa kukimbilia kutoka kwenye mateso ya kaburi baada ya jambo hili" Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1212, uk.290
2c. Abu Huraira aliripoti: "Nilimsikia Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake) akitafuta mahali pa kukimbilia kutoka kwenye mateso ys kaburi baada ya jambo hili (baada ya ufunuo)." Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1213, uk.290
2d. "‘Ai’isha alisema: Sikumuona tena (Nabii Mtakatifu) baadaye ila akiwa anatafuta mahali pa kukimbilia kutoka kwenye mateso ya kaburi kwenye maombi." Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu 4 na.1214, uk.290
2e. "Masruq aliripoti hadithi hii iliyosimuliwa na kuthibitishwa na ‘A’isha aliyesema: Nabii Mtakatifu hakuwahi hata mara moja baada ya hii ambayo sikumsikia akiomba mahali pa kukimbilia kutoka kwenye mateso ya kaburi." Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.1215, uk.291.
2f. Muhammad alitafuta mahali pa kukimbilia kutoka kwenye mateso ya kaburi. Sunan Nasa’i juzuu ya 2 na.2065, uk. 535; juzuu ya 2 na.2069, uk.537; juzuu ya 2 na.2071, uk.538
Sasa Muislamu anaweza akakubaliana, asikubaliane, au kwa uwezekano mkubwa zaidi, asiwe anafahamu wa mambo ambayo hadithi hizi zinasema. Hata hivyo, vyovyote ilivyo, hawakubaliani wala kupingana na mimi, kwani ninaripoti tu kile ambacho hadithi za kuaminika za Wasuni zinasema.
Kwa muhtasari, Yesu alimtuma Roho Mtakatifu kwetu. Tumaini langu ni kuwa utakuwa huru kutoka kwenye uovu, huru kutoka kwenye hofu ya mateso ya kaburi, na mwombe Mungu akupe Roho Mtakatifu.

S: Kwenye Mat 3:16 na Mak 1:10, ni nani aliyemwona njiwa?
J: Vifungu vyote viwili, Mat 3:16 na Mak 3:16 vinasema kuwa Yesu alimwona njiwa, na Yoh 1:32 inasema kuwa Yohana Mbatizaji alimmwona njiwa. Aya hizi hazibainishi mtu mwingine zaidi aliyemuona.

S: Je Mat 3:16-17 inaunga mkono kuwa Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni nafsi tatu zilizotenganishwa kama Wamomornini walivyodai (Talmadge, 1977, uk.39-40)?
J: Hapana. Aya hii inaonyesha kuwa wako tofauti lakini haionyeshi kuwa wametenganishwa. Badala ya kuupinga Utatu Mtakatifu, kifungu hiki kinaunga mkono Utatu Mtakatifu kwa kuonesha kuwa nafsi tatu ni tofauti. Kifungu hiki hakiupingi umodali (mafundisho kuwa nafsi tatu za Utatu Mtakatifu ni namna tatu za ufunuo wa Mungu na si namna ambayo nafsi tatu Mungu zinavyoishi pamoja) wala "Upentekoste wa Mungu mmoja", yaani, "Oneness Pentecostalism" (Upentekoste wa Mungu mmoja, ambao pia unaitwa Upentekoste wa Kimitume (Apostolic Pentecostalism) ni mafundisho ya baadhi ya madhehebu ya Kipentekoste ya umoja wa Mungu yenye kupinga dhana ya kithiolojia ya Utatu Mtakatifu).

S: Kwenye Mat 4:8, je Shetani angewezaje kumpa Yesu ulimwengu wote kwa kuwa Yesu alikuwa Mungu, kama mtu asiyeamini uwepo wa Mungu (Cappello) anavyodai?
J: Swali hili ni la ajabu. Kuna mambo manne ya kuyazingatia katiki kujibu swali hili.
1. Yesu aliendelea kuwa Mungu, lakini alihiari kujifanya kuwa hana utukufu alipokuja duniani, kama Wafilipi 2:7 na Yohana 17:5 zinavyoonyesha.
2. Ni kweli kwamba Mungu ndiye "mmiliki" wa ulimwengu wote kama Zab 24:1 inavyoonyesha. Hata hivyo, wakati Yesu alijifanya hana utukufu na kuja duniani, "walio wake" hawakumpokea, kama Yoh 1:10-11 inavyoonyesha.
3. Ingawa aliendelea kuwa na mamlaka yote, aliwaruhusu wanadamu kuutawala ulimwengu huu, kulingana na Mwa 1:28.
4. Ingawa Mungu ndiye mmiliki halali, kuanzia wakati wa anguko Shetani amepewa sehemu kubwa ya udhibiti wa ulimwengu huu kwa muda kama 1 Yoh 5:19 inavyoonyesha. Kwa mujibu wa 2 Kor 4:4, mungu wa ulimwengu huu ni Shetani. Shetani ni mkuu wa ulimwengu huu kwenye Yoh 12:31; 14:30, 16:11; Efe 6:12; na Kol 1:13.
Muhtasari: Mungu ndiye mmiliki halali kwani ya uumbaji alioufanya hapo mwanzo na utawala wa milele. Tangu wakati wa anguko, Shetani anatawala, lakini hana mamlaka yote ya kuutawala ulimwengu huu.

S: Kwenye Mat 4:10 na Mat 12:26, je uasi wa Shetani uliongelewa tu baada ya Wayahudi kupelekwa uhamishoni?
J: Hapana. Isaya 14:12-15, iliyoandikwa kabla ya uhamisho, pia inaongelea uasi wa Shetani.

S: Kwenye Mat 4:14-16, je Isa 9:1 na Isa 9:2 ziko pamoja, au Mathayo alikosea kuziweka pamoja?
J: Aya hizi ziko pamoja kwa kuwa Isa 9:1 ni mpito wa sehemu zote mbili.
Mwandishi mmoja anadai kuwa Isa 9:1 ni sehemu ya kifungu kinachotangulia na inaitwa Isa 8:23 kwenye Biblia za kisasa za Kiyahudi na Jerusalem Bible mpya. Isa 8:22 na 9:1 zinahusiana , kwani Isa 8:22 inazungumzia watu walio gizani na Isa 9:1 inasema kuwa hakutakuwa na giza tena.
Hata hivyo, Isaya 8:22 inaongelea watu watakaopelekwa gizani, Isa 9:1 inasema hakutakuwa na giza tena kwa Zabuloni na Naftali, na Isa 9:2-7 inaongelea jinsi ambavyo watu waliokuwa gizani watakavyoiona nuru kuu.
Inafurahisha kuona Asimov akijaribu kusema kuwa watu waliokuwa gizani lakini likaondolewa kwenye Isa 9:1 hawahusiani na wale waliokuwa gizani na wameiona nuru kuu kwenye mstari unaofuatia.

S: Kwenye Mat 4:15-16, je unabii kuhusu Zabuloni na Naftali kwenye Isa 9:1-2 unahusiana na Yesu?
J: Unahusiana kwa njia mbili.
Miaka ya utotoni: Miaka mingi ya utoto wake Yesu aliishi Galilaya, magharibi mwa Bahari ya Galilaya.
Mwanzo wa huduma: Huduma ya mwanzo ya Yesu ilifanyikia Galilaya, hasa magharibi mwa Bahari ya Galilaya. Ukanda huu ulikuwa eneo lililopewa makabila ya Zabuloni na Naftali.

S: Kwenye Mat 5:8, 1 Yoh 3:2, na Ufu 22:4, je watu wenye moyo safi watawezaje kumuona Mungu, kwani Kut 33:23 na aya nyingine zinasema kuwa hakuna mtu anayeweza kumwona Mungu na kuwa hai?
J: Tangia wakati wa anguko, hakuna binaadamu mtenda dhambi na ambaye huzaliwa na kufa, anayeweza kumona Mungu na akaishi. Hata hivyo, waamini watatakaswa, na watamwona Mungu mbinguni.

S: Kwenye Mat 4:18-22, wakati Yesu alipowaambia Petro na and Andrea kuziacha nyavu zao na kumfuate Yeye, kwa nini waliondoka mara moja na kumfuata?
J: Yesu alikuwepo kwenye maeneo ya Galilaya kwa muda, na huenda waliwahi kukutana naye kabla ya hapo.

S: Kwenye Mat 5:13, je Wakristo wanawezaje kuwa chumvi?
J: Kiasi kidogo cha chumvi huungwa kwenye chakula ili kifanye moja ya mambo manne. Wakristo vivyo hivyo ni chumvi ya dunia hii katika maeneo manne.
Maisha - Chumvi ni muhimu kwa maisha yetu. Katika mji wa Afrika Magharibi uitwao Timbuktu, ambako kulikuwa na dhahabu nyingi, paundi moja (nusu kilo) ya chumvi ilikuwa inauzwa kwa paundi moja ya dhahabu. Kwa kuwa Wakristo wana maisha ya Kristo ndani mwao, wanawiwa kuyaonyesha maisha hayo kwenye ulimwengu huu. Mungu hutumia mahubiri yetu, upendo, na huduma kuwaleta watu wengine kwake ili awape uzima.
Ladha - Chumvi huongeza ladha kwenye chakula na kukifanya kiwe na ladha nzuri. Vivyo hivyo, sisi tu manukato ya Kristo kwa wale wanaookolewa. Mungu pia huangalia chini na kufurahishwa kuona Wakristo wanaomfuata hapa duniani.
Hifadhi - Wakati panapokuwa hakuna majokofu, chumvi pia huwa muhimu kuhifadhi chakula kwa kukiepusha na bakteria. Vivyo hivyo, Wakristo wanapaswa kuwa chumvi na nuru hapa duniani kwa kuleta uhifadhi kwa njia ya kupingana na dhambi.
Dhabihu - Kwenye Law 2:13 dhabihu/sadaka zilikuwa zinawekwa chumvi. Sisi nasi tunapaswa kuishi maisha yetu kama dhabihu ya Mungu.

S: Je Mat 5:13 inaongelea watu wanaoutambua uungu wao kuwasaidia watu wengine kuutambua uungu wao pia, kama baadhi ya wafuasi wa New Age (harakati pana inayo tafuta namna tofauti na zile za Kimagharibi yenye kukazia mambo ya kiroho, miujiza, kuchukulia vitu kiujumla na utunzaji wa mazingira) wanavyosema? (Spangler, 1981, 80).
J: Si hivyo hata kidogo; chumvi si uungu. Kusema kuwa tungekuwa kama Mungu ilikuwa ni moja ya mambo makongwe mapotofu yaliyosemwa kwa binadamu, kwenye bustani ya Edeni. Tumeumbwa kumpenda na kumtumikia Mungu milele, si kuwa miungu wengine, kuabudiwa, au sehemu ya Mungu, na kuabudiwa.
Mtazamo huu wa ajabu unaonekana kusahau kuwa Yesu alikuwa Myahudi, dini ya Kiyahudi ilikuwa inaamini kuwa kuna Mungu mmoja. Angalia swali lililopita kuona maana ya chumvi.

S: Kwenye Mat 5:14, je sisi tu nur ya ulimwengu au Yesu ndiye nuru ya ulimwengu kama Yoh 9:5 inavyosema?
J: Wote: Yesu alileta nuru ulimwenguni, na sisi tunao wajibu wa kuionyesha hii nuru. Paulo anaongelea jambo hili kwenye 2 Kor 4:6-7. Yesu alisema kuwa alikuwa nuru ya ulimwengu "muda nilipo ulimwenguni" kwenye Yoh 9:5. Mwili wa Yesu kwa sasa uko mbinguni, si katika dunia hii, lakini uwepo wa Yesu ungalipo ulimwenguni kupitia Roho Mtakatifu aliye ndani yetu.

S: Kwenye Mat 5:17 na Mdo 10:10-16, kwa kuwa Yesu alisema hatatengua kitu chochote kwenye sheria, kwa nini Wakristo hawazifuati sheria za Agano la Kale zinazohuska na chakula kama ambavyo Waislam wanadaiwa kufanya?
J: Ingawa si Wakristo wala Waislamu wanaofuata sheria za Agano la Kale zinazohusika na chakula, Wakristo hawafanyi hivyo kwa sababu wanamsikiliza Yesu. Kuna mambo matano yanayopaswa kuzingatiwa katika kujibu swali hili.
Kwa wakati huu, wafuasi wa Yesu walizifuata sheria za Agano la Kale zinazohusika na chakula. Yesu alisema kuwa hapatakuwa na yodi moja au nukta moja ya torati itakayoondoka hata yote yatimie.
Ukweli kuhusu kufufuka kwa Yesu umebadilisha kwa kiasi kikubwa sana namna ambayo Mungu anashughulika na watoto wake. Malaika alimwambia Petro, mwanafunzi wa Yesu, kwamba Mungu amevifanya vyakula vyote kuwa safi kwenye Mdo 10:9-16. Kumbuka haisemi kuwa wanyama hawa walikuwa wasafi wakati wote, lakini Mungu amewasafisha.
Hata Waislam ambao wanapenda madai haya, wanapaswa kukubali kuwa baadhi ya sheria za Agano la Kale zinazohusika na chakula hazipaswi kufuatwa. Waislamu wanaona kuwa wanaweza kula nyama ya ngamia (na Muhammad alifanya hivyo), lakini Law 11:3-8 na Kum 14:6-8 zinazuia kuila.
Msikilize Yesu kwenye Mat 15:10,17-20 na Mak 7:14-15. Yesu alisema ni kitu kimtokacho mtu ndicho kinachomfanya najisi, si kile kimuingiacho. Mak 7:19 inaonyesha kuwa kwa kusema hivi, Yesu alivitakasa vyakula vyote. Kama tunamwita Yesu nabii, tunapaswa kusikiliza maneno yake.
Sauti kutoka mbinguni ilimwamuru Petro kula kwenye Mdo 10:10-16, ilionyesha kuwa sheria zinazohusu chakula zilitumika hadi wakati wa kafara ya Yesu, si baada ya hapo. Tunapaswa kuitii sauti ya malaika wa Mungu na mwanafunzi wa Yesu.
Kwa kumalizia, hatupaswi kuyapuuzia maneno ya manabii wa Mungu, bali kuyasikiliza.

S: Kwenye Mat 5:17, kwa kuwa Yesu alisema hatatengua kitu chochote kwenye sheria, kwa nini sikukuu za Kiyahudi hazifuatwi?
J: Mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1. Masharti ya kimaadili ya Agano la Kale ni kwa watu wote, na hayabadilika.
2. Dhabihu zinaweza kusemwa kuwa zinawahusu watu wote leo kwa namna moja au nyingine, kwa sababu Yesu ni kuhani wetu mkuu na ametoa dhabihu yote inayohitajika.
3. Sikukuu, ambzo zilikuwa kwa ajili ya Wayahudi na zilihisisha dhabihu, hazifuatwi kunzia wakati Kristo alipokufa kwa ajili ya watu wasiokuwa Wayahudi.
4. Kama Muislam ataleta hoja hii, anaweza kuulizwa kuwa kwa nini Waislam hawafuati sikukuu zilizowekwa na Mungu kwenye Agano la Kale, endapo wanafikiri kuwa Wakristo wanapaswa sikukuu za Kiyahudi za Agano la Kale.

S: Kwenye Mat 5:20, waandishi na Mafarisayo ni kina nani na wana haki ya kiwango gani?
J: Kwenye Mat 5:20, kwa kawaida waandishi walikuwa upande wa Masadukayo, wakati Mafarisayo walikuwa dhidi yao. Kisiasa, Masadukayo walikuwa miongoni mwa Wayahudi waliopenda kuafikiana na Warumi, wakati Mafarisayo walipinga jambo hilo. Mafarisayo walikuwa kikundi kidogo cheny watu 5,000 hadi 6,000 lakini walikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa sababu walitumainiwa sana na watu. Masadukayo kwa ujumla hawakuwa wanaamini ufufuo wa mwili na walivikubali vitabu vitabu tu vya kwanza vya Biblia ya Kiebrania kuwa Maandiko. Ni muhimu kuwa Yesu aliwakemea Masadukayo kwa kutokujua Maandiko wala nguvu za Mungu. Hakuwahi kawakemea Mafarisayo kwa kutokuyajua Maandiko.
Ingawa waandishi na Mafarisayo walijaribu kuonyesha sura ya haki, Yesu hakuwathibitisha au kuwaambia kuwa walikuwa na haki. Badala yake, alisema watu wanahitaji haki zaidi kuliko ya waandishi na Mafarisayo ili waweze kuingia katika ufalme wa mbinguni. Usemi huu unamaanisha vitu vitatu:
a) Waandishi na Mafarisayo hawakuwa na haki inayotakiwa kuingia katika ufalme wa mbinguni
b) Wafuasi wa Yesu walitakiwa kuwa wenye haki zaidi kuliko Waandishi na Mafarisayo
c) Ukweli ni kwamba hakuna mtu aliye na haki yake mwenyewe ya kutosha kuingia ufalme wa mbinguni. Yesu anadokeza zaidi jambo hili kwenye sura ya 6 na 7. Hatimaye wanafunzi walielewa jambo hili kwenye Mak 10:26-27.
d) Kama hakuna mtu aliye na haki ya kutosha, usiwadharau watu walio dhambini kwa sababu wewe nawe u mwenye dhambi pia. Kwa mshangao mkubwa wa Mafarisayo, Yesu alikula pamoja na watoza ushuru wengi na wenye dhambi kwenye Mat 9:9-12.
Irenaeus kwenye kazi yake iitwayo Against Heresies (mwaka 182-188 BK) kitabu 4 sura ya 13, uk.477 anatoa jibu la nyongeza. Ufuatao ni ufafanuzi wa mawazo yake manne:
1) Wakati waandishi na Mafarisayo walimwamini Mungu Baba, sisi tunapaswa kumwamini Mungu Mwana pia.
2) Tunapaswa si tu kusema, lakini pia kutenda; kwa sababu waandishi na Mafarisayo walisema lakini hawakutenda.
3) Tunapaswa kujiepusha si tu na kutenda maovu, bali pia hata na kuyatamani.
4) Yesu hakutufundisha mambo yaliyo kinyume na sheria, bali mambo yaliyoitimiza. Yesu hakutengua sheria, bali aliitimiza, na kuipanuaa na kuipa wigo mkubwa zaidi.

S: Kwenye Mat 5:21, kwa nini watu wanaua wanyama, wahalifu, n.k., kwa sababu Yesu alisema usiue?
J: Toleo la Biblia ya Kiingereza la King James linatafsiri kuwa "kuua" wakati neno la Kigiriki foneuo linaweza kumaanisha mauaji. Mtu anayefanya hivi, foneus ni muuaji wa kawaida au wa watu maarufu, si mtu anayetekeleza hukumu ya kifo au anayechinja wanyama. Kama mtu alifikiri kuwa amri ya Agano la Kale isemayo "usiue" inaongelea wanyama na utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa wahalifu, kutokuelewana kwao neno hili kutaufanya mfumo mzima wa dhabihu wa Agano la Kale uwe fumbo lisiloeleweka kwao.

S: Kwenye Mat 5:22, kwa nini alituamuru kutokumwita mtu yeyote mjinga, kwani Yeye mwenyewe na watu wengine walifanya hivyo kwenye Mat 23:17; Luk 24:25; 1 Kor 15:36 na Gal 3:1?
J: Yesu hakusema "mjinga" bali alitumia msemo wa Kiaramu usiokuwa rasmi unaomaanisha "mpumbavu", sawa na neno lisilokuwa rasmi la Kiingereza cha Marekani "mwenye kukosa hekima" au "kituko." Yesu pia aliwaita watu "wapumbavu", "viongozi vipofu" (Mat 23:16), hata "wezi na wanyang’anyi" na "nyoka." Yesu alitumia maneno yake kwa ungalifu, na hakuwakebehi.

S: Kwenye Mat 23:13-33; 21:45 na 16:4, kwa nini Yesu aliwatukana viongozi wa watu wake? (Muislam Ahmad Deedat alileta hoja hii)
J: Kabla ya kujibu swali hili, hebu natulifanya gumu zaidi kidogo. Yesu hakuwatukana tu Mafarisayo, waandishi, na viongozi wengine wa kidini waliomkataa, aliwaonya kuwa watakwenda Jehanum. Hata hivyo, Yesu hakuishia na maneno tu bali alitumia hata mjeledi na mara mbili alipindua meza za wabadilishaji fedha kwenye hekalu. Ni dhahiri kuwa kwanza kabisa alipinga hadharani mamlaka ya watu walioruhusu wabadilishaji fedha kwenye viwanja vya hekalu.
Jibu lina sehemu tatu.
1) Yesu alikuwa na mamlaka kubwa kuliko yao. Hata kama walikuwa wanamfuta Mungu kwa utiifu, (jambo ambalo hawakuwa wanafanya) Yesu kama Masihi na Mungu Mwana alikuwa na uwezo wa kuwaambia kitu alichotaka kifanyike. Mungu ana haki ya kubadilisha na kuharibu mipango yetu wakati wowote na kwa namna yoyote atakayo.
2) Yesu aliyakataa hasa mamlaka ya watu ambao si tu kuwa walikuwa wanakwenda Jehanum bali pia walikuwa wanawaongoza watu wengine kwenda Jehanamu pia kwenye Mat 23:15. Tofauti na jambo hili, ingawa Yesu alikuwa mkuu kuliko Ibrahimu, Musa, na Agano la Kale, Yesu aliafiki mamlaka yao na kuwaheshimu.
3) Leo hii tumeamriwa kutowasikiliza watu wenye wanaoipinga kweli (Tito 1:14). Tunapaswa kuwakataa watu wanaoleta matengano kwenye Tito 3:9-10. Tatizo moja ambalo limekuwepo miaka yote ya kuwepo kwa kanisa ni kuwa watu wengi wamekuwa tayari kuwafuata watu waovu tu kwa sababu ni viongozi wa kidini. Lakini, tofauti na desturi hii, Biblia pia inatuambia kuwa tutii na kuwa chini ya mamlaka ya viongozi wanaomcha Mungu (1 Thes 5:12-23; 1 Pet 5:2-5; Ebr 13:17).

S: Kwenye Mat 5:22, Yesu alisema "MTU akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanamu ya moto", lakini, yeye mwenyewe alifanya hivyo kama ilivyo ripotiwa kwenye Mat 23:17, Luk 11:40, na Luk 12:20. Je yeye naye yupo kwenye hatari ya kupelekwa jehanaamu? Isitoshe, anavunja sheria yake mwenyewe!
J: Hapana kwa sababu mbili.
a) Hatupaswi kuitwa Bwana, au kuwaruhusu watu wengine watuabudu, na jambo hilo ni sahihi kwa Yesu. Kwa ajili hiyo, si kila jambo ambalo Yesu anatufundisha linatumika kwake. Kwa kiwango cha ulimwenguni, ninapoweka amri kwa ajili ya ndege wangu wa kufuga, kama vile hawezi kula toka sehemu nyingine isipokuwa chombo chake maalumu cha kulia chakula, je jambo hili linamaanisha kuwa mimi nami napaswa kula chakula toka chombo hicho hicho?
b) Yesu hakusema "mjinga" (huu ni ufafanuzi), neno hasa alilosema ni raka ambalo ni tafsiri yake nzuri zaidi ni "mpumbavu", sawa na neno lisilokuwa rasmi la Kiingereza cha Marekani "mwenye kukosa hekima" au "kituko." Yesu aliwaita watu wajinga, kwa maana ya watu wapumbavu ya kwenye kitabu cha Mithali, lakini hakumaanisha kuwa vichwa vyao (au maisha) yao hayakuwa na thamani yoyote.

S: Je Mat 5:26 inaunga mkono dhana ya Pagatore (serch for a right word in Swahili), mahali pa mateso ambapo roho za watenda dhambi zinazofanyiwa malipo ya dhambi zao zitakaa kabla ya kwenda mbinguni, kama ambavyo mwalimu wa Mkatoliki, Ludwig Ott alivyofundusha?
J: Hapana kwa sababu saba.
Kifungu hiki hakiongelei kifo: Hakiitaji Pagatore wala kitu chochote kihusishacho maisha baada ya kifo.
Hata baadhi ya Wakatoliki kama aliyekuwa Kardinali Ratzinger (sasa Papa Benedict XVI) hakukubaliana. Hivi ndivyo alivyosema, "Pagatore si aina fulani ya kambi ya mateso ya ulimwengu wa mwingine ambako watu hulazimishwa kupata adhabu kiholela. Badala yake huu ni mchakato wa ndani ya mtu wa mabadiliko ambao unamfanya mtu kuwa na uwezo wa Kristo, uwezo wa Mungu [yaani uwezo wa kuwa na umoja mkamilifu na Kristo na Mungu] na hivyo uwezo wa kuwa na umoja na ushirika wote la watakatifu (kitabu cha Ratzinger Eschatology, 1990, uk.230).
Waebrania 10:10-15 inafundisha vitu viwili: 1) Kristo amekwisha kamilisha dhabihu yake kwenye Waebrania 10-12, na 2) Kristo ameisha tufanya wakamilifu milele kupitia dhabihu yake katika Waebrania 10:13-15. Tafadhali, tusimwambie Kristo kuwa dhabihu yake haikuwa nzuri ya kutosha, kamilifu ya kutosha, au haikukamilisha kazi ambayo Waraka kwa Waebrania unatuambia kuwa aliimaliza.
Warumi 8:1 inasema, "Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu . . ."
2 Petro 1:11 inasema kuwa baada ya kufa tutapokea makaribisho makubwa sana mbinguni. (Si makaribisho yenye joto, au ya moto yenye miale ya moto). Pagatore isingeonekana kuwa "baraza" la makaribisho makubwa ya kuingia mbinguni.
2 Wakrintho 5:8 inasema, "Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana."
Vivyo hivyo, Wafilipi 1:23 inasema Paulo alitaka ama kuwa hai katika mwili, au "kuondoka na kuwa na Kristo." Tutakuwa na Mungu mara tutakapokufa, si Pagatore huku ahadi ya kuingia mbinguni ikiwa imecheleweshwa.
Wakristo wa awali, kabla ya baraza la Nikea, hawakuwahi kusikia kuhusu Pagaore, na hakika hawakuona kitu kama pagatore katika aya hii. Katika maandiko zaidi ya 4,170 maandiko yaliyoandikwa kabla ya baraza la Nikea, tafsiri hii ya Mathayo 5:26, na dhana ya aina yoyote ya kutakaswa kwa waumini kwa njia ya moto baada ya kufa kwao haipo kabisa.
S: Kwenye Mat 5:29, je jehanamu ni mateso ambayo watu wataweza kuyahisi au kaburi tu?
J: Ni vyote. Neno la Kigirik ni Hades na linafanana na neno la Kiebrania Sheol. Kwenye Mat 5:29 ni dhahiri kuwa Jehanamu ni mahali ambapo hupendi kwenda, kwa hiyo muktadha ni "Jehanamu" ambapo watu wanaokufa bila Mungu huenda.
Luk 16:22-23 inaonyesha kuwa kutakuwa na mateso, basanois kwa Kigiriki (m. 23, 28), hali ya kufahamu (m.23), na mateso kwenye moto (mm.24, 25). Watu wasioamini si tu kwamba watakuwemo bali pia wataadhibiwa milele humo (Mat 25:41, 46; Ufu 14:9-11; 19:3; 22:15).
Mat 13:40-42, 50 inasema kutakuwa na kilio na kusaga meno KWENYE tanuru la moto (neno ekei "hapo" kwa Kigiriki linamaanisha "mahali hapo" , siyo hapo "itatokea."
2 Wathesolanike 1 inasema kuwa huu utakuwa ni uharibifu wa milele; kutengwa na uwepo wa Bwana na nguvu zake za enzi yake.
Ufunuo 14:9-11 wale wanaomwabudu mnyama watateswa kwa moto na kiberiti (salfa iunguayo) mbele ya mwana kondoo na malaika wake.
Watu wasioamini wana ufahamu wa uchungu wa maisha ya baada ya kifo (Ufu 20:10; Luk 12:5; 13:28; 16, Eze 32:31-32, Mat 3:12; 5:21; 13:42, 50; 22:13; 25:41, Isa 50:11).
Wasio amini watapotea (Luk 13:3, 5; Yoh 3:16; 2 Thes 2:9) na kuangamizwa (2 Thes 1:9; 2 Pet 3:16; Mat 10:28; 1 Kor 3:17; Flp 1:28; Yak 4:12; Ufu 11:18).

S: Je kwenye Mat 5:34 tumeagizwa kuwa tusiape, au tunapaswa kuapa kwa jina la Mungu kwenye Kumb 10:20?
J: Wakati wa kusoma Biblia ni muhimu kujua muktadha wa jumla, kwenye swali hili Agano Jipya ni nini na Agano la Kale ni nini? Yesu aliweka waziwazi mafundisho yaliyochukua nafasi za amri tano za Agano la Kale au kuzibadilisha kwenye Mat 5:21-48. Ufuatao ni muhtasari wa mambo ambayo Yesu aliyasema.

Mistari Agano la Kale Lakini Yesu alisema
Mat 5:21-26
Usiue
Pamoja na hilo, usimkasirikie ndugu yako au kumwambia "mjinga"
Mat 5:27-30 usizini Pamoja na hilo, usimwangalie mwanamke kwa kumtamani moyoni mwako
Mat 5:31-32 Utoapo talaka kwa mkeo mwandikie hati Badala ya kufanya hivyo, usitoe talaka isipokuwa kwa sababu ya zinaa
Mat 5:33-37 Usikiuke kiapo Badala ya kufanya hivi, usiape kabisa, bali sema ndiyo au siyo
Mat 5:38-42 Jicho kwa jicho Badala ya kufanya hivi, geuza shavu la pili, nenda maili ya ziada, n.k.
Mat 5:43-48 Mpende jirani yako na mchukie adui yako Badala ya kufanya hivi, wapende hata maadui zako











































































Pamoja na hayo, Yak 5:13 pia inasema kama Mat 5:34 kuwa hatutakiwi kuapa leo hii.
Yesu pia alionyesha kuwa vyakula vyote ni safi kwa sasa kwenye Mak 7:19, jambo ambalo limeongelewa tena kwenye Mdo 10:9-16.

S: Kwenye Mat 5:39-40, ni kwa jinsi gani Wakristo wanatakiwa kugeuza shavu la pili?
J: Wakristo hawakiwi kuishi kwa jinsi ya kawaida bali kwa jinsi iliyo zaidi ya kawaida (kwa jinsi inayowezeshwa na Mungu). Tunatakiwa kujiweka wazi (lakini si kwa namna ya kipumbavu kwa kuamini watenda maovu), tukitambua kuwa tunaweza kumwamini Mungu kutulinda na sisi pamoja na familia zetu.

S: Kwenye Mat 5:39, kwa nini Wakristo wanayapinga maovu?
J: Hakuna aya kwenye Biblia inayosema kuwa Wakristo hawapaswi kupinga uovu wowote ule. Badala yake Mat 5:39 inaagiza kibayana kuwa kupingana na mtu mbaya, mtu afanyaye maovu kwako. Tunapaswa kumpinga Shetani kwenye Yak 4:7 na 1 Pet 5:9. Kama tunavyoagizwa kwenye Yer 7:6 na 22:16, tunapaswa kuwatetea watu wanaoonewa. Kwenye Agano la Kale, Mit 28:4 inasema wenye haki "hushindana" na waovu wanaoiacha sheria ya Bwana. Law 5:1 inasema ni dhambi kukataa kutoa ushahidi mahakamani kuhusu uovu tuliouona. Tunapaswa kujilinda dhidi ya walimu wa uongo (1 Yoh 2:26; 3:7; 4:1; 2 Yoh 7-8, Ufu 2:16; 2 Pet 2:2;. Mdo 20:28-29). Tunapaswa kuwakanusha waalimu wa uongo (1 Tim 1:3, Tito 1:9-11; Yuda 3). Tunapaswa kupambana kwa ajili ya imani (Flp 1:27; 4:3).

S: Kwenye Mat 5:42 na Luk 6:29-30, je Wakristo wanapaswa kumpa kila mtu anayewaomba?
J: Ndiyo: agizo hili si gumu kulielewa, bali ni changamoto kulifuata. Wakristo wanatakiwa kuwaona watu wengine kuwa muhimu kuliko wao wenyewe (Flp 2:3). Tunapaswa kuwapenda jirani zetu kama sisi wenyewe, kwa hiyo hatupaswi kumpa mtu mwingine kitu chochote ambacho kinaweza kumdhuru (kama madawa ya kulevya), hata kama akiomba. Lakini tukimwona mtu ana shida ya kweli tujitahidi kuona kuwa mahitaji yao yanatimizwa. Jambo hili ni la kweli bila kujali kwamba mtu mwenye uhitaji ni Mkristo mwenzetu au la.
Kuwapenda jirani zetu kama nafsi zetu wenyewe kuna maanisha kuwa ni jambo zuri kujipenda sisi wenyewe pia. Hata hivyo, watu wengi wana hatia ya kujipenda wao wenyewe kuliko watu wengine, kutoa pungufu ya kile wanachotakiwa, kutokujipenda kiasi cha kutosha na kutoa zaidi ya kiasi wanachotakiwa.

S: Kwenye Mat 5:43, ni wapi inaposema "Umpende jirani yako, na, umchukie adui yako"?
J: Maneno haya hayamo kwenye Agano la Kale, lakini Wayahudi walikuwa wamesikia mara nyingi kwani ilikuwa kusikia hayo kwa sababu yalikuwa ni mapokeo ya waandishi. Yesu hakusema kuwa maneno haya hayakuwa kwenye Agano la Kale kwa sababu nzuri sana: hayakuwemo humo.

S: Kwenye Mat 5:48, je tunaweza kuwa wakamilifu?
J: Kama ambavyo almasi inang’aa kwa namna tofauti toka upande tofauti, Biblia inaonyesha pande nne za suala hili. Majibu rahisi kwa swali hili pana ni: Ndiyo, Ndiyo, Hapana, na Ndiyo.
Ndiyo baada ya kufa: tunapaswa kutafakari juu ya ukweli kwamba watakatifu, wasio na dhambi mbinguni. Tunapaswa kuishi na matarajio hayo, na kama unasikitika unapofikiria kuachana na dhambi ambazo umekuwa unazifanya, basi kuna shida katika kuenenda kwako kiroho. Baada ya kufa, na baada ya kufa tu ndipo tutaweza kuufikia ukamilifu Mat 5:48.
Ndiyo kimahakama: Mungu Baba ametutangaza kuwa tumesamehewa na hatia ya dhambi imetangazwa kuwa imesamehewa kwa kifo cha Yesu msalabani. Ebr 10:17 inatuambia bayana kwamba pale msalabani Yesu "aliwakamilisha" wale wanaotakaswa. Rum 4:17 inatukumbusha kuwa Mungu wetu anayataja mambo yasiyokuwapo kana kwamba yamekuwapo. Ingawa tumefanya dhambi dhidi ya Mungu na tunastahili kwenda jehanamu, kama Mungu anatuahidi msamaha wetu na maisha yasiyo na dhambi mbinguni, ahadi za Mungu zina uhakika wa 100%. Kwa mtazamo mwingine, watu wote waliomwamini Kristo, na kifo chake na kufufuka kwake kimwili wametangazwa kufikia Mat 5:48.
Hapana hapa duniani kwa sasa, lakini bado tunajaribu: hatutakuwa wakamilifu wasio na dhambi kabisa hapa duniani, na mtu yeyote anayedhani kuwa amefikia kiwango hicho anajidanganya wenyewe kama 1 Yoh 1:8 inavyosema. Hata Paulo hakuwa mkamilifu kwa mujibu wa Flp 3:12. Ingawa hatutafikia ukamilifu wa kutokuwa na dhambi hapa duniani, bado tunatakiwa kujitahidi kuufikia ukamilifu huo na kuwa kama Yesu, ingawa hatupaswi kuvunjika moyo tunaposhindwa kufikia lengo hilo, kama ambavyo waamini wengine wote wanavyoendelea kufanya. Kwa hiyo, agizo la Yesu kwenye Mat 5:48 halikuwa ahadi tu ya mambo ya baadaye, na tangazo, bali amri amri ambayo tunapaswa kujizatiti kwa dhati kabisa kuitimiza sasa.
Ndiyo tunaweza kuwa wakamilifu kwenye mapenzi ya Mungu: Tunaweza kuwa waamini "wakamilifu", kama kwa kukamilika na kuwa mahali hasa ambapo Mungu anataka tuwe. Lakini ambavyo mtoto "mkamilifu" asivyotakiwa kubakia kuwa mtoto milele, ukamilifu hapa unamaanisha kuwa tunapiga hatua muhimu katika safari yetu ya kuendelea kuwa kama Yesu katika maisha haya. Ukamilifu hutumika kwa maana hii kwenye 1 Yoh 2:5 na Flp 3:15. Hivyo ingawa tunapaswa kujizatiti kulitii kikamilifu agizo la Mat 5:48 katika maisha yetu sasa, na ingawa tutashindwa bila shaka, bado tunaweza kuwa na furaha na amani kamilifu idumuyo kwa Mungu sasa.

S: Kwenye Mat 6:1-4, je tunapaswa kufanya matendo mema kisiri, au kufanya nuru yetu iangaze mbele ya watu kama Mat 5:16 inavyosema?
J: Vyote. Tunapaswa kuwa na bidii katika kutenda matendo mema. Hata hivyo, matendo haya hayapaswi kuwa yetu wenyewe, bali ya Yesu anayeishi ndani yetu, ili kwamba watu wayaone wanapotutazama.
Ni upendeleo mkubwa kuwa Mungu alituchagua ili kutupa utukufu kwa kutenda kupitia kwetu.

S: Kwenye Mat 6:1-4, katika kutoa sadaka kwa Mungu, je Wakristo wanawezaje kuepusha mkono wao wa kulia usijue kitu ambacho mkono wa kushoto unakifanya?
J: Kama ambavyo hatupaswi kuyakuza matendo yetu mema tunayoyafanya kwa wengine, hatupaswi kuyakuza mbele ya Mungu. Pia usivunje mkono wako kwa kujipongeza kupita kiasi. Usifikirie jinsi utakavyomfanyia Mungu mema. Usije fikiri kimakosa kuwa unamtajirisha Mungu, anayemiliki kila kitu, au jinsi Mungu alivyobahatika kukuokoa wewe. Tunaokolewa si kwa sababu ya kustahili kwetu, bali kwa sababu Mungu aliona jinsi tusivyojiweza, na kwa neema yake alitupenda.

S: Kwenye Mat 6:1-4, kwa kuwa hatupaswi kutao sadaka machoni pa watu, Wakristo wanaripoti wapi michango yao kwa taasisi zisizokuwa za kiserikali, kwa malengo ya kulipa kodi, na kwa nini wengine wameandika majina yao kwenye baadhi ya majengo au minara?
J: Mbele ya watu (uwingi) inamaanisha mbele ya kadamnasi, hivyo kutoa taarifa ya msaada ambao mtu anatoa ili kusaidia watu wengine kwa lengo la kutimiza sheria ya kodi ni SAWASAWA. Hata hivyo, kama mtu anatoa hela ili kwamba jengo au mnara upewe jina lake, hapo atakuwa amepata malipo yake hapa duniani. Lakini kama mtu anajenga mnara unaokuwa na jina la mtu mwingine, na mwenye jina ama hajui, ama hafanyi kitu chochote kuhamasisha jengo au mnara huo unapewa jina lake basi aya hii haimhusu.

S: Kwenye Mat 6:5-6, kwa kuwa tunapaswa kusali sirini, kwa nini Wakristo wengi wanataka maombi ya hadharani kwenye mashule (ya Marekani)?
J: Biblia inatoa mifano mingi ya maombi ya faragha na ya binafsi. Hata hivyo, Biblia pia inatoa mifano ya maombi ya vikundi, kama kwenye Yos 7:6-9. Watu wanaweza kuwa na maombi ya pamoja endapo watakuwa wanaogea kwa kupokezana mtu mmoja akiongea baada ya mwingine kama 1 Fal 8:22-53. Katika mifano hii ya maombi ya pamoja, kila mtu anashiriki katika kusali iwe anaongea au la.
Kwenye Mdo 16:25-26, Paulo na Sila walikuwa wanaomba na kuimba pamoja wakiwa mahali ambapo wengine waliweza kuwaona. Hata hivyo, kwa kuwa walikuwa gerezani, hawakuwa na uhuru wa kuchagua mahali pa kuombea.
Jambo ambalo hatuoni likiungwa mkono ni kuomba hadharani kwa ajili ya kuonekana, au kuomba hadharani ambapo baadhi ya watu waliopo hawakuwa wanashirki maombi, huenda kwa sababu ya kutokumwamini Mungu.

S: Kwenye Mat 6:5-7, je Yesu anayakemea maombi yote ya hadharani?
J: Hapana, aya hii haisemi hivyo. Badala yake Yesu anakemea maombi yanafanywa kwa lengo la kujionyesha tu. Ukweli ni kwamba, Yesu aliomba hadharani katika Yoh 11:41-42.
Kwenye Agano la Kale, Mfalme Sulemani aliofanya maombi ya hadharani kabisa kwenye 1 Fal 8:22. Yesu hapingi maombi ya hadhara ila anapinga maombi ya hadhara ya "maonyesho", yaani maombi yanayofanywa kwa lengo la kuonekana mbele ya watu.

S: Kwenye Mat 6:7, je tunatakiwa kurudia maombi yetu wakati wowote ule?
J: Hakuna shida kurudia maombi, ili mradi yawe na maana kwako unapoomba. Kama huombi kwa moyo, basi huna haja ya kuomba. Wakati wa kusalii au kuabudu hakuna shida kurudia maneno, kama ilivyofanyika kwenye Zaburi.

S: Kwenye Mat 6:7-8, kwa nini Wakristo wengi, hasa wa kwenye makanisa yenye mapokeo ya liturujia (Katoliki, Anglikana, Lutheran, n.k.) wanaombea karibu vitu hivyo hivyo mara kwa mara kila jumapili?
J: Jambo hili halina ubaya endapo lina umuhimu kwao kila wakati. fanyika Hii ni OK ikiwa ina maana kwao kila wakati. Yesu hakukataza kurudia maombi hapa ila marudio yasiyo na maana. Kwenye baadhi ya Zaburi, kama vile Zaburi 136, marudio yametumika. Yesu alituonya kuwa marudio yanaweza yasiwe na maana, lakini jambo hilo halimaanishi kuwa marudio yote ni batili.

S: Kwenye Mat 6:7-8, je haturuhusiwi kutumia marudio yasiyo na maana, au tuombe bila kukoma kama mjane alivyokuwa mfano wetu kwenye Luk 18:5, 7?
J: Kuomba bila kukoma hakumaanishi kuwa kuwe na kurudia rudia maneno. Unaweza kusema vitu tofauti kwenye maombi yako wakati unaposali.
Yesu hakusema kuwa kurudia maneno wakati wa kusali ni makosa, isipokuwa tu yanapokuwa hayana maana. Marudio mengine, endapo yana maana, ni sawa kufanyika. Kama kielelezo, unaweza kuangalia Zab 118:1-4. Hivyo, hakuna ubaya kwa ibada ya kanisani kutumia baadhi ya maombi na vitu vingine vya ibada vyenye kurudiwa kila wiki ili mradi tu vitu hivyo viwe na umuhimu.

S: Kwenye Mat 6:9-13 na Luk 11:1-4, Yesu alifundisha nini kuhusu Sala ya Bwana?
J: Ufuatao ni muhtasari wa mafundisho hayo:
Baba yetu: tunaomba kwa Mungu Baba. Yesu ni Mungu (Ebr 1:8-9), hivyo ni sahihi kumwomba Yesu pia, kama Stefano alivyofanya kwenye Mdo 7:59.
Uliye mbinguni: Ingawa Mungu yupo kila mahali na kila wakati, usisahau kuwa Mungu anapita mipaka/uwezo wa kibinadamu (transcendent). Kiti chake cha enzi kiko mbali sana kutoka kwetu kuliko nyota.
Jina lako litukuzwe: Usifikiri kuwa Mungu ni rafiki au mwenzi tu. Kumbuka Mungu ni nani.
Ufalme wako uje: Aina hii ya maombi inapuuziwa sana siku hizi. Mbali na Sifa/kuabudu, Kuungama, Kushukuru, na Dua kwa ajili ya mwombaji mwenyewe na watu wengine, kuna kuomba kwa ajili ya Ufalme wa Mungu kuja mara moja. Kwenye 1 Thes 4:18 tunaonyeshwa kuwa tunapaswa kuwa na shauku kubwa ya ufalme wake. Aya ambazo zinaonyesha kuwa tunatakiwa kukuangalia na kuusubiri ufalme wake ni pamoja na 1 Thes 4:18, 2 Pet 3:13 na 1 Peto 4:7.
Maneno haya hayaonyeshi fikra zisizotilia uzito. Badala yake, kwa kutumia aya tunaonyesha shauku ya dhati ya kuona ufalme wa Mungu unakuja mara moja.
Mapenzi yako yatimizwe: Tunapaswa kuomba kwa ajili ya kutimizwa kwa mapenzi ya Mungu, na si tu kutumizwa kwa haja zetu binafsi (Yakobo 4:3).
Hapa duniani kama huko mbinguni: Hatupaswi kuomba kuwa mapenzi ya Mungu yatimizwe huko mbinguni, ambako hakuna majaribu, bali kuna haja ya kuomba kuwa matakwa ya Mungu yatimizwe hapa duniani. Mbingu ni kiwango chetu cha kiasi ambacho tunataka mapenzi ya Mungu yatimizwe.
Utupe leo: Tunapaswa kuomba ili tuweze kupokea vitu tunavyovihitaji, na si tu vitu tunavyotaka kuwa navyo. Ingawa matajiri wasiomcha Mungu wanaweza kupata mahitaji yao yote kifedha na hata bila kuomba, tunatakiwa kulipuuza jambo hilo na kumwomba Mungu atutimizie mahitaji yetu. (Angalia Mit 30:7-9). Ni dhahiri kuwa hakuna mpango wa kuomba siku moja kwa ajili ya mahitaji yetu ya juma zima ili kwamba tuache kusali siku sita zinazofuata.
Mkate wetu wa kila siku: Omba kila siku kwa ajili ya mahitaji yetu. Usiombe mara moja tu kwa ajili ya mahitaji ya maisha yako yote bali omba kila siku. Ombi ambalo linatakiwa kuwa mbali na maombi yetu ni matakwa yetu na haja zetu za kibinafsi, kama Yak 4:3 inavyoonyesha. Riziki yetu ya kila siku inajumuisha maombi kwa ajili ya vitu ambavyo kweli tunavihitaji.
Utusamehe makosa yetu: Tunahitaji msamaha kwa ajili ya mambo ya nje yanayoonekana kama maneno, matendo, na kutokutenda kwetu. Lakini pia tunahitaji msamaha kwa ajili ya mambo ya ndani yasiyoonekana kama mawazo na utakaso kwa ajili ya matakwa yetu. Watu wengine husema kimakosa kuwa hatupaswi kumwomba Mungu atusamehe, mara baada ya kuwa waamini na kuwa tumeishasamehewa. Sala hii 9 (ya Bwana) inaonyesha tofauti. Yak 5:16 pia inaelekeza kumwombea muamini ili kwamba dhambi zake zije kusamehewa (wakati ujao). Msamaha wa dhambi unatokana na kifo cha Kristo msalabani, si maneno yetu yoyote, ila msamaha una wakati uliopita, uliopo, na ujao na zote hizo zimetokana na msalaba.
Kama nasi tunavyowasameha waliotukosea: Msamaha wa Mungu kwa watu wanaotubu na kugeukia kwake ni mkamilifu. Hivi ndivyo msamaha wetu kwa watu wengine unavyopaswa kuwa.
S: Kwenye Mat 6:9-13 na Luk 11:2-4, kwa nini tunasali?
J: Maombi hayalengi kumfahamisha Mungu anayejua vitu vyote, wala hayamwezeshi Mungu mwenye nguvu/mamlaka/enzi yote, wala hayaubadilishi moyo wa Mungu mwenye upendo mwingi sana. Badala yake ni amri, fursa ya kuzungumza na Mungu, na ahadi kwamba Mungu atasikia maombi yetu. Maombi yanashangaza kwani Mungu mtawala wa vitu vyote siyo tu kwamba amekubali lakini pia ameanzisha wazo la kuwa anaruhusu maombi yetu "kufaa sana" (Yak 5:16) katika kubadilisha vitu kunakofanywa na Mungu.

S: Kwenye Mat 6:14-15, je tunapaswa kusamehe makosa ya makosa ya watu wngine, au dhambi zao zote?
J: Makosa hapa inamaanisha dhambi, kwa hiyo hakuna tofauti.

S: Kwenye Mat 6:13, kwa nini tunaomba kuwa Mungu asitutie majaribuni, wakati Yak 1:13 inasema kuwa Mungu hamjaribu mtu yoyote?
J: Maana hii inawasilishwa vizuri zaidi katika namna ambayo watu wengi wa Uingereza wanavyosema hii sala: "tuokoe katika saa ya uhitaji wetu." Mungu hatujaribu, lakini huturuhusu kujaribiwa, kama Yesu alivyojaribiwa, na kama Paulo alivyojaribiwa hata akakaribia kukata tamaa kwenye 2 Wakorintho 1. Mungu hutupima, lakini haruhusu tujaribiwe zaidi ya uwezo wetu wa kustahimili (1 Kor 10:13a). Tunapojaribiwa, na kufikiri kuwa tu karibu kuvuka kiwango tunachoweza kuchukuliana nacho, tunaweza kuwomba Mungu, na atatupa njia ya kuondoka na jaribu hilo au njia ya kututia nguvu.

S: Kwenye Mat 6:16-18, je Wakristo wanatakiwa kufunga?
J: Ndiyo! Kufunga ni njia ya waamini ya kuonyesha ukubwa au upendo wao kwa Mungu.
Tunapaswa kufunga kwa ajili ya ibada (Mdo 13:2-3); kuomba msaada (Isa 58:3-9; Mdo 14:23; Zab 35:13; Neh 1:4; Est 4:3, 16; 1 Fal 21:27, Ezr 8:23), na kwa ajili ya toba ya mtu mmoja mmoja au watu kadhaa pamoja (Neh 9:1; Dan 9:3; Yoe 1:14; 2:12-15; Yon 3:5).
Hatupaswi kufunga kama desturi (Zak 7:5) au kwa ajili ya kuonekana na watu wengine (Mat 6:16-18).
Utaratibu wa kula chakula ili kupunguza unene ni mzuri, lakini huko si kufunga kwani madhumuni yake ya msingi ni tofauti. Mazoea ya kula kupita kiasi kukifuatiwa na kufunga si kitu kizuri kiafya au kimaandiko.

S: Kwenye Mat 6:19-21, kwa nini Wakristo wanamiliki hela na mali nyingine hapa duniani?
J: Kumtolea Mungu si jambo la hiari (Mal 3:10-12). Tunapaswa kutoa kwa ajili ya kazi ya Mungu (2 Kor 8:1-8; 9:6-11; Mit 3:9, 10; 11:24; 1 Kor 16:2; Tit 2:13). Ni muhimu kwetu kuwasaidia maskini na watu wengine (Mit 11:24-25; 14:21; 24:11-12; 28:22; 29:7; 31:9,20; 2 Kor 9:6-7).
Idadi kubwa ya aya za Biblia inatuambia tutoe kwa maskini na watu wengine: Mit 11:24-25; 14:21; 19:9-10, 17; 21:13; 22:9; 24:11-12; 29:7; 31:9, 20; Zab 41:1; Isa 58:7-8, 10; Yer 5:28; 22:16; Mat 6:2-4; 19:21; Gal 2:10; Efe 4:28; 1 Tim 6:18-19; Yak 1:27; Kumb 15:11; Zab 68:5; Ayu 29:12-13; 1 Yoh 3:17-19; Mdo 4:32-35.
Hata hivyo, Biblia pia inatambua kuwa utajiri unaweza kuwa baraka toka kwa Mungu, kwa mujibu wa Mit 28:20. Kwa Wakristo, ni sahihi kufanya mambo yafuatayo:
a) Kuwa na mali zako (2 Tim 4:13).
b) Kutimiza mahitaji ya familia yako (1 Tim 5:4, 8; Mit 31:13-15; Mak 7:10-13; Luk 15:18-30).
c) Kutoa kwa ajili ya watu wanaotuhudumia kiroho (1 Kor 9:4-12; 1 Tim 5:18; Gal 6:6).
d) Kutoa kwa ajili yetu sisi wenyewe (Tit 3:14).
e) Kulipa kodi zitupasazo (Mat 22:17; Romans 13:7).
f) Kuweka akiba kwa ajili ya siku zijazo (Mit 6:6-8; 10:5; 31:16; Luk 15:18-30; Tit 3:14).
g) Kuacha urithi kwa ajili ya watoto wetu (Mit 13:22; 17:2; 19:14; Zab 17:14).
h) Kutunza vitu tunavyoviiliki, jambo ambalo wakati mwingine linagarimu hela za ziada, (Mit 12:10, 11, 27). Tunapaswa kujua hali ya vitu tunavyovimiliki, kwani vinaweza kupotea kwa kukosa matunzo mazuri (Mit 27:23-24).
Lakini hatupaswi kufanya vitu hivi kwa tamaa na hofu. Kama umejiwekea bima nyingi sana kiasi kwamba utaweza kutimiza mahitaji yao vema utakapokuwa umekufa kuliko unapokuwa hai, kipaumbele chako kitakuwa na kasoro. Angalia maelezo kwenye Mit 3:9 kwa ufafanuzi wa kina zaidi juu ya mitazamo sahihi na isiyofaa ya matumizi ya hela.

S: Je Mat 6:22 inaweza kuwa inaongelea aina fulani "jicho la tatu" la kiroho kama baadhi ya wafuasi wa New Age wanavyodai?
J: Hakana Mkristo wa awali, au hata wa sasa aliyewahi kuitafsiriwa aya hii namna hii. Kama hivi ndivyo kweli ilivyomaanisha, kama watu wachache wanavyodai, basi Mungu alishindwa kuwasilisha makusudio yake kwa njia ambayo Mkristo yeyote ameweza kuelewa. Tunapotafsiri kifungu, hatupaswi kuuliza, kuwa "je naweza kukifanya kimaanishe hivi au vile", badala yake tuulize, "Mungu alikusudia kutuambia kitu gani?" Watu wengi wanauliza swali la kwanza kwa sababu kuna dhambi za kiakili na dhambi za makusudio ya moyo.

S: Kwenye Mat 6:26, kwa kuwa Mungu anawaangalia ndege wa angani kama kielelezo cha kutujali, tunaweza kutegemea msaada gani kutoka kwake?
J: Kuna mambo matano ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1. Hakuna kitu kinachotokea bila Mungu kuruhusu (Ayu 1:12; 2:6).
2. Tutakuwa na matatizo (2 Tim 3:12; Yak 1:2), lakini Mungu atatutia nguvu na kutufariji kwenye shida zetu (2 Kor 1:4-5).
3. Mungu haruhusu waamini kujaribiwa zaidi ya kiwango ambacho wanaweza kustahimili (1 Kor 10:11).
4. Baadhi ya waamini watateswa, na wengine hata kuuawa (1 Pet 1:6).
5. In thamani machoni pa BWANA mauti ya wacha Mungu wake (Zab 116:15). Hata kama tutakufa kifo cha mateso kisichokuwa cha haki, Mungu atatunza mbinguni, na mateso yetu ya wakati huu si kitu kulinganisha na furaha ya mbinguni (angalia 1 Kor 2:9).

S: Je Mat Mt 6:33 inasema kuwa tuupe kipaumbele uungu wetu wa ndani tunaodaiwa kuwa nao kama baadhi ya wafuasi wa New Age wanavyosema?
J: Hapana, hatuna uungu wa ndani. Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, na waamini (wote wanawake na wanaume) ni wana wa Mungu, lakini hatuna uungu wetu wenyewe. Aya hii haisemi chochote kuhusu uungu wetu, au kitu kingine chochote kuhusu sisi. Badala yake, inatuagiza kuutafuta ufalme Wake na haki Yake. Hakuna Mungu ila mmoja, kama ambavyo Myahudi yoyote anayeamini kuwa kuna Mungu mmoja tu atakavyo kuambia, na Yesu alikuwa Myahudi na athibitisha kuwa kuna Mungu mmoja tu wa kweli, ambaye tunapaswa kutii maneno yake. Tunapaswa kuyatii Maandiko, kuliko kuyabadilisha Maandiko ili yatii maoni yetu.

S: Kwenye Mat 7:1-2, Luk 6:37 na Yoh 7:24, twawezaje kuacha kuhukumu watu wengine kwani tumeambiwa kuhukumu kwenye Yoh 7:24, 1 Kor 5:12 na 1 Kor 6:25?
J: Biblia inaruhusu kuhukumu matendo, lakini siyo kuwahukumu watu. 1 Kor 6:5 inatumia neno la Kigiriki, diakrinai, ambalo ni tofauti na maneno mengine yenye kumaanisha hakimu. Neno hili linamaanisha msuluhishi wa kikristo anayetangaza hukumu ya shauri la madai baina ya Wakristo.
Neno la Kigiriki lililotumika kwenye mafungu mengine, krinete, lina maana kadhaa. Mat 7:1-2 na Luk 6:37 zinasema hatupaswi kuwahukumu watu wengine (kuhukumu vitu au matendo hakujaongelewa). Kwa maneno mengine hatupaswi kuongelea thamani ya watu wengine, uzuri au ubaya wa Mkristo mwingine, au ubaya wa mwenye dhambi. Mwache Mungu afanye kazi hiyo; hatupaswi kuhukumu.
Yoh 7:24 pia inatumia neno krinete ikisema, "Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki."
Ni kuongea bila umakini kuwaambia watu kuwa Mat 7:1 inakataza hukumu ya aina yoyote ile, hivyo tunapaswa kutokuitii sura nzima ya Mathayo 7. Tunapaswa kuwatambua mbwa na nguruwe (Mathayo 7:6) na tunatakiwa kuchunguza matunda kwenye Mat 7:16-20.
Kuhusu kuua watu wengine, maangamizi ya idadi kubwa ya watu (kama yale ya Wayahudi wakati wa utawala wa Nazi wa Ujermani miaka ya 1941-45) kwa moto au mabomu (Holocaust), watu kufanya ngono na wanyama na watoto, n.k., wako watu wanaoweza kusema kuwa hatupaswi kulazimisha maadili kwa watu wengine, au kimsingi tusiseme kuwa jambo fulani ni sahihi au si sahihi. Hivi sivyo Biblia inavyofundisha.

S: Kwenye Mat 7:1-5, je Wakristo hawapaswi kuhukumu au tunatakiwa kuhukumu kama 1 Kor 6:2-5 inavyosema?
J: Hatupaswi kuhukumu watu wengine, ikiwa ni pamoja na kuongelea thamani yao, lakini tunapaswa kupambanua matendo mema na mabaya kama 1 Kor 6:2-5 inavyofundisha. Ingawa baadhi ya maneno yanafanana kwenye Kigiriki (yanatokana na neno krino), mazingira yako tofauti.

S: Kwenye Mat 7:6, je Yesu alimaanisha nini aliposema msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe?
J: Usiwape watu wasio na shukrani kitu kilicho na thamani, na wanaweza kukitumia kugeuka na kukushambulia. Hii dhana ya kutotoa lulu inatokea Mit 9:7-9, ambako tunaambiwa tusijaribu kumrekebisha mtu mwenye dharau au mtu mwovu. Yesu hakufanya miujiza mingi mbele ya watu wasioamini. Pia, ni bora kwa mtu kutokuijua njia ya kweli, kuliko kuijua halafu kuipuuzia kama 2 Pet 2:20-22 inavyosema.
Hebu tuangalie tafsiri mbalimbali zinazoweza kutolewa, na kisha tuzipunguze kupata maana nzuri zaidi zinazoweza kuwa ndizo zilizokusudiwa.
Kutupa kunamaanisha:
C1. Msitupe inaweza kumaanisha msilazimishe
C2. Msisumbue kwa kutafutiza makosa ya mtu na/au kubishana mara kwa mara
C3. Usifanye juhudi yoyote ile kufundisha
C4. Uwe mwangalifu sana hata usimwambie mtu yoyote yule
Hapa kitenzi "tupa" ni kauli tendi, kwa hiyo Yesu hakumaanisha ufiche lulu zako, au usiache lulu zozote chini ardhini. Kwa sababu hiyo, C4 haina uwezekano mkubwa wa kuwa tafsiri sahihi.
Lulu inaweza kumaanisha:
P1. Mafundisho ya kiungu
P2. Ujumbe wa injili
P3. Kitu chochote chenye thamani, hasa faida kubwa, au ushirki wa kwenye vitu vitakatifu Hard Sayings of the Bible, uk.370-371 ina maoni haya.
P4. Inaweza pia kumaanisha kuwa wakati kanisa linateswa, usifanye Wakristo wenzako wafahamike bila ulazima kwa kutoa majina yao kwa mtu yeyote tu.
Yesu alitoa mafundisho ya maadili mbele ya watu wengi, hivyo neno hili huenda lisimaanishe P1.
Mbele ya nguruwe inaweza kumaanisha:
S1. Watu wasiokuwa na shukrani na mambo haya
S2. Watu wasiokuwa tayari kujifunza
S3. Watu wasioamini ambao hawaweki juhudi katiak kutaka kujifunza
S4. Watu wasioamini wanaokataa kujifunza
S5. (Ina uwezekano mdogo sana) Watu wa mataifa. Hata hivyo, Mathayo anawataja watu wasiokuwa Wayahudi walioamini, hivyo haimaanishi watu wasiokuwa Wayahudi kwa ujumla.
Nguruwe lilikuwa ni tusi, hivyo kuna uwezekano kuwa maana zilizokusudiwa zilihusisha watu wasiopenda kujifunza.
Kwa ajili hiyo, maana nzuri zaidi zinawezakuwa C1 + C2 + C3, na P2 + P3, na S1 + S2 + S3 + S4.

S: Kwa kuwa Mat 7:7-8 inasema kila aombaye hupokea na kila atafutaye huona, kwa nini watu kwenye Amo 8:12 wanalitafuta neno lakini hawalipati?
J: Kwa tungalie mambo ambayo si jibu kisha jibu.
Kitu ambacho si jibu: Yesu alisema maneno haya karne kadhaa baada ya Amosi, na kwenye kipindi cha Agano Jipya mambo yalikuwa tofauti na jinsi yalivyokuwa nyakati zilizotangulia. Pia, kulikuwa na kipindi cha miaka 400 ya ukimya, kilichotangulia kuja kwa Kristo, ambapo Maandiko hayakutolewa. Hatimaye, ufahamu ambao Yesu alitupa hakuwepo hata kwa watu waliokuwa wanamcha Mungu waliouishi kabla ya kuja kwa Yesu. Lakini ingawa maelezo haya matatu ni ya kweli, hayaendani na ukweli usiofungwa na muda, na onyo, ambavyo ndilo wazo kuu la Amo 8:12-14.
Jibu: Kuna viwango vitatu vya jibu la swali hili.
Kibayana, Amo 8:12-14 inaongelea watu (wengi wao wakiwa Wasamaria) walio kwenye nchi [ya Israeli] walioabudu miungu mingine ya ufalme wa kaskazini pamoja kumwabudu Mungu. Kwa kadri walivyojaribu kufuata wote, yaani Mungu na miungu mingine, hawakuweza kulipata neno la Mungu.
Kwa ujumla, Amo 8:12-14 ni onyo kwa watu wote. Mat 7:7-8 hailengi kumuuliza mtu yoyote tu; ina lenga kuwa umuulize Mungu mmoja wa kweli. Kama unapenda kuchanganya ukweli wa Mungu na uongo wa sanamu na dini nyingine, utakuwa na janga la njaa ya ukweli, siyo ukweli unaotosheleza. Unapaswa kumtafuta Mungu kwa moyo wako wote, si kumtafuta kwa sehemu ya moyo wako huku sehemu nyingine ya moyo wako ikitafuta sanamu.

S: Kwenye Mat 7:7-11, kwa nini watu hawapati kila kitu wanachotaka?
J: Mungu ni zaidi sana ya Santa Claus wa ulimwengu wote. Watu huwa hawapati vitu wanavyotaka kwa sababu zisizopungua tano:
1. Hawombi kwa ajili ya matakwa (Yak 4:2)
2. Wanatakiwa kumwomba Mungu, si miungu wengine
3. Wanatakiwa kuomba kwa Roho na jina la Yesu (Kol 3:17; Yoh 14:13-14; 15:16; 16:26)
4. Mungu hasikii maombi ya waovu (Mit 15:29; 1 Pet 3:12; Isa 1:15; Yer 11:14; 14:12; Mik 3:4)
5. Wanagombana na watu wa Mungu (Zab 18:41. 1 Sam 22:16-17; 28:6)
Angalia pia majibu ya swali linalofuata kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Mat 7:7-11, kwa nini Wakristo mara nyingi hupata vitu wanavyoomba kwa Mungu kwa kutumia jina la Yesu?
J: Mungu hujibu baadhi ya maombi kwa kusema "ndiyo", mengine "hapana" na mengine "ngoja." Panapokuwa hakuna jibu, au jibu ambalo hulipendi, ni vema kujiuliza kuwa kwa nini imekuwa hivyo. Hatuwezi kujua sababu inayohusika na majibu ya kila ombi, lakini kwa ujumla kuna sababu zisizopungua 21 zinazohusika na sisi wenyewe, mazingira, na Mungu.
Sisi wenyewe:
1. Kumwomba Mungu asiye sahihi, sanamu (1 Fal 18:26-29
2. Vitu vinavyoombwa visiwe na lengo la kutumika kutimiza tamaa zetu wenyewe (Yak 4:3)
3. Maombi yanatakiwa yawe ya vitu vizuri (Mat 7:11)
4. Si mapenzi ya Mungu kuwa tupate vitu tulivyoomba (Mak 14:36)
5. Tunatakiwa kusibiri (Dan 10:12-14)
6. Maombi yetu ni marudio rudio yasiyokuwa na maana (Mat 6:7)
7. Hata hivyo tunapaswa kuendelea kuomba [kwa kudhamiria] (Luk 11:5-10, 18:1-7)
8. Tunatunza dhambi mioyoni mwetu (Zab 66:18-19), au tumekuwa waovu (Mit 15:29). Mungu hatusikii tunapochagua kutokumsikia Yeye (Zak 7:11-14)
9. Tunahitaji kuwa na kiasi (1 Pet 4:7)
10. Tumefanya dhambi, kama vile kuachana na wenzi wetu (Mal 2:13-14)
11. Tunampuuzia Mungu na sheria yake (Zak 7:13; Mit 28:9)
12. Tumepuuzia kilio cha maskini (Mit 21:13)
13. Hatuzingatii mahitaji ya wake zetu (1 Pet 3:7)
14. Mungu hatatusikia endapo tunaendelea kuabudu sanamu pia (Eze 8:8-18)
15. Mikono yetu imejawa na damu (Isa 1:15)
16. Mungu anajua ni aina gani ya majaribu inayotufaa zaidi (2 Kor 12:7-9)
17. Mungu anatuadhibu (2 Sam 12:16-18; 22-24)
Mazingira:
1. Kwa wakati wake, Mungu ataweza kutupa jibu la maombi yetu, lakini wakati bado haujafika kwa sasa (Hab 2:3)
2. Inawezekana kuwa tunahitaji kubadilika kwa namna fulani, au mtu mwingine anatakiwa kubadilika (1 Sam 1:10-12; Kut 2:23-24)
Mungu:
1. Mungu anaweza kuwa anajibu maombi yetu kwa kusema "hapana"
2. Mungu anaweza kuwa anaruhusu tujaribiwe.
Wakati mwingine, kama Ayu 10:2-3, 12-14 na Dan 10:2-3, 12-14 zinavyoonyesha, hatufahamu vitu vyote vinavyoendelea vyenye kuathiri mambo kisirisiri. Lakini tunajua kuwa uvumilivu na kuendelea kwetu kuomba vinamletea Mungu utukufu.

S: Je Mat 7:20 inatueleza kuonyesha kundi lipi la kidini ni dini ya kweli?
J: Ndiyo na hapana. Kwenye kila dini kuna watu wanaodai kuwa yao ndiyo dini ya kweli lakini hawafuati kile inachoagiza. Kuna Wakristo, Waislam, Wahindu, n.k. wenye kufuata dini hizo kama utamaduni tu. Kifungu hiki kinasema kuwa kinamwongelea mtu mmoja mmoja, hasa walimu wa uongo. Hivyo basi aya hii ni inafaa kutumika kwa waasisi wa dini au madhehebu.

S: Je Mat 7:24-29 inaonyesha kuwa wale tu wanaotambua "uungu wao wa ndani" unaodaiwa kuwepo ndio wanaoweza kustahimili dhoruba za maisha kama Spangler na wafuasi wengine wa New Age wanavyosema?
J: Hapana, angalia jibu la Mat 6:33. Katika kifungu hiki, uungu wetu hauongelewi; wafuasi wa New Age (harakati pana inayotafuta namna tofauti na zile za Kimagharibi yenye kukazia mambo ya kiroho, miujiza, kuchukulia vitu kiujumla na utunzaji wa mazingira) wanaweka maana hii kwenye kifungu hiki. Badala yake, suala linaloongelewa hapa ni endapo maisha yetu (nyumba yetu) yamejengwa juu ya msingi wa Mungu au mchanga.

S: Kwenye Mat 8:2, kwa nini mgonjwa wa ukoma aliuliza swali kwa namna hii?
J: Mgonjwa wa ukoma alitilia shaka uwezo wa Yesu wa kumponya. Mgonjwa wa ukoma hakuwa na uhakika kuwa Yesu anapenda kumponya.

S: Kwenye Mat 8:4, kwa nini mgonjwa wa ukoma alitakiwa kutoa dhabihu kama ushuhuda kwa makuhani?
J: Kutoa dhabihu kulikuwa ushahidi wa kuwaonyesha makuhani kuwa Yesu alikuwa anaendelea kufuata sheria.
Baadaye, baadhi ya mafarisayo walikuja kuwa Wakristo, kwa mujibu wa Mdo 15:5. Pamoja na makosa yao mengi, wengi wa mafarisayo bado walikuwa na maadili ya kulishika neno la Mungu kwa umakini, na kuamini mambo ambayo Mungu amesema kuhusu kufufuka na maisha baada ya kufa.

S: Kwenye Mat 8:5-13, je akida alikwenda yeye mwenyewe kwa Yesu au aliwatuma watu wengine kama Luk 7:1-10 inavyosema?
J: Kuna majibu mawili yanayoweza kutolewa.
1) Akida aliwatuma watu wengine kabla kisha akaja yeye mwenyewe.
2) Wakati akida "alipokuja", usemi huu haumaanishi kuwa ni lazima awe amekuja yeye mwenyewe. Kwa mfano, wakati Yoh 19:1 inasema kuwa Pilato alimpiga Yesu mijeledi, usemi huo haumaanishi kuwa Pilato alifanya hivyo kwa mikono yake mwenyewe.

S: Kwenye Mat 8:10 na Luk 7:9, kwa nini Yesu alishangazwa na akida?
J: Yesu alistaajabishwa na utofauti aliouona. Akids hakuwa Myahudi, na hakuwa amelelewa kwenye sheria (ya Kiyahudi) maisha yake yote, lakini alikuwa na imani kubwa kuliko Wayahudi wengi. Kuwa na imani hakutokani na mazingira na malezi yako tu.

S: Kwenye Mat 8:12, je kulia na kusaga meno kunaongelea mateso ya muda au ya milele?
J: Aya yenyewe haisemi. Hata hivyo, katika sehemu nyingine "kulia na kusaga meno" hakumaanishi maumivu makubwa tu bali pia heshima, faida kubwa, na furaha iliyopotea milele, hivyo msemo huu unaweza kuwa unamaanisha hukumu ya milele.

S: Kwenye Mat 8:12; 22:13 na 25:30, je jehanamu ni mahali penye giza au moto kama kwenye Ufu 20:14; Mk 9:48?
J: Vyote. Kwanza nitatoa jibu fupi kisha jibu refu.
Jibu fupi: Moto huu si moto wa kidunia, na Mungu anaweza kuufanya moto huu uwe namne yoytote atakayo. Mungu anaelezea kwetu ambacho hatujawahi kukiona hata siku moja hapa duniani, na ingawa hatujui ni kwa jinsi gani moto wa jehanamu unafanana au kutofautiana na moto wa hapa duniani, kuna kufanana kwa kiasi cha kutosha kumfanya Mungu autumie kama sitiari.
Jibu refu: Kisayansi moto ni mng’aavu kwa sababu unatoa chembechembe za mwanga kwenye spektra (mpangilio maalum wa taswira zinazotokana na miali ya mnururisho) inayoonekana (nyekundu hadi ya zambarau). Ina moto kwa sababu inatunururisha na chembechembe za mwanga kwenye sehemu nyingine za spektra pia, hasa miali isiyoonekana (chini ya upinde) toka kwenye moto, wakati mwanga wa jua kupitia kwenye anga una miali isiyoonekana kwa macho. Je unaweza kukielezaje kitu ambacho kina kinatoa karibu eksirei (x-rays) au miali gamma (gamma rays) tu? Kitu cha aina hii kinaweza kukaanga vitu vingine haraka zaidi, lakini kingeonekana cheusi kwenye macho yanayoonekana. Kama chembechembe za mwanga zingetoka, nyota ya nutroni ingetoa nyingi ya nguvu zake kama nutroni ambazo bomu la atomiki linazitoa, lakini kungekuwa giza endapo kungekuwa na chembe chache za mwanga. Sasa hatujui kama jehanamu ina moto kwa sababu ya chembechembe za mwanga, nutroni, au kitu kingine, lakini mambo haya yanayoweza kuonekana hapa ulimwenguni yanaonyesha tu kuwa kuna namna nyingi ambazo giza na moto vya jehanamu vinaweza kufanana.

S: Kwenye Mat 8:13, je msemo huu una umhimu gani hapa?
J: Hakuna sehemu ilipoandikwa kuwa Yesu alisema maneno kama haya kwa mtu mwingine yeyote yule. Akida alikuwa na imani kubwa namna hii, kiasi kwamba Yesu akamwambia hivi na binti yake alipona.

S: Kwenye Mat 8:14, kwa Petro alikuwa ameoa je jambo hilo linaonyesha kuwa desturi Kikatoliki inayozuia mapadri kuoa si sahihi?
J: Kwa kuongea kama Mkristo wa madhehebu ya Kiprotestanti, aya hii haithibitishi wala kukanusha desturi hii. Petro alioa kabla hajawa mwanafunzi wa Yesu. Kwa maana hiyohiyo, pamekuwepo na mapadri wa Kianglikana katika karne ya ishirini waliobadili dhehebu na kuwa Wakatoliki, na kanisa Katoliki liliwaruhusu waendelee kuwa mapadri wa Kikatoliki waliooa na kuendelea kwenye ndoa zao kama hapa awali.

S: Kwenye Mat 8:20 na kwingineko, je kuna uwezekano kuwa Yesu alikuwa anamwongelea mtu mwingine aliposema kuwa yeye alikuwa ni "Mwana wa Adamu"?
J: Hapana, Mak 14:41b inaonyesha kuwa Yesu alikuwa anaongea kuhusu yeye mwenyewe. Katika bustani ya Gethsemane, kabla ya kukamatwa kwake, kwenye Mat 14:41b, Yesu alisema, "Laleni sasa, mpumzike; yatosha, saa imekuja; tazama, Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwao wenye dhambi. Ondokeni, twendeni zetu; tazama, yule anayenisaliti amekaribia."

S: Kwenye Mat 8:20 na kwingineko, kwa nini Yesu alikuwa akijiita Mwana wa Adamu?
J: Mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1) Yesu alifikiri kuwa msemo huu ulikuwa muhimu sana. Yesu alitumia msemo huu mara 32 kwenye Injili ya Mathayo, mara 14 kwenye Marko, mara 26 kwenye Luka na mara 12 kwenye Injili ya Yohana.
2) Wakati jina la heshima "Mwana wa Mungu" linatumika kusisitiza uungu wa Yesu "Mwana wa Adamu" linasisitiza pia uanadamu mkamilifu wa Yesu. Lakini kama ambavyo Mwana wa Adamu inamaanisha uanadamu mkamilifu wa Yesu, Mwana wa Mungu inasistiza uungu mkamilifu wa Yesu.
3) Dan 7:13-14 inaongea kinabii kuhusu Mwana wa Adamu. Yesu huenda alitaka warudi nyuma na kusoma kifungu hiki. Inasema, "Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, wamtumikie mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa."

S: Kwenye Mat 8:21-22, kwa nini Yeus alimwambia mtu mmoja waahe wafu wawazike wafu wao?
J: Yesu alikuwa akisema kulikuwa na watu wengi waliokuwa wamekufa kiroho wanaoweza kuwazika watu wanaokufa, na usishikwe na vitu visivyokuwa na umuhimu wa milele.

S: Kwenye Mat 8:24-25, Yesu aliwezaje kulala wakati wa dhoruba kubwa namna hii?
J: Kuna mambo mawili yanayowezekana hapa.
Jambo la kawaida: Yesu alikuwa amechoka baada ya kuhubiri na alilala fofofo. Wakati ule hakukuwa na maikrofoni au vifaa vya kupazia sauti, hivyo mtu aliyekuwa anaongea na kundi la watu alilazimika kusema kwa sauti kubwa sana. Kumbuka pia kwamba Yesu hakuwa na wasiwasi wa kufikia ng’ambo ya pili ya ziwa. Kama Yesu aliweza kulala kama kawaida kwenye mashua ndogo, basi atakuwa alilala wakati kuna mawimbi makubwa na upepo.
Jambo lililo zaidi ya kawaida: Kama mawimbi yalikuwa makubwa sana kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kulala, huenda basi Mungu Baba aliruhusu Yesu apatwe na usingizi mzito sana ili apime imani ya wanafunzi ya uwezo wa Mungu kumtunza Yesu salama.

S: Kwenye Mat 8:28, je kulikuwa na watu wawili waliokuwa na mapepo kwenye nchi ya Wagerasi, au mtu mmoja tu kwa mujibu wa Mak 5:1-4; Luk 8:26-33?
J: Ingawa inawezekana kuwa haya yalikuwa matukio mawili tofauti, kuna uwezekano mkubwa zaidi kuwa hili lilikuwa ni tukio moja, na palikuwa na hitilafu ya uandikaji kwenye Injili ya Mathayo. Papias, mwanafunzi wa Mtume Yohana, aliandika kuwa Mathayo aliandika Injili yake kwa mara ya kwanza katika Kiebrania/Kiaramu. When Critics Ask, uk.337 inaongeza kuwa kama kuna watu wawili, basi taarifa zote mbili ni sahihi, kwa sababu kuna kanuni ya msingi sana ya hisabati isemayo, "panapokuwa na vitu viwili, lazima kuwe na kimoja. Kila wakati!" Tungewezakuwa na tatizo kama Marko na Luka wangekuwa wamesema kulikuwa mtu mmoja tu, lakini neno "tu" halipo hapa.

S: Kwenye Mat 8:28, je ni mji gani uliokuwa karibu na mtu aliyekuwa amepagawa mapepo?
J: Unaweza kuwa ama Gadara au Gerasa. Ugumu unakuja kwa vile kuna miji mitatu yenye majina yanayofanana. Zaidi ya hapo, kama taarifa hii iliandikwa toka kwenye lugha ya Kiebrania, herufu za Kiebrania "r" na "d" zinzfanana sana.
X Gerasenes (wa Gerasa) (mji wa sasa wa Jerash) ni mji ulioitwa kwa jina hilo. Hata hivyo upo maili 30 (km 48) kutoka kwenye Bahari ya Galilaya kwa hiyo hauwezi kuwa ndio mji ulioongelewa hapa. Jina hili lipo kwenye maandiko ya Kiitaliki, Vulgate, kwenye nafasi ya kandoni (siyo maneno halisi ya mwandishi) ya Kisiria cha Harclean, na Kisahidi (lahaja ya Kimisri).
Gadarenes (wa Gadara) ulikuwa maili 5 hadi 8 kusini mashariki mwa Bahari ya Galilaya, Wagerasi (ya Gadara) alikuwa tu 5-8 maili (km 8 hadi 13) ya kusini ya Bahari ya Galilaya, na "nchi ya Wagadari" iliifikia Bahari ya Galilaya kama ilivyothibitishwa na kutajwa kwake na Josephus na sarafu ya Gadara inayoonyesha meli. Maandiko ya Biblia ya Vaticanus, nakala ya Ephraem Rescriptus, na baadhi ya nakala za Diatessaron yanataja mji huu.
Gergesenes (wa Gergesa) ni mji uliotajwa kwenye maandiko mengi. Upo kwenye pwani ya mashariki ya Bahari ya Galilaya.
X Gaxarenes umetajwa kwenye Siniaticus ya awali tu, ingawa hakukuwa na mji wa Gaxara. Huku ni kukosea tahajia kwa dhahiri, na mwandishi wa baadaye alisahihisha katika maandiko ya Sinaiticus kuwa Gergasenes.

S: Kwenye Mat 8:29, mapepo yalimaanisha nini waliposema "kututesa kabla ya muda wetu"?
J: Mapepo yalijua kuwa yatatupwa kuzimu (Yuda 6; Ufu 20:1-2) na baadaye kwenye ziwa la moto (Ufu 20:14-15).

S: Kwenye Mat 9:2-6, kuna makosa gani Yesu kusamehe dhambi?
J: Watu wamemkosea Mungu, na wana mawazo sahihi kuwa Yesu angekuwa Mungu endapo angesamehe dhambi. Angalia kuwa Yesu hakusema "Mungu ameniruhusu au kunithibitisha kuwa dhambi zako zimesamehewa." Badala yake, Yesu alitamka tu, "Umesamehewa dhambi zako."

S: Kwenye Mat 9:12, Yesu alimaanisha nini aliposema wagonjwa wanahitaji tabibu?
J: Watu wote ni wagonjwa, lakini ni wale tu wenye kutambua kuwa wao ni wagonjwa humtafuta daktari.

S: Kwenye Mat 9:13, kwa nini Yesu alisema kuwa Mungu anahitaji rehema siyo sadaka?
J: Yesu ananukuu Hos 6:6. Kama ilivyokuwa wakati wa Hosea, baadhi ya viongozi wa kidini wakati wa Yesu hawakujali watu wengine, na walijali zaidi kuwa na watu wa "aina sahihi." Yesu alijishughulisha zaidi na watoza ushuru na wenye dhambi waliopotea, na akawakemea kwa kutotambua kuwa watu wote ni wenye dhambi mbele ya Mungu, na hawakuwa na sababu ya kujisikia kuwa bora kuliko wenye dhambi wengine. Waandishi na Mafarisayo walionyesha mioyo yao kwa sababu hawakuwahi kumtuhumu Yesu kuwa mtoza ushuru au mwenye dhambi, lakini kwa kujihusisha nao.

S: Kwenye Mat 9:14, kwa nini wanafunzi wa Yesu hawakufunga?
J: Yesu hakusema kuwa wanafunzi wake hawatafunga hata siku moja, bali hawakuhitaji kufunga wakati Yesu alipokuwa angali pamoja nao katika mwili. Kwa madhumuni sahihi ya kufunga, angalia maelezo ya Mat 6:16-18.

S: Kwenye Mat 9:16-17 na Mak 2:21-22, wazo kuu la mifano ya mavazi na viriba ni lipi?
J: Hata katika ulimwengu wa kawaida mtu hawawezi akahamia kwenye kitu kingine polepole kila wakati. Wakati mwingine unahitaji "kuvunja mazoea", kubadilisha mitizamo, au kuanza upya. Kitu ambacho Yesu alikuwa anasema hapa ni kukubali mafundisho yake, mabadiliko yalikuwa makubwa na ya haraka sana, unatakiwa kuzaliwa upya (Yoh 3:5-7) na kuwa kiumbe kipya (2 Kor 5:16-17). Angalia pia maelezo ya Mak 2:21-22.

S: Kwenye Mat 9:20-22 na Mak 5:27-34, kwa nini Yesu hakumwita mbele ya watu mwanamke aliyekuwa anatoka damu?
J: Uponyaji wa mwili haukuwa sababu ya kuja kwa Yesu ulimwenguni. Yesu alikuwa na haja na imani ya huyo mwanamke kuliko maradhi ya mwili mwake. Kama mmoja mchungaji alivyotoa maoni ya kuchekesha kuhusu muujiza huu uliofanywa mbele ya watu,"Mwisho wa kamba yetu ndio upindo wa joho la Yesu."

S: Kwenye Mat 9:20-22 na Mak 5:27-34, je kiasi cha imani tunachokuwa nacho kinasababisha maombi yetu kujibiwa au kutojibiwa?
J: Ni moja ya vigezo. Kwa maombi yaliyo katika mapenzi ya Mungu, tunahitaji kuwa na imani wakati tunapoomba. Yak 1:6-7 inasema kwamba tunapaswa kuomba bila kuwa na mashaka kwa sababu mtu wa nia mbili hawezi kupata kitu anachoomba. Hata hivyo, kama tunaamini lakini bado tukawa na mashaka kiasi, tunaweza kuomba huku tukitambua kwa wazi kabisa kutokuamini kwetu kama mtu aliyefanya hivyo kwenye Mak 9:24, na Mungu atayaheshimu maombi yetu. Ni vizuri pia kujua kuwa Roho Mtakatifu hutuombea kama Rum 8:26-27 inavyosema.
Kwa hakika, hata kama tutaomba kitu huku tukiwa na imani kubwa kuliko mtu yeyote aliyewahi kuomba kitu chochote kile, na si mapenzi ya Mungu kutupata, basi Mungu hatatupa kama Yak 4:3 inavyosema. Hii ni sehemu ya swali kubwa: wakati gani Mungu anajibu sala, na wakati gani Maandiko yanasema kuwa hajibu. Tazama maelezo ya Mat 7:7-11 kwa ufafanuzi zaidi.

Angalia makala ya Injili kwa maswali kuhusu binti wa Yairo.

S: Kwenye Mat 9:28-31, kwa nini watu hawa wawili wasioona, waliokuwa na imani kwa Yesu hawakuwa na utiifu wa kuwafanya wajiepushe na kutanga kiponywa kwao kwa watu wengine?
J: Hili ni jambo la kuvutia. Hawa watu walikuwa na imani kumgeukia Yesu, wakati hapakuwa na njia nyingine. Hata hivyo, ingawa walimgeukia Yesu kwa imani katika mambo makubwa, hawakumtii katika jambo hilo dogo. Huenda walidhani kuwa kutangaza tukio hili wakati huu kungekuwa kwa manufaa, na kwa kujiamini walidhani kuwa wanajua zaidi jambo lililo na manufaa kuliko Yesu.

S: Kwenye Mat 9:38, je tunapaswa kuomba kwa ajili ya watendakazi kwenye mavuno wakati huu wa sasa?
J: Ndio, hili ni ombi ambalo linapuuziwa mara nyingi.

S: Kwenye Mat 10:1, je wanafunzi waliweza kuponya kabla ya agizo hili?
J: Bila kujali kama waliwahi kuponya baadhi ya magonjwa kabla ya agizo hii, hapa Yesu alikuwa anawapa mamlaka juu ya magonjwa yote.

S: Kwenye Mat 10:4 na Mak 3:18, Simoni Mkananayo angewezaje kuwa miongoni mwa wanafunzi wa Yesu kwani [inadaiwa kuwa] hakuwa Myahudi?
J: Endapo Simoni hakuwa Myahudi kabisa au kwa sehemu hilo si jambo la msingi. Yesu angeweza kuita wanafunzi kutoka taifa lolote lile. Kama jambo la ziada, watu wengi kutoka katika miji ya wamataifa ya Tiro na Sidoni walikuja kumuona kwenye Mak 3:8. Tiro ilikuwa karibu maili 35 (km 56) kutoka kwenye Bahari ya Galilaya, na Sidoni ilikuwa maili 25 (km 40) kutoka Tiro.
Hata hivyo, neno la Kigiriki Kananaios linaweza kuwa ni maandishi yanayofuata herufi zenye kufanana zaidi toka kwenye neno la Kiaramu qan’an ambalo linamaanisha mkereketwa au mwanachama wa dhehebu la kale la Kiyahudi lililokuwa na lengo la kuleta utawala wa Mungu kupitia kwa makuhani na liliwapinga Warumi hadi mwaka 70 BK.Luk 6:15 inamwita "Simoni Mzelote."

S: Kwenye Mat 10:4; Mak 3:19; Luk 6:16 na Yoh 6:71, "Iskariote" inamaanisha nini?
J: Kuna maoni mawili:
1. Iskariote iliweza kumaanisha "mtu wa sime."
2. Iliweza kumaanisha mtu (ish) kutoka Kerioth, ambao ulikuwa ni mjii katika nchi ya (kabila la) Yuda.

S: Kwenye Mat 10:5-6, kwa nini Yesu alitoa amri dhahiri kabisa kwa wanafunzi wake kuwa wasiende kwenye vijiji vya Wasamaria?
J: Hii lilikuwa ni suala la muda wa kwenda, kwani Yesu alitumwa kwanza kwa Waisraeli, kisha ulimwenguni kote. Mitume wa kwanza walienda Uyahudi, kisha Samaria, na baadaye kwenye miisho ya nchi. Wakati Paulo alipokuwa anaenda kwenye mji mpya, naye pia ilifuata mfumo wa kuhubiri kwanza kwenye sunagogi. Katika mambo mengi leo kunaweza kuwa na majira ambayo Mungu anataka tuyafuate pia.

S: Kwenye Mat 10:5-6, je madai ya Waislam wa madhehebu ya Ahmadiyya kuwa watampa $20,000 mtu yeyote atakayeweza kuthibitisha kuwa Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote na si Wayahudi peke yao?
J: Biblia, kuanzia Agano la Kale hadi Ufunuo, ina ujumbe ule ule mmoja kuwa Yesu ni Mwokozi wa watu wote, si Wayahudi tu. Fikiria kwa sekunde moja kuwa ujumbe wa Yesu haukuwa kwa watu wa mataifa mengine. Je ungeweza kuwaambia Wakristo wote karibu nusu milioni wa karne tatu za kwanza baada ya Kristo, "hamtakiwi kuyafuata mafundisho ya Yesu; Mungu anataka mrudi kuziabudu sanamu zenu za kipagani" - bila shaka hungefanya hivyo, ni upuuzi! – kama lilivyo swali hili. Lakini hebu tuchunguze jambo hili kwa kina.
Kwa upande mmoja, tunaweza kutofautisha kati ya huduma ya Yesu kabla ya kusulubiwa kwake, ujumbe wa Yesu, na Yesu baada ya kufufuka kwake. Lakini katika sehemu hizi zote tatu, Yesu hakuwa wa Wayahudi tu. Wakati wa huduma yake hapa duniani, Yesu mwenyewe alikwenda kwa sehemu kubwa (lakini si huko tu) kwa "kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli" (Mat 15:24). Alitangaza wokovu wake kwanza kwa sehemu kubwa kwa Wayahudi. Lakini pia:
a) Agano la Kale lilitoa unabii kuwa Yesu alikuwa wa watu wote
b) Yesu alienda kwa Wasamaria, ambao walikuwa nusu-Wayahudi
c) Yesu alikuwa wa watu wa mataifa (wasio Wayahudi) pia, hata alisafiri kwenda kuwaona watu wa mataifa mengine nje ya Israeli
d) Yesu alisema ujumbe wake ulikuwa kwa ajili ya watu wote, si tu taifa la Wayahudi
e) Yesu hakuwahi kusema kuwa injili yake ilikuwa kwa ajili ya Wayahudi tu
f) Mwisho mitume wa Yesu mitume walikuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuelewa mambo ambayo Yesu alifundisha.
Ufuatao ni ushahidi.
a) Mungu kwenye Agano la Kale alisema Masihi atakuwa kwa ajili ya watu wote
Isa 9:1-7 ni unabii maarufu sana wa Masihi. Kwenye Isa 9:1b inasema, "lakini zamani za mwisho ameifanya kuwa utukufu, karibu na njia ya bahari; ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa."
Isa 42:1-9 ni unabii wa unaomhusu Masihi. Isa 42:6-7 inasema, "Mimi, BWANA, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa [watu wa mataifa]; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa walee walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa."
Isa 49:1-7 pia ni kifungu kinachomhusu Masihi, lakini angalia hasa Isa 49:6 "asema hivi, ‘Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia."
b) Yesu alikwenda kwa Wasamaria waliokuwa nusu Wayahudi
Kwenye Yoh 4:1-42 Yesu alihibiri si tu kwa mwanamke aliyekuwa kisimani, lakini pia Wasamaria wengine hapo kijijini. Wasamaria walimwomba Yesu abaki kwao kwa hiyo Yesu akakaa nao siku mbili. "Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake. Wakamwambia yule mwanamke, ‘Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu.’"
Lakini Luk 17:11-18 inaonyesha kuwa Wasamaria walikuwa wanachukuliwa kuwa wageni na si Wayahudi.
c) Yesu aliwatembelea watu wa mataifa waliokuwa mashariki na kaskazini mwa Israeli
Mak 7:24-30 Yesu alikwenda kwenye ukanda wa Tiro (Foinike, kaskazini mwa Israeli) na alimponya binti wa mwanamke mmoja. Mwanamke huyu hakuwa Myahudi anayeishi nje ya Israeli. Badala yake maneno ya Mwinjilisti yanasema wazi kabisa kuwa alikuwa Myunani (Mgiriki) mwenye asili ya Kisirofoinike. Kwa kuwa madai yalikuwa kwamba Yesu akuja kwa ajili ya Wayahudi tu, na si kwa Wayahudi kwa kiasi kikubwa, kifungu hiki peke yake kinathibitisha kuwa madai ya kwamba Yesu alikuja kwa ajili ya Wayahudi tu si ya kweli.
Mat 8:28-34 Yesu aliwaponya Wagerasi wawili waliokuwa wamepagawa pepo. Nchi ya Wagerasi ilikuwa upande wa mashariki wa Bahari ya Galilaya, kwenye mkoa ulioitwa Dekapoli uliokuwa na wa watu wasiokuwa Wayahudi wenye kuzungumza Kigiriki na kufuga nguruwe. Tazama pia Mak 5:1-20 na Luk 8:26-39. Kama mwanamke Msirofoinike, watu hawa waliotokea kuwepo hawakuwa Wayahudi. Yesu alikwenda kwa makusudi kabisa nje ya Israeli kuhubiri na kutoa ujumbe wake wa wokovi kwa watu hawa ambao hawakuwa Wayahudi.
Mak 7:31-37 Yesu alifanya muujiza mbele ya watu huko Dekapoli, jina la Kigiriki linalomaanisha "miji kumi." Ulikuwa ni mkoa wa walowezi wa Kigiriki kwenye nchi za Syria na Yordani za sasa; hakuna sehemu ya Dekapoli iliyokuwa Israeli.
Mak 8:1-10 Baada ya kuulisha umati wa watu elfu tano Israeli, Yesu aliivuka Bahari ya Galilaya, upande wa mashariki uliokuwa unakaliwa na watu wa mataifa, ambako aliwalisha watu elfu nne. Sehemu hii pia ilikuwa Dekapoli, miji kumi ya wakoloni wa Kigiriki.
d) Injili ya Yesu ilikuwa kwa ajili ya watu wa mataifa yote
Yesu aliwaambia wanafunzi wake kueneza ujumbe wake kwa "mataifa yote", si taifa la Wayahudi tu.
Luk 24:45-47 "Ndipo [Yesu] akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, ‘Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake toba na ondoleo la dhambi, kuanzia tangu Yerusalemu.’" Kifungu hiki hakisemi "kwenye mataifa yote", bali "kwa mataifa yote."
Mat 28:18-20 "Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, ‘Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.’" Kifungu hiki hakisemi "mkawafanye wanafunzi kwenye mataifa yote" bali "mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu."
Mat 8:11-12 Baada ya kumponya mtumishi wa akida Yesu alisema, "Nami nawaambieni, ya kwamba wangi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno." Tazama pia Luk 7:1-10 kwa maelezo zaidi ya akida na Luk 13:28-30 kwa maelezo zaidi ya wengine watakaoshiriki kwenye karamu. Yesu HASEMI tu kwamba Wayahudi watakuja kutoka nchi nyingine, kwa sababu wana wa ufalme ni Wayahudi, na wasio wana wa ufalme kutoka mashariki na magharibi watakuja.
Mak 3:7b-8 "Kutoka Galilaya, na Uyahudi, na Yerusalemu, na Idumaya, na ng’ambo ya Yoedani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu, waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea." Ikiwa mtu yeyote angejaribu kusema kuwa ilikuwa ni Wayahudi tu toka sehemu hizi waliokwenda, (ama vinginevyo hoja ya kuwa "Wayahudi tu" inakwama), mahubiri ya Yesu kwa mwanamke Mgiriki wa Kisirofoinike huko Tiro yanapingawazo hili.
Luk 2:32 Wakati Yesu alipokuwa mtoto mchanga, nabii Simeoni alitabiri kuhusu Yesu akisema kuwa atakuwa "Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa na kuwa utukufu wa watu wako Israeli." Wakati kishazi cha mwisho kinaonyesha kuwa Yesu alikuja kwa ajili ya Wayahudi pia, kishazi kilichopigiwa mstari kinaonyesha kuwa Yesu alikuwa "ufunuo" kwa Mataifa, na Mataifa si Wayahudi.
Luk 3:14 Askari wa Kirumi walimuuliza Yesu wafanyeje (ili waweze kutoa matunda yapasayo toba), na Yesu aliwaambia wasimdhulumu mtu, wala kumshitaki mtu kwa uongo na kuwa watosheke na mishahara yao. Kwa nini Yesu aliwaambia kitu cha kufanya watu hawa wasio Wayahudi wenye kuitawala nchi hiyo kama angekuwa hajaja kwa ajili yao.
Yoh 1:4 "Ndani yake ndimo ulimokuwamo uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu." Yohana angeweza kutumia neno "Wayahudi" hapa, lakini alitumia neno "watu."
Yoh 1:9-12 "Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake."
Yoh 1:29 "Siku ya pili yake akamwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!" Yohana angeweza kusema "azichukuaye dhambi za Wayahudi", badala yake alisema "aichukuaye dhambi ya ulimwengu."
Yoh 3:15b-17 "ili kila mtu aaminiye [Mwana wa Adamu] awe na uzima wa milele katika yeye. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye."
e) Yesu alionyesha kuwa injili yake haikuwa kwa ajili ya Wayahudi tu
Ni muhimu ikumbukwe kuwa mwanzoni Yesu alisema subirini Yerusalemu, lakini kisha akasema nendeni ulimwenguni kote.
Mdo 1:4-5 "Hata [Yesu] alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali wangoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku chache." Lakini kisha kwenye Mdo 1:8 Yesu alisema, "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."
Mat 25:31-46: Yesu atakaporudi katika utukufu wake, mataifa yote watakusanyika mbele yake, naye atawabagua watu kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi. Kondoo, kama tamathali ya usemi, wamlisha, kumnywesha, kumualika, na kumvika Yesu, wakati mbuzi hawakufanya hivyo.
Kwenye Yoh 5:22-23, Yesu anaongea. "Tena Baba hamhukumu mtu yeyote, bali amempa Mwana hukumu yote; ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka."
Mat 12:50: Yesu alisema, "Kwa maana yeyote atakayefanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu." Tazama pia Mak 3:34-35. Yesu hakusema "Wayahudi wataofanya mapenzi ya Baba yangu", bali "yeyote atakayefanya mapenzi ya Baba yangu."
Mat 16:25 "Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona."
Yoh 8:12a "Mimi [Yesu] ni nuru ya ulimwengu." Je Yesu alitoa madai ya uongo kwa kusema kuwa yeye ni nuru ya ulimwengu, kama yeye alikuwa ni nuru ya Wayahudi tu? Hapana, Yesu hakutupotosha!
Yoh 10:16 Yesu alisema, "‘Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta ; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi na mchungaji mmoja."
Yoh 12:32 "Nami [Yesu] nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.’ (12:33) Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa." Je baada ya kusema hivyo Yesu alisema "Nilikuwa natania! Nitawavuta Wayahudi tu?" Hakika hakusema hivyo.
Yoh 12:46 "Mimi [Yesu] nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila aniaminiye mimi asikae gizani." Je Yesu anatakiwa kurudia mara ngapi kusema kuwa nuru yake au ujumbe wake ni kwa ajili ya kila mtu, kabla hatujaanza kuchukulia jambo hili kwa uzito kuwa ni kwa ajili ya kila mtu?
Yoh 14:6 "Yesu akamwambia, ‘Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." Je Mungu alifanya njia nyingine ngapi mbali ya Yesu zinazowawezesha watu kujia kwake? Kwa taarifa yako, Wakristo wanasema kwamba wacha Mungu walioishi kabla ya kuja kwa Kristo walikwenda peponi pia kwa kupitia njia ya Yesu. Ingawa hawakujua mambo tunayoyajua kuhusu Yesu, walitarajia kuja kwa Masihi, huku wakitoa dhabihu za wanyama ambazo zilifunika dhambi zao kwa muda, wakati sisi tunaangalia nyuma kwa Masihi, ambaye kwa dhabihu yake ya kudumu amekufa kwa ajili ya dhambi zetu.
Yoh 17:20 "Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao." Hivyo kama mtu asiye Myahudi aliamini ushuhuda wa mitume, (kama Wakristo wote walivyofanya), basi anajumuishwa na katika watu ambao Yesu aliwaombea. Ingawa ni kweli kuwa Wayahudi wengi walikuwa miongoni mwa Wakristo wa kwanza, kuanzia wakati wa Stefano shahidi na kuendelea, watu wengi zaidi wasiokuwa Wayahudi wamekuwa Wakristo pia.
Yoh 18:37 Yesu anasema, "Kila aliye wa hiyo kweli huisikia sauti yangu." Kusikia, au kutokusikia, sauti ya Yesu, ujumbe wake, injili yake ni kitu kibaya sana. Yesu hakusema, "Wayahudi walio na hiyo kweli hiusikia sauti yangu, watu wa mataifa walio na kweli hawataisikia." Hapana, Yesu alisema kuwa "kila mtu" aliye wa hiyo kweli huisikia sauti yake.
f) Wanafunzi wa Yesu walisema nini kuhusu huduma yake
Petro alisema kwenye Mdo 4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo." Ingawa ni kweli kuwa Petro alikuwa anazungumza na Wayahudi, Petro aliwaambia hakuna jina jingine 1) chini ya mbingu), 2) walilopewa watu.
1 Yoh 2:1b-2 "Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote."
Kwa nini Yohana mtume alikwenda Asia ndogo, Tomaso alikwenda mashariki, pengine hadi kufika India, Andrea alienda Scythia, na mitume wengine walienda maeneo mengine, kutangaza injili kwa watu wasio Wayahudi. Wao (mitume), zaidi ya watu wote, walikuwa wanajua watu ambao Yesu alitaka wahubiriwe ujumbe wake, na walihubiri ujumbe huu duniani kote.
Hitimisho
Si haki kushindwa kusoma, au kupuuzia aya hizi zote zilizotolewa nyakati tofauti, na kuangalia aya moja tu iliyotolewa kwa ajili ya kipindi maalum. Huwezi kutumia Mat 15:24 kuwa Yesu, nuru ya ulimwengu, alikuwa kwa ajili ya kondoo waliopotea wa Israeli tu wakati huo katika huduma yake kama ambavyo huwezi kutumia Mat 16:20 "Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu yeyote ya kwamba yeye ndiye Kristo." (Kristo maana yake Masihi). Yesu alitaka wasimwambie mtu yeyote kuwa yeye ni Kristo WAKATI ULE, kwa sababu baadaye aliwaagiza kwenda ulimwenguni kote, na hivi ndivyo walivyo muelewa. Kadhalika, Yesu alitumwa kwa sehemu kubwa kwa kondoo waliopotea wa Israeli KWA WAKATI ULE (kabla ya kusulubiwa kwake), na alikwenda si tu kwa baadhi ya watu wa mataifa wakati ule, bali pia aliwaagiza wanafunzi wake kueneza ujumbe wake duniani kote.
Ushahidi kuwa Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote ni thabiti, uliokuwa unaogezeka kadri muda ulivyokwenda, wa mfululizonyongeza, na wenye nguvu zaidi. Kwa kiwango chochote cha kisheria (uzito wa ushahidi, usiotia shaka ya aina yoyote ile, nk), ushahidi wa Biblia na historia vinathibitisha kuwa Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote. Ni jaji au hakimu mwenye upendeleo tu anayeweza kusema tofauti na hivi.

S: Kwenye Mat 10:5-6 na 15:24-26, je Yesu alikuwa mbaguzi wa rangi aliyekuja kwa ajili ya Wayahudi tu? (Muislam Ahmad Deedat alidai hivi)
J: Sivyo hivyo kabisa, bali Yesu alikuwa na muda maalum wa kufanya mbalimbali.
Kabla ya kufufuka, Yesu alihubiri injili kwa watu wa Mungu, Wayahudi kwanza. Hata katika Mdo 1:8, Yesu aliagiza wanafunzi kuwa mashahidi wake katika Yerusalemu, Uyahudi, Samaria, na kisha kwenye miisho ya nchi. Hata hivyo, kabla ya kufa na kufufuka kwake, Yesu aliwahudumia si tu mwanamke Msirofoinike kwenye Mat 15:24-26, lakini pia aliwahudumia Wasamaria kwenye Yoh 4:1-42, na pia watu wa mataifa mengine walioishi mashariki mwa Bahari ya Galilaya.
Baada ya kufufuka kwake kwenye Mat 28:19-20 Yesu alisema, "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari." Ujumbe huu ulisistizwa tena kwenye Matendo 10.

S: Kwenye Mat 10:13, je kustahili baraka kwa nyumba ambayo wanafunzi wataingia au baraka kuwarudia wanafunzi kunamaanisha nini?
J: "Nyumba" hapa inamaanisha watu wanaoishi ndani ya nyumba husika. Wanafunzi hawakupaswa kuhofia kumbariki "kwa bahati mbaya" mtu ambaye hakuwa amewapokea vizuri. Barka hutoka kwa Mungu, si nguvu ya ajabu ya maneno yao.

S: Kwenye Mat 10:14 na Mak 6:11, kwa nini wanafunzi walitakwa kuwakung’utia vumbi ya miguuni watu ambao hawatawakaribisha?
J: Kitendo hiki kilikuwa ni ushuhuda dhidi yao. Yaani, watu wasio wakarimu wanaweza kufikiria upya njia zao baada ya kuona karipio hili. Pia, kingekuwa ushahidi kwa Mungu dhidi ya watu ambao wamekataa ujumbe wake.

S: Je Mat 10:14 na Mak 6:11 zinaagiza kuwa tusijadiliane na mtu yeyote bali tuondoke tu?
J: Hapana, kwa sababu tatu: itakubidi uangalie maagizo yote maalumu kwa mitume kumi na mbili ya kupeleka injili, na hayasemi kuondoka ikiwa mtu atawapinga. Badala yake, kukung’uta vumbi toka kwenye miguu yao kama ishara WAKATI wanaondoka edapo hakutakuwa na mtu anayewakaribisha. Mwishoni mitume Petro na Paulo walijadiliana na watu wengine, na Apolo, ambaye hakuwa miongoni mwa mitume, naye pia alijadiliana na watu wengine.
Agizo maalumu la kupeleka injili wakati huu:
Mat 10:5-20 inaweza kuwa ni tukio hilohilo lililoripotiwa kwenye Mak 6:11, na itakubidi uangalie vifungu hivi kikamilifu, sio tu sehemu moja. Mitume kumi na wawili hawakutakiwa kuchukua fimbo, fedha yoyote, na kukaa katika nyumba ya mtu mwingine. Huu si mfano kwa wainjilisti wote baada ya hapo. Kwamba waliagizwa kukaa sehemu moja tu na kujadili (tofauti na Paulo alivyofanya baadaye katika darasa la mtu mmoja aitwaye Tirano kwenye Mdo 19:9-10) inaeleweka kwani walikuwa wakiueneza ujumbe kwa mara ya kwanza kabisa.
Hata wakati ule, hawakutakiwa kuondoka kama mtu angewapinga. Badala yake, walipaswa kukaa kwenye nyumba ya mtu angewakaribisha. Endapo hakungekuwa na mtu katika mji ambaye amewakaribisha, waliondoka, wakikung’uta vumbi toka kwenye miguu yao.
Kung’uta vumbi WAKATI wakiondoka
Kigiriki hapa hakielekezi kuondoka. Badala yake kinasema kukung’uta vumbi toka kwenye miguu yao WAKATI wanaondoka. Wakristo wote, wa siku zijazo, na sisi, wataweza kupitia hali ambapo baadhi ya watu watawapinga na na wengine watawaunga mkono sehemu hiyo hiyo. Katika 2 Kor 10:3-6 Paulo anasema, "Maana, ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia."
Petro, Paulo, na Apolo wajadiliana na watu wengine
Petro alijadiliana na watu waliobado kuamini kwenye kitabu cha Matendo, na Paulo alijadiliana na watu wasio waamini mara kwa mara zaidi. Ili kwamba mtu asije kusema kuwa hivi iliwapaswa kufanywa na mitume tu, Apolo hakuwa mtume, na alijadiliana na watu wengine. Hata hivyo, si sahihi kudhani kuwa kila muumini anao uwezo wa kujadiliana na watu wengine.
Mwisho, endapo hukubaliani na mimi na watu watu wengine wanaoishi kwenye mji mmoja, na bado unadhani hupaswi kuwasihi au kujadiliana na watu ambao hawakubaliani na wewe badala yake uondoke kwenye mji huo, naweza kukutafutia lori linalo hamisha watu kama utahitaji. ;-)
Kusema ukweli, jambo hili linaleta maswali: jinsi gani Yesu na Wakristo wa awali walishindana na watu waliokuwa hawakubaliani nao, na, mahali gani tunatakiwa kusitisha majadiliano na kuondika. Maswali mawili yafuatayo yanaelezea mada hizi.

S: Je Mat 10:14 na Mak 6:11 zinaagiza kuwa tusijadiliane na mtu yoyote yule hata siku moja badala yake tuondoke tu?
J: Kwanza natuangalie mfano wa Yesu, kisha Paulo, na kisha Wakristo waliosihi kabla ya baraza la kanisa la Nikea.
Yesu akijadiliana na watu wengine
Yesu alijadiliana na Mafarisayo akitumia maswali kwenye Mat 22:41-46 na sehemu nyingine.
Kisha Yesu alibadilisha njia na kutumia karipio kubwa kubwa sana kwenye Mat 23:1-37.
Yesu aliwaambia Mafarisayo kuwa wangeweza kufanya dhambi isiyo samehewa ya kumkufuru Roho Mtakatifu kwenye Mat 12:22-33.
Yesu alikashifu! Aliwaita hao Wayahudi "kizazi kibaya na cha zinaa" kwenye Mat 12:39-41. Aliwaita watu waliokuwa wanaampinga "wana wa jehanamu" kwenye Mat 23:15.
Yesu aliwaambia Masadukayo waziwazi kabisa kuwa walikosea kwa sababu hawakuyajua maandiko wala nguvu ya Mungu kwenye Mat 22:29-32.
Paulo alishindana na watu wengine
Mbali ya Yesu, Paulo alikuwa akithibitisha kuwa Yesu alikuwa ndiye Kristo huko Antiokia kwenye Mdo 9:19-25. Alikuwa anafanikiwa wakati mmoja na kupata upinzani wakati mwingine. Hakuondoka hadi wakati Wayahudi walipotaka kumuua.
Wakati Elima alipompinga Paulo kwenye Mdo 13:8-12, Paulo alimkaripia, na Paulo hakuondoka.
Kulipotokea ghasia dhidi ya Paulo huko Efeso, Paulo alitaka kuongea na wafanya ghasia kwenye Mdo 19:30.
Huko Yerusalemu, Paulo aliongea na umati wa watu wenye hasira kwenye Mdo 22:2-22.
Wakristo wa awali kabla ya baraza la kanisa la Nikea
Wakristo wa awali wa kabla ya baraza la kanisa la Nikea, ambao Mungu aliwatumia kuibadilisha himaya ya Rumi, walishuhudia injili kwa kusihi na kubishana vya kiasi kikubwa sana. Hivi vilichukua kiwango tofauti tofauti kuanzia maongezi marefu ya kirafiki kati ya Justin Martyr na Trypho Myahudi, hadi kwa wengine kama Aristides, Theophilus wa Antiokia, Letter to Diognetus, na Tertullian, yakielezea kwa kina matendo ya aibu yaliyodaiwa kufanywa na miungu wa Kigiriki na Kirumi, hadi kwa Irenaeus na Hippolytus waliopambana kwa kina sana na wafuasi mbalimbali wa Gnosticism (harakati maarufu ya kizushi ya zama za kanisa la Kikristo la karne ya pili BK, na yenye sehemu iliyoanza kabla ya zama za Ukristo, iliyokazia kuwa mada ni ovu na kuwa uhuru unapatikana kwa ufahamu). Arnobius alitumia kashfa za vichekesho za upagani wa Kigiriki na Kirumi. Lactantius alionyesha kwa nini filosofia ya Kigiriki haikuwa sahihi. Unaweza kuona orodha kwenye
www.BibleQuery.org/History/ChurchHistory/WhatEarlyChristiansTaught.htm. Tafuta ukianzia "r1" yenye herufi ndogo.

S: Kwenye Mat 10:14 na Mak 6:11, ni wakati gani tunatakiwa kuacha kujadiliana na mtu asiyekuwa muamini na kuondoka?
J: Kuna mambo yasiyopungua matatu ya kuyazingatia.
Hatari ya muda mfupi
Kama maisha yako, maisha ya watu wa kwenye familia yako, au maisha ya Wakristo wengine yapo kwenye hatari inayoweza kutokea mara moja kwa sababu ya uwepo wako, utahitaji kufikiria kuwa Mungu anawza kuwa anataka uondoke. Paulo alikimbia Antiokia wakati walipojaribu kumuua, na Wakristo walikimbia mara kwa mara wakati walipoteswa. Kwa upande mmoja, tunapaswa kuwa tayari kufa kwa ajili ya Kristo, lakini kwa upande mwingine, Mungu anaweza kuwa anataka tuishi zaidi kidogo ili tuweze kuieneza injili zaidi, na kukimbia kwetu kunaweza kuwa ndio njia ambayo Mungu ameichagua ili kutuhifadhi.
Kupungua kwa manufaa dhidi ya nafasi nyingine
Nimefika mahali ambapo siwezi kupata muda wa kutosha kushuhudia kwa kadri niwezavyo kwa kila mtu anayenitumia barua pepe, na bado nina muda wa kulala, kuwa na familia yangu, na kazi za kawaida. Kwa baadhi ya watu, nitaweza kuwapa majibu mafupi, au kutoafiki baadhi ya nafasi za huduma ili niweze kufanya mambo ambayo nadhani ni muhumu zaidi kwangu kuyafanya. Wakati fulani Paulo alikwenda kwenye mji mmoja, na watu kadhaa walimokea Kristo. Paulo angeweza kufanya jambo zuri na kubakia kwenye mji ule muda wote uliobakia wa maisha yake akijaribu kumfanya kila mtu awe muumini. Lakin badala yake, Paulo alikwenda kwenye miji mingine. Usiruhusu mambo mazuri yakuzuie kufanya mambo mazuri zaidi.
Kwa upande mwingine, nimeendelea kujadiliana na watu wengine wanaofuata mafundisho ya madhehebu potofu ambao sina matumaini kuwa watatubu. Nilifanya hivi kwa sababu palikuwa na watu wengine ambao bado hawajamwamini Yesu na nilipenda kuwa waonywe ili wasijiunge na dhehebu hili.
Endapo kujadialiana au kuhubiri kwako kunaweza kuwa na madhara au kuwafanya watu wasipende kusikiliza
Nasita kueleza jambo hili kwa sababu watu wengi zaidi wana shida iliyo kinyume na hii, kutokuwa na ujasiri wa kutosha kwenye kuhubiri injili. yesu aliagiza kuomba kwa ajili ya watenda kazi zaidi watumwe kuvuna mavuno, na Paulo kwenye Fil 1:14 alifurahi kuwa mateso yake yaliwatia moyo waamini wengine kuhubiri kwa ujasiri zaidi na bila uoga. Zaidi ya hapo, 2 Kor 2:15-16 inasema kuwa (kama tunafanya mambo sahihi) TUTATOA harufu ya mauti kwa wale wanaoangamia. Injili inakwaza, na kama maneno yetu hayakwazi na kama maneno yetu hayakwazi kabisa, hatufanyi kazi yetu sawasawa. Hata hivyo, ingawa injili inakwaza kwa baadhi ya watu, hatupaswi kuongeza makwazo hayo. Tunapaswa kusema ukweli katika upendo kama Efe 4:15 inavyoagiza. Hasa katika jamii ya kisasa, tunaweza kusema ukweli kwa njia isiyovutia au isiyoangalia hali ya watu au mazingira ya sehemu tulipo na kuwakasirisha watu bila ulazima. Tunaweza kushirikisha injili mara kwa mara kwa kundi hilohilo la watu, hata kusistiza kwetu kunaweza kuchukiza. Hatutaki kuongeza kwazo la injili, lakini pia hatutaki kuondoa kwazo la aina yeyote ile la injili.

S: Kwenye Mat 10:14-15 na 40-42, kwa nini Yesu alifundisha kuwa kumpokea mwenye haki ni jambo muhimu sana?
J: Kupokea mwenye haki kulihusisha mambo mengi. Hakumaanishi kumkaribisha tu, lakini pia kumpa msaada, na katika miongo ijayo, kinga dhidi ya mamlaka zinazomtafuta. Kumpokea mwenye haki pia kulimaanisha kuyakubali mafundisho yake, na kuwa tayari kujifunza kutoka kwake. Pia kulihusisha kumsaidia kupata fursa ya kufundisha watu wengine.

S: Kwenye Mat 10:15, kwa nini itakuwa rahisi zaidi kwa Sodoma na Gomora kuvumilia kwenye siku ya hukumu kuliko kwa watu ambao hawakuwapokea mitume wa Yesu kwenye nyumba zao?
J: Maandiko hayasemi, lakini Mungu anahukumu watu kwa kufuata kiasi ambacho waliweza kujua (Rum 4:15; 5:13). Ingawa watu wa Sodoma na Gomora walikuwa wabaya sana, walifahamu mambo machache sana kuhusu Mungu. Watu ambao si waovu sana lakini wanafahamu mambo mengi zaidi kuhusu Mungu, lakini bado wanawakataa wanafunzi wa Mungu, watapata hukumu kubwa zaidi.

S: Kwenye Mat 10:16, je ni jinsi gani mitume (na sisi pia) walitakiwa kuwa na busara kama nyoka na kuwa wapole kama njiwa?
J: Kwa njia rahisi sana, tunatakiwa kufahamu mbinu na mitego ambayo watu wengine wanaweza kutuundia, lakini hatupaswi kuunda mbinu chafu dhidi ya watu wengine.

S: Kwenye Mat 10:19, je Roho Mtakatifu anawapaje Wakristo maneno ya kusema wanapokuwa kwenye mateso?
J: Ikiwa Mkristo yupo kwenye mateso au katika muda fulani au la, wakati mwingine Roho Mtakatifu huleta maneno ya kusema kwenye mawazo ya mtu. Pili, Mungu anaweza kukufanya uone au kusikia mambo yakuzungukayo yanayotokea kila siku yanayohusiana na ujumbe unaotakiwakuutoa. Kwa mfano, kabla ya kuzungumza na watu wa Athene, Paulo aliona sanamu nyingi sana, pamoja na madhabahu na mungu asiye julikana. Pia, tunakumbushwa ukweli kupitia kusoma kwetu Biblia. Hata kama Mkristo angejua kikamilifu kila kisa na kila fundisho la Biblia, bado ingekuwa muhimu kuisoma Biblia kukumbushwa ukweli.

S: Kwenye Mat 10:19-20, wakati Roho Mtakatifu anawapa Wakristo maneno ya kusema, je jambo hilo linamaanisha kuwa kwa wakati huo, maneno hayo hayawi na makosa, au hayawi na makosa makubwa ya kithiolojia?
J: Ni pale tu ambapo Roho Mtakatifu angetoa maneno halisi, na ingekuwa hakika kuwa mtu anayeambiwa amesikia hayo maneno bila makosa, ndipo inawezekana kuwa Mkristo mtiifu angeweza kusema bila makosa.

S: Kweney Mat 10:21-22 na 35-36, kwa nini ndugu wa Mkristo wanasimama dhidi ya Mkristo?
J: Ni jambo ovu kuwa dugu wa mcha Mungu wanasimama dhidi yake. Nimeambiwa kuhusu mvulana wa Kialgeria ambaye alibadili dini kutoka kuwa Muislam na kuwa Mkristo. Alipokataa kubadili msimamo, mama yake mwenyewe alimwekea sumu ya panya kwenye chakula chake.

S: Kwenye Mat 10:23, kwa nini Yesu aliwaambia Wakristo kukimbia mateso kwa sababu Mungu anawalinda?
J: Mungu anaweza kutulinda kwa njia yeyote anayotaka, na njia mojawapo ya kutulinda ni kutuambia wakati kukimbia. Kwa upande mmoja, kukimbia si aibu, kama ambavyo Wakristo wengi walifanya baada ya Stefano kupigwa mawe kwenye Mdo 8:1-8. Kwa upande mwingine, kuna nyakati ambazo Mungu hataki tukimbie bali tusimame na kuteseka kwa ajili yake. Kwa nyakati tofauti, Yesu na Paulo wakaenda Yerusalemu kwa kudhamiria kabisa huku wakijua kitu ambacho kinawasubiri huko.

S: Kwenye Mat 10:23, je kuja kwa Yesu hakukutokea kwa sababu angekuja kabla hawajaenda kwenye miji yote ya Israeli? (Muislam Ahmad Deedat alitoa hoja hii.)
J: Hapana, kwa sababu katika kukimbia kwao hawakupitia kila mji wa Israeli kabla ya Yesu kuja, na hawakukimbia kupitia kila mji wa Israeli. Tukio hili la baadaye huenda likatokea wakati wa dhiki kuu.

S: Kwenye Mat 10:23, je jambo hili linamaanisha nini kuwa Yesu atakuja kabla hawajamaliza kupita kwenye miji yote ya Israeli?
J: Kwanza tutaangalia kitu ambacho siyo jibu, kisha mambo kadhaa, na mwishoni jibu.
Jambo ambalo si jibu: Kifungu kinasema kuwa Yesu "atakuja" kwa hiyo hakiwezi kuwa kinaongelea kupaa kwake ambako kupitia huko Yesu aliondoka kwenda mbinguni. Baadhi ya watu wanafikiri kuwa kinaoongelea hukumu ijayo itakayofanywa na Yesu na kuingamiza Yerusalemu, lakini kifungu hakisemi kitu chochote kuhusu hekalu.
Mambo kaadhaa: Hatuna ushahidi wowote wenye kuonyesha wanafunzi wakiteseka kabla ya kusulubiwa kwa Yesu. Ingawa kukuteketezwa kwa Yerusalemu kulitokea mwaka 70 BK, endapo Yesu alikuja kisiri na bila kuonekana wakati ule, hakuna mtu katika kanisa la awali aliyepata fununu yoyote kuhusu jambo hili. Ukweli ni kwamba, baada ya mwaka 70BK, karibu Wakristo 14 wa awali waliandika kuhusu kuja kwa Yesu kama tukio litakalotokea siku zijazo.
Mambo mawili yaliyo sehemu ya jibu: Kwanza, Yesu haongei kuhusu kuhubiri injili kwenye Mat 10:21-22, lakini kwenda mji mmoja hadi mwingine ili kukimbia mateso. Kwa hiyo, tunaweza kusema kuwa kukimbia mateso "starts the clock." Wakati huo Wakristo hawatakimbia toka mji mmoja hadi mwingine kabla ya kurudi kwa Yesu. Jambo hili litatokea siku zijazo, na kuna uwezekano mkubwa zaidi kuwa itakuwa kwenye kioindi cha dhiki kuu.
Pili, bila kujali jambo hili litatokea lini, hakuna ushahidi kuwa mitume walipita miji yote ya Israeli, kwa hiyo jambo hili halikutokea.

S: Kwenye Mat 10:23, je injili itahubiriwa kwenye kila mji, au haitahubiiwa kwenye Mat 24:14?
J: Ni muhimu kusoma aya hizi kwa uangalifu ili kujiepusha na kushindwa kuelewa mambo ambayo zinayaongelea. Mat 24:14 inasema injili itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote. Hii haimaanishi kuwa kila mtu analazimishwa kusikia; lakini kwa kuwa kuna luninga, redio, mtandao wa kompyuta, leo hii injili imeweza kuhbiriwa karibu ulimwenguni kote, isipokuwa labda maeneo machache ya mbali yanayokaliwa na baadhi ya makabila.
Mat 10:23 haisemi kitu endapo kila mji wa Israeli utahubiriwa au la. Badala yake, inaongelea kuyakimbia mateso, na Mkristo hataiacha miji ya Israeli ili kukimbia kabla Yesu hajarudi.

S: Kwenye Mat 10:25, Mk 3:22, na Luk 11:15-19, je "Beelzebuli" ni nani?
J: Hili ni jina la pepo aliyefahamika na Wayahudi kwa jina hilo. Jina "Beelzebuli" linatokana na maneno Baal linalomaanisha Bwana na zebub linalomaanisha "nzi."

S: Kwenye Mat 10:26, je inamaanisha kuwa hakuna kitu kilichojificha ambacho hakitafunuliwa?
J: Mwisho wa mambo yote, kila kitu kitafunuliwa. Hasa, kwenye hukumu ya mwisho, Mungu atayahukumu matendo yote (Ufu 20:13), na kila neno lisilokuwa la maana (Mat 12:36-37), na hata anayajua mawazo yetu yote (Zab 139:2,4).

S: Kwenye Mat 10:28, je ni Mungu au Shetani kwa kuwa na uwezo wa kuangamiza vyote mwili na nafsi jehanamu?
J: Kifung hiki kinamwongelea Mungu.

S: Kwenye Mat 10:28, je miili inaangamizwaje jehanamu?
J: Neno la Kigiriki hapa ni Gehenna, ambalo linamaanisha jehanamu, lakini neno hilo pia humaanisha lundo la la takataka nje ya mji wa Yerusalemu. Bila kujali mahali ambapo mwili wa mtu mwovu unaangamizwa kwanza, mwili wake wa ufufuo utakwenda kwenye ziwa la moto na utaangamizwa kwa sababu walikataa kumpokea Yesu kama Mwokozi na Bwana wao.

S: Kwenye Mat 10:33, kama katika nyakati za udhaifu wake, Mkristo atamkana Kristo mbele ya watu, je Mkristo huyo atakanwa na Yesu na kwenda jehanamu?
J: Petro alifanya hivyo, lakini alisamehewa. Kumkana Kristo na kutubu si dhambi isiyosamehewa, kwa sababu hakuna dhambi isiyosamehewa, isipokuwa ya kumkufuru Roho Mtakatifu (Mat 12:31,32; Mak 3:28-30; Luk 12:10-11).

S: Kwenye Mat 10:34, ni kwa vipi Yesu, Mfalme wa amani, hakuja kuleta amani bali upanga?
J: Yesu hakumshikia upanga mtu yeyote yule (japo hadi wakati wa kuja kwake kwa mara ya pili), lakini familia nyingi zimegawanyika, na Wakristo wengi wameuawa kwa sababu ya jina la Yesu.

S: Kwenye Mat 10:37, kwa nini tunatakiwa kumpenda Mungu kuliko familia zetu?
J: Kwenye Mak 12:29-30 Yesu alisema kumpenda Mungu ndio amri ya kwanza. Mung ametuumba na anatupenda kuliko mtu mwingine yeyote, na tunapaswa kutoa utii wetu mkubwa zaidi kwake.

S: Kwenye Mat 10:41, je tunapokeaje thawabu ya nabii au mtu mwenye haki kwa kumkaribisha nabii au mtu mwenye haki?
J: Jambo hili ni kweli kwa njia angalau mbili.
1. Mtu anapowapokea na kuupokea ujumbe wao anaweza kuukubali ukristo na kuwa mtu mwenye haki pia.
2. Tunapompokea Mkristo kwa jina la Yesu, hilo ni tendo la haki, na ni kama tunampokea Yesu, kama Mat 25:33-40 inavyosema.

S: Kwenye Mat 11:3, kwa nini Yohana Mbatizaji alimuuliza Yesu endapo Yeye ndie Masihi aliyeahidiwa, kwani alimwona Roho Mtakatifu akishuka kama njiwa na kutua kwa Yesu kwenye Yoh 1:32?
J: Yohana Mbatizaji alikuwa gerezani, na huenda alikuwa hajasikia kuhusu miujiza na huduma ya Yesu. Kuna mambo angalau manne yanayoweza kuongezea uwezekano wa kuuliza swali hilo:
Mashaka: Huenda Yohana alipitia kwenye kipindi cha kuona shaka hapa. Tertullian (mwaka 198-220 BK), mwandishi toka kwenye kanisa la awali alikuwa mtu wa kwanza kupendekeza wazo hili.
Kuchanganyikiwa: Huenda Yohana aliona nabii za ujio wa kwanza zikitimizwa ila hakuwa na uhakika na nabii za ujio wa pili.
Kutokuwa na subira: William Hendrickson anasema kuwa "Shida ya Yohana huenda haikuwa imani yake, bali uvumilivu wake. Yohana alifanya uamuzi wa busara sana alipoamua kuwa badala ya kuitunza shida hii ihusikanayo na Yesu moyoni mwake, au kuwaambia watu wengine isipokuwa mtu sahihi, aliipeleka kwa Yesu." (The Gospel of Matthew 1973, uk.84).
Kumchokoza Yesu: Kwa namna hiyohiyo, Yohana huenda alikuwa anamchochea Yesu kuonyesha nguvu zaidi, au mambo yote mawili.

S: Kwenye Mat 11:3-6, kwa nini Yesu hakusema "ndiyo" au "hapana" tu?
J: Ni jambo rahisi mtu kudai kuwa ni Masihi. Ni jambo jingine kuthibitisha madai kwa kutoa ushahidi wa kimiujiza. Yesu alikuwa anawakumbusha Yohana na wasikilizaji wa Yesu wa ushahidi aliokuwa ameutoa.

S: Je Mat 11:11 na Luk 7:28 inafundisha kuwa Yohana Mbatizaji alikwenda jahanamu, kama kitabu cha Mchungaji Moon kiitwacho Divine Principle, uk.161 kinavyofundisha?
J: Hapana. Yoh 10:41-42 inaonyesha kuwa ushuhuda wa Yohana uliwasaidia watu wengi kumwamini Yesu. Tunapaswa kuwa waangalifu katika kumlaani shahidi aliyekufa kwa ajili ya Mungu kama mtu aliyeshindwa na mwenye kumuudhi Mungu. Maneno ya Yesu kuwa aliye mdogo kabisa katika ufalme mbinguni ni mkuu kuliko [Yohana Mbatizaji] yanaonyesha ukweli kuwa Yesu alikuwa bado hajafungua njia ya kwenda mbinguni, na Yohana Mbatizaji alikuwa nabii wa mwisho chini ya agano la kale. Pia, kama Yohana Mbatizaji alishindwa katika mafundisho yake, kwa nini basi katika Mat 21:32 Yesu alisema watu wanapaswa kumwamini Yohana Mbatizaji? Tazama pia swali linalofuata kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Mat 11:11 na Luk 7:28, je usemi kwamba aliye mdogo zaidi kwenye ufalme wa mbinguni ni mkuu zaidi ya Yohana Mbatizaji unamaanisha nini?
J: Kuna maoni matatu, na yote matatu yanaweza kuwa ya kweli.
Nahau ya Kiebrania: Msemo huu unafanana sana na msemo wa Kirabi wa Yohanan ben Zakkai, mmoja wa wasomi walioheshimiwa zaidi wa karne ya kwanza kwamba, kuwa mwanafunzi "mdogo zaidi" kati ya wanafunzi themanini wa Hileli; usemi huu haukuwa na lengo la kupunguza hadhi ya Yohana bali kuongeza hadhi ya watu walioishi wakati wake.
Hakuna yeyote hadi wakati wa Yesu: Hata Yohana Mbatizaji alikuwa bado hajaingia kwenye ufalme wa mbinguni. Hakuna mtu aliyekuwa ameingia, mpaka wakati Yesu alipofungua njia kupitia kufa na kufufuka kwake.
Uhusiano unaowiana mbinguni: Kumbuka kuwa Yohana Mbatizaji alijazwa Roho Mtakatifu tokea kabla ya kuzaliwa kwake. Inadhaniwa kuwa waumini huko mbinguni, ambao watatakiwa kuzaliwa upya baada ya kuwa wamezaliwa watakuwa na nafasi ya juu kuliko mtu yeyote ambaye hakuwa na haja ya kupitia hili.

S: Kwenye Mat 11:12-13, ni kwa vipi ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu?
J: Kutoka wakati wa kifungo cha Yohana Mbatizaji (na baadaye kuuawa) mpaka sasa, kutakuwa na vurugu inayofanyika dhidi ya ufalme wa mbinguni. Yesu alisema maneno haya baada ya Yohana Mbatizaji, ambaye kwa wakati huo alikuwa amefungwa na Herode, alipompelekea ujumbe.

S: Kwenye Mat 11:14 na Luk 1:15, ni kwa vipi Yohana Mbatizaji alikuwa na roho na nguvu za Elia? Je alikuwa ni Eliya aliyezaliwa tena katika mwili wa kiumbe kingine?
J: Hapana. Alikuja katika roho na nguvu za Eliya, lakini Yohana hakuwa Eliya aliyezaliwa tena katika mwili wa kiumbe kingine. Tazama maelezo ya Mak 9:11-13 kupata jibu la swali hili.

S: Kwenye Mat 11:16-17 na Luk 7:32, je kizazi kile kilikuwaje kama watoto walio sokoni?
J: Watoto wanaweza kusikiliza vibaya, wana kumbukumbu fupi, na kutokuwa na mantiki nyakati zingine. Wanaweza kupata shida kuangalia jambo kwa mtazamo wowote isipokuwa wao wenyewe. Yesu anaeleza kwa nini alisema hivi kwenye Luk 7:33-35. Kwa upande mmoja, walimkosoa Yohana Mbatizaji kwa kutokunywa divai au kula chakula cha kawaida, na kisha wanageuka na kumkosoa Yesu kwa kunywa divai na kula chakula cha kawaida.
Niliona hali kama hii huko Salt Lake City nilipokuwa nafanya huduma kwa Wamormoni. Wamormoni walikuwa wananiuliza endapo nimewahi kuwa Mmormoni, na nilikuwa nawajibu "hapana." Kwa kuwa sikuwahi kuwa Mmormoni, niliwezaje kuelewa waliokuwa wanafundisha. Walikuwa wanawauliza Wakristo waliowahi kuwa Wamormoni swali hilo hilo, na waliwajibu "ndiyo." Wangewezaje kumsikiliza mtu aliyeliasi na kuliacha kanisa lao. Wakati mwingine kunakuwa hakuna namna ya kuwafikia baadhi ya watu.

S: Kwenye Mat 11:23-24, kwa nini Sodoma iwe na haja ya kutubu hapa?
J: Yesu anatumia mbalagha hapa kusema kuwa endapo watu wa Sodoma wangekuwa na ufahamu wa Mungu ambao Wayahudi walikuwa nao, wasingekuwa waovu kiasi cha kuangamizwa. Hata Waashuri walitubu wakati Yona alipokwenda kwao, lakini baadhi ya watu wa Galilaya hawakutubu hata Mungu mwenyewe alipokuja kwao.

S: Kwenye Mat 11:25-26, kwa nini Yesu alimshukuru Mungu kwa kuuficha ukweli kwa wanaoitwa wenye hekima?
J: Je, isingekuwa ajabu endapo watu wenye akili zaidi, na wale ambao wangeweza kumudu elimu zaidi wangekuwa, kwa ufahamu wao tu, wanampendeza Mungu zaidi au karibu zaidi na mbinguni? Sivyo hivyo. Badala yake, wale ambao wako tayari kumweleza Mungu kushindwa kwao ndio walio karibu na Mungu, kama mfano wa farisayo na mtoza ushuru unavyoonyesha.

S: Kwenye Mat 11:25-26, je tunatakiwa, wakati wowote ule, kumshukuru Mungu kwa kuficha ukweli?
J: Ni vema zaidi kumshukuru Mungu kwa ukweli na jinsi alivyoufunua. Yesu anasema kuwa watu wenye ufahamu zaidi hawana manufaa yoyote kuliko watu wenye ufahamu kidogo katika kuutafuta ukweli juu ya Mungu. Ukweli ulifichwa kwa namna ambayo watu hawawezi kuupata kwa hekima yao wenyewe mbali na Mungu. Hata hivyo ukweli kinzani, kwa watu ambao wanataka kuujua ukweli, wataupata, hata kama ni watoto wadogo tu.

S: Kwenye Mat 11:27, je ni jinsi gani vitu vyote vimekabidhiwa kwa Yesu?
J: Mambo yote vimekabidhiwa kwa Yesu kwa namna tofauti. Vitu vyote vitasujudu kwa Yesu, Yesu atawahukumu watu, na Yesu ametuokoa.
Hata hivyo, jambo kubwa ambalo Yesu analisema hapa si kwamba Yesu ni "mmoja wa Waokozi", bali kuwa hakuna wokovu isipokuwa kupitia kuokolewa na Yesu. Mtu wa kisasa mkubwa, mtoto mdogo, au mtu mtu aliyekufa nyakati za zamani kabla Kristo hajajulikana kwao, ama anakwenda mbinguni kupitia njia ya Yesu, au haendi haendi kabisa.

S: Kwenye Mat 11:27, ni kwa jinsi gani hakuna mtu anayemjua Baba isipokuwa Mwana na yeyote ambaye Mwana anamfunua Baba kwake?
J: Jambo hili ni la kweli si tu kwa njia moja bali mbili.
Ufahamu: Kama Mungu amekusudia hivyo, angeweza kujificha hata tusingeweza kujua jambo lolote kuhusu Yeye. Mungu alichagua kujifunua, kwa kiasi kupitia Ibrahimu na kupitia manabii, lakini kujifunua kwake kukamilifu kumekuja kupitia kuja kwa Yesu Kristo duniani.
Wokovu: Watu wote waliookolewa, na yeyote atakayeokolewa, wanaokolewa kupitia Masihi, Yesu. Hata watu waliomfuata Mungu wa kweli kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, na hawakujua jina la Yesu, wanaokolewa kupitia Yesu. Mdo 4:12 inasema hakuna wokovu kwa katika mwingine awaye yote. Flp 2:9-11 inasema kuwa kwa jina jina la Yesu kila goti litapigwa, mbinguni, duniani, na chini ya nchi, na kila ulimi utakiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana.

S: Kwenye Mat 11:27, kwa nini Yesu anasema kuwa hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunua Baba kwake, kwani Zab 145:18 inasema Mungu yupo karibu na wote wamwitao Yeye?
J: Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
Wote ambao Yesu anapenda kumfunulia: Yesu hakuwahi kusema kuwa Yeye pekee ndiye atakayemjua Baba. Badala yake, Yesu alisema Yeye na watu ambao atapenda kuwafunulia ndio watakaomjua Baba.
Kipindi husika cha muda: Yesu hakubainisha endapo jambo hili litakuwa katika siku zijazo wakati wa hukumu ya mwisho, wakati wa sasa, wakati uliopita, au nyakati zote zilizotajwa hapo juu. Maneno haya ni ya kweli kuhusiana na siku zijazo, kwa sababu katika mwishoni watu wote watasimama mbele ya Kristo ambaye ndiye mwamuzi wetu, kama Yoh 5:22-23 inavyoonyesha. Maneno ya Yesu pia yalikuwa ya kweli wakati alipokuwa duniani, kama ambavyo Yesu mwenyewe alivyowaambia Wayahudi kwenye Yoh 8:24 kuwa endapo watamkataa watakufa katika dhambi zao. Jambo hili linaweza kuonekana kuwa si haki kwa mtu ambaye alidhani kuwa kwenda mbinguni ni kusoma Maandiko na kutegemea maneno tu, badala ya utiifu. Hata hivyo, Yesu alisema kwenye Yoh 14:6 kuwa Yeye ni njia, na kweli, na uzima, na kuwa hakuna mtu atakayefika kwa Baba isipokuwa kupitia kwake. Hata hivyo, kwa namna nyingine maneno ya Yesu yalikuwa kweli pia kabla ya kuja kwake duniani. Si tu kuwa alikuwa na Waisraeli jangwani kwa mujibu wa 1 Kor 10:4, bali kusulubiwa na kufufuka kwake kumeleta uzima kwa waamini wote, walioishi kabla na baada ya kuja kwa Kristo duniani, kulipangwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia kulingana na Mdo 2: 23.
Uhusiano maalumu: Baada ya kusema mambo yote yaliyotangulia, Yesu na Roho Mtakatifu wana uhusiano maalum na Baba uhausiano ambao mtu yeyote hanao.

S: Kwenye Mat 11:28, je Yesu anatupaje pumziko?
J: Tunaweza kuufanyia kazi ukweli huu katika maisha yetu kwa njia zisizopungua tano.
Uhuru dhidi ya hofu: Mungu atatutunza, na hakuna kitu kitakachotokea kwetu isipokuwa kile ambacho Mungu amekiruhusu. 1 Pet 1:6-9 na 1 Kor 2:9 zinaonyesha kuwa utukufu wa mbinguni utayafanya mateso tunayoyavumilia hapa duniani yaonekane kuwa madogo.
Uhuru dhidi ya masumbuko na mashaka: Kwenye Mahubiri ya Mlimani, Yesu alisistiza bayana thamani yetu kwa Mungu, na ubatilifu na kuchukiza kwa mashaka. Flp 4:6-7 inasema kuwa tusijisumbue kwa neno lolote bali kufanya haja zetu zijulikane na Mungu.
Uhuru dhidi ya kazi, malengo na makusudio vyetu: Tunapoamini, kipimo cha mafanikio yetu kinapata ufafanuzi mpya. Mafanikio si tu kufanya kitu ambacho Mungu anataka ufanye, bali kuwa kama Mungu anavyotaka uwe. Hakuna kitu cha zaidi. Hatuna haja kuwa na wasiwasi tena kuhusu kufanikiwa mbele ya macho ya watu wengine, au kuishi kwa mujibu wa matarajio ya jamii zetu.
Uhuru dhidi ya hofu ya jukumu: Kwenye siku ya hukumu, waamini wataweza kusimama bila hofu. Kristo atatoa hukumu ya thawabu (au kukosa thawabu) lakini waamini wana uhakika wa wokovu na kuepuka ziwa la moto.
Uhuru usiokuwa na mwisho: uhuru wetu unaanza sasa hapa duniani, kwa kiasi kidogo. Lakini tutakuwa na uhuru milele kama wana wa mfalme mbinguni.
When Critics Ask, uk.342 inatoa maelezo ya kuhitimisha vizuri ikisema: "Maisha ya muamini ni ;rahisi’ kwa maana ya kwamba yanatoa ‘pumziko la nafsi’ (Mat 11:29), lakini ni magumu kwenye ‘mwili’ ambao mara nyingi unahitaji kadibishwa na mkono wa Mungu ili uweze kwenda kama unavyotakiwa. Wokovu huleta ‘amani na Mungu’ God’ (Rum 5:1), lakini pia huleta migongano na ulimwengu (1 Yoh 2:15-17; Gal 5:17)."

S: Kwenye Mat 11:29-30, je kuna tofauti gani kati ya nira na mzigo?
J: Nira huvuta mkokoteni, ambao unabeba mzigo. Nira, na mzigo unaotumika kuvuta, inaweza kuwa nyepesi au nzito, na Yesu anasema nira yake ni nyepesi (laini).

S: Je Mat 11:29 inaweza kuwa inaunga mkono yoga, kama Mark na nabii Elizabeth walivyofundisha kwenye The Lost Teachings of Jesus 3 (1988), uk. 273-274?
J: Sivyo hata kidogo. Yesu anasema jitieni "nira" siyo "yoga" yangu. Neno la Kigiriki hapa, zugon, lilimaanisha kumtia maksai nira ili aweze kutumika shambani, na huusisha kumtumikia Yesu , siyo kufanya matendo maalumu ya mwili au kudhibiti kupumua.

S: Kwenye Mat 12:1-5, je wanafunzi wa Yesu walivunja sabato ya Wayahudi au la?
J: Hawkuvunja sabato kwa mujibu wa sheria ya Musa hapa, ingawa walivunja sabato kwa mujibu wa tafsiri ya Mafarisay. Hatuna kumbukumbu yeyote ya wanafunzi wa Yesu kuvunja sheria ya Musa wakati Yesu alipokuwa anahudumu hapa duniani kabla ya kufufuka kwake.

S: Kwenye Mat 12:1-8 na Mak 2:27, je maneno aliyosema Yesu hapa ni mabadiliko ya sheria ya Mungu, au Yesu alikuwa anasema jinsi walivyotakiwa kufanya hata katika nyakati za Agano la Kale?
J: Yesu hafanyi mabadiliko yoyote hapa. Kuvunja masuke ya ngano na kula kulikuwa tayari kuruhusiwa kibayana kisheria. Ingawa sheria ilivuia watu kufanya kazi siku ya sabato, mtu aliruhusiwa kuvunja masuke na kula, ili mradi hakuwa anavuna kwa kuweka kwenye mfuko.
Yesu alikuwa anaonyesha kuwa tunapaswa kuzingatia sheria yote, kwani sheria pia imetoa ruhusa maalumu kwa makuhani. Pia, Yesu anaonyesha kuwa wakati wa dharura iliyomkabili Mfalme Daudi, kuendelea kwake kuwa hai machoni pa Sauli kulikuwa kwa maana kuliko mikate ya wonyesho. Je ni kwa kiasi gani zaidi Masihi anapaswa kuwa wa maana kuliko mapokeo ya Mafarisayo.

S: Kwenye Mat 12:3-5 na Mak 2:25-27, kwa nini iliruhusiwa kuchukua mkate wa wonyesho, na jambo hili linahusiana vipi na kuitunza sabato?
J: Kanuni muhimu hapa ni msonge wa madaraka, na mwishoni waweze kumtii Mungu, siyo sabato. Makuhani tu ndio walioruhusiwa kula mikate ya wonyesho, na Daudi na watu wake walikuwa kwenye kazi maalumu ya Mungu, walikabiliwa na dharura (walikuwa wanamkimbia Sauli), na baada ya kujadiliana na makuhani walikula kwenye 1 Sam 21: 3-6.
Kwa Mafarisayo, sabato iligeika na kuwa sanamu kwao! Hii si kwa sababu sabato ilikuwa mbaya kwa namna fulani, bali walijishughulisha zaidi na sabato kuliko Mungu.

S: Kwenye Mat 12:5, ni kwa jinsi gani makuhani wanainajisi sabato lakini hawapati hatia?
J: Sheria iliwaelekeza makuhani kufanya kitu ambacho hakikuwa halali kwa watu wengine kufanya siku ya sabato. Jambo ambalo Yesu alifundisha si kwamba makuhani waache kufanya kitu ambacho Mungu amewaagiza kufanya. Badala yake, jambo ambalo Yesu alifundisha ni kwamba kama ukiangalia maagizo ya Mungu wakati unapuuzia mazingira utakuwa na kila aina ya matatizo. Mshikiliaji sheria aliyevuka mipaka ni mtu anayetazama sheria bila kuangalia muktadha.
Tertullian (mwaka 198-220 BK) kwenye Five Books Against Marcion kitabu cha 4 sura ya 12, uk.362, anaonyesha kuwa wakati Mungu alipowaamuru Waisraeli kutembea kuuzunguka mji wa Yeriko siku nane mfululizo, walitembea hata kwenye siku ya sabato. Hivyo, huu pia ni mfano wa amri ya moja kwa moja ya Mungu inayozuia sabato.

S: Kwenye Mat 12:5, wakati Yesu aliposema, "Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani huinajisi sabato wasipate hatia?", kwa nini maneno haya hayakuwa yamenukuriwa toka kwenye torati?
J: Yesu hakusema kuwa alikuwa ananukuu maandiko yoyote yale. Yesu alikuwa anatoa hitimisho la kimantiki kuwa kwa mujibu wa sheria, makuhani walifanya kazi yao ya kikuhani siku ya sabato na jambo hilo lilikuwa sahihi na lenye kumpendeza Mungu.

S: Kwenye Mat 12:3-8 na Mk 2:25-28, lengo la mifano hili lilikuwa ni nini?
J: Kumfuata Mungu si sheria tu, bali pia vipaumbele. Kumfuata Yesu kama Bwana wako ndilo lengo la utii, si sheria tu, hata kanuni za Mungu. Vifungu vingine vinaonyesha kuwa kuna vitu zaidi ya sheria na vipaumbele vinavyohusika na kumfuata Mungu, lakini Yesu alikuwa anaongelea mambo ya msingi hapa. Yesu alikuwa mvumilivu katika kutoa maelezo rahisi kwa Mafarisayo waliokuwa wanampinga, na Mungu ashukuriwe kwani angali mvumilivu kwetu pia.

S: Kwenye Mat 12:8 na Mak 2:28, je kusema kuwa Mwana wa Adamu ni Bwana wa sabato kunamaanisha nini?
J: Tuliumbwa kwa ajili ya Mungu, si kwa ajili ya sheria wala Sabato. Amri ya kupumzika siku ya sabato ilitolewa ili kuwasaidia watu, si kuwazuia. Mungu ndie Bwana wa sheria yake.

S: Kwenye Mat 12:10-14 na Mak 3:3-6, je Mafarisayo waliona ubaya gani kuponya mtu siku ya sabato?
J: Mafarisayo waliuona uponyaji kuwa kama kazi ya uumbaji.

S: Kwenye Mat 12:10-14, kwa nini aliwajibu Mafarisayo namna hii?
J: Yesu alikuwa anaonyesha kutokuwa na msimamo kwao. Hebu angalia kichekesho cha ajabu kwenye suala hili. Hawa walikuwa watu waliokuwa wanafundisha mambo yao wenyewe walio yaongeza kwenye neno la Mungu kama neno la Mungu, wakimwagiza Mungu asifanye baadhi ya vitu. Kwa kuwa muujiza ulitoka kwa Mungu, wangeweza pia kumwambia Mungu kuuondoa muujiza ule!

S: Kwenye Mat 12:31, 32, Mak 3:28-30, na Luk 12:10-11, kumkufuru Roho Mtakatifu ni kitu gani?
J: Muktadha unaonyesha kuwa ni kuiona kazi ya kimiujiza ya Mungu, kuikataa injili, na kusema kuwa mambo haya yanatoka kwa Shetani.
Si kumwambia Roho Mtakatifu atoke katika maisha yao. Namjua mmoja mwanafunzi wa chuo kikuu Mkristo aliyemwambia Mungu aachane na maisha yake. Baada ya mwezi hivi alijisikia vibaya sana, alitubu na kurudi kwa Kristo. Kama mtu atamkufuru Roho Mtakatifu, hatapenda kurudi kwa Kristo.

S: Kwenye Mat 12:31, 32, Mak 3:28-30, na Luk 12:11, kwa nini kumkufuru Roho Mtakatifu ni kubaya zaidi ya kumkufuru Yesu?
J: Yesu hakusema bayana. Hata hivyo, endapo mtu atamkana Yesu, Roho Mtakatifu anaweza kufanya kazi ndani mwake hata abadilishe mawazo yake na kumkubali Yesu baadaye. Hata hivyo, endapo mtu hatamtaka Roho Mtakatifu ndani ya maisha yake mpaka mwisho, na Roho Mtakatifu anaheshimu haja hiyo, mtu huyu hataweza kuja kwa Kristo na kwenda mbinguni.

S: Kwenye Mat 12:31-32, je kumkufuru Roho Mtakatifu kunamaanisha kuukataa mwanga kwa kuyakana madhihirisho ya Mungu (kama vile Baha’u’llah) kwa mujibu wa mafundisho ya Bahai’ kwenye Some Answered Questions, uk.127-128?
J: Hapana, huku ni kudhania kitu kinachotakiwa kuthibitishwa kwanza kwa kudhani kuwa madai ya Baha’u’llah kwamba yeye ni mwanga yanathibitisha kuwa Baha’u’llah alikuwa mwanga. Hata hivyo, hata kwa upande wa Yesu, angalia kuwa kwenye Mat 12:31 alisema kwamba mtu atakayenena neno baya dhidi ya Yesu atasamehewa, hivyo kunena neno baya dhidi ya nabii wa Mungu SI kumkufuru Roho Mtakatifu.

S: Kwenye Mat 12:32, je huku kutokusamehewa kwenye maisha ya sasa kunakotokana na kumkufuru Roho Mtakatifu hakuungi mkono mafundisho kuhusu mahali pa mateso ya muda, kama mwandishi Mkatoliki Ludwig Ott alivyosema?
J: Hapana, hata New Catholic Encyclopedia juzuu ya 11, uk.1034 inasema "mafundisho yahusuyo mahali pa mateso ya muda hayajaelezwa bayana kwenye Biblia." Mat 12:31-32 haifanyi kitu chochote kuunga mkono mahali pa mateso ya muda kwa sababu tatu:
1) Mafundisho ya Kikatoliki ni kuwa mahali pa mateso ya muda panatakasa muumini dhidi ya dhambi ndogo isiyomzuia mtu kupata neema ya Mungu, dhambi zisizo za mauti (kubwa zaidi, au zenye madhara), na kumkufuru Roho Mtakatifu kunachukuliwa kuwa dhambi ya mauti.
2) Yesu haongei kuhusu waamini, lakini waandishi na Mafarisayo waliokuwa wamemkataa.
3) Aya haisemi chochote kuhusu urefu wa muda, aina ukubwa, au mahali pa adhabu au utakaso; hausemi kitu chochote kabisa kuhusu adhabu au utakaso. Badala yake inaongelea kuhusu kutokusamehewa na Mungu.

S: Kwenye Mat 12:38-39 na 16:1-4, wakati Mafarisayo walipoomba ishara, je Yesu alisema kuwa watapewa ishara ya Yona tu, au hapakuwa na ishara yeyote kama Mak 8:11-13 inavyosema?
J: Kuna mambo matatu ya kuyazingatia katika kujibu swali hili.
1. Mat 12:38-39 lilikuwa ni ombi la kwanza la ishara, na Mat 16:1-4 na Mak 8:11-13 lilikuwa ni ombi la pili la ishara.
2. Katika matukio yote, Yesu alisema ama hawataweza kuona ishara kutoka mbinguni, au wataona ishara ambayo watu waliomsikia Yona waliiona.
3. Watu waliomsikia Yona hawakuana ishara yeyote ya miujiza, ila Yona tu. Yona hakuwahi kufanya muujiza wowote ambao ulirekodiwa kwenye Biblia.

S: Kwenye Mathayo 13, ni jambo gani lisilokuwa la kawaida kuhusu mifano?
J: Mat 13:3-52 ni ‘chiasm’, yaani, mtindo wa uandishi inayohusisha mtiririko wa mawazo na kisha kinyume chake na kufanya kama umbo la herufi ‘X’, lakini sio mkamilifu.
13:1-2 Yesu alikuja
-13:3-9 Mfano wa mpanzi, ulitolewa kwenye umati wa watu
--13:10-12 Wanafunzi wanauliza na Yesu anajibu
---13:10-17 Lengo la mifano (kwa watu wa nje)
----13:18-23 Maana ya mfano wa mpanzi
-----13:24-33 Mifano mingine mitatu iliyotolewa kwa umati wa watu "Ufalme wa mbinguni umefanana na . . ." (magugu, punje ya haradar, chachu)

kwenda nje ya mada
---13:34-35 Lengo la mifano (kwa wanafunzi)
----13:36-43 Maana ya mfano wa ngano na magugu

mwisho wa kwenda nje ya mada
-----13:44-48 Mifano mitatu zaidi iliyotolewa kwa wanafunzi "Ufalme wa mbinguni unafanana na . . ." (hazina, lulu, nyavu)
---- 13:49-50 Maelezo
- 13:51 Yesu anauliza na wanafunzi wanajibu
- 13:52 Mfano wa hazina mpya na ya zamani
13:53 Yesu anaondoka
Katika muundo huu, Mat 13:13-17 pia ni ‘chiasm.’

S: Kwenye Mat 13:1, kwa nini Yesu alikaa kwenye mtumbwi na kuongea na watu?
J: Yesu anaweza kuwa aliongea toka kwenye mtumbwi kwa sababu kwenye siku tulivu, ukubwa wa sauti yake utakwenda vizuri juu ya maji.

S: Kwenye Mat 13:10-13, kwa nini Yesu alieleza mfano huu kwa wanafunzi wake na si kwa umati wa watu waliomsikiliza?
J: Jibu linapatikana Mat 13:14-15. Yesu alikuwa na wanafunzi wengi (ikiwa ni pamoja na wale 70) na si kumi na mbili tu. Wakati huu, umati uliokuwa unamsikiliza ulionjeshwa mafundisho ya Yesu, kwa njia ambayo iliyowafanya wawe na kiu ya kutaka kujua zaidi. Yesu alikuwa mbaguzi hapa; alitoa maelezo kwa wanafunzi wake tu. Bila shaka, watu waliokuwemo kwenye umati uliomsikiliza nao walikuwa na uwezo wa kuchagua kuwa wanafunzi wa Yesu.

S: Je Mat 13:10-16 inasemaje?
J: Kuna mambo kadhaa muhimi katika kifungu hiki.
13:10 Baada ya Yesu kutoa mfano wa mpanzi kwenye Mat 13:1-9, wanafunzi walimwendea na kumuuliza kwa nini alizungumza kwa njia ya mifano. Swali hili halikuwa kwa ajili ya mfano wa mpanzi tu, bali kwa nini Yesu aliongea kwa mifano kwa ujumla.
13:11 Watu wengi hawakuwa na ufahamu au hawakukumbuka ufalme wa mbinguni.
13:12 Wale waliokuwa na elimu watapata maarifa zaidi. Wale wasio na elimu, hata ufahamu mdogo walio nao utaondolewa.
13:13 Kwa nini Yesu alizungumza na watu kwa njia ya mifano, badala ya kuelezea kila kitu kama alivyofanya kwa wanafunzi wake? Hebu tuangalie 2 Pet 2:21 na Rum 4:15; 5:13 kwa jibu. Endapo mtu atachagua kutokuufuata ukweli anaoujua kuhusu Mungu, itakuwa vema kwake kujua vitu vichache zaidi kweny hukumu ya mwisho.
13:14 inaonyesha kuwa watu watasikia ukweli wote, lakini hawataka elewa. Jambo hili HALIMAANISHI kuwa mtu awe na akili sana ili aweze kuwa muumini. Kufanya hivyo kungeenda kinyume cha 1 Kor 1:26-28. Badala yake tatizo la kufahamu vitu hata miongoni mwa Mafarisayo wenye ufahamu mkubwa na walio na elimika sana ni kuwa hawana nafasi ya neno la Yesu (Yoh 8:37), na ujumbe wa msalaba ni ujinga tu kwa watu walio na busara na hekima ya dunia hii ( 1 Kor 1:18-25). Nimeona watu wenye ufahamu mkubwa wakitoa visingizio vya maarifa vya kutokutaka kuamini jambo ambalo liko wazi kabisa kwenye Biblia.
13:15 Aya hii inaonyesha jinsi ambavyo mioyo ya watu ilivyo mizito. Wakristo wamejadili endapo Mungu ndiye aliyeufanya moyo wa Farao kuwa mgumu dhidi ya Musa na Waisraeli au Farao mwenyewe alifanya hivyo. Biblia inasema kuwa Farao aliufanya moyo wake mwenyewe kuwa mgumu katika maeneo nane, na kuwa Mungu aliufanya kuwa mgumu katika maeneo nane. Moja ya hukumu ya Mungu dhidi ya watu wanaoifanya mioyo yao kwa migumu ni kuifanya mioyo yao kuwa migumu zaidi.
Mwisho, utendaji huohuo wa Mungu unaweza kuwa na matokeo tofauti kwa watu wawili tofauti. Mwandishi mmoja toka kwenye kanisa la awali alieleza kwa njia hii: "nta huyeyushwa na tope hukaushwa na joto hilo hilo; kwa hiyo utendaji huohuo, uliofanywa kupitia mkono wa Musa, ulithibitisha ugumu wa Farao kwa upande mmoja, matokeo ya uovu wake, na kusalimu amri kwa umati mchanganyiko wa Wamisri walioondoka pamoja na Waebrania." Kitabu cha Origen kiitwacho De Principiis (mwaka 225-254 BK) kitabu cha 3 suraa ya 1.11, uk.311.
13:16 Pamoja na hayo, ingawa Yesu alikuwa na wanafunzi 12 aliowateua bayana, Yesu hakuwa na wanafunzi 12 tu; pia alikuwa na kundi pana la watu 70, na wanafunzi wengine pia. Wanafunzi wa Yesu walibarikiwa kwa kuwa na upendeleo wa kuyajua mambo haya, na ukweli kuwa hawakuyajua kama malipo ya vitu walivifanya au walistahili kwa kuwa walikuwa wamejifunza mambo hayo. Mungu angeweza kuamua kutuficha vitu vyote; lakini Mungu alipenda kuvifanya vifahamike kwetu.
13:17 inaenda mbali zaidi na kusema kuwa hata manabii waliokuwa wacha Mungu kwenye Agano la Kale walipenda kujifunza mambo haya, lakini Mungu hakuwafundisha; Mungu alisubiri hadi kuja kwa Yesu ndipo akayafunua.
Wakati mwingine watu wanadhani kimakosa kuwa Mungu anawiwa nasi kujaribu kwa bidii anayoweza kumfundisha kila mtu ukweli. Hata hivyo, ukweli ni kwamba, kama mtu atakataa ukweli ambao tayari anaufahamu kuhusu Mungu, Mungu halazimiki kwa namna yoyote ile kumlazimisha mtu huyo kuukubali ukweli huo. Jambo muhimu kutambua ni kuwa, kadri mtu asivyojua ukweli ni bora zaidi kwake (2 Pet 2:21). Lakini kwa watu wanaotaka kuufuata ukweli, Mungu anapenda kuwaonyesha ukweli zaidi na zaidi.
Ni kwa jinsi gani hasa watu wanakosa kusikia na wanaukosa ukweli. Yesu alielezea kwenye Mat 13:18-23.

S: Kwenye Mat 13:12, je Mungu hakutenda haki kwa kuwanyang’anya wale wasiokuwa navyo na kuwapa wale waliokuwa navyo?
J: Mungu hakuwa dhalimu. Kuna mambo matatu yanayotofautiana yanayofaa kuzingatiwa: haki na usawa, mshahara na zawadi, na kutimiza mahitaji na kutoa tuzo.
Haki ns usawa: Mungu ni mwenye haki kwa watu wote, lakini Mungu hatakiwi kufanya vitu vyote kwa namna moja kwa watu wote, kama Rum 9:6-18 inavyoeleza.
Mshahara na zawadi: Kwenye mfano huu endapo mfalme angeshindwa kulipa vitu vizuri alivyokuwa anadaiwa na mtu yeyote yule, jambo hilo lingekuwa dhuluma. Lakini unapowekeza fedha za mwajiri wako, mwajiri wako hatadaiwi hela hizo zote; mwajiri wako anadaiwa tu mshahara wako na kitu ambacho mlikubaliana kuwa atakupa. Mfalme kwenye mfano huu hakuwa anadaiwa na yeyote wa watumishi wake miji wowote ule. Alipompa mtumishi aliyekuwa na miji zaidi, hiyo ilikuwa ni zawadi ya neema ya bure, na mfalme (na Mungu) wanaweza kufanya kitu chochote wanachotaka.
Kutimiza mahitaji na kutoa zawadi: Mfalme aliwatunza watumishi wake wote kabla yeyote kati yao hajapewa kusimamia mji wowote. Miji ilikuwa tuzo, au marupurupu. Mungu atatimiza mahitaji yao yote kwa kiasi kikubwa sana kule mbinguni kwa kila mmoja wao (1 Kor 2:9), lakini zaidi ya hayo Mungu atatoa thawabu mbinguni kwa baadhi ya watu na si kwa wengine. Unaweza kusoma juu ya jambo hili kwenye 1 Kor 3:8-15.

S: Kwenye Mat 13:15, je hivi ndivyo Mungu afanyavyo mioyo migumu, kwa kutokulainisha mioyo yao na kufungua macho yao?
J: Sivyo kabisa. Mungu anasema kuwa endapo watamgeukia Mungu, Bwana atawaponya hakika. Hata hivyo, watawajibika na kutosikia kwa mioyo yao, kulikosababisha kutokumgeuka Mungu kwao.
Mungu anafungua macho ya vipofu, lakini mara nyingi huwa hafungui macho ya watu wanaofunga macho yao kwa nguvu. Mungu hulainisha mioyo ya watu, lakini halazimiki kulainisha moyo wa mtu yeyote ambaye tayari ameishaamua kuufanya moyo wake mgumu.

S: Kwenye Mat 13:30, je magumu yaliyokusanywa kabla ya ngano yana umuhimu gani?
J: "Magugu" huenda yakawa ni majani yaitwayo darnel yanayonekana kama ngano wakati yakiwa machanga. Katika kilimo ni busara kupalilia kabla ya kuvuna ngano. Hukumu inawang’oa watenda maovu ili waiingie mbinguni. Si kwamba tunaondolewa kwenye ulimwengu ambako ni asili ya magugu. Badala yake, magugu yanapelekwa nje ya ulimwengu wa Mungu, ambako ni nyumbani kwa watoto wa Mungu kwa jinsi ya kiroho.

S: Kwenye Mat 13:32 na Mak 4:30-34, kwa nini chembe ya haradali ni ndogo kuliko zote?
J: Kwanza kabisa, kulikuwa na aina mbili za mbegu ya haradali huko Palestina: haradali nyeusi ambayo ilikuwa inalimwa na watu, na haradali mwitu. Yesu alimaanisha haradali nyeusi, kwa sababu alikuwa anaongelea mbegu zinazopandwa, na watu hawakuwa wanapanda mbegu yeyote iliyokuwa ndogo kuliko chembe ya haradali huko Palestina.
Chembe ya haradali ni ndogo sana kwa ukubwa, na mbegu ndogo kuliko zote za mazao yaliyokuwa yanalimwa Palestina. Yesu alikuwa anaongea na watu akitaja mbegu za mazao yanayopatikana katika nchi yao.
Hata hivyo, kwa watu wanaopenda habari zaidi, neno la Kigiriki la kitu kidogo zaidi kwenye Mat 13:32 na Mak 4:30-34 ni microteron, ambalo linaweza kumaanisha ndogo kwa ukubwa au umaana, kwa lugha ya picha. Neno la mbegu lililotumika kwenye vifungu vyote viwili ni spermaton, linaweza kumaanisha kuwa kitu kinachopandwa. Bila kujali endapo Yesu alikuwa anazungumza Kiaramu au Kigiriki, alikuwa anaongelea mbegu zilizokuwa zinapandwa.

S: Kwenye Mat 13:32 na Mak 4:30-34, chembe ya haradali inawezaje kushikilia kiota cha ndege?
J: Ingawa ndege wanaweza kujenga kiota kwenye kichaka kidogo, endapo itawapasa kufanya hivyo, hili siyo jibu. Chembe ya haradali inaweza kukua na kuwa mti wenye urefu wa hadi futi kumi (mita tatu hivi), urefu ambao ni mkubwa wa kutosha kwa ndege kujenga kiota.

S: Kwenye Mat 13:33, je chachu ina umuhimu gani hapa?
J: Yesu alisema kuwa chachu katika mfano huu inawakilisha ufalme wa mbinguni, wakati kwenye mifano mingine chachu ni mbaya. Kanuni muhimu kanuni ya kutafsiri tunayoweza kujifunza hapa ni kuwa huwezi kuchukua maana ya ishara toka kwenye mfano mmoja, na kuiweka maana ileile ya ishara hiyo kwenye mifano mingine yote.

S: Kwenye Mat 13:33, katika mfano huu, kwa nini mwanamke kwenye mfano huu alificha chachu kwenye vipimo vitatu vya mlo?
J: Mikate mitatu ya unga wa ngano ni mlo kamili wa familia. Ilihitaji kiasi kidogo cha chachu kubadili hali ya mlo wote.

S: Kwenye Mat 13:34, ni kwa jinsi gani Yesu alizungumza kwa mifano tu kwani mahali pengine kama kwenye Mahubiri ya Mlimani Yesu hakutumia mfano wowote?
J: Mat 13:34 inafafanua kuwa jambo hili wakati (kuongea kwa mifano) ni wakati Yesu alipokuwa anazungumza na umati wa watu. Wakati anaongea na wanafunzi wake alieleza kila kitu. Wakati watu wengine walipokuwa miongoni mwa wasikilizaji wake, Hotuba ya Mlimani ilitolewa kwa wanafunzi. Isitoshe, Mat 3:34 inaongelea wakati Yesu alipotoa mafundisho haya, na si lazima iwe kabla au baada ya kipindi hiki katika huduma yake.

S: Kwenye Mat 13:38, je kila mtu ni mwana wa ufalme?
J: Hapana. Kama aya hii inavyoonyesha, kabla ya kuja kwa Kristo hatuwi wana wa ufalme. Efe 2:3 inasema kuwa sisi (akiwemo Paulo), tulikuwa wana wa ghadhabu kabla hatujaenda kwa Kristo.

S: Kwenye Mat 13:52, kwa nini Yesu alizitaja hazina mpya na za zamani?
J: Hii ilikuwa ni njia ya upole ya ya kusema kuwa wanapaswa kuendelea kuyathamani mambo waliojifunza zamani sawa na mambo mapya ambayo Yesu anayasema.

S: Kwenye Mat 13:53-58, je Yesu hakuwa nabii kwani unabii unaweza kuwepo Israeli endapo tu nchi inapokaliwa na wengi wa Wayahudi waliopo duniani. Wakati wa Ezra (karibu mwaka 300 KK), wakati sehemu kubwa zaidi ya Wayahudi walikataa kutoka Babeli na kwenda Israeli, unabii uliisha pale manabii wa mwisho -- Hagai, Zakaria na Malaki walipokufa (Myahudi mmoja alileta pingamiza hili)
J: Wazo hili si sahihi kwa sababu tatu:
1) Hakuna aya kwenye Biblia inayosema hivyo; kanuni hii si ya kweli.
2) Daniel na Ezekiel walikuwa manabii wakati wa uhamisho. Wakati huo, wengi wa Wayahudi duniani hawakuwa wanaishi Palestina. Ukweli ni kwamba, Daniel na Ezekieli walikuwa manabii walioishi nje ya Israeli, ingawa Daniel aliishi Uyahudi alipokuwa kijana.
3) Hatupaswi kumwambia Mungu Mwenyezi kitu ambacho tutamwambia kuwa anaweza kufanya na kitu ambacho hawawezi kufanya!
Bila kuangalia kuwa wengi wa Wayahudi waliishi Palestina wakati wa Kristo (endapo walikuwa wengi zaidi au la mimi sijui), haijalishi, kwa sababu Mwenyezi Mungu inaweza kutuma nabii wakati wowote anaotaka.
Biblia (Agano la Kale na Agano Jipya) inataja vitu ambavyo Mungu hafanyi (kubadilisha mawazo yake kwenye Hes 23:19; 1 Sam 15:29, n.k.) lakini kuna mambo manne tu kwenye Biblia nzima ambayo Maandiko yanasema Mungu HAWEZI kufanya. (Unapaswa kuangalia kwenye Agano Jipya ili kuyasoma mambo haya.) Mambo haya manne ni: Mungu hawezi kujaribiwa na uovu (Yak 1:13), Mungu hawezi kusema uongo (Ebr 6:18), Mungu hawezi kuapa kwa mtu yeyote mkubwa kuliko Yeye mwenyewe (Ebr 6:13), na Mungu hawezi kujikana (2 Tim 2:13). Zaidi ya hayo, siwezi kusema kitu ambacho Mungu hawezi kufanya. Kwa unyenyekevu, nitaangalia tu kwenye Biblia ili niweze kujifunza mambo ambayo Mungu amechagua kuyafanya, na yale ambayo amechagua kutokuyafanya.

S: Kwenye Mat 13:55, je Yesu aliwezaje kuwa na kaka na dada zake kwani (kulingana na kanisa Katoliki) Mariamu alikuwa bikira siku zote?
J: Mat 1:25 inajibu swali hili kiwazi kabisa: "but [Joseph] did not have marital relations with her [Mary] until she gave birth to a son, whom he named Jesus." Kwa hiyo, Mariamu alikuwa bikira Yesu alipozaliwa, lakini baada ya hapo, Mariamu na Yusufu alikuwa na watoto wengine.
Wakatoliki kwa ujumla wanajibu kuwa katika jamii nyingi za Mashariki ya Kati, binamu waliweza kuitwa kaka na dada pia.
Hata hivyo, hakuna sehemu kwenye Biblia inayofundisha kuwa Mariamu alikuwa bikira daima. Tofauti na hivi, kuna sehemu nyingine ambapo kaka au dada wa Yesu wanatajwa: Yoh 7:5, Gal 1:19, Mak 3:31; Yoh 2:12; na Mdo 1:14. Itakuwa ajabu endapo walikuwa binamu tu, kwamba neno "binamu" halilikuwa limetumika hata mara moja sehemu zote hizi sita.
Kama angalizo la kihistoria, sehemu pekee mbili kabla ya Baraza la Kanisa la Nikea ambapo Mariamu aliitwa bikira ni:
Hippolytus askofu wa Portus (mwaka 225-235/6 BK) alimwita Mariamu bikira wa milele, kwenye Against Beron and Helix kipande cha 8, uk.234.
Petro wa Alexandria (mwaka 306, 285-311 BK) "wa Mungu, na bikira wa milele, na, wa kweli, wa Mariamu Mama wa Mungu" kwenye kipande cha 5.7, uk.282.
Mariamu alisemwa rasmi kuwa "bikira wa milele" kwenye Baraza la Kanisa la Constantinople II (mwaka 553 BK), sura ya 2, uk.312. Mwaka huohuo Papa maneno hayohayo kwenye barua yake, uk.322.

S: Kwenye Mat 13:55-56, kwa nini nabii hakuheshimika kwenye mji wa nyumbani kwake?
J: Yesu hakuwa anatoa amri au unabii, bali maelezo ya mambo yaliyokuwepo. Manabii hawakuwa wanaheshimiwa sana miongoni mwa watu waliokua nao. Kwa mtu aliyekulia sehemu fulani, na kupitia mengi ya mambo ya sehemu hiyo, inaweza kuwa vigumu kuamini kuwa Mungu anaweza kumtumia mtu wa kawaida katika njia isiyokuwa ya kawaida. Kwa bahati mbaya, kuna kweli kiasi kwenye usemi kuwa "kufahamiana kunaweza kuleta dharau."

S: Kwenye Mat 13:58, je kutokuwa na imani kwa watu kuliwezaje kumzuia Yesu kufanya mambo makubwa?
J: Aya hii haisemi kwamba Mungu Mwenyezi hakuweza kufanya muujiza hapa. Badala yake, Yesu alimaua kutokufanya muujiza wowote ule hapa kwa sababu ya kutokuamini kwao.

S: Kwenye Mathayo 14, kwa nini kifo cha Yohana Mbatizaji kimewekwa mahali kilipowekwa na Mathayo?
J: Ingawa haisemi hivi, na Mathayo angeweza kuweka kumbusho hili la ghafla popote pale, sababu ya kuweka hapa inaweza kuwa ni kuashiria sababu ya Yesu kutaka kuondoka mbele ya umati wa watu wakati huu. Yesu alijua kuwa wangeweza kuja kumuua, na Yeye alitaka kusubiri hadi atimize mambo mengine kabla hajasulubiwa.

S: Kwenye Mat 14:3-4, kwa nini hasa Yohana Mbatizaji alimtaja hadharani Herode Antipas kuwa hakuwa sahihi?
J: Kwanza, genealogical background na kisha jibu.
Background:
Herode Antipas: mtoto wa Herode (Mkuu) na Malthace, mmoja wa wake zake kumi.
Filipo: mtoto wa Herode (Mkuu) na Mariamne II.
(usimchanganye na mtoto mwingine wa Herode (Mkuu) aliyeitwa Gavana Filipo (Philip the Tetrarch)
Aristobulus: mtoto wa Herode (Mkuu) na Mariamne I.
Herodias: binti wa Aristobulus
Jibu: Herode Antipas alikuwa baba mdogo nusu wa Herodias, lakini jambo hili LILIRUHUSIWA kwa mujibu wa Law 18:1-17 na 20:12,14. Kumtaliki mke KULIRUHUSIWA wakati wa Agano la Kale. Tatizo lilikuwa kwamba Law 18:16 inakataza bayana mtu kuoa mke wa ndugu (kaka) yake, na Herodias alikuwa mke wa Filipo, ndugu yake Herode Antipas.

S: Kwenye Mat 14:6-12, kwa nini jambo hili lenye kutisha limo kwenye Biblia?
J: Wakati mwingine watu wanaweza kuwa na mtazamo wenye matumaini bandiala maisha duniani. Maisha wakati mwingine ni yanatisha pale watu waovu waovu wanapotawala. Tunaweza kujifunza hapa kuwa hata waamini kama Yohana Mbatizaji wanaweza kutendewa mambo yasiyo ya haki katika maisha haya.

S: Kwenye Mat 14:15, kwa kuwa mahali hapa palikuwa ni jangwa, inakuwaje pawe na majani kwa mujibu wa mstari wa 19?
J: Hili halikuwa jangwa kavu, lakini sehemu ya faragha. Pia, Palestina ina misimu miwili: msimu wa mvua na msimu wa ukame, na yaelekea tukio hili lilitokea msimu wa mvua. Msimu wa mvua haukuwa na pepo za msimu zinazotoka baharini kama Asia ya Kusini, lakini Mto Yordani ulikuwa mkubwa sana kiasi kushindwa kuuvuka muda huo na palikuwa na majani mengi ya kijani katika maeneo ambayo yalionekana kama jangwa wakati wa kiangazi.

S: Kwenye Mat 14:24-32, je Wakristo wanawezaje kukabili dhoruba bila woga?
J: Kifungu hiki kinafundisha namna ya kukabili dhoruba bila woga na jinsi ya KUTOKABILI dhoruba bila woga.
1. Usiogope Mungu anapofanya kazi ambayo haikutegemewa (14:25-26).
2. Wakati Yesu anatuambia tuwe jasiri, tunatakiwa kuwa jasiri na kufanya kazi bila woga (14:27-28).
3. Tunapaswa kumtii Yesu, tukijua kuwa Yeye si tu mkuu kuliko hatari iliyo karibu nasi, Yeye pia ni mkuu zaidi kuliko hofu, mashaka, na udhaifu wetu (14:29).
4. Mwangalie Yesu, si upepo au hatari nyingine zozote zinayoweze kutokea (14:30).
5. Wakati tumefanya makosa au kutia shaka, tunapaswa kumlilia Yesu ili atuokoe (14:30-32).
6. Baada ya kuwa salama, usisahau kumwabudu Mungu (14:33).

S: Kwenye Mat 14:25, wakati wa zamu ya nne ya usiku ni saa ngapi?
J: Usiku uligawanywa katika zamu nne, na zamu ya nne ilikuwa karibu saa tisa usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.

S: Kwenye Mat 15:1-3, je Yesu alikuwa anapinga kuosha mikono?
J: Hapana. Ingawa hakupinga usafi, Yesu alipinga kufanya uoshaji wa mikono kuwa taratibu ya kidini. Siku hizi, mambo mengine ya kiafya, kama vile lishe bora, madawa yatokanayo na mimea, na mazoezi ni mazuri, lakini nayo pia yanaweza kuwa sanamu endapo watu wataabudu afya zao badala ya Mungu.

S: Kwenye Mat 15:3-6, wazo la Korban lilitoka wapi?
J: Neno lenyewe, na dhana ya kutoa kitu kwa Mungu, zinapatikana katika Law 1:2-3, 2:1, 3:1, Hes 7:12-17. Hata hivyo, Mafarisayo waliruhusu mtu kuuacha wajibu wa kuwatunza wazazi wao kwa kuweka wakfu kwa Mungu msaada waliokuwa watoe kwa wazazi wao.
Mafarisayo walikuwa wamechanganya vipaumbele vyao hapo. Kumruhusu mtu kutoa vitu alivyonavyo kwa Mungu kulipewa kipaumbele zaidi ya kufanya mambo ambayo Mungu anayataka, ambayo ni pamoja na kutunza wazazi wetu. Jambo hili linaweza kutokea wanapojizatiti kutii mapokeo zaidi ya kumtii Mungu.

S: Kwenye Mat 15:8, kwa nini watu wanachugua kumkaribia Mungu kwa midomo wakati mioyo yao iko mbali naye?
J: Watu wanakuja kwenye dini, na kwa Mungu kwa jina tu kwa Mungu, na si wote walio bora. Wengine wanakuja ili wasifiwe na watu wengine, wengine wanatafuta fedha, na wengine wanatafuta wake au waume wa kuoana nao.
Wengine wanatafura kazi ambayo itawawezesha kuwasaidia watu wengine, na hili ndilo lengo lao kuu, na si kwa sababu wampenda Mungu. Inapotokea kuwa hivyo, kuna mashirikia mengi ya yenye kutoa misaada kama vile Msalaba Mwekundu, Peace Corps, Goodwill, au UNICEF. Wanapaswa kujiunga nayo, na kutokujionyesha kuwa wanampenda Mungu kwa kutaka kufanya kazi kupitia kanisa la kikristo.
Kama nyongeza, Biblia inasema kuwa Wakristo wanapaswa kusaidia maskini, watu wasiojiweza, yatima, n.k. Jambo hili halimaanishi kuwa tutoe pesa kwa mashirika ya kikristo tu. Ni vizuri kuyawezesha hata mashirika ya misaada ya jamii yasiyohusiana na dini.

S: Kwenye Mat 15:9, ni lini mapokeo ya wanadamu yanakuwa mazuri na ni lini yanakuwa mabaya?
J: Mapokeo hupitisha imani za zamani na maoni kuhusu mafundisho na sheria kwenye vizazi vinavyofuata. Kuna mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
Ovu: Endapo mapokeo ya zamani yalikuwa si sahihi au mbaya, basi kosa na huenda dhambi zinaweza kuwa zinafunzwa na kunakiriwa. Biblia inaongelea mapokeo ya dhambi kama vile Malkia wa Mbingu kwenye Yer 44:17-19.
Tupu: Mara nyingi mapokeo huwa hayana maana (Kol 2:16-19). Yakichukuliwa kwa uzito, mapokeo haya yanaweza kudhoofisha kujitoa kwetu kwa Mungu. Biblia inaongelea mila tupu na potofu kwenye Kol 2:8 na 1 Tim 1:4.
Korbani: Hata kama maoni au matendo ya zamani hayakupingana na Maandiko, watu wana njia ya kuyafanya mapokeo ya kibinadamu yawe kama Maandiko, na jambo lililokuwa maoni ya binadamu sasa linakuwa katika macho ya watu, "Mungu anasema" na matendo ya binadamu, ambayo huenda yalikuwa sahihi kabisa wakati na kwenye mazingira fulani, yanaishia kudhaniwa kuwa ni "sheria ya Mungu" kwa wakati na hali zote. Mapokeo huwa hata yanapewa kipaumbele kuliko neno la Mungu na baadhi ya watu, kama wale ambao wanaofanya "Korbani" kwenye Mak 7:10-13.
Sheria ya Mungu: Tunapaswa kufanya vitu ambavyo Mungu ameamuru, kama vile ubatizo wa maji na meza ya Bwana. Hata hivyo, hatupaswi kuvifanya kwa sababu ni mapokea ya kikristo, bali kwa sababu Mungu anatuhitaji tufuate. Tunapaswa kuwa makini kutokuifanya alama kuwa muhimu kuliko ukweli wenyewe. Hatupaswi kufuata sheria tu (Mak 7:6-7), bali tunatumika katika roho hali mpya, si njia ya zamani ya sheria iliyoandikwa (Rum 7:6; 2:29, Kol 2:14) .

S: Kwenye Mat 15:10-20 na Mak 7:15-23, kwa nini Yesu alitangua sheria zinazohusu vyakula za Agano la Kale hapa?
J: Yesu hakutangua sheria zinazohusu vyakula za Agano la Kale, alizizidi. Kuna mambo manne ya kuzingatia hapa.
1. Ingawa Yesu na wanafunzi wake wakati mwingine walivunja mapokeo ya kibinadamu yaliyokuwa yanafuatwa na Mafarisayo, wakiishi katika utii wa sheria za Agano la Kale.
2. Hata kwenye Agano la Kale, Mungu alipendezwa zaidi na utii wao, na ulaji wa vyakula kama ilivyotakiwa na sheria ulikuwa ni njia moja tu kwao kuonyesha utii wao.
3. Baada ya kipindi kipya kilichoanzishwa na kufufuka kwa Yesu, wanafunzi walichagua kutokula baadhi ya nyama. Malaika wa Mungu alikuja na kumueleza Petro aliyekuwa anasita kula kwenye Mdo 10:11-16. Petro angewezaje kubishana na malaika wa mbinguni?
4. Waislamu hawapaswi kuwa na tatizo lolote na jibu hili, kwani Muhammad anadaiwa kufanya hivyo hivyo. Aliongeleaa sheria zilizotanguliwa, (ingawa kutangua ni dhana tofauti kidogo na Agano Jipya kupitia kwa Yesu). Pia, alionyesha kuwa Waislamu wanaweza kula nyama ya ngamia wakati Agano la Kale linaichukulia nyama ya ngamia kuwa kama nyama ya nguruwe (Law 11:4, 7, 26, Kum 14:7, 8).

S: Kwenye Mat 15:11, 17-18, ni kwa vipi kitu kinachomtoka mtu tu ndicho kimtiacho unajisi?
J: Muktadha hapa umetolewa kwenye Mat 15:20, ambapo Mafarisayo waliangalia zaidi kula bila kuosha mikono wakati Yesu aliangalia zaidi kuwa safi ndani.
Kama ulikuwa unapika kitu kwenye chombo, na kimiminika kilikuwa kinaongezwa polepole na kinachukuliwa polepole, je ungeweza kupima kimiminika kitokacho au kiingiacho kuona kama ndani kulikuwa na joto sahihi kabisa? Bila shaka, unapaswa kupima kimiminika kinachochukuliwa. Vivyo hivyo, Yesu alikuwa anasema usishikwe sana na chakula, kwa sababu ni kitu kitokacho ndicho kinachoweza kutia unajisi.

S: Kwenye Mat 15:12, je lingekuwa jambo la ajabu kwa baadhi ya Mafarisayo kutoka Yerusalemu kwenda kumtafuta Yesu ili kumuuliza maoni yake kuhusu usafi wa mwili?
J: Hili halikuwa ndilo lengo lao. Swali hili lilikuwa ni kisingizio cha kutaka kumnasa. Shida yao halisi haikuwa usafi wa mwili; hawakufahamu kanuni ya vijidudu vya ugonjwa. Badala yake shida yao ilikuwa ni vitu vilivyoongezewa kwenye sheria inayohusu utaratibu wa kidini wa kuosha. Walimwona Yesu kuwa tishio la ukuu wao kwani aliwaambia watu kitu gani ni mapenzi ya Mungu kwao.

S: Kwenye Mat 15:12, kwa nini Yesu hakuwa na nia ya kuwakasirisha Mafarisayo?
J: Nyakati zingine Yesu alinuia kufanya hivyo; alitaka wajisikie vibaya. Hasa kwenye Mathayo 23, Yesu aliwakemea sana kwa sababu mbili tofauti. Kwa kuwa walisika kukemewa huko, baadhi yao wanaweza kuwa walichukua muda, na kuyafikiria maneno ya Yesu, na kutubu. Pili, bila kujali toba ya Mafarisayo, umati wa watu uliweza kusikia na kujua kutokuwaamini Mafarisayo waliomkataa Yesu.

S: Kwenye Mat 15:14, kwa nini Mungu wakati mwingine huruhusu vipofu waongozwe na vipofu wengine?
J: Kama mtu mmoja alivyosema, hakuna mtu aliye kipofu kuliko yule anayekataa kuona. Mungu huruhusu watu kwenda mahali wanapotaka kwenda. Swali bora zaidi ni kuwa kwa nini kipofu anamruhusu, au hata anapendelea kuongozwa na kipofu mwingine?

S: Kwenye Mat 15:21-29 na Mak 7:24, kwa nini Yesu alikwenda Tiro na Sidoni?
J: Kwa kuangalia kwa mara ya kwanza (na kwa haraka), miji hii isiyokuwa ya Kiyahudi inaonekana kuwa mbali sana na njia aliyokuwa anaipitia Yesu. Mistari inayofuata inaonyesha kuwa alitumia pepo kufukuza mapepo (Mak 7:29), na kwamba watu wengi kutoka pwani ya Foenike walimsikiliza Yesu. Tiro ilikuwa juu karibu maili 35 (kilomita 56) kutoka bahari ya Galilaya, na Sidoni ilikuwa maili 25 (kilomita 40) kutoka Tiro.

S: Kwenye Mat 15:21-22, je Yesu alipokuwa na mwanamke Mkanaani, inaonekana kuwa aliagiza wawapende Wayahudi na wale tu wanaomwabudu Mungu katika namna inayokubalika? (kama Muislam Ahmad Deedat alivyosema)
J: Hapana, hoja hii ni ngumu kuithibitisha kwani Yesu alikwenda mbali na njia yake ili kwenda ukanda wa Tiro na Sidoni.
Yesu alitumwa kwanza kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli, lakini baadaye alivuka Bahari ya Galilaya (mara nyingi). Umuhimu wa jambo hili ni kuwa kwa kiasi kikubwa Wayahudi waliishi upande wa magharibi ya Bahari ya Galilaya, lakini watu wa mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na wapagani waliokuwa wanafuga nguruwe, waliishi upande wa mashariki. Hata kabla ya jambo hili, Wasamaria hawakumuabudu Mungu kwa namna inayokubalika, na Yesu alizungumza na mwanamke Msamaria mwanzoni mwa huduma yake.

S: Kwenye Mat 15:24-26, je Yesu alikuwa mbaguzi wa rangi kwani alimlinganisha mwanamke Mkanaani (Msiro-Foenike) na mbwa? (kama Muislam Ahmad Deedat alivyosema)
J: Hebu tujibu swali hili kwa kuuliza swali moja. Wakati Yesu aliposema kuwa ametumwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli alikuwa wapi? Jibu ni kwamba alikuwa ametoka Israeli, na kutembea zaidi ya maili 30 (kilomita 48), umbali ambao kunguru wanaoruka, juu au kuzunguka milima na kwenda Tiro, mji ambao haukuwa na haujawahi kuwa mji wa Kiisraeli. Yesu alikwenda huko kuongea na, si mwanamke wa Kiyahudi aliyeishi nje ya Israeli, bali na mwanamke aliyetambuliwa kibayana kuwa mtu wa mataifa. Lakini alipokuwa amekwishaenda maili za ziada (au maili 30 za ukweli kweli), Yesu alitaka mwanamke awe na uhakika kwamba hakuwa na anafikiri kuwa alikuwa anapata kitu alichokuwa na haki kukipata, bali alikuwa anapata kwa neema. Pamoja na hayo, neno la Kigiriki la "mbwa" hapa kwenye Mat 15:26 linamaanisha "kitoto cha mbwa" au "kijibwa cha kupakata", na si mbwa mwitu.

S: Kwenye Mat 15:21-29 na Mak 7:27-29, je Yesu na mwanamke Msirofonike walizungumza nini hasa?
J: Mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1. Baada ya Yesu kwenda pwani ya Foinike, mwanamke alimwuliza Yesu jambo moja, kumto pepo aliyempagawa binti yake. Kumbuka kuwa hapakuwa na ushahidi kuwa huyu mwanamke Msirofoinike, aliyeitwa Mgiriki, alibadili dini na kuwa Myahudi au hata kumwamini Mungu wa kweli.
2. Baada ya kutembea umbali mkubwa namna hii, maili nyingi nje ya Israeli, Yesu alimfahamisha kinaga ubaga kuwa ujumbe wa Mungu ulikuja kupitia kwa Wayahudi, ambao wanapaswa kuponywa kwanza (Marko 7:27). Kwa maneno mengine, Yesu hakuwa anaenda kumtimizia ombi lake bila ya yeye (mwanamke) kujitoa kuuamini ujumbe wa Mungu, kama ulivyotolewa kwa Wayahudi.
3. Mwanamke huyu alikubali kwa unyenyekevu kuja kwa Yesu akiafiki matakwa yake (Yesu), si matakwa mengine yeyote yale. Sisi pia tunapaswa kuamini neema ya Mungu.
4. Ingawa watu wa mataifa na mbwa hawakuwa wanathaminiwa sana na Wayahudi, Yesu hakutumia neno la kawaida kwa mbwa hapa. Hili neno linaweza kutafsiriwa vizuri zaidi kuwa "kama mbwa" au "kitoto cha mbwa." Warumi na Wagiriki walikuwa wanawathamini mbwa sana. Yesu alitumia neno ambalo linaweza kuwa na maana mbili tofauti moja ikiwa rahisi kueleweka na nyingine ngumu kueleweka la kitu kinachothamiwa na Wayahudi kuthaminiwa na watu wa mataifa mengine kwa kumlinganisha yeye (mwanamke Msirofoenike) na mnyama kipenzi. Hata hivyo, Yesu aliweka wazi jambo hili kuwa ujumbe wake ulikuwa kwa Wayahudi kwanza. Kama Mungu amembariki sana mtu mwingine, na si sisi, bado tunatakiwa kuwa na furaha kwa sababu ya baraka ambazo Mungu ametupa.
Kwa muhtasari, mwendo mrefu wa Yesu, pamoja na maneno yake ya mkato, yanaonyesha kwa uzuri sana kweli kinza kuwa Yesu atatembea umbali mrefu ili kutufikia sisi, lakini tunapaswa kuja kwake bila kiburi na tukifuata matakwa yake, sio yetu.

S: Kwenye Mat 15:24, je "kondoo hawa waliopotea wa nyumba ya Israel" ni watu wanaodaiwa kuhamia kutoka Israeli na kwenda Marekani karibu na wakati wa Kutoka kama inavyofundishwa na Mmormoni Joseph Fielding Smith kwenye Doctrines of Salvation 1975 juzuu ya 3, uk.214?
J: Hapana. Tafsiri hii haikuwa inafahamika kabisa kwa Wayahudi au Wakristo wowote wale. Yesu hakuwa anaongelea watu waliokuwa wameopotea kijiografia, lakini wale waliokuwa wamepotea kiroho. Yesu alikuwa mwokozi, si GPS. Yesu aliwaagiza wanafunzi wake kwenda "kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli . . ." (Mat 10:6-7), na walitimiza jambo hilo katika siku zilizofuata kwa kwenda Israeli yote si kupanda ndege na kwenda Marekani.

S: Kwenye Mat 16:1, 4, kwa nini haikuwa sahihi kumwomba Yesu ishara kutoka mbinguni?
J: Haikosi ilikuwa ajabu kwa wanafunzi kusikia Mafarisayo na Masadukayo wakiomba kupewa ishara mara tu baada ya Yesu kufanya miujiza yote hii, mingi kati ya hiyo mbele ya Mafarisayo na Masadukayo. Miujiza ya Yesu ilikuwa tayari imewasaidia viwete, vipofu, na watu waliopagawa na pepo, na Mafarisayo wakaomba ishara kutoka mbinguni, ambayo haitamsaidia mtu yeyote. Yesu alikataa kufanya kitu chochote kwa ajili ya kutimiza matakwa yao.

S: Kwenye Mat 16:2-4, je mzunguko wa asubuhi na jioni unahusika vipi na alama za nyakati?
J: Mzunguko unaoweza kutabirika wa mchana na usiku ni ukweli rahisi sana ambao hata watoto wanaweza kuutambua. Yesu anasema kuna mizunguko mengine pia, kama vile ishara ya kuja kwake, ikfuatiwa na kuja kwake kwenyewe. Yesu atakuja mara ya pili, na nyingi za ishara zilizotangulia kuja kwake kwa mara ya kwanza zitakuwepo pia kabla ya kuja kwake kwa pili.

S: Kwenye Mat 16:4, ishara ya nabii Yona ilikuwa ni ipi hasa?
J: Kitu alichokisema Yesu ni kuwa hapakuwa na ishara yeyote ya muujiza isipokuwa ushuhuda wa mtu huyu aliyekuwa anamcha Mungu.

S: Kwenye Mat 16:7-11 na Mak 6:52, je mikate mitano na watu 5,000, na mikate saba na watu 4,000?
J: Kuna mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
Yesu ni mkate wa uzima. Kwa kuwa aliweza kuwalisha watu wengi sana, hawakuwa na haja ya kuwa na mashaka kuwa wamechukua mikate yeyote au la.
Kwa ujumla, Yesu Yesu ameyashughulikia, na hawapaswi kuwa na hofu kuwa Mungu hataweza au hatataka kuyashughulikia katika siku zijazo.
Kufundisha somo hilohilo tena, kwa kuwa Marko anasema wanafunzi wake hawakuelewa lengo la kuwalisha mara ya kwanza.
Masomo mawili yanaweza kuwa yamekusudiwa hapa: moja kuwa Mungu huwalisha Wayahudi, na pia kuwa Mungu huwalisha watu wa mataifa mengine.

S: Kwenye Mat 16:7-11 na Mak 8:19-20, je Yesu anasema umuhimu wa namba hizi ni nini?
J: Wako watu wanaoweza kuona umuhimu wa kimafumbo katika ile mikate mitano na watu 5000, na vitabu vitano vya sheria kwa ajili ya Wayahudi katika tukio la kwanza la kulisha watu, na mikate 7 (namba kamili) na watu 4000 (4 huenda ikiwa inawakilisha pembe nne za dunia) kwenye tukio la pili la kulisha ambalo liliwahusu watu wa mataifa mengine kwa ujumla.
Hata hivyo, kuna maelezo rahisi zaidi. Yesu akiwepo, idadi ndogo sana ya mikate inaweza kulisha idadi kubwa ya watu.

S: Kwenye Mat 16:8, kwa nini Yesu aliwaambia wanafunzi kuwa wana imani haba hapa?
J: Hawakuwa na wasiwasi kuhusu chakula chao kwa sababu ya ukomo wa ufahamu wao, ukizingatia mambo yote waliyoyaona. Badala yake, walitilia mkazo matatizo yao ya muda mfupi, na kuepoteza mtazamo wa jinsi Mungu anavyoweza kufanya.
Wakati mwingine siku hizi, Wakristo wanaweza kuwa na wasiwasi, si kwa sababu hawajajifunza kiasi cha kutosha, bali wanajishughulisha zaidi na matatizo yao hata wanapoteza mtazamo wao juu ya Mungu.

S: Kwenye Mat 16:11-12, je mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo yanafananaje na chachu kwenye mkate?
J: Chachu ianaweza kuwa kitu kidogo sana cha kuongezea kwenye pishi, lakini ikawa na athari kubwa kwenye mkate wote. Kadhalika baadhi ya mafundisho yanaweza kuwa kitu kidogo sana cha kuongezea, lakini yakawa na athari mbaya sana.

S: Je Mat 16:11-12 inaonyesha kuwa Injili hii iliandikwa miaka ya baadaye zaidi, kwani mwandishi hakuweza kutofautisha kati ya Mafarisayo na Masadukayo?
J: Kinyume na madai ya baadhi ya wakosoaji wenye kutilia shaka msimamo wa asili, hakuna kitu kama hicho. Kusema kuwa watu wajihadhari na mafundisho ya makundi mawili haimaanishi kuwa mwandishi hakuweza kutofautisha makundi hayo mawili. Kisiasa, tunaweza kusema kuwa tunapaswa kujihadhari na mafundisho ya mlengo wa kushoto zaidi na ya wa kulia zaidi.

S: Kwenye Mat 16:13-14 na Mak 8:27-29, kwa nini Yesu alitaka kujua watu wengine walikuwa wanasema Yeye ni nani?
J: Hii inaitwa njia ya ufundishaji ya Socrates, kwa kuuliza maswali. Mara nyingi inafaa zaidi kuuliza swali ambalo tayari unajua jibu lake. Inaweza kukufahamisha mtu anayejibu anafikiria nini, na hata kumsaidia mwenye kujibu kupanga mawazo yake.

S: Kwenye Mat 16:16-17, je Petro aliwezaje kujua jambo hili kwa msaada wa Roho Mtakatifu?
J: Inavyoonekana Petro alikuwa bado hajamsikia Yesu akisema jambo hili waziwazi. Petro hakusema, "Nadhani . . ." au "Natumaini . . ." lakini alijua kwa hakika. Isitoshe, ni jambo moja kwa mtu kumwambia Petro ukiri huu, na jambo jingine kwa Petro kuamini hii yeye mwenyewe.

S: Kwenye Mat 16:18, je Wakatoliki na Waprotestanti wanaweza kukubaliana vipi kuhusu aya hii?
J: Kuna mambo saba ambayo Wakatoliki na Waprotestanti wanaweza kukubaliana nayo.
1) Mat 16:16-18 haisemi chochote kuhusu watu warithi wa Petro. Kwa kweli, hakuna aya Biblia inayosema kitu chochote kuhusu warithi wa Petro.
2) Kwa hakika kanisa limejengwa juu ya "mwamba" wa mtume huyu; hata hivyo kanisa limejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii wote kwa mujibu wa Efe 2:20. Petro ni msingi mkuu wa kanisa, lakini yeye si tu msingi mkuu pekee, kama Ufu 21:14 inavyosema kuna misingi kumi na miwili ya Yerusalemu Mpya, na hiyo inawawakilisha mitume kumi na wawili wa Yesu.
3) Petro ni si "mwamba" wa muuhimu zaidi kuliko Yesu mwenyewe, jiwe la msingi, kama Efe 2:20 inavyosema. Kama mwamba mmoja uliowekwa imara juu ya mwingine, Petro mwenyewe alituambia kuwa Yesu ni jiwe kuu la pembeni kwenye Mdo 4:10-11 na 1 Pet 2:6-7.
4) Petro hakuwa mkamilifu katika mambo aliyosema au kufanya, ama kabla kufufuka kwa Yesu (Mat 16:22-23) au baadaye (Gal 2:11-14).
5) Hata hivyo, Petro aliongea kwa mamlaka kama mtume (1 Pet 1:01 na Mdo 1:15-22) nasi tunapaswa kukubali mafundisho yake namna hiyo. Kama Wakristo wa awali, tunapaswa kujitoa kwenye mafundisho ya mitume (Mdo 2:42).
6) Petro alipewa funguo za ufalme, za kufunga na kufungua kwenye Mat 16:19. Hakika mitume wote walipewa mamlaka hayo hayo ya kufunga na kufungua kwenye Mat 18:18.
7) Hakuna mafundisho ya kikristo yanayoweza kuwa ya msingi zaidi kuliko ukiri alioufanya Petro hapa. Kama mtu hatamkiri Yesu kuwa Masihi aliyeahidiwa, Mwana wa Mungu aliye hai, na kama hatakiri kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuka kutoka kwa wafu (1 Kor 15:1-11), basi yake ni bure na haitamfikisha mbinguni.

S: Kwenye Mat 16:18, mwamba ni nani au kitu gani hapa?
J: Kuna maoni makubwa mawili, na yote yanaweza kuwa ya kweli.
Mwamba ni ukiri wa Petro kuwa Yesu ni Kristo. Hakukuwa na neno moja, bali mawili tofauti, ya Kigiriki kwa mwamba. Simoni aliitwa Petro "mwamba" kwa sababu ndiye alitoa ukiri kwanza kwamba Yesu ni Kristo. Yesu aliongea na Petro katika nafsi ya pili "wewe", lakini "mwamba huu" ni katika nafsi ya tatu. Yesu na wanafunzi, kwa kuwa walitoka Galilaya, kuna uwezekano mkubwa kuwa alizungumza Kigiriki. Bila kujali tafsiri ya kikristo ya aya hii, 1 Yoh 4:1-3 na 2 Yoh 7-10 zinaonyesha kuwa yeyote yeyote ambaye hatambui kuwa Yesu amekuja katika mwili hapaswi kukubaliwa au kukaribishwa. 1 Kor 15:1-4 inaonyesha kuwa mtu yeyote asiyeamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kuwa alifufuka kiimwili kutoka kwa wafu kuamini kwake ni bure. 1 Kor 12:3 inasema kuwa hakuna mtu anayeweza kusema kuwa Yesu ni Bwana ila kwa Roho Mtakatifu. Kusema ukweli, kanisa limejengwa juu ya ukiri wa Yesu Kristo.
Mwamba ni Petro mwenyewe. Yesu na wanafunzi wake watakuwa walifahamu Kiaramu, na hivyo Yesu anaweza kuwa alisema Kigiriki hapa. Maneno mawili (ya mwamba) yako tofauti kwenye Kigiriki kwa sababu moja ni jina la mtu la kike, na lingine ni la kiume. Hata hivyo, lugha ya Kiaramu haina miisho ya kiume, kike na ile isiyokuwa na jinsiayeyote. Pia, Papias, mwanafunzi wa Mtume Yohana, anasema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwanza kwa Kiebrania [huenda inamaanisha Kiaramu] na baadaye ilitafsiriwa kwenye Kigiriki. Kwenye Kiaramu, neno linalofanana kepha lingetumika. Wakatoliki kwa ujumla wana maoni kuwa mwamba hapa ni Petro, kwani wanaamini kuwa tafsiri hii inaunga mkono hoja ya kuwa kanisa lilianzishwa juu ya Petro. Kisha wanaongeza kuwa Petro alihamisha Upapa kwa warithi wake. Ingawa hakuna dokezo la sehemu hii ya mwisho kwenye Biblia, hakuna tatizo kwa Waprotestanti pia kutafsiri Petro kama mwamba hapa. Bila kujali tafsiri ya kikristo ya aya hii, misingi bora hujengwa kwa kutumia mwamba, na mitume na manabii wote ni msingi wa kanisa kwenye Efe 2:20. Kwa kusema ukweli, kanisa limejengwa juu ya Biblia, ambayo ni mafundisho ya mitume na manabii.

S: Kwenye Mat 16:18, je Yesu alikuwa anasema kimsingi kuwa Petro alikuwa Papa wa kwanza, kama kanisa Katoliki linavyodai?
J: Maoni haya yalitumiwa kwa mara ya kwanza na Papa Damaso mwaka 382 BK kuthibitisha urithi wa upapa. Kama Dave Hunt alivyoandika kwenye A Woman Rides the Beast, uk.101 "Moja ya mifano ya mwanzoni zaidi ya mapapa mbalimbali iliundwa na uchaguzi uliofanyika wakati mmoja wa makundi pinzani ya Mapapa Ursinus na Damaso. Wafuasi wa Ursinus walishinda baada ya vurugu nyingi, kumsimika kuwa papa. Baadaye, baada ya vita vilivyohusisha umwagaji damu vya siku tatu, Damaso, kwa msaada wa mfalme, aliibuka mshindi na kuendelea kama mwakilishi wa Kristo kwa miaka 18 (mwaka 366-384 BK). Hivyo "urithi wa kimitume" na "kwa mfuatano usiovunjika kutoka kwa Petro" uliendeshwa na jeshi? Kweli?"
Kutoka kitabu hicho hicho, uk.135-136, Askofu Joseph Hefele wa Rottenberg anasema, "‘Lakini katika nyaraka zile zote [historia na mafundisho ya kanisa] sijawahi kuona mafundisho [ya kutokosea kwa papa kutoka kwenye chanzo kinachoaminika].’ . . . Von Dollinger, mmoja wa wana historia ya kanisa aliyeaminika san wakati ule, alikubaliana kabisa na Hefele. Kitabu chake (kilichopigwa marufuku na Rumi) alionya kuhusu jaribio lililokuwa linatarajiwa kuja la Pius IX kushinikiza kupitia imani ya kanisa isiyoruhusiwa kupingwa ya kutokukosea na aliwakumbusha maaskofu waliokuwa wanakaribia kukusanyika kujadili uamuzi huu muhimu: Hakuna ukiri wowotw wa imani wa awali, hakuna katekisimu, hakuna maandiko ya waandishi wa kikristo wa awali yaliyoandikwa kwa ajili ya maelekezo ya watu, yana silabi kuhusu Papa, na tena hakuna dokezo lolote ambalo uhakika wote wa imani na mafundisho unautegemea."
Augustine wa Hippo (mwaka 388-430 BK) alisema, "kwa hiyo, juu ya mwamba huu [Yesu] alisema, ambao umeukiri, nitalijenga kanisa langu. Kwa sababu mwamba (Petra) ni Kristo; na ni juu ya msingi huu Petro mwenyewe alijengwa." Kisha Augustine anaendelea kunukuu 1 Kor 3:11, na anasema kuwa kanisa lilikuwemo kwenye mwamba huu kwa njia ya kuwakilishwa na Petro (On the Gospel of John Tractate 124 sura ya 21.5 juzuu ya 7, uk.450).

S: Kwenye Mat 16:18, je "mwamba" uliwezaje kuwa mchezo wa maneno muhimu zaidi kwenye historia yote?
J: Ingawa ni lazima kukubaliana na watu wote kwamba Yesu alikusudia kuwa Petro na mitume wengine wawe na mamlaka makubwa zaidi duniani juu ya kanisa, Yesu hakuwahi kusema kitu chochote kuhusu warithi wanaodaiwa kuwepo. Hivyo, hayakuwa maneno yenyewe, bali kupanuliwa kwake kusikokuwa halali hadi kwa Mapapa ambako kumewafanya wawe mchezo wa maneno wenye mvuto mkubwa sana kwenye historia yote.
Pamoja na hayo, msomaji mmoja amechangia kuwa mchezo wa maneno unaweza kuwepo kwenye Kiebrania SIYO Kigiriki. Kwenye Kiebrania inawezekan ilikuwa "jiwe"eben na "nitalijemga" ebneh. Kwa mfano, George Howard anaonyesha andiko la Kiebrania lenye mada moja la karne ya 14 lililoandikwa na rabi mmoja aliyetwaye Shemu-Tobu Ben Shaprut, ambaye maneno yake mwenyewe ya Kiebrania yanasomeka "Wewe ni jiwe (eben) na, juu yako nitaijenga (ebneh) nyumba yangu ya maombi." Tazama www.jerusalemperspective.com/Default.aspx?tabid=27&ArticleID=1859 kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Mat 16:18, je jina Petro limeisha wahi kukutwa Qumran miongoni mwa Hati za Kale toka Bahari Chumvi (Dead Sea Scrolls)?
J: Hapana. Kulikuwa na ripoti kwenye tafsiri ya unukuzi uliofanywa na John Allegro katika hati ambayo sasa inaitwa 4Q432. Hata hivyo, Martin Abeg wa Trinity Western University kwenye barua pepe anasema kuwa haipo kwenye 4Q432.

S: Kwenye Mat 16:19, je kufunga na kufungua ni kitu gani?
J: Fikiria Wakristo wakijaribu kupambanua wafuasi wa vikundi vidogo vya watu vyenye imani au mafundisho yanayoonekana na watu wengine kuwa potofu au yasiyo ya kawaida kutoka Wakristo wenye makosa, na mafundisho yasiyo ya kawaida kutoka kwenye mafundisho ya kiungu, kama wangekuwa hawana Agano Jipya. Hivyo ndivyo hali ilivyokuwa kwenye kanisa la awali. Mungu aliwapa mitume uwezo wa kupambanua na mamlaka ya kutamka mafundisho yaliyokuwa mazuri.
Halikuwa suala la kutafuta endapo kuna hatia au au hakuna hatia, bali kuitangaza, kama Petro alivyowatangaza Anania na Safira kuwa na hatia ya kusema uongo kwa Roho Mtakatifu kwenye Mdo 5:1-10. Maneno "kufunga" na "kufungua" yalikuwa yanafahamika sana kwa marabi wa Kiyahudi marabi. Misemo hii ilimaanisha kutawala, kutoa kibali au kuzuia vitu vya aina mbalimbali.

S: Kwenye Mat 16:19, je funguo za ufalme mbinguni ni kitu gani hasa?
J: Hakuna chuma, au kitu chenye maumbile ya kimwili. Funguo ziliweza kuwa ama ujumbe wa injili, wa Petro kufungua mlango wa injili kwa Wayahudi (Matendo 2) na baadaye kwa watu wa mataifa mengine kwenye Matendo 10.
Yesu pia alisema kuwa waandishi na Mafarisayo waliwafungia watu ufalme wa mbinguni kwenye Mathayo 23:13. Kwenye Luk 11:52, wanasheria waliondoa ufunguo wa maarifa.

S: Kwenye Mat 16:19, je funguo hizo za ufalme wa mbinguni zingeweza kutolewa kwa mtu/watu wengine?
J: Maandiko hayatoa dokezo lolote endapo "funguo" zinaweza kutolewa kwa mtu/watu wengine, isipokuwa tu kuwa Yesu alitoa hizo kwa mitume wote. Hata hivyo, Yesu akiwaambia mitume, kisitiari kuwa wanazo "funguo" haimaanishi kuwa Yesu mwenyewe aliacha kuwa na funguo, kwani Yesu bado ana "funguo za mauti za kuzimu" kwenye Ufu 1:18.
Kuzungumza kinadharia tete, hata kama papa wa awali angekuwa na hizi funguo na angekuwa na uwezo wa kuzitoa kwa mtu/watu wengine, jambo hili lisingemaanisha urithi wa kipapa, endapo urithi ungevinjika. Papa achukuaye madarak kwa kumpindua papa aliyetangulia ni dhihaka. Endapo papa angekuwa mwovu, kama Alexander VI (mwaka 1492-1503 BK), jambo hilo pia lingevunja urithi wa kipapa. Kwa jinsi hiyo, kuanzia wakati huo na kuendelea, hakuna mtu ambaye angeweza kutoa kwa mtu/watu wengine kitu ambacho yeye mwenyewe hakuwahi kuwa nacho.

S: Kwenye Mat 16:20 na Mak 8:30, kwa nini Yesu hakupenda wanafunzi wake wawaambie watu wengine wakati huu kuwa Yeye ni Kristo (yaani Masihi)?
J: Kwanza tambua kuwa Yesu hakuwahi kuwaambia waseme uongo na kukana kuwa Yeye ni Masihi, ila tu kuwa wasiongelee jambo hilo. Kuna sababu zisizopungua mbili za kufanya hivyo.
1. Katika hatua hii ya huduma yake, Yesu alitaka wasikie maneno yake kabla ya kuamua endapo Yeye alikuwa Masihi au la. Ni vema wakati mwingine kuwaacha wasikilizaji wenyewe wa injili kusikia maneno ya Yesu kuliko kutumia muda mrefu sana kuongelea muktadha wa injili au kuifanya ilingane na mazingira ya sasa.
2. Kama Mat 16:21 inavyoonyesha, wanafunzi walitakiwa kufahamu kabisa kuwa Yesu ni nani kabla hawajaenda kuwaeleza watu wengine.
Yesu alitangaza jambo hili mbele ya watu kufikia wakati alipoingia Yerusalemu kwa shangwa kwenye jumapili ya mitende. Vivyo hivyo, baada ya kufufuka kwake, Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuuambia ulimwengu wote kwenye Mat 28:18-20 na Mdo 1:8.

S: Kwenye Mat 16:21 na Marko 29, kwa nini ukiri wa Petro ulikuwa moja ya matukio muhimu sana kwenye huduma ya Yesu?
J: Toka wakati alipotambuliwa kuwa Masihi, Yesu alianza kuwafundisha kuwa anapaswa kwenda Yerusalemu kufa. Wanafunzi walipaswa kumwamini Yesu kabla hawajaelewa kwa nini ilimpasa afe kwa ajili ya dhambi zao.

S: Kwenye Mat 16:21 na Mak 8:31, wakati huu kwenye huduma yake, na si kabla, kwa nini Yesu alianza kuwaambia wanafunzi wake kuwa atateswa na kukataliwa na watu?
J: Yesu hakusema kuwa atateseka na kuuawa mpaka angalau mmoja wa wanafunzi wake amtambue na kumuamini kuwa Yeye (Yesu) alikuwa ndiye Masihi aliyeahidiwa.

S: Kwenye Mat 16:21; 17:22; 20:19 na Mak 8:31, kwa kuwa Yesu angefufuka baada ya siku tatu au kwenye siku ya tatu, ndio kusema kuwa alikufa kwa angalau masaa 24 X 3 = 72?
J: Hapana, kwa sababu Luk 24:21 inasema kuwa siku ya ufufuo ilikuwa siku ya tatu. Yesu alikufa ijumaa alasiri, na kufufuka jumapili karibu na alfajiri. ‘Baada ya siku tatu’ ulikuwa ni nahau ya Kiebrania iliyofahamika sana yenye kumaanisha siku zote tatu au sehemu zake. Ifuatao ni mifano ya "nahau ya siku tatu."
1. Rehoboamu kwenye 2 Nya 10:5, aliwaambia watu "mnirudie baada ya siku tatu." Lakini kwenye 2 Nya 10:12, watu walirudi "siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru."
2.
Kwenye 1 Sam 30:12, mtumwa wa Kimisri aliyekuwa mgonjwa alimwambia Daudi kuwa hakuwa amekula chakula chochote wala kunywa maji yeyote kwa siku tatu mchana na usiku. Hata hivyo mtu asingeweza kuishi nje ya nyumba jangwa nani bila kunywa maji kwa muda wa masaa 72. Bila shaka mtumwa huyu alimaanisha sehemu ya siku tatu.
2. Akiongelea kufa na kufufuka kwake msalabani, Yesu mwenyewe alisema kwenye Mat 12:40 "siku tatu mchana na usiku", Mak 8:31 inasema "baada ya siku tatu atafufuka", Mak 14:58 inasema "katika siku ya tatu", Yoh 2:19 inasema "katika siku tatu", na Luk 24:21 inasema "leo ni siku ya tatu."
3. Kwenye Est 4:16, Esta anaagiza kufunga kwa ajili yake, "muda wa siku tatu, usiku wala mchana" naye atafanya vivyo hivyo. Lakini Est 5:1 inasema ikawa "siku ya tatu", Esta aliandaa karamu, kwa hiyo huu ni muda unaofanana na ule aliousema Esta kwenye 4:16.
Kwa muhtasari, tumethibitisha kuwa nahau hii ya Kiebrania inaweza kumaanisha katika muda wa siku tatu, nausemi huu ulieleweka kuanzia wakati wa Rehoboamu hadi wakati wa Yesu.

S: Kwenye Mat 16:22-23 na Mak 8:32-33, kwa nini Yesu alimkemea Petro hapa akisema "Nenda nyuma yangu, Shetani"?
J: Petro alikuwa anawazia mambo ya wanadamu, siyo Mungu. Shetani alimtumia Petro, rafiki wa karibu wa Yesu, kumjaribu Yesu. Hata hivyo, Yesu alilitambua jaribu kwa jinsi lilivyokuwa.

S: Kwenye Mat 16:22-23 na Mak 8:33, je Petro aliwezaje kupata ujasiri wa kumrekebisha na kumkemea Yesu?
J: Yesu alimchagua mwanafunzi jasiri wakati alipomchagua Petro. Ujasiri wenyewe si kitu kizuri wala kibaya. Ujasiri katika kumfuata Mungu ni mzuri, lakini ujasiri wa kwenda njia yako mwenyewe si mzuri kwa kawaida.

S: Kwenye Mat 16:22, kwa nini Petro alimkemea Yesu kijinga hapa?
J: Petro alifikiri kuwa Yesu alihitaji kurekebishwa na kushauriwa. Hata leo, baadhi ya watu wanaweza kuwa na mtazamo kuwa wanajua vitu vema kuliko Mungu.

S: Kwenye Mat 16:23 na Mak 8:33, ni kwa namna gani watu wanaweza kuwa wanawazia mambo ya kibinadamu badala ya kuwazia mambo ya Mungu siku hizi?
J: Tunaweza kuweka hekima ya binadamu mahali pa hekima ya Mungu. Tunaweza kuamua kufanya mambo kwa njia zetu wenyewe, wakati ni kinyume na njia ya Mungu. Tunaweza kusahau kuwa tumaini letu liko kwa Mungu, si kwenye nguvu au hekima zetu. Tunaweza kutumia njia zetu wenyewe za kidunia. Hatimaye, tunaweza kuwa na hamu kubwa sana ya kufanya "majukumu" kwa haraka hata tukakosa kufurahia kuwa kwenye uwepo wa Mungu kiasi kikubwa zaidi, na kupendelea aina ya "chakula cha haraka haraka" ya ibada kuliko kujitoa kwa Mungu.

S: Kwenye Mat 16:24, kwa nini Yesu aliutaja msalaba hapa kabla ya kuwaambia wanafunzi wake kuwa atasulubiwa?
J: Yesu alijua kuwa atasulubiwa kabla ya kuwaambia wanafunzi wake jambo hili. Tayari waliishajua kuhusu kusulubiwa, kwani Warumi walikuwa wanawasulubisha waasi na majambazi mara kwa mara. Kusulibisha ikulikuwa ni motisha kwa watu wengine kutii mamlaka. Kama wanamapinduzi wa Kizelote walijihatarisha kusulubiwa kwa ajili ya mambo madogo ya kidunia, wanafunzi wanapaswa kuwa tayari kujihatarisha kusulubiwa kwa ajili ya mambo ya kimbinguni ambayo yana thamani kubwa zaidi. Mwishoni, kila mmoja wa mitume kumi na mbili aliuawa kwa sababu ya imani yao, isipokuwa Yohana, aliyepelekwa uhamishoni kisiwani Patmo ambako alikufa kifo cha kawaida.

S: Kwenye Mat 16:27, je Yesu atkuja na utukufu wa Baba yake, au utukufu wake Yeye mwenyewe kama Yoh 1:14 inavyosema?
J: Yoh 1:14 inasema waliuona utukufu wa Yesu. Kwa mfano, waliuona utukufu wa kiasi fulani siku ya Pentekosti. Mat 16:27 inaongelea tukio la wakati wa mbali zaidi ujao, pale Yesu atakapokuja tena. Kwa maneno mengine, bado hujaona kitu chochote kile!

S: Kwenye Mat 16:27, je aya hii haiongelei mwisho wa dunia, bali kudhihilishwa kukubwa kwa Baha’u’llah, kama Wabaha’i wanavyofundisha kwenye Baha’u’llah and the New Era, uk.268-269?
J: Hapana, soma aya kwa makini zaidi. Inasema Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika wake, na atamlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Watu hawakuwaona malaika wowote wakiwa pamoja na Baha’u’llah, na Baha’u’llah hakuwalipa Wabaha’i waaminifu waliopelekwa uhamishoni au kuuawa, wala Waislam waliowatesa.

S: Kwenye Mat 16:28 na Mak 9:1, Yesu alimaanisha nini aliposema kuna watu ambao hawatakufa hadi watakapouona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu?
J: Kwanza tutaangalia kitu ambacho si jibu la swali hili kisha kitu ambacho ni jibu.
 X1. Hakuna ushahidi kuwa Yesu aliwafundisha wanafunzi kuwa wataishi muda mrefu. Kwa kweli, kutoka kwenye historia ya kanisa tunajua kuwa mitume 11 kati ya 12 waliuawa kama mashahidi wa imani. Mmoja tu, Yohana, alikufa kifo cha kawaida. Hata hivyo, naye alipelekwa uhamishoni katika kisiwa cha Patmo.
X2. HAIMAANISHI miaka elfu moja ya utawala Yesu ulimwenguni mwote ulioongelewa kwenye Ufu 20:1-6.
X3. Hawezi kuwa inaongelea kuzaliwa kwa nafsi kwenye mwili mwingine/tofauti kabla hawajamwona Mwana wa Adamu akija kwenye ufalme wake, kwa sababu watu ambao nafsi zao zimepata miili mingine wangali wanakufa.
X4: Wako wanaofikiri kuwa inaongelea kugeuzwa kwa sura ya Yesu, ambako kulikuwa tayari kumetokea. Hata hivyo, ufalme wa Mungu hakuja bayana wakati huo.
Jibu: Inaongelea wakati Yesu aliposhinda kwenye ufalme wake kwa kusulubiwa kwake kama kulivyothibitishwa na kufufuka kwake. Alikuja katika ufalme wake baada ya kumshinda shetani. Wakristo hawakubaliani endapo siku hiyo ilikuwa ni ya kufufuka kwa Yesu, au Pentekosti, lakini jambo hilo si muhimu kabisa.
Mathayo anatoa msistizo maalum kuhusu ufalme wa mbinguni. Ufalme wa mbinguni utaanza kwa kuonekana mdogo kama chembe ya haradali (Mat 13:31), kama chachu, haitaonekana lakini madhara yake yataonekana kwenye pishi za unga wa dunia (Mathayo 13:33), lakini mwishoni malaika wataondosha kwenye ufalme wa mbinguni vitu vyote vyenye kusababisha dhambina watu wote wanaotenda maovu (Mat 13:41-42). Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyofukiwa ambayo mtu huipata kisiri (Mat 13:44), lakini ni ya thamani sana kama mfanyabiashara aliyeuza vitu vyote ili anunue lulu nzuri (Mat 13:45-46). Hivyo kama mfano wa nyavu unavyoonyesha kwenye Mat 13:47-50, ufalme wa mbinguni ni chombo kilichopo kwenye maisha haya chenye samaki na wazuri na wabaya, lakini pia kina utimilifu wake kwenye mwisho wa dunia. Ufalme wa Mungu uko ndani yetu (Lk 17:21).
Petro, kwenye Mat 16:19, na mitume wengine baadaye walipewa funguo za ufalme.
Kwenye karamu ya mwisho, Yesu alisema hatakunywa matunda ya mzabibu tena mpaka atakapokunywa upya pamoja nao kwenye ufalme wa Baba (Mat 26:29). Yesu alikula na kunywa pamoja na wanafunzi baada ya kufufuka kwake.
Muhtasari: Wanafunzi, walioishi urefu wa kawaida wa maisha, wanasema ufalme wa mbinguni, ulikuja duniani baada ya kufufuka kwa Yesu. Ingawa Wayahudi wanaweza kuwa walitegemea ufalme wa kijeshi ambao ungewapindua Warumi, Yesu alifundisha kuwa ufalme ulikuwa kama chembe ya haradali, chachu, au lulu ya bei kubwa. Ulikuwa ndogo, mgumu kuonekana kwa mara ya kwanza, wenye thamani kubwa, na utakaokuwa na athari kubwa.

S: Kwenye Mat 17:1-8, kwa nini Yesu aligeuka sura na mavazi yake?
J: Ingawa Maandiko hayasemi chochote kuhusu jambo hili, inaweza kuwa mchanganyiko wa sababu.
1. Ufunuo huu ulikuwa ishara yenye kuthibitisha imani zao, na kuwatia moya na kuwaimarisha wanafunzi watatu walioshuhudia tukio hili.
2. Tukio hili liliwatenga wanafunzi watatu kama viongozi wa wanafunzi wengine.
3. Baba na Roho Mtakatifu wanaweza kuwa walilitumia tukio kumfundisha Yesu na kumtia moyo Yesu.
Ni kweli, Mungu haitaji kutueleza sababu za vitu vyote.

S: Kwenye Mat 17:2 na Mak 9:3, kwa nini mavazi ya Yesu yalikuwa meupe sana?
J: Maandiko hayasemi kwa mavazi yalikuwa meupe utukufu ulipoonyeshwa. Mifano mingine ya mavazi meupe kwenye utukufu ni malaika walioonekana.

S: Kwenye Mat 17:3-4 na Mak 9:4, je Mathayo na Marko waliwezaje kujua kuwa hawa walikuwa ni Musa na Eliya?
J: Pengine ni kwa sababu Petro, au Yakobo, na Yohana waliwaambia. Na Petro, Yakobo na Yohana walijuaje? Aidha Yesu aliwaambia baadaye, na inawezekana Baba aliwaeleza moja kwa moja.

S: Kwenye Mat 17:1-8, je kugeuka kwa sura na mavazi ya Yesu kulikuwa ni kufufuka au maono?
J: Hakukuwa kitu chochote kati ya hivyo kwa uhakika. Musa na Eliya walikuwepo kabisa, angalau katika roho, wakizungumza na Yesu. Maandiko hayasemi endapo kuonekana kwao kulikuwa kwa mwili au la. Musa na Eliya walikuja kwenye wingu jeupe, na kisha wakaondoka. Eliya alikwenda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli (2 Fal 2:1), na ingawa Musa alikufa, mwili wake haukuwahi kuonekana (Kum 34:6), na shetani alishindana na malaika mkuu Mikaeli kwa ajili ya mwili wa Musa (Jud 9).

S: Kwenye Mat 17:9 na Mak 9:9, kwa nini Yesu hakupenda wanafunzi wake wamwambie mtu yeyote yule kuhusu kugeuka kwa sura na mavazi vyake mpaka wakati alipofufuka toka kwa wafu?
J: Wengi wa Wayahudi walimkataa Yesu kuwa Masihi; je wangewezaje kuamini kugeuzwa kwa sura na mavazi vyake? Ni muhimu kuamini kuwa Yesu ni Masihi, Mwana wa Mungu. Haikuwa muhimu kujua au kuamini mambo mengine ya ziada kama kugeuka kwa sura na mavazi vya Yesu. Kama mtu hakumkubali Yesu kama Masihi baada ya kuona miujiza, kuna uwezekano mdogo sana kuwa ataweza kuamini kwa sababu ya ripoti ya kugeuka kwa sura na mavazi ya yake (Yesu). Baada ya Yesu kufufuka kutoka kwa wafu, mtu aliyemwamini Yesu hangepata shida kukubali taarifa ya kugeuka kwa sura na mavazi vya Yesu.
Kwa jinsi hiyo hiyo, tuunapoongea na watu wengine kuhusu Kristo, hasa kwa mara ya kwanza, kati ya mambo yote tunayoweza kuongelea, hakikisha kuwa unatumia muda huo wa thamani kuzungumzia mambo muhimu zaidi.

S: Kwenye Mat 17:11-13, Yohana Mbatizaji aliwezaje kuwa Eliya aliyekuwa anatarajiwa kuja?
J: Kwanza tutamwongelea Eliya kisha Yohana Mbatizaji.
Eliya mwenyewe alikuwepo wakati sura na mavazi vya Yesu vilipobadilika. Kwenye Mat 17:11, Yesu anaposema Eliya atarejesha vitu vyote anatumia wakati ujao, na Eliya mwenyewe atatokwa kabla ya kuja kwa Yesu kwa mara ya pili. Wako watu wanaofikiri kuwa Eliya ni mmoja wa mashahidi wawili kwenye Ufu 11:1-2.
Yohana Mbatizaji alikuja katika Roho na nguvu ya Eliya, na ni Yohana Mbatizaji ambaye Yesu anamwongelea kisitiari kwenye Mat 17:12-13.
Kwenye michezo ya kuigiza, mtu anaweza kuchukua nafasi ya mwigizaji wakati wa mazoezi, na mwigizaji mwenyewe akatokea wakati wa mchezo wenyewe.
Hitimisho: wakati wa kuja kwa mara ya kwanza, Yohana Mbatizaji alikuja kutimiza jukumu la Eliya, lakini jambo hilo halimzuii Eliya mwenyewe kuja tena kabla ya kuja tena mara ya pili.

S: Kwenye Mat 17:12 na Mak 9:11-13, je Yohana Mbatizaji alitimiza vipi unabii wa Eliya? Je Eliya alifanyika mwili tena?
J: Hapana. Kwenye ujio wa kwanza wa Yesu, Yohana alikuwa na lengo na makusudi vya Eliya. Isitoshe Eliya (siyo Yohana) mwenyewe alitokea kwa ufupi wakati wa kugeuka kwa sura na mavazi vya Yesu. Watu wengi wanadhani kuwa Eliya atakuwa moja wa mashahidi wawili kabla ya baragumu ya saba kwenye Ufu 11:3-12.

S: Kwenye Mat 17:14-16 na Luk 9:37-39, kwa nini mapepo mara nyingi huwaumiza watu yanaowapagawa?
J: Labda kwa sababu kama hizo kama watu wabaya wanavyowaumiza watu ambao wamewasaidia. Kwa maelezo ya mantiki, maelezo ya mantiki hasa ya jambo hili, kitabu cha Michiavelli wa Rotten The Prince anaongelea mikasa ambayo kiongozi mamluki ni mwenye hatari wakati anamhudumia mwana wa mfalme, na ni mwenye hatari zaidi anapoasi. Aliandika kuwa kitu cha usalama zaidi mara nyingi huwa ni kumuua, hata kama mtu amethibitika kuwa mwaminifu katika siku za nyuma! Endapo anacheza na maovu, asishangae akikuta mabaya yamefanyika kwake na watu aliokuwa anawasaidia.

S: Kwenye Mat 17:15-21, Mak 9:17-18, 28-29, na Luk 9:40, kwa nini wanafunzi walishindwa kumtoa pepo huyu?
J: Haikuwa kwa sababu ya wanafunzi walikuwa watu gani, au ukomo wa nguvu za Mungu. Bali walichukulia suala la kutoa pepo ni jambo la kawaida wakati huu, na hawakuomba wala kufunga, huenda ni kwa sababu ya kiburi au kuridhika. Leo hii kuna Wakristo ambao hawaoni matokeo ambayo walitakiwa kuyaona kwa sababu hawawekezi katika kuomba na kufunga.

S: Kwenye Mat 17:15-21, Mak 9:17-18, 28-29, na Luk 9:40, je ni lazima tuweke mikono tunapokemea mapepo, au jambo hili ni moja ya vitendo vinavyoweza kufanywa?
J: Mikono yetu haina nguvu yoyote ya ajabu. Lakini kama vile inavyoweza kutusaidia kwenye maombi kwa kuomba kwenye hali (positions) mbalimbali, ni jambo zuri na lenye kuruhusiwa na Biblia kuweka mikono juu ya mtu aliyepagawa na pepo. Si lazima kufanya hivyo, hata kwamba "pepo asiweze kutoka endapo hatutaweza kuweka mikono."

S: Kwenye Mat 17:15-21, je pepo lililotolewa linaweza kurusi na kumpagawa mtu dhaifu miongoni mwa wale wanaojaribu kulitoa?
J: Mapepo hayampagawi muamini wa kweli, lakini yanaweza mdhuru muamini, na kwa njia hiyo kumshambulia muamini kwa njia ya majaribu makubwa, hofu, huzuni, na njia nyingine hata kuyapeleka macho yao mbali na Yesu. Kwa hiyo washiriki wa maombezi ya kutoa mapepo wanatakiwa waenende vizuri na Bwana.
Pamoja na hayo, kuna hatari nyingine katika kukemea mapepo. Endapo mtu ambaye anatolewa mapepo hataki kuweka tumaini lake kwa Kristo moyoni wake, basi mapepo hurudi na hata kuleta mapepo mengine zaidi pamoja nayo. Angalia Mat 12:43-45 na Luk 11:24-26.

S: Kwenye Mat 17:15-21, makanisa mengine yanasema kuwa mtu aliyepagwa mapepo lazima aletwe kanisani, na siyo kwenda nyumbani kwake. Je jambo hili linafanywa kwa sababu ni salama zaidi kukemea mapepo kanisani kuliko kwenye nyumba ya mtu?
J: Nadhani kanisa au nyumba ya mtu zinaweza kutumika kufanyia maombi haya. Lakini kama inawezekana, sitapenda kufanya hivyo kwenye nyumba ambayo ina sanamu (Wabuddha, n.k.) au unajimu au upigaji ramli ndani yake.

S: Kwenye Mat 17:15-21, endapo mwanamke asiye muamini amepagawa na mapepo, na mwanzoni mumewe hapingi. Lakini baada ya ziara 2-3, mume amebadilisha mawazo yake na hawakaribishi tena waamini, au anaizuia wasije nyumbani, na mke bado yuko wazi kuombewa, una maoni gani? Je mke analazimika kumtii mumewe?
J: Hii ni hali ngumu. Wake wanapaswa kuwatii waume zao, lakini wanatakiwa kumtii Mungu kwanza. Hivyo, kama mume anamuamuru mkewe kufanya kitu kisichokubalika kibiblia, mke analazimika kutokumtii mume wake hapa. Hata hivyo, atalazimika kuendelea kumtii mumewe katika mambo mengine. Lakini kama mke atapenda waamini waje, nadhani atakuwa hajapagawa mapepo; ingawa anaweza kuwa ameshambuliwa na mapepo. Je mwanamke huyu yuko tayari kuja kanisa? Kama mume hataki mkewe ajihusishe na waamini, na Ebr 10:25 inatuamuru tusiache kukutana pamoja, wajibu wa mke ni kumtii Mungu kwanza.

S: Kwenye Mat 17:15-21, je itakuwaje endapo mtu aliyepagawa mapepo atajiumiza au kujirusha toka dirishani wakati wa kuombewa, na ndugu zake wanaamua kuanzisha madai au kufungua kesi dhidi ya kiongozi wa timu ya watu waliokuwa wanamuombea au timu nzima, je kanisa linatakiwa kufanya nini hapa?
J: Jambo hili linawezekana; watu wanaweza kufungua mashtaka na kuwalaumu wengine kwa kitu chochote kile. Bila kujali kitu kilichotokea, washiriki wa kanisa wanapaswa kuchukua tahadhari kwa ajili ya usalama wa watu wanaohusika na maombi.

S: Kwenye Mat 17:15-21, je ni lazima kutoa taarifa na kupata kibali cha mchungaji kabla ya kumtembelea mtu aliyepagawa mapepo?
J: Ushauri wangu ni kuwa mfahamisha mchungaji wako jambo hili. Ebr 13:17 inasema kuwa tunapaswa kuwatii watu wanaotuongoza, na jambo hili linamaanisha wachungaji au wazee.

S: Kwenye Mat 17:25-27, kwa nini Yesu alisema wana wa wafalme hawatozwi kodi au ushuru, lakini Yesu bado alilipa kodi?
J: Inaonekana kama kicheko kuwa muumbaji na Bwana wa ulimwengu kulipa kodi. Hata hivyo, Yesu alifanya hivyo kwa kwa unyenyekevu, bila kulalamika ili kutowakwaza.
Licha ya mfano huu, Rum 13:6-7 pia inawaamuru waamini kulipa kodi kwa serikali, hata serikali ya kifisadi kama Himaya ya Kirumi.
Watu wengine wanaweza kutafsiri vibaya maneno ya Yesu kuwa hayaeleweki, kwani Yesu alikuwa akisema kinadharia tete wakati ambapo mtu yeyote aliyekwenda kwa Kaisari angeweza kutolewa kwake, kwa kweli hapakuwa na kitu kilichotakiwa kwenda kwa Warumi. Hata hivyo, kama hivi ndivyo Yesu alivyomaanisha, kuwaambia wanafunzi wakalipe dinari moja kungekuwa ama hakuna maana au, mbaya zaidi, kunapotosha watu.

S: Kwenye Mat 18:5 na Mak 9:35-37, ni kwa namna gani kumkaribisha mtoto kwa jina la Yesu kunakuwa ni kumkaribisha Yesu?
J: Yesu alikuwa anasisitiza jinsi iivyokuwa tofauti kati ya kumpokea Yeye kimwili na kuwapokea watu wengine kwa jina lake. Katika nyakati za zamani, mjumbe wa mfalme alipokelewa kama mfalme kwa sababu alikuwa mwakilishi wa mfalme.

S: Kwenye Mat 18:8 na Mak 9:43,47, je tunatakiwa kukata mikono yetu au kung’oa macho endapo yanatufanya tufanye dhambi?
J: Hapana, kwa sababu rahisi kuwa mikono na macho vyetu havitufanyi tufanye dhambi. Yesu anasema kwamba dhambi ni sana mbaya, kiasi kwamba ingekuwa bora kutokuwa na viungo hivi kuliko kutenda dhambi.

S: Kwenye Mat 18:9 na Mak 9:43-44, 48, je kutajwa kwa moto usiozimika hapa kunathibitisha adhabu ya milele?
J: Kunadokeza ukweli wa adhabu ya milele, lakini hakuthibitishi, kwa sababu moto unaweza kuwa wa milele, lakini watu wanaoishi ndani mwake wasiwe hivyo. Bila shaka, katika suala hili, moto una nishati au jinsi nyingine zinazousaidia kuendelea kuwaka.

S: Kwenye Mat 18:11, je Mungu Baba ana uso?
J: Hapana. Hakuna ambaye alitarajia Yesu atoe mafundisho ya kina juu ya ukaribu na mtazamo wa malaika katika muktadha wa mbinguni hapa. Badala yake, Yesu alitumika sitiari tu kusema kuwa malaika wanaowaangalia watoto hawa wadogo wanawasiliana moja kwa moja na Baba. Hata hivyo, hakuna kitu kinachosema kuwa malaika wengine pia hawawasiliani moja kwa moja na Baba.

S: Kwenye Mat 18:14, kwa kuwa Mungu hapendi mtu yeyote miongoni mwa wadogo aangamie, kwa nini watu wanaangamia?
J: Haya ni maswali mawili ndani ya moja: kwa nini watoto wadogo wanakufa, na kwa nini watu wanakwenda jehanaamu?
Watoto wadogo wanakufa, kama ambavyo sisi sote tutakufa hatimaye, kama matokeo ya kuwa sehemu ya viumbe walioanguka. Tunaishi kwenye ulimwengu ulio na maovu mengi na udhalimu, na Mungu atayarekebisha mambo yote siku ya hukumu.
Watoto wadogo na vijusi wana asili ya dhambi, lakini kufa kwa vijusi hakuthibitishi kuwa vijusi vina hatia ya dhambi kama ambavyo kufa kwa mtoto wa paka kusivyo thibitisha kuwa ana hatia ya dhambi.
Watu wanakwenda jehanamu, kwa mujibu wa 2 Thes 1:7, inayosema wale wote ambao hawaitii injili ya ya Bwana Yesu Kristo watahukumiwa, hivyo injili ni kitu ambacho sisi sote tunapaswa kukitii. Kifo cha Yesu msalabani kilitosheleza vitu vyote. Lakini Mungu bado anawaruhusu watu wanaomkataa Mungu mmoja tu na wa kweli kupata malipo ya uchaguzi wao ambao waliohusika kuufanya.

S: Je Mat 18:15-18 inamaanisha kuwa tusiyakosoe mafundhisho ya kiongozi wa kikristo?
J: Hapana kabisa. Mat 18:15-18 inaongelea mwenendo si mahubiri ya uongo au uasi yanayotolewa mbele ya watu. Ingawa ni vizuri kuwasiliana mtu akiwa peke yake, ili kujaribu kumleta kwa Yesu kabla ya kutangaza kwa watu wote, ikiwa uongo ulihubiriwa hadharani, basi uongo unatakiwa kusahihishwa hadharani pia. Ikiwa utasahihishwa na mtu aliyeufanya na aliwahi kuamini maelezo ya uongo, itakuwa bora zaidi. Lakini kama si hivyo, basi utapaswa kusahihishwa na mtu mwingine. Lakini jambo hili halipaswi kufanywa kwa chuki au kwa mtu aliyeongeo makosa, bali kwa upendo na kwa nia ya kumuonyesha ukweli.

S: Kwenye Mat 18:18, kufunga na kufungua kunamaanisha nini?
J: Kufunga kunamaanisha kusimamisha, kuzuia, au kukataza, na kufungua kunamaanisha kuruhusu kuendelea. Maneno "kufunga" na "kufungua" yalikuwa ni nahau ya Kiyahudi iliyomaanisha kuwa kitu kilichotangazwa duniani kiliisha amuliwa hivyo muda uliopita mbinguni. Nguvu hii ya kufunga na kufungua ilitolewa kwa mitume wote.

S: Kwenye Mat 18:32-35, je Mungu ameisha wahi kutokusamehe au kutangua msamaha wa dhambi?
J: Deni halikurudishwa, badala yake msamaha haukutumika. Mfalme alisamehe deni la mtumishi, lakini wakati mtumishi mwovu alimpomshurutisha mtumishi mwingine kulipa deni lake, mfalme alikasirishwa na udhalimu huu na akatangua msamaha na kulifufua deni la mtumwa huyu. Mungu ametusamehe dhambi zetu bure na kwa neema, ingawa hatukustahili, lakini suala la msamaha kutumika au la linategemea itikio letu. Ebr 4:2 inasema kuwa injili halikuwanufaisha baadhi ya watu kwa sababu haikuenda pamoja na imani. Rum 11:29 inasema kuwa karama za Mungu na wito wake havina majuto (havibadilishwi kamwe).

S: Kwenye Mat 18:32-35, je mfano huu unaweza kumaanisha kuwa mfalme alimpeleka gerezani mtumwa mwovu kwa ajili ya madeni yaliyofuata baada ya wakati huo, badala ya kuyafufua madeni ya zamani?
J: Hapana, hili jambo linaloongelewa hapa, kwani mfano unaonyesha kuwa mfalme alimpeleka gerezani mtumishi mwovu kwa sababu ya (mtumishi mwovu) kutokuwa kwake na rehema.

S: Kwenye Mat 18:35, je baadhi ya kazi, kama kuwasamehe ndugu zetu, zinatakiwa kwa ajili ya kupata wokovu?
J: Si kusamehe wengine wala kazi nyingine yeyote haitamsaidia mtu kupata wokovu. Badala yake, ikiwa mtu atakuwa amepokea wokovu ataweza kuwasamehe kitu chochote ambacho wamefanya. Kama mtu amepokea rehema za Mungu, ni jambo dogo sana kwake kuwasamehe watu wengine.

S: Kwenye Mat 19:3-9 na Mak 10:11-12, je talaka inaruhusiwa katika mazingira gani?
J: Kwenye Agano la Kale (Kum 24:1-4, n.k.) talaka iliruhusiwa karibu kwa sababu yoyote ile kwani mioyo ya watu ilikuwa migumu, lakini Yesu aliiondoa sababu hii. Talaka hairuhusiwi isipokuwa kwenye mazingira yafuatayo:
1. Mke/mume asiyeamini anataka kuondoka (1 Kor 7:12-15)
2. Inaruhusiwa wakati mke au mume amefanya dhambi ya uzinzi (Mat 5:31-32)
3. Wakristo wengi wanaona talaka kuwa haiepukiki panapotokea utelekezwaji, kwani mke au mume ameisha "mtaliki" mwenzie kwa uhalisi wa mambo
4. Bila shaka tunapaswa kuyafuata mafundisho mengine ya neno la Mungu pia, na Wakristo wengi wanaona haja ya talaka endapo maisha ya mke/mume au mtoto yako hatarini kwa ajili ya mwenzi wake
Chuck Swindoll kwenye kijitabu chake kiitwacho Divorce, anataja mazingira ya aina tatu tu yanayomruhusu Mkristo kuoa/olewa tena baada ya talaka:
4a. Kuoa/kuolewa na kuacha/achika kabla ya kupokea wokovu
4b. Mwenzi mwovu na asiyekubali kutubu
4c. Kutelekezwa/ktalikiwa na mwenzi ambaye si muamini
Kumbuka kuwa kufiwa na mke/mume si talaka, na Rum 7:3 inasema kuwa kuoa/kuolewa tena baada ya kifo cha mke/mume.

S: Kwenye Mat 19:8, 9, je Yesu alipobadilisha sheria alionyesha Maandiko yaliyovuviwa na Mungu ambayo hakukubaliana nayo?
J: Kwa mujibu wa Agano la Kale, Yesu alisema talaka iliruhusiwa kwa sababu mioyo yao ilikuwa migumu. Jambo hili linaonyesha kuwa Mungu huruhusu asiyoyataka, kwa kipindi fulani. Hata hivyo, kwa mujibu wa Agano Jipya, mtu haruhusiwi kumwacha mke wake isipokuwa kwa sababu ya uzinifu.

S: Kwenye Mat 19:9, kwa nini mtu anayemtaliki mke wake na kumuoa mwanamke mwingine anazini, kwani kuoa wake wengi (mitala) kulikuwa kunaruhusiwa?
J: Hapana, mitala sio uzinzi. Mafundisho ya Yesu hapa ni yale yale kwa ndoa ya mitala au ya mke mmoja. Kuna mambo matano ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
Mtazamo wa Mungu kuhusu talaka uko wazi kwenye Mal 2:16: Mungu anaichukia. Wakati wa sheria ya Musa, Mungu aliiruhusu tu kwa sababu mioyo yao ilikuwa migumu, kwa mujibu wa Mat 19:8. Katika Agano Jipya, hairuhusiwi kumtaliki mkeo, isipokuwa tu kwa sababu ya uzinzi.
Hata hivyo, kama mke au mume wako ambaye si muamini anasisitiza kuwa akutaliki, Mungu anatuagiza kuruhusu jambo hili kwani Mungu ametuita kwa ajili ya amani, kama 1 Kor 7:15 inavyosema. Kibiblia, kutii amri ya Mungu na kumruhusu [kwa shingo upande] mwenzi kukutaliki, ni tofauti na kutotii amri ya Mungu kwa kuchagua kumtaliki mke wako.
Mtazamo wa Mungu kuhusu mitala. Adamu na Hawa walikuwa mfano watu wawili (si wengi) kuwa mwili mmoja (1 Kor 6:16). Mitala iliruhusiwa kwenye Agano la Kale na hata Jipya. Lakin kwenye Agano Jipya, imepingwa kwani viongozi wa kanisa hawawezi kuwa na mitala.
Jambo la msingi zaidi kuliko mfano wa Mungu wa ndoa ya mke mmoja na mume mmoja ni amri ya Mungu kuhusu talaka. Wamisionari wa kikristo wanapohubiri kwa watu ambao bado hawasikia injili, wamekuwa wanawaagiza watu wenye mitala moja ya mambo haya. Baadhi ya wamisionari wanawaagiza watu wa jinsi hii kuwaacha wake zao wengine na kubaki na mmoja (hasa yule wa kwanza kuolewa). Wake wengine hugawiwa mashamba na/au mali nyingine za mume wao wa zamani ili waweze kutimiza mahitaji yao. Mume huendelea kuwajibika kuwalea watoto waliozaliwa na wanawake hawa. Wengine wanawaagiza kutokumwacha mke yeyote ili kutokumnyima msaada wa kifedha. Hata hivyo, wamisionari hawaagiza wanaume hawa kutokuoa wake zaidi.
Kwa hiyo, ilikuwa kuchagua kuvunja nadhiri kwamba ndoa ilikuwa ni sababu ya uzinzi, si mitala. Bila kujali kama mtu alikuwa na mke zaidi ya mmoja au siyo, kama mtu kwa dhambi anachagua talaka, ambayo Mungu anachukia, basi Mungu hataki yeye kuolewa tena.
Kwa hiyo, kuchagua kuvunja kiapo cha ndoa ndiyo iliyokuwa sababu ya uzinzi, siyo mitala. Bila kujali kama mtu alikuwa na mke zaidi ya mmoja au la, endapo mtu atachagua talaka kwa dhambi, jambo ambalo Mungu analichukia, basi Mungu hataki mtu huyo aoe/aolewe tena.

S: Kwenye Mat 19:9, je kuna hati yeyote ya maandiko ya kale ambayo hayana kishazi "isipokuwa kwa sababu ya uasherati"?
J: Hati zote za maandiko ambazo Aland na wenzake (toleo la tatu) wanazirekodi zinasema ama "isipokuwa kwa sababu ya uasherati" au "kama si kwa sababu ya uasherati" isipokuwa hati ya maandiko iitwayo 1574. Hat hii iliandikwa karne ya 14 (BK), muda mfupi tu kabla ya mwisho wa Zama za Kati (karne ya 5 hadi 15 BK.
Pia, maandiko ya Tertullian aliyeandika mwaka 198-220 BK, alisema kuwa talaka hairuhusiwi isipokuwa kwa sababu ya uasherati kwenye Tertullian To His Wife kitabu cha 2 sura ya 2, uk.45, na On Modesty sura ya16, uk.92. Kwa hiyo, kishazi hiki hakikuwa kimeongezwa baada ya Tertullian kufa. Hakuna ushahidi unaoweza kutufanya tutie shaka kuwa kishazi hiki hakikuwepo awali.

S: Kwenye Mat 19:12, kwa ufupi, je aya hii inafundisha kuwa mtu anaweza kujifanya towashi kwa ajili ya ufalme wa Mungu kama mtu mmoja asiyeamini uwepo wa Mungu alivyosema?
J: Hapana. Hebu tuchambue mambo yote mawili yanayowezekana hapa. Kwa kuwa kuhasi kwa njia ya oparesheni nako kunaweza kuwa utowashi, suala hapa ni endapo aya hii inahusu utowashi tu, au pia utowashi unaotokana na kuhasiwa. Tumekubaliana?
Kwa kuwa kuhasi kimwili kunakwenda kinyume cha Kum 23:1, kuitafsiri aya hii kuwa utowashi kunafanana sana na 1 Kor 7:2, 7, na Wakristo wa awali walielewa kwa pamoja kuwa ni utowashi, tunapaswa kuitafsiri sawa na Agano la Kale, Agano Jipya, na jinsi Wakristo walivyo tafsiri. Angalia swali linalofuata kwa jibu la kina zaidi.

S: Kwenye Mat 19:12, Yesu anasema ". . . tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee." Hapa tunalo [kama inavyodaiwa] idhinisho la Yesu la mtu kujihasi mwenyewe. Najiuliza ni Wakristo wangapi watakaopenda kuthibitisha kujitoa kwao kwa Mungu kwa kufanya hivi? Kwa udadisi, ithinisho hili la utowashi linapingana na Kum Dt 23:1.
J: Aya hii inaongelea utowashi, si kujihasi. Lakini hebu tuangalie mambo yote haya mawili yanayowezekana.
Utowashi: Yesu hakuona shida kutumia mbalagha (kutia chumvi katika kueleza kitu) kwenye hotuba (unamaana nitoe jicho langu na kukata mkono wangu bila sababu yeyote!), na inaonekana hakuwa na wasiwasi kuwa Wayahudi hawa ambao waliijua sheria wangeshindwa kuelewa. Mafarisayo na Masadukayo walimkosoa Yesu kwa sababu nyingi, lakini Yesu hakukosolewa kwa jambo hili, kama mbalagha ilivyoeleweka.
Kuhasiwa kimwili: Kama aya hii inaongelea kuhasiwa kimwili, itakuwa inapingana na Agano la Kale kwenye Kum 23:1, na hakuna kitu kwenye Maandiko au kazi mbalimbali za waandishi toka kanisa la awali zinazoonyesha kuwa Yesu alifundisha kitu chochote kinyume na sheria ya Agano la Kale, isipokuwa sheria zinazohusu vyakula, ambapo hakuzuia vitu vingi, na talaka na upendo, ambapo Yesu alikuwa na viwango vya juu zaidi.
Kama ni kweli kuwa Yesu alimaanisha kuhasiwa kimwili, basi pasingekuwa na tofauti kwenye mstari huu kati ya watu wanaofanywa matowashi na watu wengine, na wale wanaochagua kuwa matowashi kwa ufalme wa Mungu.
Pia, hii mafundisho haya Yesu yanafanana sana na mafundisho ya Paulo kwenye 1 Kor 7:2, 7, ambapo Paulo anaongea kwa wazi kabisa kuhusu utowashi (wa wanaume na wanawake) kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Mwishoni, hatupaswi kujiuliza jinsi watu wanaoishi miaka 2,000 baada ya tukio wanavyoweza kutafsiri mstari huu katika jamii ya kisasa, bali jinsi Wakristo wa awali walivyo usoma mstari huu. Justin Martyr kwenye First Apology sura ya 14 ananukuu mstari huu, na anaongelea watu ambao wameoa/olewa marea mbili maishanin mwao. Ingawa kunaweza kuwa na maoni tofauti endapo Justin alikuwa anaongelea mitala, kuoa/olewa tena baada ya talaka, au kuoa/olewa tena baada ya kifo cha mume au mke, Justin alikuwa anazungumzia utowashi, siyo kuhasiwa. Tertullian kwenye On the Resurrection of the Flesh sura ya 27anatumia mstari huu na anaongelea "upande mzuri wa mtu ambaye hajaoa/olewa" (yaani, utowashi kwa ujumla).
Kwa muhtasari, watu wanaotafuta maongozi ya Biblia kwa maisha yao, iwe waliishi katika karne ya pili au ya ishirini na moja, wanaweza kujua maana ya jambo hili.

S: Kwenye Mat 19:14, ni kwa jinsi gani ufalme wa Mungu ni wa watoto wadogo?
J: Jambo hili linaweza kweli kwa namna kadhaa.
a) Tunapaswa kuutambua utegemezi wetu kwa Mungu kwa wokovu unaofanana na utegemezi wa watoto wadogo. Mungu huwasaidia watu wanakiri unyonge wao kwake.
b) Mungu huwatunza watoto wanaofariki kabla ya kufikia umri wa kuwajibika. Biblia inamaanisha kuwa wako mbinguni, ingawa hawana malipo yoyote.

S: Kwenye Mat 19:14, je mafundisho ya Calvin, kusema vilevile yasemavyo, yanafundusha kuwa watu wote wanaokufa wakiwa watoto wadogo wanakwenda jehanamu?
J: Hapana, haya ni madai ya uongo niliyowahi kuyasikia. Wakati Augustine, Prosper wa Aquitaine na watu wengine walifundisha kuwa watoto wote wasiobatizwa wanapokufa wanakwenda jehanamu, hawakuwa watu wenye kufuata mafundisho ya Calvin bali Augustine.
Watu wenye kufuata mafundisho ya Calvin wanaamini mtazamo wa Biblia kuwa Mungu ndiye mwenye hatima ya mwisho ya kuokoa; si ubatizo, matendo yetu wala imani yetu. Mungu anaweza kuchagua kuokoa kupita Kristo kwa namna yeyote anayotaka. Hivi ndivyo wafuasi wa Calvin wenyewe wanavyosema.
"Watu wote wanaokufa wakiwa watoto wachanga ni miongoni mwa wateule", kwa mujibu wa Lorraine Boettner kwenye The Reformed Doctrine of Predestination, uk.148, 149. Tangazo la Pili la Waskoti (The Second Scots Confession) la mwaka 1580 BK linasema, "Tunauchukia na hatuupendi kabisa uamuzi wa [kikatili wa papa] dhidi ya watoto wachanga wanaokufa kabla ya kubatizwa." C.H. Spurgeon, akitumia (kimakosa) Eze16:21, aliamini kuwa watoto wachanga wanaokufa wanaenda mbinguni. Wafuasi wengine wa Calvin wanaokubaliana na maoni haya ni pamoja na Charles Hodge, W.G.T. Shedd na B.B. Warfield. Mfuasi wamafundisho ya Calvin Curt Daniel kwenye tasnifu yake The History and Theology of Calvinism, uk.336-339, ana sehemu yenye kichwa "Dying Infants are Saved" ("Watoto wachanga wanaokufa wanaokolewa").
Hivi ndivyo Calvin mwenyewe alivyosema kwenye Institutes of the Christian Religion kitabu cha 4 sura ya 16, uk.2:541, "Lakini kwa vipi, wanauliza, je watoto wachanga wanaweza kuzaliwa upya, wakiwa hawana ujuzi wa ama mema au mabaya? Tunajibu kuwa, kazi ya Mungu, ingawa imezidi upeo wa uwezo wetu wa kuifikia, si tupu. Isitoshe, watoto wachanga wanaotakiwa kuokolewa (na ni hakika kuwa wako wanaookolewa katika umri huu) ni lazima, bila maswali, wawe wamezaliwa upya na Bwana. Kwa sababu kama wanakuja na uruthi wa uharibifu kutoka kwenye matumbo ya mama zao, ni lazima watakaswe kabla ya kuingizwa kwenye ufalme wa Mungu . . . Lakini ili kuwanyamazisha wapinzani [wakosoaji] wa aina hii, Mungu ametupa, kupitia Yohana Mbatizaji . . . uthibitisho wa kitu ambacho anaweza kufanya kwa watu wengine."

S: Kwenye Mat 19:16-17, je alikuwa anakana kuwa alikuwa mwema, au kwamba alikuwa Mungu?
J: Hapana, angalia maelezo ya Injili kwenye Mat 19:16-17 kupata jibu la swali hili.

S: Kwenye Mat 19:17, je kitu gani ni kizuri?
J: Kwenye Mwanzo 1 na 2, Mungu alisema kuwa uumbaji wote ulikuwa nzuri kabla ya anguko la wanadamu. Yesu alisema kwenye Mak 10:18 na Luk 18:19 kuwa hakuna mtu aliye mwema isipokuwa Mungu peke yake. Mungu ni chanzo cha wema, lakini kama Thomas Aquinas alivyosema, kumwelezea Mungu kuwa mwema tu kwa sababu Yeye ni chanzo cha wema, hakuna ukweli wowote zaidi ya kumwelezea Mungu kuwa na umbo la kimwili kwa sababu Mungu Yeye ni chanzo cha watu/vitu vyote vyeny umbo la kimwili.
Kwa upande wetu, wema ni sifa inayoendana na tabia na mapenzi ya Mungu. Tumeamriwa kutenda mema kwenye 1 Tim 6:18, hivyo tunaweza kuwa wema kwa kiasi fulani. Mungu ni mwema kwa namna kubwa zaidi, kwa sababu 1) Yeye ni chanzo cha wema wote, anaotupa sisi 2) Yeye ni kiwango ambacho kwacho wema unaonekana 3) na hakuna kitu kilicho kizuri kabisa isipokuwa Yeye (Mak 10:18 na Luk 18:19).

S: Kwenye Mat 19:23, je ni kweli kuwa matajiri hawawezi kuingia mbinguni?
J: Hapana, vinginevyo Ibrahimu angekuwa matatani, na Paulo, Yakobo, na mwandishi wa Waebrania, bila kumtaja Yesu, wangekuwa wamekosea kumtaja kuwa shujaa wa imani. Badala yake, ni kupenda mali, na kuzitumaini kunakoleta ugumu kwa mtu kuingia mbinguni. Mtu anaweza kuwa na utajiri mkubwa, kama Ibrahimu, lakini asipende au kutumaini mali zake.

S: Kwenye Mat 19:23, Mak 10:25 na Luk 18;25, je Yesu alimaanisha nini aliposema ngamia kupita kwenye tundu la sindano?
J: Kuna watu wanaodhani kuwa "tundu la sindano" lilikuwa ni jina la utani la lango jembamba la Yerusalemu. Ingawa Yerusalemu na miji mingine ilikuwa na malango yaliyokuwa membamba sana, hakuna lango lililoitwa "tundu la sindano" linalojulikana kwetu. Juhudi za kuufanya usemi huu wa mbalagha kuwa unaongelea lango la Yerusalemu zimepotoka.
Inaelekea kuwa Yesu alikuwa anatumia mbalagha hapa. Haiwezekani kabisa ngamia, hasa ngamia aliyebeba mizigo kupita kwenye tundu la sindano. Yesu alitumia mlinganisho huu wa kuchekesha kuonyesha jambo hili. Wayahudi kwenye Babylonian Talmud (Babylonian Berakoth 55b) wanatumia mbalagha inayofanana na hii, "tembo kupita kwenye tundu la sindano.") (Tembo walikuwa wengi sana Babeli, na kutumika kwao kunaonyesha kuwa halikuwa lango la Yerusalemu).
a) kwa kawaida, haiwezekani kwa mtu anayejidhani kuwa tajiri kuingia mbinguni, na
b) mambo yote, hata mtu tajiri kuingia mbinguni, yanawezekana kwa Mungu.

S: Kwenye Mat 19:28 na Luk 22:28-30, kwa kuwa wanafunzi watakaa kwenye vitu kumi na mbili, je Yuda Iskariote na yeye pia atakaa?
J: Hapana. Kwanza kabisa, Luk 22:28-30 haitaji viti kumi na mbili vya enzi, ila makabila kumi na mbili tu. Ni kweli Mat 19:28 HAISEMI wanafunzi kumi na wawili wataketi kwenye viti kumi na mbili. Badala yake, inasema, ". . . ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli." Hivyo inasema kutakuwa na vitu kumi na viwili vya enzi, lakini haisemi kuwa wanafunzi kumi na wawili watakaa juu yake. Badala yake, Yesu aliahidi jambo hili kwa "ninyi mlionifuata" tu. Yuda hakuendelea kumfuata Yesu na kuondoka na nafasi yake kama mwanafunzi baada ya kumsaliti Yesu, kama Mdo 1:20 inavyosema. Kwenye Mat 19:28, Yesu aliahidi jambo hili kwa "ninyi mlionifuata" tu.

S: Kwenye Mat 19:29, watu watawezaje kuwa na baba, mama, n.k. mara 100 kwenye maisha haya?
J: Aya hii inatumika kwa maisha haya na maisha yajayo. Fikiria kuwa una nyumba duniani kote zilizo tayari kukukaribisha, na watu wa rangi zote za duniani ambao ni kaka zako na dada zako wapendwa. Hivi ndivyo tulivyo navyo, au tunavyopaswa kuwa navyo kwenye jamii ya Kikristo tunayoiita kanisa. Zaidi ya hapo, mbinguni tutakuwa navyo katika hali ya ukamilifu vitu tulivyo navyo duniani katika hali isyokuwa ya ukamilifu.

S: Kwenye Mat 19:30, Mak 10:31 na Luk 13:30, ni kwa jinsi gani walio wa kwanza watakwenda kuwa wa mwisho na wa mwisho watakwenda kuwa wa kwanza?
J: Ni kwa jinsi walau nne:
Kiburi: Watu waliokuwa na kiburi katika maisha haya watadhiliwa, na wanyenyekevu watakwezwa (Yak 4:6, Luk 2:51-52).
Mali: Kwa ujumla, watu wengi walio na fedha nyingi hawaoni sana haja ya kuja kwa Mungu, kama Mit 30:8-9 inavyodokeza, na Luk 16:19-21 inatoa mfano mzuri. Paulo anasema kwenye 1 Kor 1:26-31 kuwa si wengi wa watu kwenye kanisa la Korintho waliokuwa na hekima ya dunia, au ushawishi mkubwa. Yak 2:5 inaonyesha kuwa jambo hili lilikuwa kweli katika mengi ya makanisa ya awali. Angalia pia Luk 2:53 na Yak 5:1-6.
Malipo: Mungu atawahukumu waamini kwa kuzingatia vitu walivyopewa. Kwa wale waliopewa vingi, kiasi kikubwa kitadaiwa toka kwao.
Utumishi: Waamini wakuu zaidi katika macho ya Mungu, ni watumishi wa watu wengine, kama Mak 9:35-37, Luk 9:46-48 na Mat 18:1-4 zinavyoonyesha.

S: Kwenye Mat 20:1-16, je mtu mwenye nyumba anatenda haki kwenye mfano huu?
J: Mwenye nyumba anamwakilisha Mungu, na Mungu ni mwenye haki kwa viwango vyake. Siwezi kujibu swali hili kama si mwenye haki kwa viwango vyako kwa sababu baadhi ya watu wana mawazo ya ajabu sana kuhusu haki. Mungu anatufundisha kuwa kiwango vyake vya haki vinaruhusu ukarimu maalum.
Mungu ni mwenye haki, na alimlipa kiusahihi kila mfanyakazi kitu alichoahidi.

S: Kwenye Mat 20:1-16, je watu wote watapata malipo yanayofanana mbinguni?
J: Hapana. Ingawa Mat 20:1-16 inaonyesha kuwa hayafanani, 1 Kor 3:12-15 inasema wazi kabisa kuwa tusidhani kuwa tutapata tuzo zinazofanana mbinguni.

S: Kwenye Mat 20:17-19, ni jinsi gani Mungu Mwenye enzi yote anaweza kumruhusu nabii wake Yesu kutolewa kwa watu wa mataifa kudhihakiwa na kuuawa?
J: Wakati mwingine inahitaji kuwa radhi kuonekana kuwa umeshindwa ili kupata ushindi mkamilifu.

S: Kwenye Mat 20:20-28, kwa kuwa Wakristo wakubwa ni watumishi, si watawala wa watu wengine, kwa nini baadhi ya viongozi wa kikristo wanaonekana kusahau jambo hili?
J: Madaraka huharibu watu, na watu wengi wasiomcha Mungu hujiita waamini. Unaweza kusoma baadhi ya mifano ya kusikitisha ambayo Mungu ametufundisha kwenye vitabu vya Wafalme na Mambo ya Nyakati.

S: Kwenye Mat 20:30, je walikuwa vipofu wawili, au kipofu mmoja aliyeitwa Bartimayo kama Mark 10:46-52 inavyosema?
J: Inaweza kuwa haya yalikuwa matukio mawili tofauti, kwani watu wote vipofu Yeriko walitaka kumwona Yesu. Hata hivyo, kwa kuwa katika Injili zote mbili maneno "Mwana wa Daudi, unirehemu/uturehemu" yalitamkwa, inaelekea kuwa lilikuwa tukio moja. Kwa ajili Bartimayo itakuwa ni jina la mmoja wa vipofu hao wawili. Marko, ambaye huenda alisikia habari hii kutoka kwa Petro alimfahamu kipofu mmoja tu lakini alijua jina lake. Mathayo, ambaye alikuwa pale, aliwaona vipofu wote wawili.

S: Kwenye Mat 20:32, kwa nini Yesu alimuuliza mtu ambaye ni dhahiri alikuwa kipofu kitu gali alitaka Yesu amtendee?
J: Panaweza kuwa na sababu mbili tofaauti.
Kwanza, Yesu alitaka mtu aombe kwa maneno zawadi ya kuweza kuona kabla hajapewa, na Yesu alikuwa anampa mtu huyu nafasi ya kufanya hivyo.
Pili, si kila mtu mwenye ulemavu anataka kuponywa. Kumekuwa na matukio ya watu kwenye jamii ya watu wenye ukoma ambao wamekuwa wakiwambukiza watoto wao ukoma kwa makusudi kabisa ili kwamba watoto wao nao pia waweze kusaidiwa maisha yao yote.

S: Kwenye Mat 21:1-3, Mak 11:2-3 na Luk 19:30-31, kwa nini Yesu aliwaambia wanafunzi wake wamchukue punda?
J: Wakati mfalme anaingia mjini, angeweza kupanda farasi, mnyama wa vita, ili kuashiria kuwa yeye ni mshindi. Wakati mfalme au jaji anaingia mjini akiwa amepand punda, jambo hili liliashiria kuwa amekuja kwa amani, bila jeshi lake. Pia lilitimiza unabii wa Zak 9:9-10.
S: Kwenye Mat 21:12-13, Mak 11:12-19 na Luk 19:43-48, kwa nini Yesu aliwakasirikia wabadilisha fedha hekaluni?
J: Watu hawa walikuwa kwenye nyumba ya Mungu bila ya kuwa na haina nia ya kumwabudu Mungu. Walikuwa wanawasumbua na kuwavunja moyo watu waliokuja kumwabudu Mungu. Mungu anaipa ibada yetu uzito mkubwa sana.
Mishna (mkusanyiko rasmi wa tafsiri za mapokeo yasiyoandikwa ya sheria ya Kiyahudi yenye kufanya sehemu ya kwanza ya Talmud) ya Kiyahudi inarekodi matukio ya kupandisha bei za wanyama. (Mishna za mwanzo kabisa ziliandikwa mwaka 200 BK). Endapo mtu alitakiwa kupeleka mnyama wa kumtoa kama sadaka hekaluni, na bei za kumnunua mnyama zilikuwa kubwa isivyo haki, basi maskini wangezuiliwa kumwabudu Mungu kwa jinsi inavyotakiwa.

S: Kwenye Mat 21:16-17, kwa kuwa tunapaswa lumwbudu Mungu tu, kwa nini Yesu alikubali kusifiwa?
J: Kuna mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1. Yesu hakupokea sifa na pongezi tu bali pia ibada kwenye Yoh 9:38. (Neno la Kigiriki proskuneo hapa linamaana zaidi ya shukrani na heshima).
2. Ni vizuri kuwapa viongozi watauwa sifa na heshima (lakini siyo ibada), kama Flp 2:29 inavyoonyesha. Hata hivyo, tunatakiwa kumwabudu Mungu tu (Mat 4:9-10; Luk 4:7-8, Ufu 19:10; 22:8-9).
3. Si wanadamu tu (Mat 2:2), bali hata malaika wanamwabudu Yesu kama Mungu (Ebr 1:6).
4. Yesu ni Mungu (Yoh 1:1, Ebr 1:8, 9), na Yesu ni Bwana wetu na Mungu wetu (Yoh 20:28-29).

S: Kwenye Mat 21:18-19, Mak 11:14 na 20-21, kwa nini Yesu anaonekana kuwa mkatili sana hata kuufanya mti mtini usiofikiri kukauka?
J: Swali hili linakaribia kuwa sawa na kuuliza kuwa ni mimea mingapi ya ngano iliyouawa kikatili ili uweze kula kipande chako cha mkate. Hapa hakuna jibu, kwa sababu mimea isiyo fikiri haiwezi kuuawa kikatili.
Yesu hakujishughulisha na hisia za mimea zisizokuwepo. Badala yake, kwenye Mak 13:28-29, Yesu anatuambia tuangalie mfano wa mti mtini. Wakati matawi na majani yanapochanua, ndipo wakati wa kiangazi unapokaribia. Kadhalika, wakati Masihi anakuja Yerusalemu, ukombozi wa mwanadamu u karibu.
Baada ya Yesu kufanya hivi, alitumia mfano wa mti mtini kwenye Mat 24:32.
Mwishoni mwa mwezi Machi majani huanza kuchomoza kwenye mti mitini, na vinundu vidogo vidogo vinaitwa taqsh kwa Kiarabu cha Palestina, vyenye ukubwa wa badamu mbichi, huota. Hivi hudondoka kwani si mitini ya ukweli, lakini wakulima huzila wakati wanapokuwa na njaa. Hata hivyo, kama majani ya mtini yataonekana bila taqsh, basi hapatakuwa na matunda (mitini).

S: Kwenye Mat 21:21-22 na Mak 11:24, kwa kuwa tunaweza kuomba kitu chochote kwenye sala zetu, kwa nini Wakristo hawaombi, na kuweza kujibiwa kuwa kila mtu awe Mkristo? Pia, nina orodha ndefu ya vitu ninavyovitaka . . . .
J: Mungu anaweza kufanya kitu chochote (isipokuwa kusema uongo, kujaribiwa na uovu, kujikanusha mwenyewe, au kuapa kwa mtu yeyote mkubwa kuliko Yeye mwenyewe), lakini jambo lisilowezekana kimantiki si kitu. Mungu hawezi kuumba watu ambao wanachagua kwa hiari kumpenda na kumtii bila kuwa na uwezo wa kuchagua kwa uhuru kumpenda na kumtii.
Hata Yesu mwenyewe aliulilia mji wa Yerusalemu kwa sababu ya kumkataa kwenye Mat 23:37-39. Hata Mafarisayo waliruhusiwa "walilipinga shauri la Mungu juu yao" kwenye Luk 7:30.
Kuhusiana na orodha ndefu ya vitu vinavyotakiwa, angalia maelezo ya Mat 7:7-11, kujua jinsi Mungu, kama Baba mwenye hekima, anatupa vitu vizuri tu tunavyomwomba kwa njia sahihi. Mungu asifiwe kwani hatuambii "Ndiyo" kila wakati!

S: Kwenye Mat 21:21-22 na Mk 11:24, je unapoomba na kuamini unahakikishiwa kupata kitu ulichoomba kila wakati?
J: Hapana, aya hii inasema unapaswa kuamini hasa (kuwa umepokea) kitu unachoomba. Kama unaifurahia dhambi moyoni wako (Zab 66:18), au kuomba ili utumie kitu uombacho kwa yako mwenyewe (Yak 4:3), Mungu, kama Baba mwenye hekima, hatakupa.

S: Kwenye Mat 21:23, je ua wa hekalu ulikuwa na ukubwa gani?
J: Kabla ya huduma ya Yesu, Herode (Mkuu) aliuongeza ukubwa wa ua wa hekalu kwa karibu yadi 330 kwa futi 500 (mita 300 kwa mita 460).

S: Kwenye Mat 21:23-24, kwa nini Yesu hakujibu tu swali lao kuhusu Yeye kuwa Masihi?
J: Jibu lilikuwa dhahiri kwa watu waliokuwa wanataka kujua. Hata hivyo, hata baada ya miujiza yote, haikuwezekana kutoa jibu ambalo wangelikubali, kwa sababu walikuwa wameamua kwa ukaidi kukataa kuamini. Kwa hiyo, Yesu aliongea kwa namna ambayo kama wangependa kujibu swali lake kwa uaminifu, wangeweza pia kujibu swali lao wenyewe. Kwa bahati mbaya, wauliza swali walipoulizwa, walitafuta jibu rahisi lakini huenda si lenye kufaa, na si jibu la kweli.

S: Kwenye Mat 21:24-27, Mak 11:33 na Luk 20:7-8, kwa nini Yesu alikataa kuwaambia ni kwa mamlaka gani alikuwa anafanya mambo haya?
J: Kuna mambo mawili ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1. Yesu hakuwa analazimika kujibu swali la mtu yeyote, hasa maswali ambayo hayaulizwi kwa lengo la kujua ukweli, bali kumtega.
2. Waliishajua majibu. Yesu aliishasema kuwa anatoka kwa Mungu kupitia mambo hayo aliyoyafanya. Walitaka tu usemi wa moja kwa moja wa maneno yake mwenyewe wakati huo.
Kwa kuwa tunashiriki kwenye kweli, hatupaswi kusema uongo, lakini ni SAWASAWA kukataa kujibu maswali wakati mwingine, hasa kama watu wanaotuuliza hawataki kujua ukweli, bali wanataka kukujaribu na kukutegatega.

S: Kwenye Mat 21:33-41, kwa kuwa Mungu anafananishwa na mwenye shamba, je kuna wakati ambapo hajui kitu kinachoendelea?
J: Mwenye shamba anafananishwa na Mungu, lakini anajua kitu kinachotokea, kama ilivyothibitishwa na kutolewa kwa mfano huu na Yesu. Mungu ni mvumilivu na mstahimilivu sana, mfano huu unatuonyesha kuwa yuko tayari kuruhusu hata kuendelea kwa kutokutii na udhalimu, na hata kifo cha Mwana wake, kwa ajili ya watu waliopotea. Hii ni kwa lengo kuwa waweze kuja kwake. Hata hivyo, uvumilivu wa Mungu una mwisho, kwenye siku ya hukumu, wakati mambo yote yatakapowekwa sawa.

S: Kwenye Mat 21:46, je Yesu alikuwa nabii kweli au watu walimwona tu kuwa nabii?
J: Kwamba watu "walimuona kuwa nabii" hakuonyeshi endapo alikuwa nabii kweli au la. Alitoka kwa Mungu, aliongea maneno ya Mungu, na alitabiri mambo ya baadaye, kwa hiyo alikuwa nabii, na watu wengi walimwona hivyo.

S: Kwenye Mat 22:13-14, inakuwaje Mungu mwenye upendo tu ageuke na kuwatupa kwenye giza?
J: Ni nani aliyesema kuwa Mungu ni mwenye upendo tu? Biblia haisemi hivyo. Kama Rum 11:22 inavyosema, tazama wema na ukali wa Mungu. Mungu ni mwenye upendo zaidi ulimwenguni. Lakini, hapendi kwa jinsi watu wengine wanavyoelezea, endapo maelezo yao yanapingana na sifa zake nyingine za utakatifu, haki, na hasira. [???? recheck the meaning of ‘God, all-loving??]

S: Kwenye Mat 22:14, je msemo "waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache" unaongelea kutofautiana na viwango vya imani na uhakika, kama Wabaha’i wanavyofundisha kwenye Some Questions Answered, uk.129-131?
J: Hapana. Ukisoma mfano wote kwenye Mat 22:1-14, unaweka watu katika makundi mawili: wale wanaoingia kwenye karamu ya harusi na wale wasioingia. Msemo "waitwao ni wengi, bali wateule wachache" unawaongelea watu walioalikwa kuingia karamuni lakini walikataa, na mtu aliyetaka kuingia bila vazi linalotakiwa.
Kuna somo kwa kila mtu hapa. Huwezi kusoma aya moja tu ya Biblia na kupuuzia mambo yaliyoandikwa kabla au baada ya aya hiyo, na kutarajia kupata maana sahihi.

S: Kwenye Mat 22:29, kwa nini Yesu aliwaambia Masadukayo, ambao ni dhahiri kuwa walisoma Maandiko, kuwa wanapotea kwa sababu hawayajui Maandiko wala uwezo wa Mungu?
J: Masadukayo waliamini vitabu vitano tu vya kwanza vya Agano la Kale (Mwanzo hadi Kumbukumbu la Torati) kuwa Maandiko, si sehemu iliyobaki ya Biblia, kwa mujibu wa waandishi wa awali wa Kikristo. Josephus pia alisema kuwa walifuata vitu vile tu vilivyokuwemo kwenye Torati. Hata leo, watu wanaweza kusoma na kujifunza Biblia, lakini bado wanachagua kuwa wajinga wa nguvu za Mungu na maana ya kuamini Maandiko.

S: Je Mat 22:30 inamaanisha kuwa hatutakuwa na miili hii tuliyo nayo huko mbinguni, kwa kuwa tutakuwa kama malaika na malaika ni roho (Ebr 1:14)?
J: Hapana. Ulinganifu unahusu ndoa. Aya hii haisemi tutakuwa kama malaika kwa namna zote, bali kwa namna hii tu.

S: Kwenye Mat 22:30, Mak 12:25 na Luk 20:34-35, je maneno haya yanamaanisha kuwa hakuna ndoa mbinguni, au tu kwamba hakutakuwa na sherehe mpya za ndoa, lakini baadhi ya ndoa za duniani zitaendelea hadi mbinguni?
J: Tunajua kuwa hakuna ndoa mbinguni kwa kusoma Rum 7:2. Mwanamke hangeweza kuolewa na watu zaidi ya mmoja. Hata hivyo, endapo mume wake amekufa, anafunguliwa kutoka kwenye ndoa na anaweza kuolewa tena. Hivyo, haendelei kuwa ameolewa mbinguni.
Kama nyongeza, dini ya uongo ya Umormoni inaamini kuwa baadhi ya "Ndoa za Hekaluni" zinadumu milele. Hata hivyo, mume akifa, mke anaweza kuolewa tena. Ila hataweza kuwa na ndoa mbili za hekaluni kwa muda mfupi na milele yote. Kwa mtazamo wa Kimormoni, mwanaume Mmormoni mbinguni atakuwa anafikiri nini wakati mke wake "anajihusisha na uzinifu" kwenye ndoa ya kawaida mara baada ya yeye (mwanaume) kufa?

S: Kwenye Mat 22:30, je aya hii inaunga mkono vitendo vya ndoa nje ya ndoa, kama dhehebu linalojulikana kuwa na imani potofu la Family of Love (zamani liliitwa Children of God) linavyodai?
J: Sivyo hata kidogo. Kusema kuwa hatutakuwa na ndoa mbinguni, inamaana tu kitu Yesu alichosema inamaanisha, kwamba hakutakuwa na haja ya ndoa mbinguni. Aya hii haisemi kuwa tunapaswa kuwa aidha tunajamiiana ovyo, au matowashi kabisa wasiokuwa na ndoa duniani. Madai ya jinsi hii yanaonyesha namna watu wanavyoweza kwenda mbali zaidi wanapojaribu kuingiza maoni yao wenyewe ambayo hayapo kwenye Biblia.

S: Kwenye Mat 22:30, Mak 12:25 na Luk 20:34-35, baba yangu amefariki dunia hivi punde. Mama yangu amehuzunishwa sana na anataka kujua endapo ataendelea kuwa mke wake mbinguni. Sijui jinsi ya kujibu maswali yake. Ninajua kuwa Mat 16:19 inasema kuwa kilichofungwa duniani kitafungwa mbinguni na kilichofunguliwa duniani kitafunguliwa mbinguni. Hata hivyo, nimesikia ikisemwa kuwa "hakuna ndoa mbinguni." Sina aya inayounga mkono maoni haya, lakini nimesikia yakisemwa. Unaweza kunisaidia kuelewa?
J: Pole zangu nyingi sana kwako na familia yako kwa kufiwa na baba yako. Sidhani Mat 16:19 ilikusudiwa kuahusishwa na ndoa, lakini kuwa huru kwenda mbinguni. Badala yake Mat 22:23-32 inahusishwa. Masadukayo, waliokuwa wanakataa kuwa kuna kufufuka, walikusudia kuwaaibisha Yesu na Mafarisayo kwa kusema kuwa endapo ndoa ziko mbinguni kama zilivyo duniani, je itakuwaje kwa mwanamke anayekuwa mjane mara kdhaa?
Kwenye Mat 22:30, Yesu alijibu kwamba watu hawaoi wala kuolewa mbinguni lakini ni kama malaika wa Mungu, na malaika wanatarajiwa kutokuoa. Wako watu ambao wamejaribu kuifanya aya hii imaanishe kuwa hakuna harusi mbinguni, lakini watu waliokuwa wameoana waliendelea kuwa na ndoa. Hata hivyo, hii si tafsiri sahihi ya aya hii, kwa sababu kama Yesu angekuwa amemaanisha hivyo, basi hoja ya Masadukayo isingekanushwa. Kwa maneno ya kisasa, endapo mjane angeolewa tena, basi ingekuwa:
1) Mume wake wa kwanza mbinguni amepotez mke tu, au
2) Mjane angekuwa na waume wawili mbinguni, au
3) Kama yeye (mjane) hangekuwa na uhakika wa wokovu wa mume wake, asingeweza kujua endapo angali ameolewa au hajaolewa mpaka atakapofariki, kwa sababu inatarajiwa kuwa mtu aliyeko mbinguni hawezi kuolewa na mtu aliyeko jahannamu.
Hapana, kama kiapo cha ndoa kinavyosema, "hadi kifo kitakapo tutenganisha." Kama mama yako angeamua kuolewa baadaye hakuna ubaya wowote kwenye jambo hilo, kama Paulo anavyofundisha kwenye Rum 7:1-3. Jambo hili linaweza kukufanya ujisikie vibaya mwanzoni, kumuona akiwa na mtu mwingine, lakini utahitaji kulizoeza jambo hilo, kitu ambacho Mungu amekiidhinisha tusiseme kuwa ni makosa.
Baada ya kusema yote haya, haimaanishi kuwa (mama yako) hawezi kuwa pamoja na mume wake wa zamani kwa miaka maelfu kwa maelfu, kama marafiki mbinguni. Natarajia kuwa mbinguni tutakapokuwa wakamilifu, mumewe atampenda zaidi mkewe hata zaidi kuliko alivyompenda hapa duniani, na mke naye vivyo hivyo. Kwa hakika, wote wawili watampenda Mungu hata zaidi.

S: Kwenye Mat 22:31-32 na Mak 12:26, je Yesu yuko sahihi kuongea hivi kwa kuzingatia wakati wa kitenzi (mimi) "ni?"
J: Inaonekana ni hivyo, kwa sababu Masadukayo hawabishana na Yesu kuhusu wakati wa kitenzi cha neno la Kiebrania.
Zaidi ya hapo, hapangekuwa na maanaa yoyote ile ya kuwataja Ibrahimu, Isaka na Yakobo kama hawapo, na kama Mungu angekuwa anakwenda kuwatelekeza watu wengine wakati wanapokufa.

S: Kwenye Mat 22:35-36 na Mak 12:28-29, kwa nini Yesu hakukemea swali hili kama alivyofanya kwenye swali lingine lililopita linalohusu ndoa?
J: Swali lililopita lililomhusu mwanamke aliyekuwa na waume saba halikuulizwa kwa ajili ya kupata ukweli lakini kumtega Yesu. Swali hili liliulizwa kwa sababu muulizaji alikuwa na nia ya kweli ya kutaka kusikiliza kitu ambacho Yesu angesema. Kumuliza Mungu swali lolote lile kwa heshima ni SAHHI, ili mradi tunauliza ili kujua ukweli na kuufuata.

S: Kwenye Mat 22:37-40 na Mak 12:30, je Yesu aliongeza maneno kwenye Kum 6:4, au aliielezea bila kuongeza?
J: Mara nyingi Injili hufafanua maneno ambayo Yesu alisema, na hazisemi maneno yale yale aliyoyasema. Mat 22:37-40 inasema moyo, roho na akili. Mak 12:30 inasema moyo, roho, akili na na nguvu. Matini Kimasoretiki (Kiebrania) ya Agano la Kaleyanasema moyo, roho na nguvu, lakini baadhi ya maandiko ya tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale (Septuagint) yanaongeza neno "akili", hivyo Yesu hakuwa wa kwanza kuongeza neno "akili." (Maandiko ya Philo Myahudi, tuliyo nayo hayaongelei Kum 6:4. Hati za Kale toka Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scroll) 4Q43 (= 4QDt (p)) ina Kum 6:4-11., lakini sijaona tafsiri yake.)

S: Kwenye Mat 22:37, je amri kuu inahususha "moyo, roho, na akili" au hata "nguvu" kama kama Mak 12:29-30 inavyosema?
J: Kuna majibu mawili yanayoweza kutolewa.
1. Yesu angeweza kusema kwa njia tofauti, hivyo inaweza kuwa yote mawili ni sahihi.
2. Maelezo ya Injili yanaandika mambo ambayo Mungu aliwawezesha wainjilisti kuyakumbuka. Hakuna tatizo hapa kuwa na tafsiri yenye kushikilia maoni ya kale (ya kanisa) ya Maandiko na kusema kuwa kumbukumbu ya Mathayo haikuwa sahihi hapa, kwa sababu alisahau neno "nguvu."
Je ni jibu lipi kai ya haya mawili ni kweli? Kwa kweli haijalishi, kama ambavyo jibu la swali linalofuta linavyoonyesha.

S: Kwenye Mat 22:37, kwa nini Mungu Mwenye enzi aruhusu "amri kuu" ihifadhiwa kimakosa, kwa namna mbili tofauti, kama "moyo, roho, na akili" kwenye Mat 22:37, na kama "moyo, roho, akili na nguvu" kwenye Mak 12:29-30?
J: Sababu ya Mungu kuruhusu kwa makusudi kabisa jambo hili inaweza kutolewa kwenye 2 Tim 2:14. Ni rahisi sana kwa watu kupata kunasa kwenye maneno halisi, na kupuzia kuliamini na kulifanyia kazi wazo kuu.
Biblia ni sahihi na ya kweli kabisa, lakini haikuandikwa na kuhifadhiwa kwa usahihi mkamilifu. Kutokana na kwamba Biblia iliandikwa na kuenezwa kwa usahihi wote ambao Mungu aliutaka (na ni sahihi sana kwenye baadhi ya sehemu), upungufu wa usahihi kwenye Biblia una umuhimu mkubwa kwenye macho ya baadhi ya watu kuliko kwa Mungu.
Mungu angeweza kuihifadhi amri hii na sehemu nyingine za Biblia kwa usahihi zaidi, lakini inawezekana kutokuwepo kwa usahihi kwenye sehemu za Biblia kulifanywa kwa makusudi na Mungu. Mungu amesisitiza ni jinsi gani tunapaswa kuwa makini katika kuyatii Maandiko, lakini tunapoanza kubishana juu ya kutokuwepo kwa usahihi tunaanza kutokutii Maandiko kwenye 1 Tim 6:4 na 2 Tim 2:14.

S: Kwenye Mat 22:40, ni kwa vipi torati na manabii hutegemea amri hizi mbili?
J: Sheria zote zinahusika na jinsi tunavyompendeza Mungu na kuhusiana naye, na jinsi tunavyowapenda watu wengine na kuhusiana nao. Ni kweli sheria ilikuwa na matokeo mengine yenye manufaa, kama kupunguza magonjwa, kambi safi zaidi, familia bora zaidi, n.k. lakini Waisraeli hawakufahamu matokeo haya yenye manufaa.

S: Kwenye Mat 22:41-45, je Mathayo alikuwa anapinga kuwa Yesu alikuwa Mwana wa Daudi kwa kunukuu Zaburi 110?
J: Sivyo hivyo kabisa, kwani Mathayo alimtaja Yesu kuwa Mwana wa Mungu kwa wazi kabisa kwenye Mat 4:3, 6; 8:29; 14:33; 16:16; 26:63; 27:40, 43, 54. Pia Yesu ameelezwa bila kutajwa moja kwa moja kuwa Mwana wa Mungu kwenye Mat 2:15; 3:17; 17:5; 22:45. Yesu aliitwa Mwana wa Daudi kwenye Mat 1:1; 9:27; 15:22; 20:30, 31; 21:9, 15; 22:42. Yesu alikuwa anawapa Mafarisayo fumbo, ambalo wasingeweza kupata jibu lake hadi watakapompokea. Kukubaliana kwa Yesu na nukuu ya Zaburi 110 kunaonyesha kuwa Yeye ni Bwana wa Daudi, na hakukanushi ukweli kuwa Yesu alikubaliana na Zaburi 110 na alinukuu kuwa Yeye alikuwa Mwana wa Daudi pia.

S: Je Mat 22:42 inathibitisha Yesu kufanyika mwili kwa kuonyesha kuwa Yesu, Mwana wa Daudi, alikuwa ni kufanyika mwili upya kwa Daudi, kama washiriki wa dhehebu (linalojiita kwa uongo) Unity School of Christianity linavyodai?
J: Hapana. Msemo "Mwana wa Daudi" unaweza kumaanisha mtoto wa kuzaliwa na, au mtu aliyetokana na (wa ukoo wa). Yesu alikuwa alitokana na (wa ukoo wa) Daudi. Hakuna ushahidi wa kufanyika mwili upya kwenye Maandiko, lakini kuna mafundisho dhidi ya dhana ya kufanyika mwili upya. Ebr 9:27 inasema watu wamewekewa kufa mara moja na baada ya kufa hukumu. Pia mawazo kuwa tunajaribu tena na tena, labda mpaka tunapoelewa "sawasawa", yanakwenda kinyume kabisa na na mafundisho ya watu kufa kisha kwenda mbinguni au jehanamu.
Mwandishi toka kanisa la awali aliyeitwa Minucius Felix (mwaka 210 BK) analijumuisha jambo hili vizuri sana. Anasema dhana ya nafsi za watu kurudi kwa wanyama ni "mzaha wa wachekeshaji wapumbavu" The Octavius of Minucius Felix ch.34 p.194

S: Kwenye Mathayo 23, je Yesu alikuwa sahihi kuwa mbishi kiasi hicho?
J: Ingawa kujadiliana ni kitu SAHIHI (kama Paulo alivyofanya), Yesu habishani kwenye sura hii. Yeye anasema tu mambo kama yalivyo, na anawakemea sana Mafarisayo. Kama wazo la Yesu kumkemea mtu sana ni geni kwenye thiolojia yako, thilojia yako inaweza kuhitaji mabadiliko ili ifanane na kitu ambacho Yesu angefanya.

S: Kwenye Mat 23:9, kwa ufupi, kwa kuwa hatupaswi kumwita mtu yoyote baba, je tunaweza kuwaita baba zetu wa hapa duniani namna hiyo?
J: Ndiyo. Yesu hakuwa anapinga kumwita mtu mwenye uhusiano wa moja kwa moja wa kimwili na uhusiano wa kiukoo wa baba, kama Yesu mwenyewe alivyotumia neno hili katika muktadha huu kwenye Luk 11:47, Yoh 6:58. Yesu alipinga kutumia vyeo vya kidini vya baba, bwana, mwalimu, rabi, kama Wayahudi walivyofanya.

S: Kwenye Mat 23:9, je Yesu anamaanisha nini anaposema "wala msimwite mtu baba duniani?" Ni dhahiri tunaweza kuwaita wazazi wetu wanaume "baba." Pia tunaweza kuwaita viongozi wetu wa kiroho -- wachungaji -- "baba." Paulo mwenyewe aliwaita viongozi wa kiroho "baba." 1 Kor 4:15, "Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili." Mdo 7:2 "Naye akasema, Ndugu zangu na BABA zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Ibrahimu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Harani." Kwa mujibu wa Maandiko haya, je Wakatoliki wako sahihi wanapowaita wachungaji/mapadri wao "baba?"
J: Ndiyo, Wakatoliki wanaikosea aya hii wanapowaita wachungaji/mapadri baba. Hata hivyo, endapo kanisa Katoliki lingebadilisha jina "baba" (father) kuwa "nyoa" (feather) jambo hilo peke yake lisingetatua kitu chochote. Nadhani kuna njia za msing zaidi kwenye aya hii ambazo hawazifuati.
Hili ni swali nzuri lenye kugusa somo muhimu sana katika ukristo: jinsi gani hasa Mungu ni Baba yetu, kwa namna ambayo hakuna binadamu atakayeweza kuwa? Kwanza tuangalie kitu gani si jibu, kisha jibu.
Mat 23:9 HAIMAANISHI mambo haya matatu
Uhusiano wa kuzaliwa au kuasiliwa haupaswi kukataliwa. Biblia inasema fulani-na-fulani alikuwa baba wa fulani-na-fualni, ikitumia neno baba kwa mzazi na mhenga kama kwenye Isa 38:5. Yesu aliongea bayana kuhusu uhusiano wa kuzaliwa wakati alipozungumzia baba na mama wa kidunia wa watu kwenye Mat 10:37.
Majukumu ya kifamilia hayawezi kukwepekwa. Kwenye 1 Tim 5:8, Biblia inasema kuwa mtu asiyewatunza ndugu zake, hasa familia yake mwenyewe, ameikana imani na ni mbaya kuliko mtu asiyeamini. Kwenye Mak 7:11, Yesu alithibitisha jambo hili kwa kuongelea dhambi ya kuuita msaada ambao mtu angeutoa kwa familia yake Korban au kitu kilichotolewa kwa Mungu.
Mtu aliyekuleta kwa Kristo. Paulo anaelekea kuwa hakumuasili Timotheo, badala yake kuna uwezekano mkubwa kuwa Paulo alimwita Timotheo mtoto wake kwa sababu alimleta kwa Yesu (1 Tim 1:2, 18; 2 Tim 1:2; 2:2; Fil 2:22). Hili pia ni wazo la 1 Kor 4:15-17. Kuna wazo hapa ambalo Wakristo wengine wanawezakuwa wamelisahau. Kama ambavyo kuwezi kumwacha mtoto wako wa kumzaa, usimwache mtoto wako wa kiroho. Kwa kadri inavyowezekana, hakikisha kuwa wanashiriki kwenye kanisa linaloamini Biblia. Wasaidie kithiolojia, na kwa mahitaji ya kimwili kama watakuwa nayo, na hakikisha kuwa wanakula na kushiba maziwa ambayo ni neno la Mungu.
Mat 23:9 haitumiki kwenye mambo haya manne:
Kwenye mamlaka na majukumu, usimpe mtu yeyote duniani jukumu la Mungu Baba. Yeye (Mungu) ndiye chanzo cha wokovu, chanzo chetu cha kweli, cha chanzo halisi cha mamlaka. Ingawa baadhi ya Wayahudi walifikiri kuwa Musa ndiye aliyewapa mana, mkate kutoka mbinguni, Yesu alilazimika kuwakubusha kuwa HAKUWA Musa, bali Mungu aliyewapa chakula kutoka mbingunikwenye Yoh 6:32. When Critics Ask, uk.356 inaongeza kuwa tusimchukulie mwanadamu yeyote yule kuwa kiongozi wetu wa kiroho asiyefanya makosa, lakini ni vema kuwa na washauri/wanasihi wanadamu tunaowajua kuwa wana weza kutenda dhambi.
Kwenye uhusiano, Mungu ni chanzo cha wokovu, na si mtu yeyote ambaye maisha yake hapa duniani yanaishia kwenye kifo. Kufanyika kwetu watoto wa Mungu hakuletwi na ukoo wetu wa asili au njia za kibinadamu, bali tunazaliwa na Mungu kwenye Yoh 1:13. Mkristo mmoja alisema "Mungu hana wajukuu." Ama unakuwa mtoto wake aliyezaliwa naye Yeye mwenyewe ama si mtoto wake (1 Yoh 3:1-2), lakini huwezi kuwa mjukuu wa Mungu. Kama unaweza kuwa na watu kadhaa ambao ni watakatifu sana wanaosimama mbele ya Mungu kwa ajili yako, je jambo hilo litakuokoa? Yer 15:1 inasema kuwa hata kama manabii Musa na Samweli wangesimama mbele ya Mungu kwa ajili ya Wayahudi, ingewasaidia kuokolewa. Hakuna mtu anayeweza kumpeleka mtu mbinguni ilsipokuwa Mungu, na hakuna njia ya kwendea mbinguni isipokuwa kumjua Mungu.
Kunyume na hayo, angalia heshima kubwa wanafunzi wa Kiyahudi waliyokuwa nayo kwa waalimu wao, na usiwape heshima kubwa namna hiyo waalimu wako wa kidini ambao ni wanadamu. Wayahudi waliweka matumaini yao kwa Musa (Yoh 5:45-46). Musa alikuwa mtu mkubwa, na mwenye kucha Mung, lakini hata hivyo, tumaini letu liwe kwa Mungu tu.
Kwenye jina, kuweza kwetu kumwita Mungu Baba ni heshima ya thamani sana kwenye Efe 3:14. Aya kadhaa za kuziangalia miongoni mwa aya nyingi zenye kumwita Mungu Baba yetu ni Mal 1:6; 2-10 na Isa 63:16. Wayahudi walijiita watoto wa Ibrahimu kwenye Yoh 8:39. Yesu hakukataa ukweli kuhusu nasaba kwenye Yoh 8:39 b-40, lakini alikanusha kwamba mahusiano na vizazi vya mtu vilivyotangulia hayamhakikishii mtu uhusiano wa kiroho. Yohana Mbatizaji aliwaambia Mafarisayo na Masadukayo, "wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye Baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya mit; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni" (Mat 3:9-10.
Kitabu kiitwacho When Critics Ask, uk.356 kinajumuisha vizuri kikisema kuwa zaidi ya Mungu na neno lake hatuna viongozi wa kiroho wasiofanya makosa na ambao hawatakufa, lakini tunawakubali washauri wa kiroho wenye uwezo wa kutenda dhambi.
Lakini je . . .
Ayu 29:16 inasema "Nalikuwa baba kwa mhitaji." Haimaanishi kuwa Ayubu aliwasaidia kiroho, badala yake alisimama na kutimiza familia majukumu ya kifedha, kwa watu ambao hakuwa na uhusiano nao. Kadhalika Zab 68:5 inaonyesha kuwa tunapaswa kuwa baba wa yatima.
Isa 51:2 inasema mwangalie Ibrahimu Baba yenu, na Sara aliyewazaa? Ibrahimu na Sara kwa pamoja inaonyesha kuwa msemo huu unaongelea uhusiano na mababu. Mungu anaagiza kuangalia mababu hawa, ambao mnawatamani, na kuiga imani yao, na kuona jinsi walivyobarikiwa. Hata hivyo, hakuna kitu chochote kwenye Isaya 51 kinachoonyesha kuwa Ibrahimu (au Sara) angeweza kufanya kitu chochote kile kwao sasa; Mungu tu ndiye anayetuokoa.
2 Fal 2:12 Elisha alimwita Eliya, "baba yangu, baba yangu." Maneno haya hayaelekei kuonyesha uhusiano wa karibu wa ufuasi. Ingawa wengi wanaona kuwa Elisha alimkuchukuliwa Eliya kuwa baba yake wa kiroho, Yesu kwenye Mat 23:9 anasema kuwa hatupaswi kuwachukulia watu jinsi hiyo siku hizi.
1 Kor 4:15-17 "Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili. (16) Basi, nawasihi mnifuate mimi. (17) Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana." Maneno haya yanaongelea Paulo kuwaleta wasomaji wake kwa Kristo, siyo jukumu. Paulo alikuwa mtume kanisani, hapakuwa na jukumu la "baba" kanisani. Kwa maelezo zaidi kuhusu majukumu kanisani angalia 1 Kor 12:28-29; Mdo 6:1-4; 1 Tim 3:1-13; Tit 1:5-9.
Kwenye Mdo 7:2 wakati Stefano alipowaita ndugu/kaka na baba, kuna mambo mawili yanayoweza kumaanishwa. Kwanza ni kwamba Stefano alikuwa anawaheshimu tu viongozi wake kwenye jamii ile, bila kukubaliana na imani zao. Mtazamo wa pili ni kuwa Stefno alikosea kuwaita namna hii hapa.
Kwenye 1 Yoh 2:12, 13, 18 aliwaita wasomaji wake "watoto wadogo" na "watoto" kwenye 1 Yoh 2:1. Yohana alikuwa mzee kuweza kuwaita watoto. Ebr 13:17 inasema kuwa viongozi kanisani wana mamlaka, na watatakiwa kutoa hesabu ya usimamizi wao kwa Mungu. Hivyo ingawa hakuna aya kwenye 1 Yohana inayosema mtu yeyote aliwahi kumwita Yohana "baba", Yohan aliwachukulia watu aliowahudumia kuwa kama watoto wake.
1 Yoh 2:13, 14 zinawaongelea "fathers" pamoja na vijana na watoto. Ingawa kifungu hiki cha kishairi kinaweza pia kuwa kinaongelea uhusiano na kuwaleta watu kwa Kristo, kifungu hiki hakiungi mkono jukumu la kikanisa la baba, isipokuwa kama kuna jukumu la kikanisa la "kijana" na "mtoto."
Kwa kuhitimisha, Wakatoliki wanakosea kuwaita wachungaji/mapadri baba, lakini tusibishane juu ya manena. Suala halisi ni kuwaamini makuhani wenye uwezo wa kutenda dhambi kuliko neno la Mungu lisilokuwa na makosa, na kuamini mamlaka ya mapapa na mabaraza ya kanisa ambavyo wakati mwingine vinakuwa viouvu sana kuliko Mungu mwenyewe kupitia neno lake.
Onyo: Mwisho, usidhani kuwa kuuona ukweli wa Biblia kunatoa idhini ya kuacha kuangalia kweli nyingine zilizomo kwenye Biblia. Kifungu kizima cha Mat 23:5-13 kinaonyesha jinsi viongozi wa kanisa wanavyotakiwa kuwa viongozi-watumishi, kinyume na Mafarisayo na watu wengine waliokuwa wanawaamrisha watu wengine.

S: Kwenye Mat 23:14 na Mak 12:40, je waandishi walikulaje kwenye nyumba za wajane?
J: Labda ni kwa njia inayofanana na jinsi walimu wa uongo wanavyofanya siku hizi. Wanapowaambia watu kutoa kwa ajili ya huduma yao, kwa nia binafsi ya kutaka kupokea kwenye maisha haya, wanaweza kuwa wanawaambia watu kutoa kwenye huduma ambayo Mungu anaweza kuwa hataki wachangie.

S: Kwenye Mat 23:17, kwa nini Yesu aliwaita watu wapumbavu, kwani alituambia tusifanye hivyo kwenye Mat 5:22?
J: Kuna mambo mawili ya kuyazingatia katika kujibu swali hili, ingawa sehemu ya pili ni ya muhimu zaidi.
Neno "mpumbavu" kwenye Mat 5:22, raca, ni msemo usiokuwa rasmi wenye kudharirisha ambao maana yake iliyo wazi ni "empty-head." Msemo wa kiingereza "mjinga" unafanana nalo sana. Yesu hakuwatukana watu kwa kuwadharau wakati alipotumia neno hili kwenye Mat 23:17 na hatupaswi kuwaita watu hivyo. Yesu alitumia neno mjinga lililoelezea lakini si neno lisilokuwa rasmi: meroi. Isitoshe, tunapaswa kuwaona watu kuwa wenye thamani kubwa, walioumbwa kwa mfano wa Mungu, na siyo watu wasiokuwa na thamani.

S: Kwenye Mat 23:35 na Luk 11:51, kwa kifupi, Zakaria alikuwa ni nani?
J: Huyu siye nabii Zakaria. Badala yake, huyu alikuwa Zakaria kuhani, ambaye Yoashi alimuua kwenye 2 Nya 24:20-21. Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati kilikuwa cha mwisho cha Agano la Kale kwa kufuata mpangilio wa Biblia ya Kiebrania. Hivyo Yesu alipotaja watu walifia imani kutoka Habili hadi Zakaria, alikuwa anamtaja shahidi wa kwanza hadi wa mwisho kwenye Agano la Kale.

S: Kwenye Mat 23:35, je Zakaria aliyekufa ni yule mwana wa Birakira, au mwana wa Yehoyada aliyeuawa kati ya ua wa nyumba ya Bwana kwenye 2 Nya 24:21?
J: Tuanze kwa kuangalia maoni manne ya Wakristo, na kisha vigezo vinavyotumiwa kuunga mkono kila moja ya maoni hayo.
1. Zakaria mwana wa Yehoyada
Maoni haya yanakubaliana na kila kitu, endapo msemo "mwana wa Birakira" utachukuliwa kuwa ni nyongeza ya wanakili maandishi
2. Zakaria mwana wa Birakira
Maoni haya yanakubaliana na kila kitu, ikichukuliwa kuwa Kristo anatupa habari mpya ya jinsi nabii Zakaria alivyokufa.
3. Yehoyada alikuwa na majina mawili: Birakira linaweza kuwa jina la utani lenye kumaanisha aliyebarikiwa na Mungu. Maoni haya yalianzishwa zamani na Jerome (mwaka 373-420 BK).
4. Babu: Inawezekana Zakaria mwana wa Yehoyada, alikuwa babu/mhenga wa Zakaria na walikuwa ni mtu mmoja.
Vigezo vinavyounga mkono maoni mbalimbali:
Zakaria mwana wa Birakira alihudumu mwaka 520-480 KK. Alikuwa mmoja wa waandishi wa mwisho wa Agano la Kale kwa kufuata muda halisi wa kuandika, na Agano la Kale halijaandika jinsi alivyokufa.
Zakaria mwana wa Yehoyada kuhani aliuawa karibu mwaka 800 KK, kabla ya uhamisho wa Babeli. Baba yake Yehoyada aliishi miaka 130 na alizikwa pamoja na wafalme huko Yerusalemu kwa mujibu wa 2 Nya 24:15-16. Kwa sababu ya utofauti wa muda wa kuishi kwao, hakuna uwezekano kuwa kina Zakaria hawa wawili walikuwa ni mtu mmoja.
Tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale (Septuagint) inamwita mwana wa Yehoyada "Azaria mwana wa Yodae kuhani", na mwandishi wa kitabu anaitwa "Zakaria mwana wa Barakia mwana wa nabii Addo." Hivyo Septuagint haionyeshi tofauti yoyote hapa, ila matamshi ya majina.
Targumu (tafsiri ya Kiaramu ya Biblia ya Kiebrania, yaani Agano la Kale) ya Omb 2:20 na John Chrysostom wanasema nabii Zakaria mwana wa Birakira aliuawa kati ya ua wa hekalu; hata hivyo, walikosea. (Hata hivyo, sijafanikiwa kuthibitisha maoni haya ya John Chrysostom).
Kaburi la Zakaria lilikuwa ni alama mashuhuri sana iliyokuwa Yerusalemu ya wakati wa Kristo.
Zakaria lililotumiwa na watu wengi. Kuna watu 32 kwenye Biblia walioitwa Zakaria.
Nje ya Biblia, Zakaria mwana wa Baruch/Baris/Bariscaeus aliuawa na Waziloti (wanachama wa dhehebu la kale la Kiyahudi lililokuwa na lengo la kuleta utawala wa Mungu kupitia kwa makuhani na liliwapinga Warumi hadi mwaka 70 BK) wawili kwa mujibu wa Josephus kwenye The Jewish Wars 4:334-344. Aliuawa kwenye eneo la hekalu, lakini huenda isiwe kwenye ua wa hekalu, hivyo maelezo haya yanaweza yasiwe sahihi, hasa kwa sababu vita vya Wayahudi vilitokea baada ya Yesu kuondoka.
2 Mambo ya Nyakati kilikuwa ndio kitabu cha mwisho kwenye mpangilio wa Agano la Kale la Kiebrania. Ingawa mwana wa Yehoyada hakuwa shahidi wa mwisho wa imani kuuawa kwa kufuata muda halisi wa matukio, kusema Habilihadi Zakaria mwana wa Yehoyada, kulikuwa kama aina ya msemo wa kikristo usemao "kutoka Mwanzo hadi Ufunuo."
Luk 33:50 haina msemo "mwana wa Birakira."
Irenaeus (mwaka 182-188 BK) kwenye Against Heresies kitabu cha 5, sura ya 14.1, uk.541 ananukuu Mat 23:35 akisema, "Zakaria mwana wa Barakia." Kwa hiyo, kama hii ilikuwa ni nyongeza ya wanakili maandishi, ilikuwepo kabla ya Irenaeus kuandika. Tatian (karibu mwaka 170 BK), kwenye Diatessaron pia anamtaja Zakaria mwana wa Birakiya (sehemu ya 41). Pia kuna hati ya maandiko ya kale ya Kigiriki iliyoandikwa kabla ya hati za Sinaiticus na Vaticanus ambayo ina Mat 23:35. Hii ni p77 (iliandikwa kati ya katikati hadi mwisho wa karne ya pili) nayo pia inamtaja mwana wa Birakiya. Kwa hiyo, kama "mwana wa Birakiya" ilikuwa ni nyongeza, itakuwa iliongezwa mapema sana, kabla ya mwaka 170 BK.
Origen (mwaka 225-254 BK) pia anaiongelea aya hii na anamtaja Zakaria mwana wa Birakira kwenye Origen to Africanus sura ya 9, uk.389.

S: Kwenye Mat 23:35, je ni haki kuwa Mafarisayo waadhibiwe kwa ajili ya dhambi za baba zao, kwani Ezekieli 18 na Kum 24:16 zinasema watu hawatauchukua hatia ya dhambi za baba zao?
J: Watu hawachukui hatia ya dhambi zilizofanya na baba zao. Hata hivyo, kama a) hawazikani dhambi za baba zao, na b) wao nao wanafanya dhambi hizo hizo, basi wataadhibiwa kwa sababu ya hatia yao wao wenyewe kwa sababu wamefanya dhambi hizo kama baba zao.

S: Kwenye Mat 23:37-40, kwa kuwa Yesu alitaka kuikusanya Yerusalemu, kwa nini haikutokea hivyo, kwani Mungu [kama inavyodaiwa] ni Mwenye enzi yote, Mwenye kujua vyote, na Mwenye upendo tu?
J: Mungu si mwenye upendo tu. Kuwa kwake Mungu wa upendo hakumaanishi kuwa Mungu si kitu kingine chochote isipokuwa upendo, au kuwa Mungu ni upendo tu, hakumaanishi kitu chochote zaidi ya Mungu mwenye hasira kunavyomaanisha kuwa Mungu si kitu kingine chochote isipokuwa hasira, au Mungu ni mwenye hasira tu. Ukweli huohuo unahusuka kwa sifa nyingine za Mung kama vile upole au wivu. Mungu ni mwenye upendo zaidi ulimwenguni, lakini upendo wa Mungu haumwondolei sifa zake nyingine.
Mungu alichagua kutuumba na utashi, na walipomkataa Kristo, na kustahili matokeo yake ya milele, Mungu alichagua kutokuwalazimisha kumkubali Kristo, lakini kubaki na uamuzi wao, ingawa ulimfanya Yesu alie machozi.

S: Je Mat 24:3-44 inaonyesha kuwa Yesu alirudi kimwili mwaka 1914, kama Mashahidi wa Yehova wanavyosema?
J: Hapana. Neno la Kigiriki hapa, parousia, linaweza kumaanisha "kuja" au "uwepo", na tafsiri ya Biblia ya Mashahidi wa Yehova, New World Translation, inalichukulia neno hili luwa "uwepo." Kama Kristo angekuwa arudi mwaka 1914, hakuna mtu aliyemwona, na ujio wake haukuathiri kitu chochote, na umeikana Ufu 1:7 ambayo inasema kila jicho litamwona, na Mdo 1:11. Kabla ya kuja kwa Yesu, kwanza kutakuweko madai mengi ya uongo ya kuja Kristo, kulingana na Mat 24:5. Ingawa Mashahidi wa Yehova hawakusema kuwa "wao no Wakristo", madai yote ya watu ambao wamesema kuwa walikuwa Kristo, kama vile Mchungaji Moon, Guru Maharaj Ji, Jim Jones, n.k. yalitolewa baada ya wakati huu.

S: Kwenye Mat 24:19-20, kwa nini jambo hili litakuwa la kutisha hasa kwa wanawake wanaotarajia kujifungua na wale wanyonyeshao?
J: Wale ambao hawajapokea alama ya yule mnyama watakuwa na wakati mgumu. Kwenye nyakati za mwisho, kutakuwa na watu wasioamini, na kabla hawajapokea alama ya huyo mnyama, watakuwa na uchaguzi wa kufanya.

S: Kwenye Mat 24:20, kwa nini tuombe kwa ajili ya jambo lolote la siku zijazo, kwani Mungu tayari anajua mambo yatakayotokea?
J: Angalia maelezo ya 1 Tim 2:1 ili kupata jibu la swali hili.

S: Kwenye Mat 24:20, kuna tofauti gani endapo kukimbia huku kunatokea siku ya sabato?
J: Angalia lini jambo hili litatokea. Kweny nyakati za mwisho, Wayahudi wengi watakuja kwa Kristo, kama Zak 12:10-12 na Warumi 11 zinavyosema. Wayahudi wataendelea kuitii sheria ya Agano la Kale na wataendelea kuishika sabato.

S: Kwenye Mat 24:20, je tunatakiwa kushika sabato (macheo ya jua ya ijumaa hadi ya jumamosi) siku hizi?
J: Wakristo wana majibu mawili.
1. Kuna idadi ndogo ya Wakristo wa kweli, kama vile Wabaptisti wa Kisabato, wanaosema ‘ndiyo.’
2. Jibu la pili ni ‘hapana’, kwa sababu aya hii inaongelea Wayahudi wanaomtafuta Mungu. Kunyakuliwa kwa kanisa kunaweza kuwa tayari kumeishatokea wakati huu.

S: Kwenye Mat 24:22, je Mungu anawezaje kuzipunguza siku za wakati ujao?
J: Jambo hili halimaanishi kuwa siku zitakuwa na chini ya masaa 24, bali ni vipindi vifupi vya muda, au siku chache, kwenye wakati huu wa mateso makali.

S: Kwenye Mat 24:23-27, kwa nini anawaruhusu watu wanaomtafuta Yesu wadanganywe na makristo wa uongo?
J: Wakati mwingine watu wanadai kuwa wanatafuta jibu, lakini wanakubali moja ya majibu yaliyokwisha amuriwa ambayo tayari wameisha ya chagua.
Swali hili lingekuwa gumu kulijibu endapo Mungu angekuwa hajatoa njia yoyote inayowezekana ya kumtofautisha Kristo wa kweli kutoka kwa makristo wa uongo. Mungu ametoa angalau namna saba za kupambanua endapo kundi la kidini ni la uongo kiroho au la.
1. Je, wanakubali na kufundisha mambo ya Mungu anasema kwenye Biblia, au wanapingana nayo? Sasa kama kundi haliko sahihi kwenye kila jambo dogo, jambo hilo halimaanishi kuwa ni la uongo kiroho, kama Warumi 14 na 1 Kor 8:9-11 zinavyothibitisha. Lakini, kama haliko sahihi kwenye mambo ambayo Paulo anayaita ya msingi, kwenye 1 Kor 15:1-5, au kama linakana kuwa Yesu Masihi amekuja katika mwili (1 Yoh 4:1-3), au kama wanamhubiri Yesu mwingine (2 Kor 11:1-15), au wana injili tofauti (Gal 1:6-10), basi jiepushe nao wewe mwenyewe pamoja na familia yako.
2. Jambo linalofanana na hili, je watu hawa hawaikani Biblia hata kukataa kuthibitisha mambo muhimu inayoyafundisha? Kwenye 2 Tim 3:5-7, Biblia inasema tujiepushe na watu wenye mfano wa utauwa lakini wanazikana nguvu zake.
3. Je kukutana kwao na Yesu maishani mwao hakupo au ni kwa ajabu? Je wanakuwa na muda wa maombi na kusoma neno la Mungu? Je wana mambo yoyote waliyoyapitia katika maisha yao ya kidini ambayo hayapatikani kwenye Biblia?
4. Je, wanaishi maisha yao kwa mujibu wa mafundisho ya Biblia? Endapo mtu anadai kuwa Mkristo, lakini anaishi maisha yaliyo kinyume na Mungu kwenye baadhi ya maeneo muhimu, 1 Kor 5:9-13 na 2 Thes 3:10,14 zinasema tusishirikiane na watu hao.
5. Je, kushirikiana nao kidini kunaweza kuwa jambo dhahiri la "kuabudu mashetani" au kufungiwa nira pamoja na wasio amini. Kwenye 1 Kor 10:20 na 2 Kor 6:14-17 tunaonywa dhidi ya jambo hili na kutuamuru tujiepushe nalo.
6. Endapo mtu atadai kuwa yeye ndiye Kristo aliyerudi, je ni kweli kuwa alikuja kutoka mbinguni na mawingu, akawanyakua Wakristo, na kutimiza nabii za kwenye Injili na Ufunuo?
7. Waamini wanaweza pia kumwomba Mungu wa kweli, naye atatusaidia kuona kitu kilicho sahihi. Rafiki yangu mmoja Mkristo aliniambia kuwa mara baada ya kuamini, baadhi ya wamishenari Kimormoni walikuja kuzungumza naye. Alitambua ya kwamba kulingana na ufinyu wake wa ufahamu wa Biblia wa wakati ule, hakujua endapo Wmormoni walikuwa sahihi au walikuwa na makosa. Basi akamwomba Mungu ili amsaidie, kisha akafungua Biblia aisome. Kwenye ukurasa wa kwanza kabisa alioufungua, akasoma Mat 7:15! Inasema, "Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali."

S: Kwenye Mat 24:23-27, kama mtu atamfuata kristo wa uongo au viongozi wengine wa kidini wenye kudanganya watu, na kwa kutokujua kwake hakuweza kutambua kuwa alikuwa kristo au mwalimu wa uongo, kwa nini Mungu aruhusu jambo hili?
J: Kuna majibu mawili ya nyongeza.
Mungu angali anatenda kazi: Anaweza kuamuru mambo yatukie ili Mkristo aweze kukutana na mtu huyo (kristo/mwalimu wa uongo) ili amwonyeshe ukweli. Kisha mtu huyo atapaswa kuchagua endapo ataendelea analipenda hilo dhehebu lao zaidi, au endapo anaupenda ukweli zaidi. Ni vema kujua kuwa mungu yeyote asiyekuwa Mungu wa kweli hastahili kuabudiwa. Nimewahi kusikia kuhusu wamisionari huko Afrika na Asia, ambao wamekuwa wanafuatwa na watu wanaosema kuwa Mungu amesema nao na kuwaambia kwa mmisionari ametoka kwa Mungu. Hatuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya Mungu kuwa anajali au anatenda kazi. Hata hivyo, tunapaswa kuwatia moyo Wakristo kuwa wenye kujali na kutenda.
Mungu ni mwenye haki: Mungu anahukumu watu kwa kuzingatia kiasi ambacho wanajua (Rum 4:15; 5:13), na dhambi haihesabiwi mahali ambapo hakuna sheria. Mtu yeyote ambaye leo hii hajapata nafasi ya kusikia injili anaweza kuwa kwenye hali kama waliyokuwa nayo watu wa mataifa mengine kabla ya kuja kwa Kristo ambao hawakuwahi kusikia injili, au mtoto aliyekufa.

S: Je Mat 24:23-24 inasema kuwa kila mmoja wetu ana "cosmic Christ" ndani yetu, kama baadhi ya wafuasi wa New Age wanavyosema?
J: Si hivyo kabisa. Aya hii inafundisha kuwa kutakuwa na wengi ambao kwa uongo wanadai kuwa Kristo. Yesu ni Kristo, na ingawa tunapaswa kujizatiti kuishi kama Kristo zaidi na zaidi, hakuna kitu chochote kwenye aya hii, au mahali pengine popote kwenye Biblia, kinachosema tujaribu kuuchukua utukufu na heshima ambavyo ni vya Kristo na kudai kwa ni vyetu wenyewe. Wakristo wataishi na Mungu milele katika utukufu, lakini sisi hatutakuwa Mungu, au hata miungu wadogo.

S: Kwenye Mat 24:24, jinsi gani wateule (watu walio kusudiwa kwenda mbinugni) wanaweza kudanganywa?
J: Rahisi sana. Wateule ni watu waliookolewa, na wale ambao bado hawajaokolewa lakini watakwenda kuokolewa. Wakristo wengi waliwahi kuwa Wamormoni, Mashahidi wa Yehova, na washiriki wa madhehebu mengine yenye mafundisho ya uongo.

S: Kwenye Mat 24:27, je kumulika kwa umeme kutoka mashariki hadi magharibi kunahusika kwa jinsi yeyote ile na masihi wa Kibaha’i, aitwaye Ba’haullah, na kutokea kwa simu za upepo (telegrafu) mwaka huo huo (1863)?
J: Hapana. Ingawa Wabaha’i wameniambia kuwa telegrafu ilitimiza unabii huu wa kwenye Injili ya Mathayo, jambo hili si sahihi kwa sababu angalau tano.
1. Telegrafu haiwezi kuwa utimilifu unaofanana na unabii wa ngurumo, umeme, mlipuko wa nuklia, au kitu kingine chochote kinachoonekana. Kumbuka kuwa Mat 24:27 inasema, "Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi . . ."
2. Kristo wa kweli atarudi kwa kuonekana kwenye mawingu (Mdo 1:11, Ufu 1:7), na Ba’haullah hakusimama au kuja toka kwenye mawingu yeyote, isipokuwa usiwe unajua kitu chochote.
3. Pia, Ba’haullah si Kristo aliyerudi, kwa sababu mafundisho yake yanayataja mafundisho ya Kristo kuwa ni uongo. Kristo wa kweli alisema hakuna njia nyingine ya kwenda kwa Baba ila kupitia kwake.
4. Isitoshe, nabii za kurudi kwa Kristo, ikiwa ni pamoja na unyakuo wa kanisa, robo ya watu wote duniani kuuawa kwa upanga, njaa, tauni na matukio mengine yaliyoandikwa kwenye kitabu cha Ufunuo bado hayajatimizwa.
5. Mathayo 24 pia inasema kuwa kabla Kristo wa kweli hajaja tena, kutakuwa na makristo wengi wa uongo.

S: Kwenye Mat 24:28 na Lk 17:37, nini maana ya msemo kuwa ulipo mzoga ndipo wanapokusanyika tai?
J: Kwa maelezo ya wazi zaidi, kama tai wanavyoweza kupata mizoga popote inapokuwepo, kisasi cha Mungu kitawapata watu wanaomkataa na wamekufa kiroho. Inavutia kuwa Yesu alitumia mfano wa ndege, hapa; ndege pia wameelezwa kwenye Ufu 19:17-21.

S: Kwenye Mat 24:29, jua linawezaje kutiwa giza na nyota kuanguka kutoka mawinguni?
J: Ingawa Mungu ana uwezo wa kubadilisha mwanga unaotolewa na jua na kuzifanya nyota zitembee au ziharibiwe, maneno haya yanaweza kuwa yanamaanisha jua kutiwa giza, na nyota kutoonekana tena kwa watu wanaoziangalia hapa duniani. Vitu vingi vinaweza kusababisha jambo hili, kama vile uchafuzi wa mazingira, volkano, kuungua kwa visima vya mafuta, na milipuko ya kinuklia.

S: Kwenye Mat 24:30, je mawingu yanamaanisha vitu vilivyo kinyume cha njia na matakwa ya watu kama Wabaha’i wanavyosema kwenye Baha’u’llah and the New Era, uk.280-281?
J: Hapana. Si tu kuwa kila mtu atamwona Yesu atakaporudi na mawingu, na watu wa dunia wataomboleza kwa ajili yake (Ufu 1:7), bali pia Yesu huyo huyo atarudi na mawingu kwa njia ile ile aliyoondoka kulingana na Mdo 1:9-11.

S: Kwenye Mat 24:31, una maoni gani kuhusu kunyakuliwa kwa kanisa (kama Mkristo mmoja alivyoniuliza swali hili)?
J: Sina shida! Ni kweli, hebu nikupe maoni ya Wakristo walio wengi mwishoni mwa maoni yangu.
Kabla ya ghadhabu (Pre-Wrath): Unyakuo utatokea wakati wa dhiki, lakini muda mfupi tu kabla ya ghadhabu ya Mungu kumwagwa. Kigezo kikubwa chenye kuunga mkono maoni haya ni uamuzi uliofikiwa tokana na ushahidi na kufikiria kimantiki: waamini watiifu mara nyingi hukumbwa na ghadhabu ya wanadamu, lakini huwa hawakumbwi na ghadhabu ya Mungu. Marvin Rosenthal aliandika kitabu chenye kuyatetea maoni haya. Aliwahi kuwa ni mtetezi wa maoni ya ‘Kabla ya dhiki kuu.’
Kabla ya dhiki kuu (Pre-trib): Unyakuo utatokea muda mfupi tu kabla ya dhiki kuu kuanza. Pamoja na kuunga mkon maoni yaliyotangulia, kanisa halijatajwa kwenye kitabu cha Ufunuo baada ya barua kwa makanisa saba. Watetezi wa maoni haya wanaamini kuwa unyakuo utatokea kwenye Ufu 4:1, wakati Mungu anasema kwa Yohana, "Panda hata huku."
Kwa kuwa hakuna mtu atakayeijua saa kwenye Mathayo 24, na kama watu wangejua wakati wa taabu kuanza, basi waamini wangeweza kujua wakati ambapo unyakuo utatokea, endapo maoni ya ‘Baada ya dhiki kuu’ yangekuwa ya kweli.
Msemo unaopendelewa sana na watetezi wa maoni ya ‘Kabla ya dhiki kuu’ ni "tukio linatarajiwa kwenye kalenda ya kinabii ni unyakuo wa kanisa." Kigezo kikubwa cha kuunga mkono maoni haya ni kuwa 1 Thes 5:2 inasema kwamba Bwana atakuja kama vile "mwivi ajavyo usiku." Hata hivyo, kinyume na maoni haya, 2 Thes 2:1-3 inasema kwamba "kukusanyika" hakutatokea hadi ukengeufu na mtu wa kuasi atakapofunuliwa. Hivyo matukio mawili yanayotarajiwa kwenye kalenda ya kinabii ni ukengeufu na kufunuliwa kwa mtu wa kuasi, SIYO unyakuo. (Bila shaka, mtetezi wa maoni ya ‘Kabla ya dhiki kuu’ anaweza kubishia akisema kunyakuliwa kunaweza kuwa mara tu baada ya mambo haya kutokea, na dhiki kuu isianza mpaka hapo.)
Kati ya dhiki kuu yanaamini unyakuo huenda ukatokea muda mfupi kidogo kabla ya maoni ya ‘Kabla dihiki kuu’ yakitumia vigezo hivyo hivyo kuunga mkono hoja yake.
Baada ya dhiki kuu yaanaamini unyakuo utatokea mwishoni mwa dhiki kuu. Kigezo chake kikubwa cha kuunga mkono 1 Kor 15:52, ambapo inaonyesha kuwa tutabadilishwa "wakati wa parapanda ya mwisho." Hata hivyo, maoni mengine yanadai kuwa hii ni parapanda ya mwisho kwa waamini kuisikia, si parapanda ya mwisho kupigwa.
Hakuna dhiki kuu: Wapreteristi wengi wanaamini kuwa hakutakuwepo kabisa na dhiki kuu yoyote. Wanafikia uamuzi huo baada ya kutafsiri Mat 24:31 na sehemu kubwa ya kitabu cha Ufunuo kama mfano. Lakini unapaswa kuwa mwangalifu wa namna yeyote kama hii ya kutafsiri ambayo inavifanya vifungu vya Biblia ama visiwe na maana, au inayosema kuwa mtu wa kawaida anaposoma kifungu cha Biblia mara nyingi hupotezwa na vitu anavyovisoma.
Dhiki kuu popote: Mungu anaweza kuufanya unyakuo utokee wakati wowote anaoutaka Yeye, na hasemi wazi kwenye Maandiko muda ambapo jambo hili litaotkea. Mtu anaweza kusema yeye ni "Dhiki kuu popote" endapo itatokea mwishoni.
Mimi ninapendelea maoni ya ‘Kabla ya ghadhabu’, lakini bado ni mtetezi wa maoni ya ‘Dhiki kuu popote.’

S: Kwenye Mat 24:31, 1 Thes 4:16 na 1 Kor 15:52, parapanda ipi itakuwa ya mwisho?
J: 1 Thes 4:16 inasema parapanda ya Mungu, lakini 1 Kor 15:52 inahusisha hii na "parapanda ya mwisho" ya Mungu. Baragumu saba zinapigwa kwenye Ufu 8:6-9, 21; 10:8, 15, lakini kama 1001 Bible Questions Answered, uk.270-271 inavyosema, hakuna haja kuifanya "parapanda ya mwisho" kuwa miongoni mwa parapanda saba, inaweza kuwa parapanda nyingine.

S: Kwenye Mat 24:32, je mti mtini uanwakilisha kitu gani?
J: Huenda huu ni ufananisho wa hukumu, mti mtini usiozaa matunda ukiiwakilisha Israeli, ambayo itakauka.
Huwezi kuangalia kila sehemu ya mfano na kuipa maana tofauti. Maana ya mfano wa mti mtini ni kuwa macho na kuwa tayari kwa ajili ya hali ya baadaye, na Yesu "anatumia desturi ya mti mtini kuchanua na kuzaa matunda kama kionyeshi chanya cha kuangalia hali ya baadaye."

S: Kwenye Mat 24:34, kwa kuwa "kizazi hiki" hakitapita hadi Yesu arudi, jambo hili linawezekanaje? (Mwana harakati za kuboresha ustawi wa watu mwenye mtazamo unaopingana na wa asili Albert Schweitzer alileta pingamizi hili)
J: Wakristo wana majibu matatu tofauti.
a) Neno la Kigiriki la kizazi, genea linaweza kumaanisha aina. Kulingana na Thayer’s Greek Lexicon of the New Testament, (uk.112), genea inamaanisha:
a1) watu wenye asili au familia moja: Josephus Antiquities of the Jews 51.1 (iliyoandikwa karibu mwaka 93-94 BK), tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale kwenye Mwa 31:3, n.k.
a2) wazao wanaofuatana kizazi hadi kizazi: Philo
a3) nyakati: Herodotus 2,132, Heraclitus kwenye Plutarch, Mdo 14:16.
a) Kuna tofauti ya herufi moja tu kati ya neno hili na neno lingine la Kigiriki linalofanana nalo lenye kumaanisha uzao tu, gonea, hivyo neno hili hapa linaweza kuwa limetokana na makosa ya kunakili. Hata hivyo, hati zote za kale za Agano Jipya zilizopo sasa zinatumia neno genea.
c) Neno la Kigiriki la vitu hivi vyote ni, ponta touta, likimaanisha kizazi hiki ndicho kilichoona ishara zinazoendelea kutokea.

S: Je Mat 24:34 inamaanisha kuwa mambo haya yote yatatokea katika kizazi kimoja cha mwama 1914, kama gazeti la Mashahidi wa Yehovah, Watchtower juzuu ya 15 la Feb 1986, uk.5 lilivyosema?
J: Hapana. Mashahidi wa Yehova walisema kuwa Yesu Kristo alirudi kwa jinsi isiyoonekana mwaka 1914, na mambo yaliyoandikwa kwenye Mathayo 24 yangetokea katika kizazi hicho. Hata hivyo, kama dhana ya msingi, kuwa Yesu alirudi mwaka 1914, ina walakini, basi hoja yao ina walakini. Huu ni mfano wa kitu kinachoitwa "isogesis", au kupachika maana unayoitaka kwenye Maandiko, badala ya "exegisis" ambayo ni kutoa kwenye Maandiko kitu ambacho yanasema.

S: Kwenye Mat 24:36 na Mak 13:32, kwa kuwa Mungu anajua vitu vyote, na Yesu ni Mungu, inakuwaje Yesu hakujua siku ya kurudi kwake?
J: Yesu alijifanya kuwa hana utukufu kwa kuchukua upungufu wa kibinadamu wakati alipokuwa hapa duniani kama Flp 2:6-8 na Yoh 17:5 zinavyoonyesha. Hivyo, hata kama maneno haya hayangekuwa kwenye Injili ya Mathayo, itakuwa busara kwa Yesu kutokujua kila kitu wakati akiwa hapa duniani. Hata hivyo, akiwa mbinguni, kama sehemu ya Utatu Mtakatifu, Yesu ni Mwenye kujua vitu vyote.
Hivi ndivyo askofu wa kikristo, Hilary wa Poitiers (mwaka 353-368 BK) alivyoandika: "Hivyo basi, matendo ya Mungu yanazidi ufahamu wa asili yetu ya kibinadamu na haulingani na mchakato wetu wa kimantiki wa kufikiri kwani utendaji wa umilele usiokuwa na kikomo unahitaji ufahamu usio na kikomo wa kupima mambo. Hivyo si hitimisho la fikra bali ukomo wa uwezo wakati Mungu alipofanyika mtu, wakati Yeye asiye kufa alipokufa, Yeye aliye wa Milele alipozikwa. Tena, kwa upande mwingine, haitegemei namna yetu ya kufikiri bali nguvu zisizo na kikomo kuwa amekuja kama Mungu kutoka kwa mtu, kama aliye wa milele kutoka kwa aliyekufa, na kama wa milele kutoka kwa aliyezikwa. Kwa ajili hiyo, tunapewa uhai mpyana Mungu katika Kristo kupitia kifo chake." Trinity 1:14.

S: Kwenye Mat 24:36, je Roho Mtakatifu, kwa wakati ule, alijua muda wa kurudi kwa Yesu au la? (Mkristo mmoja aliuliza swali hili).
J: Kwanza hebu tulielewe swali. Kuna utofauti wa matini kwenye hati za kale kwenye msemo huu, lakini tutachukua matini ya kawaida, isemayo "wala mwana" kuwa sahihi. Yesu, aliyejifanya kuwa hana utukufu (Flp 2:7) hakujua wakati alipokuwa duniani. Aya hii haisemi endapo Yesu na Roho Mtakatifu wanajua kwa sasa. Lakini swali hasa ni, je Roho Mtakatifu alijua wakati Yesu aliposema maneno haya?
Hebu tuangalie mambo yote matatu yanayowezekana.
Ndiyo, Roho Mtakatifu alijua:
Y1: Kwa hiyo: "hakuna ajuaye . . . wala Mwana" inaongelea viumbe wote na Yesu, lakini siyo Roho Mtakatifu, ambaye Yesu alikuwa bado hajafundisha habari zake, na hawakumjua kuwa alikuwa tofauti na Mungu Baba.
Y2: Roho Mtakatifu huchunguza mambo yote, hata mafumbo ya Mungu kama 1 Kor 2:10 inavyosema.
Y3: Mungu kujua kila kitu inamaanisha kila nafsi ya Utatu Mtakatifu, mbinguni, inajua vitu vyote.
Hapana Roho Mtakatifu hakujua:
N1: "Hakuna ajuaye . . . ila Baba peke yake" inamhusisha Roho Mtakatifu pia.
N2: Kwa hiyo, Mungu kujua kila kitu inamaanisha kuwa angalau moja ya nafsi za Utatu Mtakatifu inajua vituu vyote. Maoni yangepaswa kuafiki kuwa inawezekana kwa Mungu Baba kujua kitu fulani na wengine kutokujua mpaka wakati wa baadaye.
N3: Roho Mtakatifu huchunguza vitu vyote, lakini anachunguza na si kujua vitu vyote kwa mara moja. Hakukamilisha uchunguzi wa ukweli kuhusu jambo hili kwa wakati huu.
Hasemi:
D1: Yesu alikuwa anaongelea viumbe, Mungu Baba, na Yeye mwenyewe; Roho Mtakatifu hakuwemo kwenye maongezi haya hapa.
D2: Jambo hili linaweza kuwa ni tofauti ya matini isiyokuwa sahihi.
D3: Kwa hiyo, jibu linaweza kuwa ‘ndiyo’ au ‘hapana.’
Hitimisho: Hakuna mtu atayekuwa anaishi duniani atakayejua wakati wa kurudi kwa Yesu. Mtu yeyote na asiunde mafundisho kuhusu Roho Mtakatifu kwa kutumia kutokutajwa kwake kwenye aya hii moja. Hili baadhi ya mambo tutakayoyaelewa tukifika mbinguni.

S: Kwenye Mat 24:42, kwa nini Yesu alisema, "ni siku ipi atakayokuja Bwana", badala ya "siku ipi nitakayokuja"?
J: Hatujui maneno halisi aliyoyasema Yesu, kwa sababu waandishi wa Injili walifafanua maneno aliyosema Yesu. Mak 13:34-36 inaweka maneno haya kwenye muktadha wa wa mfano mfupi, na kwa ajili hiyo, yatakuwa kwenye nafsi ya tatu. Kwenye Luk 21:36, Yesu alitumia msemo "Mwana wa Adamu", ambao aliutumia mara nyingi kujitaja Yeye mwenyewe, kwenye nafsi ya tatu tena.

S: Kwenye Mt 24:42, kwa kuwa hatujui wakati Yesu atakaporudi, kwa nini tunaangalia dalili za kuja kwake?
J: Kuna sababu mbili za kufanya hivyo.
1. Kwa bahati mbaya, watu wengi wanafikiri kimakosa kuwa wanaweza kuonyesha wakati Yesu atakaporudi.
2. Biblia inaonyesha kuwa tunaweza kuona ishara zitakazo tuwezsha kuyajua "majira" ya kurudi kwa Yesu. Kwa kuona jinsi mambo yasivyoendana ni moja ya njia ya kuwatambua makristo wa uongo. Angalia pia maelezo kwenye Ufu 22:6, 7, 10, 12, 20.

S: Kwenye Mat 24:45-47, je mtumwa mwaminifu na mwenye busara inamaanisha dhehebu la Mashahidi wa Yehovsa kama wao wenyewe wanavyodai?
J: Hapana. Mtumishi mwaminifu na mwenye busara ni Wakristo wote wa kweli, wanaomfuata Kristo kwa utiifu na wanasubiri kurudi kwake. Ni dhahiri msemo huu hauwezi kuwa unamaanisha dhehebu ambalo limetoa nabii nyingi za uongo.

S: Kwenye Mat 24:51, ni kweli kuwa Mungu mwenye upendo "atawakata watu vipande?"
J: Mungu ni mkali zaidi kuliko hata sitiari hii; Anawatupa watu jahanamu. Kwa maelezo zaidi, angalia ukurasa "Ghadhabu ya Mungu" www.BibleQuery.org/Doctrine/WrathOfGod/TheJustWrathOfGod.htm.

S: Kwenye Mat 25:1, kwa kuwa Wakristo wanatakiwa kuwagawia watu vitu walivyo navyo, je wanawali watano wenye busara walikuwa sahihi kutokuwagawia wanawali wapumbavu mafuta yao?
J: Wakristo wanatakiwa kuwagawia watu vitu walivyo navyo, lakini kwenye hali zifuatazo:
1. Vitu ambavyo hatuna uwezo wa kuvitoa, kama vile haki na utakatifu
2. Vitu mbalimbali (vya kimwili) kwa watu wanaokataa kufanya kazi (2 Thes 3:10)
3. Kuwakaribisha au kwenye nyumba zetu waalimu wa uongo wasiokuwa na Mungu
4. Kuwafundisha watu ambao wanaukanyaga ukweli kama nguruwe (Mat 7:6)
Huwezi kufanya kila sehemu ya mfano iwe na maana maalum, lakini katika mfano huu, wanawali wapumbavu waliomba kitu ambacho wale wenye busara hakuweza kuwapa, kwa kuzungumza kiistiari.

S: Kwenye Mat 25:1-13, je wanawali watano wajinga ni Wakristo ambao hawakuwa watiifu na kwa ajili hiyo walikosa kunyakuliwa?
J: Hapana. Waamini wote watashiriki kwenye unyakuo. Sasa tano wapate kuwa watu ambao walidhani wenyewe Wakristo, ingawa.

S: Kwenye Mat 25:24-26, ni kwa jinsi gani Mungu ni "mtu mgumu" ambaye anavuna asipopanda?
J: Mungu analinganishwa na tajiri katika mfano huu. Watu wengine wanaweza kufikiri kuwa Mungu ni mtu ngumu kwa sababu
1. Mungu huwapa watu viwango tofauti vya "talanta"
2. Mungu anatutazamia tuvifanyie kazi vitu vyote alivyotupa, na ufalme wake utapata faida ya kazi yetu tuliyoifanya kwa bidii. (Bila shaka, kitu chochote chema tunachoweza kukifanya, natukifanye kwa sababu Mungu ametuwezesha. Hata hivyo, jambo hili linaweza kupuuzwa na mtu ambaye anauliza kuwa kwa nini anafaida na kazi yetu).
3. Mungu hajisikia kushtakiwa na dhamira yake kwa ajili ya kuchukua baadhi vitu toka waumini, au watu wengine, vitu ambavyo hawvitumii, wanavitumia vibaya, au wanavitumia kibinafsi.
Kama mtu anataka kumwelezea mtu anayefanya mambo haya kuwa "mtu mgumu" kwenye mfano huu, basi Mungu ni kama mtu mgumu.

S: Kwenye Mat 25:26-27 na Luk 19:23, kwenye mfano wa watumwa na mafungu kumi ya fedha, kwa nini mtu aliyekuwa na talanta moja aliambiwa angeweka kwa watoa riba ili apate faida, kwani Waisraeli waliamriwa kutokutozana riba?
J: Kuna mambo matatu katika jibu la swali hili.
1) Huu ulikuwa ni mfano tu, na Yesu hakuwa anatuagiza tuwe ama kama mtumishi mvivu ama bwana wao.
b) Mfano huu haujasema popote endapo bwana au watumishi walikuwa Wayahudi. Palestina ya wakati wa Yesu ilikuwa na watu wengi wa mataifa mengine.
c) Waisraeli hawakuruhusiwa kuwatoza riba watu wao, lakini waliruhusiwa kutoa mkopo wa riba kwa watu wengine.

S: Kwenye Mat 25:28-29, je Mungu ni mwenye haki anapochukua talanta kutoka kwa mtu aliye na moja na kumpa mtu aliye na nyingi?
J: Hakika, Mungu ni mwenye haki hapa. Mungu alianza na kuwaazima watumwa wote talanta. Hata leo, meneja wa uwekezaji atachukua fedha toka kwenye asasi isiyofanya kazi vizuri na kuiweka kwenye asasi zinazofanya kazi vizuri. Wakati mwingine tusahau kuwa Mungu "ametuazima talanta." Si mali zetu za kudumu, na hatuna haki ya kuzitumia jinsi tutakavyo.

S: Kwenye Mat 25:31-46, inaonekana kuwa tofauti pekee ya kondoo na mbuzi ni vitu walivyofanya na vile ambavyo hawakufanya. Je ni kweli?
J: Hapana. Usipuuzie ukweli kuwa kondoo walikuwa kondoo na mbuzi walikuwa mbuzi. Yesu alionyesha mambo "yafananayo na kondoo" ambayo kondoo waliyafanya lakini mbuzi walishindwa kuyafanya, na kuthibitisha kuwa kondoo walikuwa kondoo. Kwenye hukumu hawakugeuka kuwa kondoo na mbuzi, bali walitambuliwa kuwa kondoo na mbuzi.

S: Kwenye Mat 25:31-46, kwa kuwa jambo la msingi [kama inavyodaiwa] lilikuwa ni kuwasaidia watu wengine, je siyo kweli kwamba kila mtu anayewasaidia watu wengine atakwenda mbinguni?
J: Hapana. Haya yalikuwa ni matendo ya huruma yaliyofanywa kwa Yesu kupitia kuwasaidia watu wengine. Kama hayakufanyika kwa Yesu, basi hayakuwa ya Yesu. Kwa mfano, "hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao" kwenye Luk 6:32-34. Kwenye 1 Kor 13:3 Biblia inasema kuwa hata kama tutatoa kila kitu tulichonacho na kuwapa maskini, lakini hatuna upendo, haitatusaidia kitu chochote.

S: Je Mat 25:46 inaonyesha kuwa hakuna mateso ambayo mtu ataweza kuyatambua kwa watenda maovu kama Mashahidi wa Yehova wanavyosema?
J: Sivyo hata kidogo. Mashahidi wa Yehova wanaamini kuwa msemo "adhabu ya milele" unafaa utafsiriwe "kukatwa." Kuna mambo makubwa mawili kwenye jibu la swali hili.
Neno la Kigiriki ni adhabu. Miili yetu inayokufa ni gamba tu, na endapo kuna kitu chochote kitakachotokea kwenye miili yetu baada ya kufa si adhabu. Mashahidi wa Yehova wanaamini kuwa watu waovu wataangamizwa, na hakutakuwa na kitu chochote cha zaidi kwa watu ambo hawatakuwepo.
Tafsiri ya Mashahidi wa Yehova inakwenda kinyume kabisa na mafundisho ya Yesu ya kuishi kwa kujitambua kwa wacha Mungu na waovu kwenye Luk 16:22-28. Watu watakuwa wanalia na kusaga meno yao kwnye Mat 8:12; 22:13; 24:51 na 25:30, kwa hiyo, ni kwa nini wawe na wasiwasi wakati hawapo tena.
Kwa kuwa mnyama na nabii wa uongo watatupwa wakiwa "hai" kwenye ziwa la moto mwanzoni mwa miaka elfu kwenye Ufu 19:20, na kwa vile waliendelea kuwepo, na hata waliachiwa baada ya miaka elfu kwisha, basi angalau baadhi ya viumbe vinaweza kuishi vikiwepo kwenye ziwa la moto. Je, unakubali? Na kama kuna viumbe vilivyohibitika kuishi kwenye ziwa la moto, na na hakuna Maandiko yanayosema hakuna viumbe vinavyoishi kwenye ziwa la moto, basi hakuna ulazima kuwa watu hawaishi tena kwenye ziwa la moto.
Jambo hili pia linaongeza umuhimu wa kuwepo kwa moto usiozimika milele kwenye Mak 9:43-48 na maeneo mengine, ambapo miili ya waovu haitakufa (Luk 12:4-5) pamoja na roho.

S: Tunajua kitu gani kuhusu kibweta kwenye Mat 26:7; Mak 14:3 na Luk 7:37?
J: Kwenye nyakati za kale, madini tofauti yaliitwa kibweta.
Kibweta chenyewe ni laini (ugumu = 2) na kinaweza kukwanguliwa na ukucha wa kidole gumba. Kinafaa kuchongea, na ni aina ya jasi. Kina rangi nyepesi lakini kinaweza kuwa na madoadoa ya rangi mbalimbali. Mara nyingi huwa kinaundwa kwenye mapango.
Marumaru nayo pia iliitwa kibweta. Ni ngumu kidogo kuichonga (ugumu = 3) ina madini ya Kalisi (chokaa) au aragonite. Ni chokaa iliyo gandishwa upya.

S: Kwenye Mat 26:7-11, wakati mwanamke wa Bethania alipomwaga manukato kichwani pa Yesu, je Yesu alijifikiria mwenyewe? (Muslam Ahmad Deedat aliuliza hivi)
J: Kabla ya kujibu swali la Deedat, hebu na tulifanye swali kuwa gumu zaidi. Yesu si kwamba alisifia mambo aliyofanya mwanamke huyu hapa, bali pia alikubali kaubudiwa kama Mungu afanyavyo kwa malaika na watu mbinguni (Ebr 1:6, Ufu 5:12). Yesu pia alikubali kuabudiwa na watu kama Mungu (Mat 21:15-16; 28:9, Yoh 9:38).
Unaweza kushangaa kusikia kuwa tunakubaliana na Deedat juu ya jambo hili moja. Tunaweza kuona kuwa mtazamo Deedat kuhusu umuhimu wa Yesu na mtazamo wa Yesu kuhusu umuhimu wake ni tofauti sana. Kwa kukubali kibweta ghali cha manukato kichwani pake, ambacho ni kitendo cha kuabudu, na kukubali kuabudiwa, wakati Wayahudi wote walijua kuwa Mungu ndiye anayestahili kuabudiwa, ingekuwa ni kwenda mbali mno ISIPOKUWA YESU ALIKUWA MUNGU.

S: Kwenye Mat 26:11, je Yesu ilikuwa asiwe pamoja nao siku zote, au atakuwa nao siku zote hata mwisho wa dahari kama Mat Mt 28:20 inavyosema?
J: Yote ni sahihi. Wasingekuwa na uwepo wa Yesu kimwili pamoja nao, hivyo hii ni sababu ilifaa kuwa mwanamke ampake Yesu mafuta wakati alipokuwa pamoja nao kimwili. Lakini Yesu atakuwa pamoja nao kiroho hata baada ya kupaa mbinguni.

S: Kwenye Mat 26:27; Mak 14:23; Luk 22:17, 22 na 1 Kor 11:25, je ni lazima tutumie kikombe kimoja cha ushirika mtakatifu?
J: Wote wamejiegesha (si kuketi) kwenye meza moja, kwenye kundi la watu kumi na mbili pamoja na Yesu, wakiwa na msaliti kati yao. Kama tusivyohitaji kufanya mambo haya leo, hatuna haja ya kutumia kikombe kimoja.
Ninamfahamu mchungaji mmoja, anayefikiri watu wote wanatakiwa kutumia kikombe hicho hcho kwenye ushirika mtakatifu. Hata hivyo, inafaa kutofautisha desturi tunayotakiwa kuifuata, na mambo yasiyo muhimu yanayofanyika wakati huo, kama watu wote kujiegesha kwenye meza moja.

S: Kwenye Mat 26:28 na Mak 14:24, je neno agano linatakiwa litanguliwe na kisifa "jipya"?
J: Huenda sivyo.
Kwenye Mat 26:28
Neno "Jipya" lipo kwenye hati za kale Alexandrinus (karibu mwaka 450 BK), Ephraemi Rescriptus (karne ya 5 BK), Bezae Cantabrigiensis, Freer Gospels, Sahidic Coptic (karne ya 3/4), Bohairic Coptic (karne ya 3/4 BK), Lekshenari ya Kibezantini, familia ya f1, familia ya f13, Kiarmenia, Kiethiopic, n.k.
Neno ‘jipya" halipo kwenye hati za kale p37 (katikati ya karne ya 3 BK), Sinaiticus (mwaka 340-350 BK), Vaticanus (mwaka 325-350 BK), n.k.
Kwenye Mak 14:24
Neno "jipya" lipo kwenye hati za kale Alexandrinus, Sahidic Coptic, Diatessaron, Lekshenari ya Kibezantini, familia ya f1, familia ya f13, Kiarmenia, Kiethiopic, n.k.
Neno "jipya" halimi kwenye hati za kala Sinaiticus, Vaticanus, Ephraemi Rescriptus, Bezae Cantabrigiensis, Freer Gospels, Bohairic Coptic, n.k.
Kwa ukumla hati hizi mbili za kale ni zinavutia katika kuonyesha mielekeo miwili ya uwiano baina ya matini.
1. Hati za kale za aina ya Alexandria, ikiwa ni pamoja na Sinaiticus, Vaticanus, Coptic, n.k., kwa ujumla ni fupi kuliko tofauti za matini za Kibezantini.
2. Hakuna uwiano mkubwa wenye kuonyesha mielekeo ya kithiolojia. Kwa mfano, Bezae Cantabrigiensis, Freer Gospels, Ephraemi Rescriptus na Bohairic Coptic haziwiani na tofauti hizi za matini, wakatinyngine zinawiana.

S: Kwenye Mat 26:39, 42, kwa kuwa Yesu ni Mungu na ana mawazo ya Mungu, aliwezaje kuomba "Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe?"
J: Flp 2:6-7 inaonyesha kuwa Yesu alihiari kujifanya kuwa hana utukufu kwa kuchukua asili ya kibinadamu iliyo na mipaka/kikomo wakati alipokuja hapa duniani. Kwa mfano, Yesu alikuwa anajisikia kuchoka (Yohana 4:6), na Yesu alijifunza kutii (Ebr 5:8), ambao huenda hakuwa na haja ya kuujua mbinguni. Pia duniani Yesu hakujua kila kitu, kwani hakujua siku wala saa ya kurudi kwake kwenye Mat 24:36 na Mak 13:32.
Hapa Yesu hasemi kuwa anaijua njia nyingine. Bali anaona kuwa safari iliyo mbele yake inakwenda kuwa na maumivu makali sana, na kwamba anamuomba Mungu Baba endapo anaweza kuwa na njia nyingine yeyote tofauti.
Swali hili liliwahi kujibiwa mwaka 246-265 BK, wakati Dionysius, askofu wa Alexandria alipotoa jibu hili hili kimsingi kwenye kipande cha hati ya kale Exegetical 3 kwenye The Ante-Nicene Fathers juzuu ya 6, uk.108.

S: Kwenye Mat 26:52, je Yesu anapinga vita vya aina yeyote ile na adhabu ya kifo (kunyonga)?
J: Kwanza, jambo ambalo si jibu la swali hili, na kisha jibu.
Jambo ambalo siyo jibu: Wakati Yesu atakaporudi alisema kuwa atawachinja wale wote waliompinga kwenye Mat 24:5-7, 31; Mak 13:7-8 na Ufu 19:15, 17-21. Hata hivyo, jambo hili halisemi kitu chochote kuhusu swali, kwa sababu kitu ambacho Mungu anafanya na ambacho ametuamuru kukitii si lazima vifanane.
Jibu: Hapana kwa sababu nne.
1) Yesu hakuweza kuwa anamaanisha kuwa waamini wasichukue panga hata mara moja; vinginevyo kwa nini masaa machache tu yaliyokuwa yametangulia Yesu alisema kuwa wale ambao hawana panga wanapaswa kwenda kununua kwenye Luk 22:36-38? Isitoshe, baada ya mitume kusema kuwa walikuwa na mapanga mawili, Yesu hakuwaambia waachane nayo, bali alisema, lakini alisema "basi."
2) Yesu alikuwa anamwambia Petro hapa, mara tu baada ya (Petro) kumpiga mtumwa wa kuhani mkuu, kuwa asimkaate mtu mwingine yeyote, kwa upanga wake.
3) Yesu alisema watu ambao "wanaishi kwa upanga", si watu wote walio na mapanga. Jambo hili linaweza kumaanisha watu wote wanaoendesha maisha yao kwa kuua watu, na wale wanaotafuta kuua watu kama ufumbuzi wa matatizo yao.
4) Sehemu ya pili ya aya ni maelezo, si amri.
Aya nyingine zenye kuonyesha kuwa mapanga HAYANA SHIDA ni Rum 13:1-4, Luk 14:31; 19:27; 20:14-16, Mdo 25:11; 1 Kor 9:7. Wakati askari walimuuliza Yohana Mbatizaji kuwa wafanye nini kwenye Luk 3:14, Yohana alikuwa na nafasi nzuri kabisa ya kuwaambia kuachana na jeshi, lakini Yohana hakufanya hivyo. Kadhalika kwenye Matendo 10, akida Kornelio alikuwa mcha Mungu. Kutekeleza hukumu ya kifo hakukuwa kumeruhusiwa tu bali pia kuamuriwa katika Agano la Kale kwenye Hes 35:31, 33 na kabla ya sheria ya Musa kwenye Mwa 9:4.
Aya nyingine zenye kusema au kuashiria kuwa hatupaswi kuishi kwa upanga ni: 2 Kor 10:4-5, Mat 5:25; Yoh 18:36; na Rum 12:17.
Wakati Yesu kwenye Luk 22:36 na Agano Jipya kwa ujumla zinazungumzia matumizi ya kujihami ya upanga, na matumizi ya upanga ya dola kwenye Rum 13:1-4, kamwe haziungi mkono matumizi yanayovuka mpaka ya upanga, au kanisa kutumia upanga. Hakuna Mkristo wa awali aliyetetea matumizi ya upanga na kanisa. Kihistoria, mafundisho haya yasiyo lingana na Biblia yalifundishwa kwa mara ya kwanza mwaka 386 BK, na Augustine wa Hippo.

S: Kwenye Mat 26:64, Yesu aliwezaje kusema mbele ya baraza la Wayahudi, kwani Isa 53:7 inasema Masihi asingefungua mdomo wake?
J: Maneno haya hayamaanishi kuwa Yesu angezaliwa na kuishi maisha yake yote bila kuzungumza. Badala yake, Isaya 53 inafafanua maneno haya kwa kusema "kama vile kondoo anyamazavyo mbele yao wakatao manyoya yake." Yesu alisema siku hiyo, lakini wakati washtaki wake walipozungumza dhidi yake mbele ya Pontio Pilato, Pilato alishangaa na kushtushwa kuona kuwa Yesu hasemi wakati huo wala hajibu hata dai moja, kama Mat 27:17 na Mak 15:4-5 zinavyosema.

S: Kwenye Mat 26:69-75, je Petro, mwanafunzi wa Yesu, aliwezaje kuogopa hata kuongopa?
J: Petro alifanya dhambi hapa, kama yeye mwenyewe alivyotambua kwa uchungu kwenye Mat 26:75, Mao 14:72 na Luk 22:62. Petro alimtumaini Yesu, na ingawa Yesu aliwaonya, mitume wakakimbia tokana na uoga wakati Yesu alipokamatwa. Yesu alimsamehe Petro kibayana kabisa kwa kumkana mara tatu kwenye Yoh 21:15-19.

S: Kwenye Mat 26:73 na Mak 14:70, je lafudhi ya Kigalilaya ilikuwa na sifa gani?
J: Ingawa hatujui kwa uhakika, Wagiriki wengi na Wayahudi waliokuwa wanazungumza Kigiriki waliishi Galilaya, karibu na Dekapoli, na labda ilikuwa na sifa zilizochukuliwa kutoka kwenye lugha ya Kigiriki. Mbali ya matamshi ya maneno, huenda pia ilihusisha nahau na uchaguzi wa maneno.

S: Kwenye Mat 26:74 na Mak 14:71, kwa nini Petro alilaani hapa?
J: Ingawa Maandiko hayasemi, inawezekana ilikuwa kwa sababu mbili.
Uoga: Petro anaweza kuwa alikuwa na hofu.
Kutaka kuwavutia watu: Inawezekana kuwa alijaribu "kuwathibitishia" Wayahudi kuwa hakuwa mwanafunzi wa Yesu.
Vyovyote ilivyokuwa, kulaani kwa Petro, kama kulivyokuwa kumkana kwake Yesu, si mfano wa sisi leo kuufuata. Hatutakiwi kutumia lugha chafu kulingana na Efe 5:4, na tutahukumiwa kwa kila neno lisilokuwa na maana kwa mujibu wa Mat 12:36.

S: Kwenye Mat 27:5, je Yuda alijinyonga, au mwili wake ulipasuka na matumbo yake yalitoka kama Mdo 1:18-19 inavyosema?
J: Mdo 1:18-19 inasema Yuda aliaanguka kwa kasi kondeni, maneno ambayo yanaashiria kuanguka kutoka urefu wa kiasi fulani. Kuzitazama aya hizi pamoja kunatoa mambo mawili yanayowezekana. Katika mandhari hizi zote mbili, Yuda alijinyonga, yaelekea zaidi kwenye mti, ambao huenda ulikwa unaning’inia kwenye mteremko wa ghafla.
Kujinyonga hakukufanikiwa: Wakati Yuda alipokuwa bado hai, kamba ilikatika, na akaanguka kwa kasi kondeni, na mwili wake ukapasuka.
Kijinyonga kulifanikiwa, na Yuda alikufa kutokana na kunyongwa. Hata hivyo, kama hakuna mtu aliyekwenda kumshusha, mwili wake ungeanguka chinu mara, kwa njia moja au nyingine.
Kwa namna yeyote ile, kulikuwa na kamba iliyokatika iliyokuwa inaning’inia, na mwili uliopasuka.

S: Kwenye Mat 27:7 na Mdo 1:18, je ni makuhani au Yuda aliyenunua shamba?
J: Yuda alikuwa amekwisha kufa, hivyo makuhani walifanya kazi hii kama mawakala wa Yudawakitumia vipande "vyake" 30 vya fedha. Katika njia ya kutisha na kufedhehesha, Yuda mwenyewe alichukua milki ya shamba. Kwenye Mat 27:6, makuhani hawakutaka vipande 30 vya fedha ya damu kurudi kwenye hazina ya Hekalu.

S: Kwenye Mat 27:9-10, je inakuwaje maneno haya kuwa utimilifu wa Yeremia, kwani Yeremia alisema sehemu yake tu, na zakaria alisema sehemu yake?
J: Wakristo wana majibu matano.
Makosa ya kunakili, hakuna nabii aliyesemwa bayana – Augustine Hippo alisema kuwa hati nyingi za kale hazina jina la nabii, ingawa alifikiri kuwa hati nzuri zaidi zilikuwa na jina "Zakaria" (Augustine’s Harmony of the Gospels kitabu cha 3 sura ya 7.30-31, uk.191-192.
Makosa ya kunakili ya jina Zakaria – hati chache za kale za Kigiriki zinasema Zakaria badala ya Yeremia.
Makosa ya kutafsiri: Papias, mwanafunzi wa Mtume Yohana, aliandika kuwa Mathayo aliandika Injili yake kwa mara ya kwanza Kiebrania. Kama jambo hili ni la kweli, na Injili hiyo ilitafsiriwa kuwa Kigiriki, undani huu unaweza kuwa umebadilishwa baadaye.
Unabii usiotambuliwa wa Yeremia. Zak 1:4 yenyewe itself quotes Jeremiah 18:11. inanukuu Yer 18:11. Zak 7:7 inamtaja yeye (nabii Zakaria) kuwa anasema maneno kutoka kwa manabii wa zamani. Difficulties in the Bible, uk.139 inasema jambo hili.
Mnyororo wa shuhuda: Moja mambo desturi ya Midrashi ilikuwa ni kunukuu nabii tofauti na kuzihusiana pamoja kwenye kitu tunachokiita "Mnyororo shuhuda" (testimonia chain).Marko 1:1 ni inawe kuwa ni mnyororo wa shuhuda. Kwa mfano, ikiwa kazi ina waandishi wawili, na mwandishi wa pili amedokezwa kwa ufupi tu, ni kawaida kumtaja mwandishi wa kwanza tu. Mnyororo wa shuhuda (pia unaitwa ‘catenas’, yaani mlolongo au mnyororo uliounganika) ulitumika sana, si tu kwenye Biblia bali pia kwenye kazi za kikristo za awali mno. Ni kawaida kumtaja mwandishi maarufu zaidi tu, na tunapaswa kuuangalia uandishi wa kale na desturi zao, siyo zetu.

S: Kwenye Mat 27:11 na Mak 15:2, wakati Yesu aliposema "Wewe wasema", je alikuwa anathibitisha kuwa alikuwa mfalme wa Wayahudi?
J: Ndiyo. Msemo unaweza kutafsiriwa pia kama "Ndivyo kama unavyosema."

S: Kwenye Mat 27:15 na Mak 15:6, kwa nini Pilato alimfungua mfungwa mmoja wakati wa sikukuu?
J: Inavyoonekana hii ilikuwa desturi yake binafsi. Inaonekana, alidhani kuwa Wayahudi watamwon kuwa mwenye haki zaidi au utu endapo atafanya hivyo. Ni wazi mawazo yake ya haki na rehema yalitofautiana na yetu siku hizi, na Biblia haiafikiani na mawazo yake.

S: Kwenye Mat 27:19, ni vitu gani zaidi tunavyojua kuhusu mke wa Pilato?
J: Biblia haisemi kitu chochote kingine. Mapokeo ya kanisa yanasema jina lake lilikuwa Claudia Procula. Baadaye alikuja kuwa Mkristo siri, na kanisa la Greek Orthodox linamchukulia kuwa mtakatifu.

S: Kwenye Mat 27:22; Mak 15:14; Luk 23:23 na Yoh 19:14, je Yesu alikufa kifo cha polepole msalabani, au je angeweza kufa kwa maumivu madogo zaidi kwa upanga au ugonjwa? (Mke wangu aliuliza hivi)
J: Maandiko yanasema tu kiu kilichotokea, na si vitu vyote vilivyokuwa na uwezekano wa kutokea. Shetani alipowaongoza watu kumuua Yesu, inaonekana shetani alimfanya Yesu auawe kwa kifo kichungu zaidi kilichojulikana na watu wakati ule. Yesu alipata adhabu mbaya sana, ili atuletee zawadi nzuri zaidi.

S: Kwenye Mat 27:25, kwa nini Wayahudi walitaka dsmu ya Yesu iwe juu yao na watoto wao?
J: Kuna mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili.
1. Pilato alionekana kusita sana kuchukua dhamana, na umati wa watu unaweza kuwa ulifikiri kwamba Pilato hataweza kutoa hukumu ya kifo dhidi ya Yesu kama wao wenyewe hawatakuwa wameonyesha kuwa tayari kuchukua dhamana.
2. Pia, ingawa mke wa Pilato alimwoonya asihusike na kifo cha Yesu, Pilato alijieonyesha mwenyewe kuwa na hamu ya kumwaga damu kwenye matukio mengine nje ya Biblia. Kwa vyovyote vile, Pilato alitaka umati wa watu useme kuwa unachukua dhamana, kwa namna hiyo kumwepusha kuwa peke yake mwenye dhamana ya kumuua Yesu. Pilato anaweza kuwa aliuchokoza umati ili ajikinge, kwa njia hiyo, maneno ya makutano yahalalishe uamuzi wake endapo Wayahudi au Warumi wangehoji uamuzi baadaye.
3. Wazazi hawawezi kuchagua endapo wataweka hatia yao binafsi kwa watoto au vizazi vyao vitakavyokuja. Kwa bahati mbaya zaidi, Hitler na Wanazi wengine waliwaita Wayahudi wa wakati wao "Wauaji wa Kristo", na walitumia usemi huo kujaribu kuhalalisha uhalifu wao wa kutisha. Hitler mwenyewe aliamrisha kupotea kwa mapadri wengi wa Kikatoliki na Wakristo wengine. Bila shaka Warumi walikuwa Wataliano, na Hitler mwenyewe alikuwa rafiki wa Italia. Ndiyo, dhambi za Warumi na Wayahudi zilimpeleka Yesu juu ya msalaba, lakini dhambi zetu sisi sote ndizo hasa zilizompleleka Yesu juu ya msalaba.
4. Mwishoni wa yote, watu ambao wamefunikwa na damu ya Yesu, dhambi zao zimeoshwa lakini hivi sivyo uamti ulivyomaanisha hapa.

S: Kwenye Mat 27:28-29, je vazi la Yesu liikuwa na rangi nyekundu, au ya zambarau kama kwenye Yoh 19:2-3?
J: Kuna majibu mawili tofauti, na yote yanaweza kuwa kweli.
Nyekundu ya zambarau: Kwenye kiingereza rangi nyekundu ya zambarau inaweza kuchukuliwa kuwa aina ya rangi ya zambarau au nyekundu. Kwenye Kigiriki cha kale, hakuna uhakika juu ya wigo halisi wa spektra ya mwanga wa kila rangi. Kiebrania/ Kiaramu kilipotafsiriwa kuwa Kigiriki, kama Papias alivyoonyesha kwa njia ya Mathayo, kuna uhakika kidogo zaidi.
Rangi mchanganyiko: Ingekuwa ajabu sana endapo joho ghali la mfalme lilikuwa na rangi moja tu. Michoro ya watu ya kale yenye rangi ya Misri inaonyesha rangi nyingi. Mavazi yenye mchanganyiko yalikuwa yanapatikana kwa watu wa kawaida angalau kuanzia wakati wa Yusufu, miaka 1900 miaka kabla ya Yesu.
Kwa ujumla, ingawa jibu hili haliko bayana kabisa, hatuna haja ya kuwa mtazamo usiokuwa wa kihalisia kuona kuwa jambo olotee kati ya hayi mawili yanawezekana.

S: Kwenye Mat 27:32 na Mak 15:21, kwa nini Simoni Mkirene alibeba msalaba wa Yesu?
J: Yesu alikuwa dhaifu mno kuweza kubebe, na Warumi hawakutaka kuubeba. Warumi hawakupenda kujionyesha kuwa walikuwa wanatenda haki hapa.

S: Kwenye Mat 27:32, je Simoni Mkirene aliyeubeba msalaba wa Yesu ni yule yule Simoni mwenye ukoma kwenye Mat 26:6?
J: Jambo hili linawezekana, lakini laelekea kutokuwa hivyo kabisa hapa. Simoni lilikuwa ni jina la watu wengi tu.

S: Kwenye Mat 27:34, 48 na Mak 15:36, kwa nini mtu mmoja aliweka siki kwenye sifongo na kumpa Yesu?
J: Yesu alisema alikuwa na kiu. Mapokeo yanasema kuwa wanawake wa Yerusalemu waliweka nyongo, dawa ya kutia usingizi yenye kuondoa maumivu, kwenye siki.

S: Kwenye Mat 27:46-47 na Mak 15:36, kwa nini mtu mmoja alisema kuwa Yesu alikuwa anamwita Eliya?
J: Watu kwenye umati ule walikuwa wanazungumza Kilatini, Kigiriki, Kiaramu/Kiebrania, na pengine lugha nyingine chache. Yesu aliposema "Eli, Eli", baadhi yao walidhani alikuwa anasema "Eliya." Kumbuka Kiebrania na Kilatini cha Rumi havikuwa na sauti "j."

S: Katika Mat 27:46 na Mak 15:34, je, yaonesha kuwa Yesu si Mungu, kama kiongozi wa kidini Mch. Moon afundishavyo?
J: Na. Kwanza hivi ndivyo Masihi potofu Mch. Moon alivyosema, na kisha kanusho lake. Kanuni ya Kimungu (toleo la tano 1977) uk. 210-212 "…Yesu, kama mwanadamu aliyetimiza kusudi la uumbaji, yeye ni mwili mmoja na Mungu….Hata hivyo kwa namna yoyote hawezi kuwa Mungu mwenyewe…Yesu, akiwa mwili mmoja na Mungu, anaweza kuitwa Mungu wa pili (sura ya Mungu), lakini kwa vyovyote hawezi kuwa Mungu mwenyewe…Yesu alikuwa mwanadamu aliyekamilisha kusudi la uumbaji, na hii haimanishi kuwa alikuwa Mwuumbaji yeye mwenyewe . …Zaidi ya hayo, tunapoona kuwa Yesu alisema msalabani, "Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?" hapa huwa bayana kuwa Yesu si Mungu mwenyewe. Hata hivyo, Yesu ni Mungu kulingana na Waebrania 1:8, 10 na Tito 2:13, ana utimilifu wote wa kiungu katika Wakolosai 1:19. Mistari mingine inayoonesha kuwa Yesu ni Mungu ni Warumi 9:5, Yohana 5:23, na 1 Yohana 5:20. Mwanafunzi wake Tomaso alimwita Yesu "Mungu wangu" katika Yohana 20:28. Yohana 1:3, 10, 11, 14 na Wakolosai 2:16 inaonesha kuwa Yesu hakuwa eti mwanadamu tu, kwa kuwa vitu vyote vya mbinguni na duniani viliumbwa kupitia kwake na kwa ajili yake Yesu.
Kuchanganyikiwa kunaweza kutokea kwa kuwa jina la Mungu limetumika kwa maana zaidi ya moja katika Biblia. Hakika angalau duniani, Mungu Baba alihudumu kama Mungu wa Yesu, na kama Yesu duniani alijifunza utii (Waebrania 5:8)

S: Katika Mat 27:51 na Mak 15:38, ni nini maana ya pazia la Hekalu kupasuka vipande viwili?
J: Pazia liligawanyika kati ya mahali hasa patakatifu pa Mungu na sehemu nyingine yote ya hekalu. Mpasuko ulionesha kwisha kwa umuhimu wa matumizi ya hekalu na kanuni za sheria zilizolisimamia hekalu. Mpasuko ulionesha kuwa kwasababu ya sadaka ya Yesu ya ondoleo la dhambi, kizuizi kilivunjwa na tunaweza kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na Mungu

S: Katika Mat 27:51, je, kuna uthibitisho wowote wa ziada kwa ajili ya hekalu kupasuka?
J: Kuna kitu fulani kinachofanana katika b Yoma 39b (uk. 580). Inasema milango ya hekalu ilijifungua yenyewe.

S: Katika Mat 27:51 hivi ni kweli kwamba hakuna uthibitisho kwa ajili ya tetemeko mbali na Matayo?
J: Hapana, hili si sahihi. Aidha watu wasioamini wako sahihi na Matayo aliunda simulizi ikiwa na mantiki yenye kusisimua, ambayo kanisa la kwanza lilirubuniwa kuamini kama ni kweli, ama vinginevyo kulikuwa na tetemeko kweli, makaburi yalifunguka, baadhi ya wafu walifufuka, na kusadikika kuwa walikwenda mbinguni baada ya ufufuo wa Yesu.
Kauli isemayo kwamba hapajawa na mtu mwingine aliyewahi kuyataja haya licha ya Matayo si sahihi. Tuna vyanzo viwili licha ya Biblia visivyo vya Kikristo na vyanzo vinne licha ya Biblia vilivyo vya Kikristo ambavyo hivi vyote vyataja matukio haya.
Phlegon alikuwa mwandishi wa Kiyunani kutoka Karia (Asia Ndogo), aliyeandika muda mfupi baada ya 137 B.K. kwamba katika mwaka wa wanne wa Olympiad ya 202 [33 B.K.]. kwamba "kulikuwa na tukio kubwa la kukamatwa kwa jua" na kwamba "ilikuwa usiku kwenye saa ya sita siku ya tetemeko katika Bithynia, na mambo mengi yalibadilishwa huko Nikea" (imenukuriwa kutoka Kesi ya Kristo uk. 111) Origen Dhidi ya Celsus kitabu cha 2 sura 14 uk. 437, kitabu 2 sura 33 uk. 445, kitabu cha 2 sura 59 uk.455.
Thales (au Thallus) alikuwa mwanahistoria wa Kipalestina aliyetunukiwa na Julius Africanus (andiko 232-245 B.K.). Julius anasema, "Hili giza Thallus, katika kitabu cha tatu cha historia yake, analiita, bila sababu katika mtizamo wangu, ni kukamatwa kwa jua." (imenukuriwa kutoka Waandishi wa kikristo walioandika kabla ya baraza la kwanza la kanisa la awali lililofanyika Nikea mwaka 325 BK juzuu 6 uk. 136.) Muktadha anaoujadili Julius ni jinsi gani tangu wakati wa amri ya kifalme ya Artaxerxes hadi kusulibiwa kwa Kristo, unavyotimiza Danieli 9. (Hata hivyo hatuna uthibitisho wowote kwamba Thales alilitaja tetemeko.
Irenaeus (182-188 B.K.), katika "Vipande vya Uandishi vilivyopotea" sura 28 uk. 573 (katika Waandishi wa Kikristo Walioandika kabla ya Baraza la Kwanza la Kanisa la Awali Lililofanyika Nikea Mwaka 325 B.K.), ametaja kuwa "Yesu aliposhuka kuzimu, roho nyingi zilipaa na walionekana katika miili yao." Na pia aliandika, katika Dhidi ya Mafundisho Potofu, kitabu cha 4 sura 34 uk. 512 asema, "Na mantiki zilizounganishwa na mateso ya Bwana, ambazo zilitabiriwa, hazikutokea katika kesi zingine zozote. Kwa kuwa hapajatokea kwenye kifo cha mtu mwingine yeyote kati ya watu wa zamani za kale kwamba jua lilizama saa sita, au pazia la hekalu kupasuka, au ardhi kutetemeka, au miamba kupasuka, au wafu kufufuka, au mmojawapo kati ya watu hao [wa zamani] kufufuka siku ya tatu, au kupokelewa mbinguni...Kwa hiyo manabii walisema hasha si mtu mwingine yeyote ila Bwana, kwa ajili yake mambo yote haya yalisemwa kabla ya wakati na ishara mbalimbali kutimia." Ignatius (kabla ya 116 B.K.), mwanafunzi wa Yohana, katika Barua Yake kwa Magnesians, sura 9, anawataja wale ambao Yesu aliwafufua.
Clement wa Alexandria katika The Stromata (193-202 B.K.) kitabu cha 6 sura 6 uk.491 asema, "Lakini wale waliokuwa wamekwisha kulala, wafu walioshuka, lakini wakapaa wakiwa hai.’ Injili yasema, ‘kwamba miili mingi ya wale waliokuwa wamelala ilifufuka- bayana ikiwa imebadilishwa kuwa katika hali nzuri zaidi. Basi hilo lilitokea, mlipuko wa kiulimwengu na tafsiri kupitia uchumi wa Mwakozi."
Waandishi wa kwanza aidha "walirubuniwa ama walidanganyika" kwa kufikiri kuwa hili lilitokea, kufuatana na fikria za baadhi ya watu wasioamini. Vile vile kwa miujiza mingine ukiwemo ufufuo, aidha Wakristo wa kwanza walirubuniwa ama walidanganyika kuwa hakika hili lilitokea wakati halikutokea kamwe. Hakuna mashahidi zaidi walioona kwa macho, hivyo tunaamini kile walichosema waandishi wa Injili au hatuamini kabisa. Hili linakwenda kwa Paulo pia, aliyesema katika 1 Wakorintho 15:13-19 kwamba ikiwa ufufuo haukutokea, basi Paulo alisema mahubiri yake yote yalikuwa hayana maana yoyote, angekuwa shahidi batili, na imani yetu ingekuwa batili, na Wakristo wangekuwa watu wa kuhurumiwa kuliko watu wote. Kama mtume Paulo, binafsi sioni jambo hili kuwa labda badala ya hakika. Origen (225-254 B.K.) anataja giza juu ya nchi, na makaburi yalifumuka wazi katika Dhidi ya Celsus kitabu cha 2 sura 33 uk. 445. Dionysius wa Alexandria (246-265 B.K.) anataja tetemeko la ardhi katika Matayo Barua kwa Askofu Basilides Kanuni za kanisa Katoliki (Canon) 1 uk.94.
Kwa kuhitimisha, tuna sababu ya kusimamia maandishi ya watu wachache waliobainiwa hapa ya kuwa watu walifufuka kwasababu
1. Imani yetu katika waandishi wa Injili na taarifa zao juu ya mambo mengine
2. Waandishi wa Kanisa la kwanza walilitaja hili
3. Hili lisingewezekana kwa mtu yeyote ambaye hakumjua mtu aliyekufa kuweza kuthibitisha, kwa hiyo waandishi wa Kiyahudi na Kiroma wasingeyajua haya.
4. Waandishi wa Kiyahudi wasingekuwa na hamasa yoyote kuyataja haya,
5. Tukio la watu waliofufuka lingefunikwa na ufufuo wa Yesu.
Kinusu nakubaliana na wewe ulichosema juu ya tetemeko. Lakini badala ya kusema kuwa waandishi wa Injili walitumia matukio haya ya ajabu kama kielelezo cha umuhimu wa pekee na matokeo ya utendaji kazi wa Mungu, binfasi naamini kuwa Mungu aliyatumia matukio hayo ya ajabu. Kwa kuongezea kwenye Injili usisahau [takwimu za] matetemeko katika Ufunuo au wakati Uzzia alipokufa katika Isaya 6. Pia katika historia ya kanisa, wakati John Chrysostom alipofukuzwa kutoka Constantinople mnamo mwaka 403 B.K., kulikuwa na tetemeko wakati huo. Isingetegemewa kuwa waandishi wa wakati huo walikuwa wakiweka takwimu za matetemeko madogo madogo. Kwa kuwa matetemeko madogo madogo yalikuwa yakitokea katika ukanda ule, nina takwimu kwa ajili ya Ugiriki na Uturuki. Encyclopedia Britannica ina taarifa za Ugiriki na Uturuki kwamba:
Kati ya 1902 na 1946 kulikuwa na matetemeko 58
Kati ya 1947 na 1966 kulikuwa na matetemeko 82
Kati ya 1967 na 1976 kulikuwa na matetemeko 45
Kati ya 1977na 1981 kulikuwa na matetemeko 9
Jambo jingine la nyongeza ni kwamba utafiti wa Arkiolojia kule Qumran unaonesha kulikuwa na tetemeko lenye uharibifu katika mwaka 31 K.K. (kabla ya Kristo), lakini hata hivyo waandishi wa zamani hawakuweka kumbukumbu za tukio hili.
Hitimisho: Yaonekana kuna kuchagua kati ya mambo mawili (hakuna cha kubaki katikati)
1. Hakuna tetemeko: Waandishi wa Injili pengine walikuwa sahihi katika mafundisho yao ya kimaadili, lakini walitoa taarifa za matetemeko ambayo hayakutokea. Hatuwezi kuamini wanachokisema, angalau kuhusiana na matukio halisi ulimwenguni.
2. Tetemeko: Waandishi wa Injili wanaweza kuaminiwa wanachokisema, na walitoa taarifa ya kuhusu matetemeko yaliyotokea.

S: Katika Mat 27:52-53, ingewezekanaje wafu watoke makaburini mwao?
J: Mungu mwenyezi ana uwezo kufanya chochote anachotaka kufanya, ni pamoja na kufufua watu waliokufa wakaishi tena. Kw baadhi ya watu wasioamini hili lingevunja kanuni za asili zinazotegemeza uumbaji wote; naam Mungu ndiye aliyezifanya kanuni hizo za asili.
Malaika mbinguni lazima wanayaangalia maneno ya watu wasioamini sawa na jinsi tunavyoyaangalia maneno ya watu ambao hawakuamini wakati wa enzi za makaka wale akina Wright, waliosema, "mwanadamu hawezi kupaa". Utaalam wa kupaa anga za mbali unafifisha kanuni zinazotawala uwiano wa angani (law of gravity), si zaidi sana kwa Muumba kubatilisha kanuni za uumbaji wake!

S: Katika Mat 27:52-53, wakati watu walipotoka makaburini mwao wakati wa ufufuo wa Yesu, je, hii yaonesha uwezekano wa Maria kukwepuliwa mbinguni akiwa hai kama ambavyo mwandishi mmoja wa Kikatoliki hufundisha?
J: Na. Ludwig Ott alitoa hili, si kama uthibitisho, lakini kama hoja saidizi katika Misingi ya Dogma za Kikatoliki (1960) uk.209. Hii haisimamii wazo kwamba Maria aliinuliwa mbinguni akiwa hai kwa sababu mbili:
a) Haieleweki ikiwa watu waliotoka makaburini walihuishwa katika miili yao (kama Lazaro) au walifufuliwa
b) Maria alikuwa bado hai wakati wa kufa na kuinuka toka makaburini, kwa hiyo hawezi kuwekwa katika kundi hili..

S: Katika Mat 27:65, je, tunajuaje kuwa "kuchukua mlinzi" ina maana ya askari wa Kirumi 4-16, badala ya askari mmoja wa Hekalu?
J: Kwa Wayunani ingeweza kuwa vyovyote vile ni sawa.
Kauli au tamko: umeshapata mlizi tayari
Amri: chukua huyu mlinzi wa Kirumi ninayekupatia. Hizi ndizo tafsiri tatu zenye uwezekano na zinazokubaliana na zinazopingana na hoja
Tayari una mlinzi wako wa hekalu: Kwa mantinki hii ni walinzi wa hekalu waliomkamata Yesu. Kwa kuwa mwili wa mhalifu aliyeteswa ulikuwa mali ya Warumi, ilibidi waombe ruhusa kwa Pilato kuulinda mwili. Pingamizi la hoja hii ni ukweli kuwa muhuri wa makuhani wa Kiyahudi ungekuwa na maana kidogo sana, wakati muhuri wa Ufalme wa Kirumi, uliotengezwa kwa waya mgumu na madini magumu sana, isingekuwa rahisi kuchakachuliwa. Ingemaanisha mauti kwa yeyote ambaye angeuvunja.

Tayari una mlinzi wa Kirumi aliyekabidhiwa kwako: Labda mlinzi wa Kirumi alikuwa amekabidhiwa tayari kwa makuhani
Chukua mlinzi wa Kirumi: Take a Roman guard: kinyume na hoja hii hakuna mfano wowote wa kutumia neno la Kiyunani echein katika maana ya "kuchukua" linaloonekana katika aidha Kiyunani za zamani (Classical) au Kiyunani walichoongea Wayahudi wenye utamaduni wa Kiyunani (Hellenistic Greek) wakati ule.

S: Katika Mat 28:9, je, Yesu alitokea mara ya kwanza kwa Mariam Magdalena, au mara ya kwanza kwa Petro (Kefa) kama Paulo anavyoashiria katika 1 Wakor. 15:5?
J: Mariam Magdalena alikuwa mtu wa kwanza kumwona Yesu, lakini Petro alikuwa mtume wa kwanza kumwona Yesu. Na kwa kweli Paulo hakusema kuwa Petro alikuwa mtu wa kwanza ambaye Yesu alimtokea. Kati ya watu Paulo aliowaorodhesha, Petro alikuwa wa kwanza katika orodha yake kumwona Yesu, akifuatiwa na wanafunzi wengine, kisha watu wengine zaidi ya 500. Kwa upande mmoja, labda Paulo hakutaja wanawake kwa makusudi kwani kwa wakati ule ushuhuda wa wanawake haukuthaminiwa. Kwa upande mwingine, labda wanawake walisahaulika kuwa walikuwa kaburini kabla ya Petro. Hata hivyo, kwa vyovyote hapana mgongano wowote, kulingana na ukweli kwamba Paulo hajakanusha kuwa hakuna mtu yeyote aliyemwona Yesu kabla ya Petro.

S: Katika Mat 28:19, kwa kuwa kuna Mungu mmoja tu, kwa vipi Yesu anaweza kuwa Mungu, na kwa jinsi gani Utatu wa Mungu utakuwa ni kweli?
J: Hapo kunaweza kuwa "uwingi" kwa Mungu mmoja bila kuwapo na miungu mingine tofauti. Hata katika Korani, wakati Mungu anapoongea, neno "sisi" (Nahnu), na neno "Mimi" nalo limetumika.
Mungu hadhibitiwi na mipaka ya kibinadamu, na Mungu anaweza kujidhihirisha Mwenyewe kwetu kwa jinsi anavyotaka.
Kuna utatu katika Maandiko: Matayo 28:19; 1 Petro 1:2; Waefeso 2:18; Ufunuo 4:8; 2 Wakorintho 13:14; Yohana 15:26.
Kuna Mungu mmoja tu asiyegawanyika. Kumbukumbu la Torati 4:35-39; 6:4; Isaya 43: 10-2; 44:6,8; 45:5-6,14,21; 46:9; 1 Timotheo 1:17; 6:15-16.
Nafsi tatu zinazojitegemea: Matayo 3:16-17; Luka 3:21-22; Yohana 1:1; 6:38;14:31;15:26; 16:28; 17:5; Matendo ya Mitume 5:31-32; Marko 10:38-40
Yesu ni Mungu. Yohana 1:3; Wakolosai 1:16-17; Waebrania 1:6-9; Yohana 9:38; 2 Wakorintho 11:3; Yohana 20:28-29; Ufunuo 5:8-9; 22:20
Roho ni Mungu. Warumi 8:9-16; Luka 1:35; 1 Yohana 4:12-16; 1 Wakorintho 3:16 dhidi ya 1 Wakorintho 6:19; Matendo ya Mitume 5:4;
Wako sawa katika asili, utukufu, na heshima. Yohana 5:18; 5:23; Wakolosai 2:9-10; (Isaya 44:6; Ufunuo 1:8 dhidi ya Ufunuo 1:17-18; 22:13)
Wanatofautiana katika utendaji na daraja. 1 Wakorintho 11:3; 1 Wakorintho 15:25-28; Matayo 12:18; Waefeso1:3, 17; Yohana 1:33; 14:16, 26, 28; Warumi 8:26-27.
Pamoja na hayo, Yesu kuwa katika Utatu haina maana kuwa Yesu ni moja ya tatu ya Mungu, chochote zaidi ya urefu wa moja ya tatu ya meza ni moja ya tatu ya meza. Huwezi kumwelezea Mungu kimahesabu, hata ukijaribu Utatu wa Mungu hauwezi kuwa 1 + 1 + 1 = 1 lakini 1 mara 1 mara 1 =1.

S: Katika Mat 28:19, Mat 24:36, na Mat 3:16-17, ni nini maana ya mafundisho kuwa Mungu hagawanyiki na ni Roho au Mungu hujihirisha katika sura tofauti kwa vipindi tofauti (modalism), na kwanini imani na fundisho hili si sahihi?
J: Mafundisho juu Utatu wa Mungu hufundisha kuwa kuna Mungu mmoja asiyegawanyika katika nafsi tatu zinazojitegemea. Mungu asiyegawanyika na ni Roho au anayejidhihirisha katika sura tatu tofauti katika vipindi tofauti (modalism), hufundisha juu ya Mungu mmoja asiyegawanyika na ana nafsi moja. Na hasa kuna aina mbili za mafundisho haya (modalism). Patripassianism ni fundisho linalosema Mungu baba ni mwana ambaye ni Roho. Dynamic modalism fundisho lasema Mungu baba alikuja kuwa mwana, ambaye naye alikuja kuwa Roho. Aina zote mbili za mafundisho haya si sahihi kwa sababu zifuatazo.
1. Yesu alisema "Baba ni mkuu kuliko mimi" katika Yohana 14:28. Wakati Yesu akiwa amevua utukufu wake hapa duniani aliposema hivyo, ukweli unabaki kuwa kama Baba alikuwa mkuu kuliko Yeye, basi kulikuwa na utofauti kati ya Baba na Mwana.
2. Ikiwa mafundisho ya modalism ni kweli, Yesu lazima atakuwa alikuwa mwigizaji kwa kubadili sauti, mwanamazingaombwe, na zaidi ya yote mwongo wakati wa ubatizo wake (Matayo 3:16-17; Marko 1:10-12; Luka 3:21-22). Wakati akiwa duniani, Yesu alikuwa akitumika kwa kumtii Baba (Waebrania 5:16-17). Hili lisingekuwa na maana yoyote ikiwa pasingekuwa na yeyote kwa ambaye Yesu angelimtii.
3. Vile vile, Yesu alifanya kile ambacho Baba alimwamru (Yohana 14:31). Yesu alijifunza kuwa mtii kwa Baba katika Waebrania 5:8.
4. Matayo 24:36 yasema kuwa hakuna ajuaye siku wala saa ambapo Kristo atarudi, wala hata mwana, ila ni Baba pekee yake. Hivyo angalau wakati Yesu akiwa duniani, kulikuwa na tofauti kati ya alichokijua Baba na kile alichokijua Yesu. Wakati baadhi ya nyaraka za maandiko ya Kiyunani hazina "wala mwana" waraka wa andiko lililo bora zaidi na mengi ya maandiko ya Kiyunani yana "wala mwana".
5. Yesu alitumwa na mwingine licha ya Yeye binafsi, kama Yohana 5:36-37; 6:29, 38 ina maana yoyote. Mbingu haikuwa tupu Yesu aliposhuka duniani.
6. Kwa kuwa Baba alitoa kitu kwa Mwana, na akampa Mwana mamlaka katika Yohana 5:22, 26, 27, hii inaonesha Baba na Mwana wako tofauti.
7. Kwanini Yesu aliomba kwa Baba, au kuomba kitu kutoka kwa Baba, katika Yohana 17:5, Yohana 14:16, 26, 28, na sehemu zingine, kama Yesu alikuwa akijiongelea mwenyewe.
Zaidi ya hayo, kwasababu maombi ya Yesu yalitolewa kama alikuwa akiongea na mtu mwingine, Biblia ingekuwa inapotosha kama pasingekuwa na mtu mwingine yeyote ambaye Yesu alikuwa akiongea naye.
8. Ni nani Roho huyo anayeomba kwa niaba yetu katika Warumi 8:26-27?
9. Ikiwa Yesu alikuwa mtumishi, Yesu alikuwa mtumishi wa nani katika Matayo 12:18?
10. Ni nani aliyemtelekeza Yesu pale Kalvari katika Marko 15:34 na Matayo 27:46.
11. Mistari mingine inayoonesha utofauti ni Yohana 1:33; 1 Wakorintho 11:3; 15:25-28; Waefeso 1:3, 17; Waebrania 1:9
Hapa kuna baadhi ya nukuru kutoka kwa Witness Lee, aliyeanzisha kanisa la mtaa. Kanisa hili la mtaa lina vikundi vya wanafunzi viitwavyo "Wakristo katika Eneo la Kanisa." Kwa ujumla makanisa yao yanaitwa "Kanisa katika [jina la mji]" "Hivyo nafsi tatu za Utatu wa Mungu ikawa ni hatua tatu za kupokezana katika mchakato wa uchumi wa Mungu." W. Lee. Uchumi wa Mungu, Kijito Kilichohai 1968 uk.10.
"Tena, Baba, Mwana na Roho si Mungu watatu, bali hatua tatu za Mungu mmoja, kwa ajili yetu kumiliki na kufurahia" W. Lee. Kuhusu Mungu wa Utatu Kijito Kilichohai bila tarehe uk.31
"Katika mbingu ambako mwanadamu hawezi kuona, Mungu Baba, anapoelezwa miongoni mwa wanadamu, ni Mwana; na anapokuja kati ya wanadamu Yeye ni Roho. Mungu Baba alielezwa miongoni mwa wanadamu katika Mwana na Mwana akawa Roho kuja katikati ya wanadamu. Baba yuko ndani ya Mwana, na Mwana akawa Roho—hawa watatu watatu ni Mungu mmoja tu." W. Lee. Kuhusu Mungu wa Utatu Kijito Kilichohai bila tarehe uk. 8-9
Baada ya kifo na ufufuo [Mwana] akawa Roho na kuwavuvia wanafunzi W. Lee. Kuhusu Mungu wa Utatu Kijito Kilichohai bila tarehe uk.8
"...Mwana akawa Roho kwa ajili yetu tunywe kama maji ya uzima…" W. Lee. Kuhusu Mungu wa Utatu Kijito Kilichohai bila tarehe uk.8
"...Tunajua Mwana ni Bwana na kwamba Yeye ni Roho. Kwa hiyo ni lazima tuelewe wazi kuwa Kristo Bwana ni Roho pia." W. Lee. Roho wa Kristo Ajumlimshaye Wote Kijito Kilichohai 1969 uk. 4, 6, 8
"Hivyo, nafsi tatu za Utatu wa Mungu zikawa hatua tatu za kupokezana katika mchakato wa uchumi wa Mungu." W. Lee. Uchumi wa Mungu Kijito Kilichohai uk. 10
Kumbuka kwamba hoja hii imekanushwa na mistari iliyotolewa mwanzoni mwa jibu hili. Angalia pia Wakati Wenye Imani Potofu Wakiuliza uk. 130-131 kwa maelezo zaidi kwanini mafundisho ya modalism si sahihi.

S: Katika Mat 28:19, kwa kuwa modalism si sahihi, na bado Baba na Mwana wako karibu sana, na kwa kiasi gani wako karibu?
J: Japokuwa maandiko hayatoi maelezo mengi, hapa kuna mambo sita tunayoweza kuyasema.
1. Kama Yesu alivyo katika Baba, tu katika Yesu, na Yesu yumo ndani yetu.
Kuna muunganiko katika ya aina za uhusiano hizi mbili: Baba-Yesu, Yesu-nasi, Sisi-Yesu. Yohana 14:20; 17:23; 6:57
Hata hivyo, kuna zaidi juu ya Utatu wa Mungu kuliko uhusiano huu wa kimfano. Matayo 28:19; Yohana 1:1,18; Wafilipi 2:6-7; Wakolosai 1:15
Baba, Yesu, na sisi sote tunashirikiana baadhi ya mambo, kama vile uzima wa milele Yohana 16:13-15
Baba na Yesu "humiliki" vyote bila tofauti Yohana 16:15;17:10. Roho Mtakatifu hudhihirisha hili kwetu Yohana 16:14-5
Hata hivyo, Baba hana mambo mengine tunayoshirikiana na Yesu baada ya kuzaliwa kwake katika hali ya mwanadamu Waebrania 1:6-10; 2:14; 7:3
2. Kama Baba na Yesu ni mmoja, tunapaswa kuwa wamoja
Tunapaswa kuwa wamoja wenyewe kwa wenyewe kwa namna moja ama nyingine ni sawa kama Baba na Yesu Yohana 17:11,21-22
Japokuwa wao ni Mmoja kwa namna moja ama nyingine sisi hatuwezi kuwa mmoja Yohana 5:23
3. Baba huishi ndani ya Yesu
Duniani Baba aliishi ndani ya Yesu Yohana 10:38;14:10-11. Yesu alikuwa amejazwa na Roho Luka 4:1,18
Kama unamjua Yesu kwa hakika, basi unamjua Baba na umeshamwona Baba. Yohana 14:7-9
Japokuwa Baba hakuwa, kimchakato, au kugeuka kuwa Yesu. Waebrania 13:8; 1:9; Yohana 14:10,24,26; 15:1; 16:27-8,32; 17:5
4. Yesu huishi ndani ya Baba
Duniani Yesu alikuwa ndani ya Baba. Yohana 10:38; 14:11
Japokuwa [hawa wawili] ni tofuati; Yesu hakuwa mwigizaji kwa kubadili sauti. Matayo 3:16; John 8:18. Yesu alitelekezwa pale Kalvari Marko 15:34; Matayo 27:46
Hakuna ajaye kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwa Yesu Yohana 14:6; 6:45; Matendo ya Mitume 3:12
Japokuwa kama walivyo karibu duniani, Yesu alikuwa bado aende kwa Baba. Yohana 14:12; Marko 16:19; Yohana 20:11
Yesu anaitwa Baba wa milele, jina linaloashiria kuwa chanzo cha uzima wa milele. Isaya 9:6
Hata hivyo, Yesu hakuja kuwa katika mchakato, au kugeuka kuwa Baba. Waebrania 13:8; Yohana 20:17; 14:10,24,26; 15:1
5. Mungu/Baba/Kristo/Roho yumo ndani yetu
Watu humwona Mungu kupitia kwetu na ndani yetu.
Japokuwa Mungu haishi kikamilifu ndani yetu, si tofauti na nyota zinavyokuwa katika vyombo vya kuchunguzia nyota zake safari angani (telescopes). 1 Timotheo 6:16; Yeremia 23:24; Ufunuo 19:11
Baba/Yesu/Roho pia hukaa hasa/hutengeneza makao yao katika kila mwumini. Yohana 14:17,23; 17:26; Warumi 8:9-11; Wagalatia 3:6; 1 Wakorintho 6:19; 1 Yohana 4:15-16; 2 Timotheo 1:14
Hata hivyo, Mungu/Baba/Kristo/Roho hakuwa sisi, au kubadilika kuwa mwanadamu mwenye dhambi. Yakobo 1:13; Waebrania 4:15: 1 Petro 2:22; 1 Yohana 3:5
Mungu hutenda kazi na hutenda ndani yetu na kupitia kwetu Wafilipi 2:13; mifano:1 Wafilipi 15:10; Warumi 15:18-19
Watu wa Mungu, kanisa, wako pamoja mwili wa Kristo. 1 Wakorintho 6:15; 10:17; 12:27; Waefeso 4:12; Wakolosai 1:24.
Japokuwa, sisi si mwili wa Kristo kibinadamu. Wakolosai 1:22. Mungu hana mipaka kutenda kazi kupitia kwetu. Mwanzo 1; Matendo ya Mitume 9:1-6; Ufunuo
Kusaidia/kutotusaidia ni sawa kama ilivyo kwa Yesu Kristo. Matayo 25:35-45; Yohana 13:20; Matendo ya Mitume 9:4-5; 22:7-8; 26:14-15
Japokuwa, watu wanaweza kumsifu au kumkashifu Mungu moja kwa moja bila kufanya chochote kwa waumini. Warumi 1:18-32; Ufunuo 9:20-21
6. Tunaishi ndani ya Mungu/Baba/Kristo/Roho
Tumo ndani ya Yesu na Baba. 17:21; Wakolosai 2:6,12; 3:3-4; 1 Yohana 4:12,15-16; 5:20.
Ni lazima tubaki ndani ya Yesu Kristo na ndani ya upendo wake. Yohana 15:1-9; 1 Yohana 2:27
Japokuwa, hatuko pamoja na Mungu kikamilifu sasa; bado tunahitaji kwenda na kuwa pamoja na Mungu. 2 Wakorintho 5:8; 1 Wakorintho 13:12; Wafilipi 1:23
Kwasababu Yesu yu hai, tutakuwa hai. Yohana 14:19; Wakolosai 3:4; 1 Wakorintho 15:12-22
Japokuwa, huwa hatubadiliki kuwa, kimchakato, kubadilika kibailojia ama kimfumo, au kubadilika kuwa Mungu au Kristo; bali tunakuwa watauwa na wa kufanana kitabia na Kristo. Isaya 42:8; 43:10; Warumi 8:29; 1 John 3:2; Wafilipi 3:21
Tu viumbe vipya katika Kristo. 2 Wakorintho 5:17. Tuna nia ya fikra ya Kristo. 1 Wakorintho 2:16.
Japokuwa, hatubadiliki kuwa mizuka; bado tunapaswa kuwa na nia ya fikra na hulka zetu. 1 Wakorintho 6:2-6; 11:13; 13:11+14:20; Warumi 14:5-6



S: Katika Mat 28:19, je, mstari huu ulichakachuliwa wakati wa Baraza la Nikea, kwa kuwa Eusebius anaunukuru mara 18 kabla ya Nikea bila kutaja Utatu wa Mungu, na Eusebius anaunukuru tu kwa mfumo wenye kanuni katika Utatu wa Mungu kitheolojia (Trinitarian) baada ya Nikea? Victor Paul Wierwille, mwasisi wa The Way, alidai katika kitabu chake Yesu Kristo si Mungu (1981) uk.19-20.
J: Kutoka katika hali ya utulivu hoja hii ni ya hovyo kwasababu kadhaa zifuatazo. Eusebius wa Kaisaria hasa alikuwa mwanahistoria, na si mwanatheolojia hasa, hata Wierwille anakiri kuwa Eusebius anaunukuru baada Nikea.
Pili, na cha muhimu zaidi, waandishi wengi Wakristo karne nyingi kabla ya Eusebius waliunukuru mstari huu kikamilifu.
Mafundisho ya Mitume (kabla ya 125 B.K.) sura 7 uk.379 yaunukuru kama, "Baada ya kusema kwanza yote haya, batizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, katika maji yaliyo hai. [i.e. maji yanayotiririka]. Lakini kama hamtakuwa na maji yaliyo hai, batizeni katika maji mengine; na kama haitakuwa katika maji baridi, katika maji vuguvugu. Lakini kama hamtafanya hivyo, mwagieni maji mara tatu kichwani katika jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu."
Irenaeus (182-188 B.K.) aliunukuru "Nendeni na kawafundisheni mataifa yote, mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu." (Irenaeus Dhidi ya Mafundisho Potofu kitabu cha 3 sura 17.1 uk.444)
Tertullian (198-220 B.K.) kwa namna fulani analiandika wazo la mstari huu: "Yeye [Yesu] aliwaamru wale kumi na mmoja wengine, wakati wa kuondoka kwake kwenda kwa Baba, ‘kwenda kuyafundisha mataifa yote, ambao walipaswa kubatizwa katika jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu." Juu ya Maelezo Dhidi ya Walimu Potofu, sura 20 uk.252.
Tertullian anausema tofauti kidogo katika Juu ya Ubatizo sura 13 uk.676 "Mungu, Yeye [Yesu] alisema, ‘yafundisheni mataifa, mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana na Roho Mtakatifu."
Hippolytus (222-235/6 B.K.) anaunukuru kama "Nendeni ninyi na yafundisheni mataifa yote, mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu" Dhidi ya Mafundisho Potofu ya Noetus mmoja sura ya 14 uk.228
Andiko la Kitaaluma Dhidi ya Mafundisho ya Novatian (254-256 B.K.) sura 3 uk.658 "Nendeni na hubirini Injili kwa mataifa, mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Hii ina maana kuwa Utatu wa Mungu ule ule uliotenda kazi kwa njia ya mifano mbadala katika siku za Nuhu kupitia njiwa, sasa unatenda kazi katika Kanisa kiroho kupitia wafuasi."
Andiko la Kitaaluma juu ya Kubatizwa Mara ya Pili (c.250-258 B.K.) sura 7 uk.671 "Nendeni, fundisheni mataifa; wabatizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho."
Baraza la Saba la Carthage (258 B.K.) uk.567 Munnulus wa Girba alisema, "… hata hasa hasa katika Utatu wa Mungu wa ubatizo, kama Bwana wetu asemavyo, ‘Nendeni na wabatizeni mataifa, katika jina la Baba, la Mwana, na la Roho."
Baraza la Saba la Carthage (258 B.K.) uk.569 Vincentius wa Thibaris alisema, "Nendeni na wafundisheni mataifa, mkiwabatiza katika jina la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu."
Victorinus wa Pettau (-307 B.K.) anaukuru kama, "Yeye [Yesu] aliwatuma mitume, akisema: Nendeni, wafundisheni mataifa yote, mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu."
Commentary juu ya Siku za Mwisho kutoka sura ya kwanza na. 15 uk.345
Kwa hiyo kwanini basi, Wierwille anajaribu kuligubika jambo hili na kuepusha ukweli kwa uzushi mdogo mdogo kuhusiana na sehemu zipi alizonukuru Eusebius wakati tuna waandishi hawa wote kabla yake waliokuwa wazi zaidi.
Hatimaye, angalia swali kuhusu mambo mengine ambayo Wakristo wa kwanza waliyasema juu ya Utatu wa Mungu

S: Katika Mat 28:19, ni mafundisho gani mengine ya kanisa la kwanza juu ya Utatu wa Mungu?
J: Haya hapa ni baadhi yake.
Kwa Diognetus (imeandikwa c.130 B.K.)
"Kama mfalme anavyomtuma mwanaye, ambaye ni Mfalme pia, kwa hiyo anamtuma; kama Mungu (1) Alimtuma kama kwa watu alimtuma; kama Mwokozi alimtuma,…" sura 7 Nukuru (1) inasema "Mungu" hapa ikihusu mtu aliyetumwa.
Justin Martyr (mnamo 138-165 B.K.)
"kwa kuwa tunapotoa neno fulani, tunalizaa neno; bali si kwa kutenganisha, ili kulipunguza neno [ambalo hubaki lilivyo] ndani yetu, tunapolitoa; na kama vile tunavyoona vile vile kinachotokea kunapotokea moto, ambao haupunguzwi unapokuwa umewaka [kuwasha kitu kingine], lakini hubaki kama ulivyo;…Neno la hekima, ambaye ndiye Mungu mwenyewe aliyezaliwa na Baba kati ya vitu vyote, na Neno, na Hekima, na Nguvu, na Utukufu wa Mzazi, utatoa uthibitisho kwangu…"
Maongezi na Trypho sura 61. Hakika sura zote 57-63 zinajadili uungu wa Yesu.
Theofilo wa Antiokia (168-181/188 B.K.)
"Katika maana ile ile pia siku tatu zilikuwa kabla ya mianga [jua, mwezi, na nyota] ni aina za Utatu (Kiyunani triad), wa Mungu, na Neno lake, na Hekima yake." Kwa Autolycus kitabu cha 2 sura 15 uk.101.
Theofilo askofu wa Antiokia (168-181/188 B.K.)
"Kwa kuwa maandiko ya kimungu pekee yake hutufundisha kuwa Adamu alisema kuwa alikuwa ameisikia sauti. Lakini ni nini zaidi juu ya sauti hii isipokuwa ni Neno la Mungu, na Mwana ni nani pia?" Theofilo kwa Autolycus kitabu cha 2 sura 22 uk.103. Irenaeus (182-188 B.K.)
"Lakini kwamba Yeye [Yesu] yeye mwenyewe katika haki yake mwenyewe, zaidi ya mwanadamu yeyote aliyewahi kusishi, Mungu na Bwana na Mfalme wa milele, na Neno lililofanyika mwili, lililohubiriwa na manabii wote, mitume wote, na kwa Roho mwenyewe, ili lionekane kwa wote waliopokea hata sehemu kidogo ya kweli." (Irenaeus Dhidi ya Mafundisho Potofu, kitabu cha 3 sura 19.2 uk.449).
"Ujue kuwa kila mtu aidha ni tupu au amejaa. Kwa kuwa kama hana Roho Mtakatifu, hana ufahamu wa Mwuumbaji; hajampokea Yesu aliye uhai; hamjui Baba aliye mbinguni;…" (Dhidi ya Mafundisho Potofu 3:16)
"Yeye (akike) [kanisa] pia anaamini hoja hizi [za kanuni za imani] kama vile ana roho moja…Kwa kuwa makanisa yaliyopandwa Ujerumani hayaamini hivyo au kupokezana chochote kilichotofauti wala makanisa yaliyoko Hispania wala yale yaliyomo Gau wala yale yaliyoko Misri wala yale yaliyoko Libya, wala…"
Clement wa Alexandria alinena juu ya "Utatu Mtakatifu" katika The Stromata (193-202 B.K.) kitabu cha 5 sura14 uk.468.
Tertullian (198-220 B.K.)
"Kwa hiyo, Neno ni mara zote limo ndani ya Baba, kama asemavyo, ‘Mimi nimo ndani ya Baba,’ na wakati wote huwa pamoja na Mungu, kufuatana na ilivyoandikwa, ‘Na Neno lilikuwa pamoja na Mungu;’ na halikutengana na Baba kamwe, au tofauti licha ya Baba, kwasababu ‘Mimi na Baba ni mmoja.’" Dhidi ya Praxeas sura 8.
Hippolytus (170-235/6 B.K.) baada ya kunukuru Yohana 1:1
"Ikiwa, basi Neno lilikuwa pamoja na Mungu na lilikuwa Mungu ni nini kinafuata? Mtu anaweza kusema anaongelea Mungu wawili? Hakika sitaongelea juu ya Mungu wawili bali mmoja; wa Nafsi mbili hata hivyo na juu ya uchumi wa tatu (kubadilishwa kinafasi), ikiwa na maana kuwa neema ya Roho Mtakatifu. Kwa hiyo Baba hakika ni mmoja lakini wakiwa Nafsi mbili kwasababu kuna Mwana pia; na tena kuna nafsi ya tatu Roho Mtakatifu. Baba aamru, Neno hutekeleza na Mwana hudhihirisha, kupitia kwake watu humwamini Baba. Mwafaka wa uchumi hurudi nyuma kwa Mungu mmoja; kwa kuwa Mungu ni mmoja. Ni Baba aamruye na Mwana ndiye atiiye na Roho Mtakatifu ndiye atoaye ufahamu; Baba ni juu ya wote, na Mwana ni kupitia wote na Roho Mtakatifu ni katika wote. Na hatuwezi kufikiri vinginevyo juu ya Mungu mmoja, lakini kwa kuamini katika kweli, katika Baba na Mwana na Roho Mtakatifu." Dhidi ya Mafundisho Potofu ya Noetus Mmoja sura 14.
Athanasius (296-373 B.K.)
"Kuungana bila kusababisha kuchanganyikiwa, kubainika bila kutengana. Kutogawanyika bila madaraja." Mahubiri juu ya Luka 10:22
"Kwa kuwa ni msalabani pekee ambapo mtu hufa na mikono yake ikiwa imetandazwa. Ilikuwa jambo sahihi na mwafaka kwa Bwana kubeba jambo hili na kutandaza mikono yake ili kupitia mtu mmoja angewavuta watu wa zamani na wengine kutoka kwa watu wa mataifa na kuwaunganisha wote katika Yeye." Kufanyika Mwili 25:3
Basil wa Cappadocia (329-379 B.K.)
"wakati wote wanapaswa kukiri kuwa Baba ni Mungu, Mwana wa Mungu, na Roho Mtakatifu, kama walivyofundishwa na maandiko ya Mungu,…" Barua ya 7 kwa Wakaisaria (uk. 116)
Hilary (353-368 B.K.)
"Matendo ya Mungu kwa hiyo ni zaidi ya ufahamu wetu wa asili ya kibinadamu na hayaingiliani na mfumo wa fikira zetu zinazotegemea upembuzi wa mambo kwasababu ya utendaji wa milele isiyo na mwisho unaohitaji ufahamu wa kimungu kuyapima mambo mbalimbali. Kwa hiyo siyo hitimisho la upembuzi wa kibinadamu lakini uwezo ulio na kikomo wakati Mungu alifanyika mwanadamu, wakati Kisichokufa kinakufa, wakati Kilicho cha milele kinazikwa. Tena kwa upande mwingine haitegemei namna yetu ya kufikiri lakini hutegemea uwezo usio na mipaka wa Mungu kwamba hudhihirika kama Mungu kutoka kwa mwanadamu, kama asiyekufa kutoka kwa aliyekufa, na kama wa milele kutoka kwa aliyezikwa. Hivyo tumehuishwa na Mungu katika Kristo kupitia kifo chake." Utatu 1:14
"Isipokuwa mambo ni ya asili ile ile hayawezi kuwekwa kumbukumbu na heshima sawa, usawa wa heshima hauleti utengano katika wale wanaoheshimiwa. Lakini mwuujiza wa kuzaliwa hulazimu usawa wa heshima." (juu ya Yohana 5:23)
Gregory wa Nyssa (335-394 B.K.)
"Wakati tunaposema kuwa Mungu wa utatu wa Baba na wa Mwana na wa Roho Mtakatifu ni mmoja, na huku tukiwazuia watu kusema ‘kuna Mungu watatu’? Juu "Si Mungu Watatu"
Ambrose wa Milan (340-397 B.K.)
"Maneno haya, basi yameandikwa kwa ajili ya Mungu, kwa Jina ambalo heshima kuu na kweli ni ya kawaida kwa [wote wawili Baba na] Mwana." Ya Imani ya Kikristo 3:3:17.
Hitimisho
Kanisa halikuwa na watu wasioamini katika Utatu. Waliotegemea ufahamu wa kibinadamu (Gnostics), Waariani na wengine wenye imani potofu walitengwa na kanisa. Kanuni ya imani ya Mashahidi wa Yehova, Wamormon na wengineo ni ugunduzi wa imani za kisasa.

S: Kwenye Mat 27:46 na Mak 15:34, je Yesu alimaanisha nini aliposema, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?"
J: Hili halikua ni swali tulivi la kithiolojia, kilikuwa ni kilio cha uchungu. Hiki kilikuwa ni kilio cha kihisia, si tu maumivu ya kimwili. Kwa njia ambayo huenda tusiifahamu kikamilifu, Mungu Baba alimwacha Yesu, aliyekuwa amechukua mzogo wa dhambi zetu zote juu ya mabega yake.

S: Katika Mat 27:46 na Mak 15:34, je, yaonesha kuwa Yesu si Mungu, kama kiongozi wa kidini Mch. Moon afundishavyo?
J: Na. Kwanza hivi ndivyo Masihi potofu Mch. Moon alivyosema, na kisha kanusho lake. Kanuni ya Kimungu (toleo la tano 1977) uk. 210-212 "…Yesu, kama mwanadamu aliyetimiza kusudi la uumbaji, yeye ni mwili mmoja na Mungu….Hata hivyo kwa namna yoyote hawezi kuwa Mungu mwenyewe…Yesu, akiwa mwili mmoja na Mungu, anaweza kuitwa Mungu wa pili (sura ya Mungu), lakini kwa vyovyote hawezi kuwa Mungu mwenyewe…Yesu alikuwa mwanadamu aliyekamilisha kusudi la uumbaji, na hii haimanishi kuwa alikuwa Mwuumbaji yeye mwenyewe . …Zaidi ya hayo, tunapoona kuwa Yesu alisema msalabani, "Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?" hapa huwa bayana kuwa Yesu si Mungu mwenyewe. Hata hivyo, Yesu ni Mungu kulingana na Waebrania 1:8, 10 na Tito 2:13, ana utimilifu wote wa kiungu katika Wakolosai 1:19. Mistari mingine inayoonesha kuwa Yesu ni Mungu ni Warumi 9:5, Yohana 5:23, na 1 Yohana 5:20. Mwanafunzi wake Tomaso alimwita Yesu "Mungu wangu" katika Yohana 20:28. Yohana 1:3, 10, 11, 14 na Wakolosai 2:16 inaonesha kuwa Yesu hakuwa eti mwanadamu tu, kwa kuwa vitu vyote vya mbinguni na duniani viliumbwa kupitia kwake na kwa ajili yake Yesu.
Kuchanganyikiwa kunaweza kutokea kwa kuwa jina la Mungu limetumika kwa maana zaidi ya moja katika Biblia. Hakika angalau duniani, Mungu Baba alihudumu kama Mungu wa Yesu, na kama Yesu duniani alijifunza utii (Waebrania 5:8)

S: Katika Mat 27:51 na Mak 15:38, ni nini maana ya pazia la Hekalu kupasuka vipande viwili?
J: Pazia liligawanyika kati ya mahali hasa patakatifu pa Mungu na sehemu nyingine yote ya hekalu. Mpasuko ulionesha kwisha kwa umuhimu wa matumizi ya hekalu na kanuni za sheria zilizolisimamia hekalu. Mpasuko ulionesha kuwa kwasababu ya sadaka ya Yesu ya ondoleo la dhambi, kizuizi kilivunjwa na tunaweza kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na Mungu

S: Katika Mat 27:51, je, kuna uthibitisho wowote wa ziada kwa ajili ya hekalu kupasuka?
J: Kuna kitu fulani kinachofanana katika b Yoma 39b (uk. 580). Inasema milango ya hekalu ilijifungua yenyewe.

S: Katika Mat 27:51 hivi ni kweli kwamba hakuna uthibitisho kwa ajili ya tetemeko mbali na Matayo?
J: Hapana, hili si sahihi. Aidha watu wasioamini wako sahihi na Matayo aliunda simulizi ikiwa na mantiki yenye kusisimua, ambayo kanisa la kwanza lilirubuniwa kuamini kama ni kweli, ama vinginevyo kulikuwa na tetemeko kweli, makaburi yalifunguka, baadhi ya wafu walifufuka, na kusadikika kuwa walikwenda mbinguni baada ya ufufuo wa Yesu.
Kauli isemayo kwamba hapajawa na mtu mwingine aliyewahi kuyataja haya licha ya Matayo si sahihi. Tuna vyanzo viwili licha ya Biblia visivyo vya Kikristo na vyanzo vinne licha ya Biblia vilivyo vya Kikristo ambavyo hivi vyote vyataja matukio haya.
Phlegon alikuwa mwandishi wa Kiyunani kutoka Karia (Asia Ndogo), aliyeandika muda mfupi baada ya 137 B.K. kwamba katika mwaka wa wanne wa Olympiad ya 202 [33 B.K.]. kwamba "kulikuwa na tukio kubwa la kukamatwa kwa jua" na kwamba "ilikuwa usiku kwenye saa ya sita siku ya tetemeko katika Bithynia, na mambo mengi yalibadilishwa huko Nikea" (imenukuriwa kutoka Kesi ya Kristo uk. 111) Origen Dhidi ya Celsus kitabu cha 2 sura 14 uk. 437, kitabu 2 sura 33 uk. 445, kitabu cha 2 sura 59 uk.455.
Thales (au Thallus) alikuwa mwanahistoria wa Kipalestina aliyetunukiwa na Julius Africanus (andiko 232-245 B.K.). Julius anasema, "Hili giza Thallus, katika kitabu cha tatu cha historia yake, analiita, bila sababu katika mtizamo wangu, ni kukamatwa kwa jua." (imenukuriwa kutoka Waandishi wa kikristo walioandika kabla ya baraza la kwanza la kanisa la awali lililofanyika Nikea mwaka 325 BK juzuu 6 uk. 136.) Muktadha anaoujadili Julius ni jinsi gani tangu wakati wa amri ya kifalme ya Artaxerxes hadi kusulibiwa kwa Kristo, unavyotimiza Danieli 9. (Hata hivyo hatuna uthibitisho wowote kwamba Thales alilitaja tetemeko.
Irenaeus (182-188 B.K.), katika "Vipande vya Uandishi vilivyopotea" sura 28 uk. 573 (katika Waandishi wa Kikristo Walioandika kabla ya Baraza la Kwanza la Kanisa la Awali Lililofanyika Nikea Mwaka 325 B.K.), ametaja kuwa "Yesu aliposhuka kuzimu, roho nyingi zilipaa na walionekana katika miili yao." Na pia aliandika, katika Dhidi ya Mafundisho Potofu, kitabu cha 4 sura 34 uk. 512 asema, "Na mantiki zilizounganishwa na mateso ya Bwana, ambazo zilitabiriwa, hazikutokea katika kesi zingine zozote. Kwa kuwa hapajatokea kwenye kifo cha mtu mwingine yeyote kati ya watu wa zamani za kale kwamba jua lilizama saa sita, au pazia la hekalu kupasuka, au ardhi kutetemeka, au miamba kupasuka, au wafu kufufuka, au mmojawapo kati ya watu hao [wa zamani] kufufuka siku ya tatu, au kupokelewa mbinguni...Kwa hiyo manabii walisema hasha si mtu mwingine yeyote ila Bwana, kwa ajili yake mambo yote haya yalisemwa kabla ya wakati na ishara mbalimbali kutimia." Ignatius (kabla ya 116 B.K.), mwanafunzi wa Yohana, katika Barua Yake kwa Magnesians, sura 9, anawataja wale ambao Yesu aliwafufua.
Clement wa Alexandria katika The Stromata (193-202 B.K.) kitabu cha 6 sura 6 uk.491 asema, "Lakini wale waliokuwa wamekwisha kulala, wafu walioshuka, lakini wakapaa wakiwa hai.’ Injili yasema, ‘kwamba miili mingi ya wale waliokuwa wamelala ilifufuka- bayana ikiwa imebadilishwa kuwa katika hali nzuri zaidi. Basi hilo lilitokea, mlipuko wa kiulimwengu na tafsiri kupitia uchumi wa Mwakozi."
Waandishi wa kwanza aidha "walirubuniwa ama walidanganyika" kwa kufikiri kuwa hili lilitokea, kufuatana na fikria za baadhi ya watu wasioamini. Vile vile kwa miujiza mingine ukiwemo ufufuo, aidha Wakristo wa kwanza walirubuniwa ama walidanganyika kuwa hakika hili lilitokea wakati halikutokea kamwe. Hakuna mashahidi zaidi walioona kwa macho, hivyo tunaamini kile walichosema waandishi wa Injili au hatuamini kabisa. Hili linakwenda kwa Paulo pia, aliyesema katika 1 Wakorintho 15:13-19 kwamba ikiwa ufufuo haukutokea, basi Paulo alisema mahubiri yake yote yalikuwa hayana maana yoyote, angekuwa shahidi batili, na imani yetu ingekuwa batili, na Wakristo wangekuwa watu wa kuhurumiwa kuliko watu wote. Kama mtume Paulo, binafsi sioni jambo hili kuwa labda badala ya hakika. Origen (225-254 B.K.) anataja giza juu ya nchi, na makaburi yalifumuka wazi katika Dhidi ya Celsus kitabu cha 2 sura 33 uk. 445. Dionysius wa Alexandria (246-265 B.K.) anataja tetemeko la ardhi katika Matayo Barua kwa Askofu Basilides Kanuni za kanisa Katoliki (Canon) 1 uk.94.
Kwa kuhitimisha, tuna sababu ya kusimamia maandishi ya watu wachache waliobainiwa hapa ya kuwa watu walifufuka kwasababu
1. Imani yetu katika waandishi wa Injili na taarifa zao juu ya mambo mengine
2. Waandishi wa Kanisa la kwanza walilitaja hili
3. Hili lisingewezekana kwa mtu yeyote ambaye hakumjua mtu aliyekufa kuweza kuthibitisha, kwa hiyo waandishi wa Kiyahudi na Kiroma wasingeyajua haya.
4. Waandishi wa Kiyahudi wasingekuwa na hamasa yoyote kuyataja haya,
5. Tukio la watu waliofufuka lingefunikwa na ufufuo wa Yesu.
Kinusu nakubaliana na wewe ulichosema juu ya tetemeko. Lakini badala ya kusema kuwa waandishi wa Injili walitumia matukio haya ya ajabu kama kielelezo cha umuhimu wa pekee na matokeo ya utendaji kazi wa Mungu, binfasi naamini kuwa Mungu aliyatumia matukio hayo ya ajabu. Kwa kuongezea kwenye Injili usisahau [takwimu za] matetemeko katika Ufunuo au wakati Uzzia alipokufa katika Isaya 6. Pia katika historia ya kanisa, wakati John Chrysostom alipofukuzwa kutoka Constantinople mnamo mwaka 403 B.K., kulikuwa na tetemeko wakati huo. Isingetegemewa kuwa waandishi wa wakati huo walikuwa wakiweka takwimu za matetemeko madogo madogo. Kwa kuwa matetemeko madogo madogo yalikuwa yakitokea katika ukanda ule, nina takwimu kwa ajili ya Ugiriki na Uturuki. Encyclopedia Britannica ina taarifa za Ugiriki na Uturuki kwamba:
Kati ya 1902 na 1946 kulikuwa na matetemeko 58
Kati ya 1947 na 1966 kulikuwa na matetemeko 82
Kati ya 1967 na 1976 kulikuwa na matetemeko 45
Kati ya 1977na 1981 kulikuwa na matetemeko 9
Jambo jingine la nyongeza ni kwamba utafiti wa Arkiolojia kule Qumran unaonesha kulikuwa na tetemeko lenye uharibifu katika mwaka 31 K.K. (kabla ya Kristo), lakini hata hivyo waandishi wa zamani hawakuweka kumbukumbu za tukio hili.
Hitimisho: Yaonekana kuna kuchagua kati ya mambo mawili (hakuna cha kubaki katikati)
1. Hakuna tetemeko: Waandishi wa Injili pengine walikuwa sahihi katika mafundisho yao ya kimaadili, lakini walitoa taarifa za matetemeko ambayo hayakutokea. Hatuwezi kuamini wanachokisema, angalau kuhusiana na matukio halisi ulimwenguni.
2. Tetemeko: Waandishi wa Injili wanaweza kuaminiwa wanachokisema, na walitoa taarifa ya kuhusu matetemeko yaliyotokea.

S: Katika Mat 27:52-53, ingewezekanaje wafu watoke makaburini mwao?
J: Mungu mwenyezi ana uwezo kufanya chochote anachotaka kufanya, ni pamoja na kufufua watu waliokufa wakaishi tena. Kw baadhi ya watu wasioamini hili lingevunja kanuni za asili zinazotegemeza uumbaji wote; naam Mungu ndiye aliyezifanya kanuni hizo za asili.
Malaika mbinguni lazima wanayaangalia maneno ya watu wasioamini sawa na jinsi tunavyoyaangalia maneno ya watu ambao hawakuamini wakati wa enzi za makaka wale akina Wright, waliosema, "mwanadamu hawezi kupaa". Utaalam wa kupaa anga za mbali unafifisha kanuni zinazotawala uwiano wa angani (law of gravity), si zaidi sana kwa Muumba kubatilisha kanuni za uumbaji wake!

S: Katika Mat 27:52-53, wakati watu walipotoka makaburini mwao wakati wa ufufuo wa Yesu, je, hii yaonesha uwezekano wa Maria kukwepuliwa mbinguni akiwa hai kama ambavyo mwandishi mmoja wa Kikatoliki hufundisha?
J: Na. Ludwig Ott alitoa hili, si kama uthibitisho, lakini kama hoja saidizi katika Misingi ya Dogma za Kikatoliki (1960) uk.209. Hii haisimamii wazo kwamba Maria aliinuliwa mbinguni akiwa hai kwa sababu mbili:
a) Haieleweki ikiwa watu waliotoka makaburini walihuishwa katika miili yao (kama Lazaro) au walifufuliwa
b) Maria alikuwa bado hai wakati wa kufa na kuinuka toka makaburini, kwa hiyo hawezi kuwekwa katika kundi hili..

S: Katika Mat 27:65, je, tunajuaje kuwa "kuchukua mlinzi" ina maana ya askari wa Kirumi 4-16, badala ya askari mmoja wa Hekalu?
J: Kwa Wayunani ingeweza kuwa vyovyote vile ni sawa.
Kauli au tamko: umeshapata mlizi tayari
Amri: chukua huyu mlinzi wa Kirumi ninayekupatia. Hizi ndizo tafsiri tatu zenye uwezekano na zinazokubaliana na zinazopingana na hoja
Tayari una mlinzi wako wa hekalu: Kwa mantinki hii ni walinzi wa hekalu waliomkamata Yesu. Kwa kuwa mwili wa mhalifu aliyeteswa ulikuwa mali ya Warumi, ilibidi waombe ruhusa kwa Pilato kuulinda mwili. Pingamizi la hoja hii ni ukweli kuwa muhuri wa makuhani wa Kiyahudi ungekuwa na maana kidogo sana, wakati muhuri wa Ufalme wa Kirumi, uliotengezwa kwa waya mgumu na madini magumu sana, isingekuwa rahisi kuchakachuliwa. Ingemaanisha mauti kwa yeyote ambaye angeuvunja.

Tayari una mlinzi wa Kirumi aliyekabidhiwa kwako: Labda mlinzi wa Kirumi alikuwa amekabidhiwa tayari kwa makuhani
Chukua mlinzi wa Kirumi: Take a Roman guard: kinyume na hoja hii hakuna mfano wowote wa kutumia neno la Kiyunani echein katika maana ya "kuchukua" linaloonekana katika aidha Kiyunani za zamani (Classical) au Kiyunani walichoongea Wayahudi wenye utamaduni wa Kiyunani (Hellenistic Greek) wakati ule.

S: Katika Mat 28:9, je, Yesu alitokea mara ya kwanza kwa Mariam Magdalena, au mara ya kwanza kwa Petro (Kefa) kama Paulo anavyoashiria katika 1 Wakor. 15:5?
J: Mariam Magdalena alikuwa mtu wa kwanza kumwona Yesu, lakini Petro alikuwa mtume wa kwanza kumwona Yesu. Na kwa kweli Paulo hakusema kuwa Petro alikuwa mtu wa kwanza ambaye Yesu alimtokea. Kati ya watu Paulo aliowaorodhesha, Petro alikuwa wa kwanza katika orodha yake kumwona Yesu, akifuatiwa na wanafunzi wengine, kisha watu wengine zaidi ya 500. Kwa upande mmoja, labda Paulo hakutaja wanawake kwa makusudi kwani kwa wakati ule ushuhuda wa wanawake haukuthaminiwa. Kwa upande mwingine, labda wanawake walisahaulika kuwa walikuwa kaburini kabla ya Petro. Hata hivyo, kwa vyovyote hapana mgongano wowote, kulingana na ukweli kwamba Paulo hajakanusha kuwa hakuna mtu yeyote aliyemwona Yesu kabla ya Petro.

S: Katika Mat 28:19, kwa kuwa kuna Mungu mmoja tu, kwa vipi Yesu anaweza kuwa Mungu, na kwa jinsi gani Utatu wa Mungu utakuwa ni kweli?
J: Hapo kunaweza kuwa "uwingi" kwa Mungu mmoja bila kuwapo na miungu mingine tofauti. Hata katika Korani, wakati Mungu anapoongea, neno "sisi" (Nahnu), na neno "Mimi" nalo limetumika.
Mungu hadhibitiwi na mipaka ya kibinadamu, na Mungu anaweza kujidhihirisha Mwenyewe kwetu kwa jinsi anavyotaka.
Kuna utatu katika Maandiko: Matayo 28:19; 1 Petro 1:2; Waefeso 2:18; Ufunuo 4:8; 2 Wakorintho 13:14; Yohana 15:26.
Kuna Mungu mmoja tu asiyegawanyika. Kumbukumbu la Torati 4:35-39; 6:4; Isaya 43: 10-2; 44:6,8; 45:5-6,14,21; 46:9; 1 Timotheo 1:17; 6:15-16.
Nafsi tatu zinazojitegemea: Matayo 3:16-17; Luka 3:21-22; Yohana 1:1; 6:38;14:31;15:26; 16:28; 17:5; Matendo ya Mitume 5:31-32; Marko 10:38-40
Yesu ni Mungu. Yohana 1:3; Wakolosai 1:16-17; Waebrania 1:6-9; Yohana 9:38; 2 Wakorintho 11:3; Yohana 20:28-29; Ufunuo 5:8-9; 22:20
Roho ni Mungu. Warumi 8:9-16; Luka 1:35; 1 Yohana 4:12-16; 1 Wakorintho 3:16 dhidi ya 1 Wakorintho 6:19; Matendo ya Mitume 5:4;
Wako sawa katika asili, utukufu, na heshima. Yohana 5:18; 5:23; Wakolosai 2:9-10; (Isaya 44:6; Ufunuo 1:8 dhidi ya Ufunuo 1:17-18; 22:13)
Wanatofautiana katika utendaji na daraja. 1 Wakorintho 11:3; 1 Wakorintho 15:25-28; Matayo 12:18; Waefeso1:3, 17; Yohana 1:33; 14:16, 26, 28; Warumi 8:26-27.
Pamoja na hayo, Yesu kuwa katika Utatu haina maana kuwa Yesu ni moja ya tatu ya Mungu, chochote zaidi ya urefu wa moja ya tatu ya meza ni moja ya tatu ya meza. Huwezi kumwelezea Mungu kimahesabu, hata ukijaribu Utatu wa Mungu hauwezi kuwa 1 + 1 + 1 = 1 lakini 1 mara 1 mara 1 =1.

S: Katika Mat 28:19, Mat 24:36, na Mat 3:16-17, ni nini maana ya mafundisho kuwa Mungu hagawanyiki na ni Roho au Mungu hujihirisha katika sura tofauti kwa vipindi tofauti (modalism), na kwanini imani na fundisho hili si sahihi?
J: Mafundisho juu Utatu wa Mungu hufundisha kuwa kuna Mungu mmoja asiyegawanyika katika nafsi tatu zinazojitegemea. Mungu asiyegawanyika na ni Roho au anayejidhihirisha katika sura tatu tofauti katika vipindi tofauti (modalism), hufundisha juu ya Mungu mmoja asiyegawanyika na ana nafsi moja. Na hasa kuna aina mbili za mafundisho haya (modalism). Patripassianism ni fundisho linalosema Mungu baba ni mwana ambaye ni Roho. Dynamic modalism fundisho lasema Mungu baba alikuja kuwa mwana, ambaye naye alikuja kuwa Roho. Aina zote mbili za mafundisho haya si sahihi kwa sababu zifuatazo.
1. Yesu alisema "Baba ni mkuu kuliko mimi" katika Yohana 14:28. Wakati Yesu akiwa amevua utukufu wake hapa duniani aliposema hivyo, ukweli unabaki kuwa kama Baba alikuwa mkuu kuliko Yeye, basi kulikuwa na utofauti kati ya Baba na Mwana.
2. Ikiwa mafundisho ya modalism ni kweli, Yesu lazima atakuwa alikuwa mwigizaji kwa kubadili sauti, mwanamazingaombwe, na zaidi ya yote mwongo wakati wa ubatizo wake (Matayo 3:16-17; Marko 1:10-12; Luka 3:21-22). Wakati akiwa duniani, Yesu alikuwa akitumika kwa kumtii Baba (Waebrania 5:16-17). Hili lisingekuwa na maana yoyote ikiwa pasingekuwa na yeyote kwa ambaye Yesu angelimtii.
3. Vile vile, Yesu alifanya kile ambacho Baba alimwamru (Yohana 14:31). Yesu alijifunza kuwa mtii kwa Baba katika Waebrania 5:8.
4. Matayo 24:36 yasema kuwa hakuna ajuaye siku wala saa ambapo Kristo atarudi, wala hata mwana, ila ni Baba pekee yake. Hivyo angalau wakati Yesu akiwa duniani, kulikuwa na tofauti kati ya alichokijua Baba na kile alichokijua Yesu. Wakati baadhi ya nyaraka za maandiko ya Kiyunani hazina "wala mwana" waraka wa andiko lililo bora zaidi na mengi ya maandiko ya Kiyunani yana "wala mwana".
5. Yesu alitumwa na mwingine licha ya Yeye binafsi, kama Yohana 5:36-37; 6:29, 38 ina maana yoyote. Mbingu haikuwa tupu Yesu aliposhuka duniani.
6. Kwa kuwa Baba alitoa kitu kwa Mwana, na akampa Mwana mamlaka katika Yohana 5:22, 26, 27, hii inaonesha Baba na Mwana wako tofauti.
7. Kwanini Yesu aliomba kwa Baba, au kuomba kitu kutoka kwa Baba, katika Yohana 17:5, Yohana 14:16, 26, 28, na sehemu zingine, kama Yesu alikuwa akijiongelea mwenyewe.
Zaidi ya hayo, kwasababu maombi ya Yesu yalitolewa kama alikuwa akiongea na mtu mwingine, Biblia ingekuwa inapotosha kama pasingekuwa na mtu mwingine yeyote ambaye Yesu alikuwa akiongea naye.
8. Ni nani Roho huyo anayeomba kwa niaba yetu katika Warumi 8:26-27?
9. Ikiwa Yesu alikuwa mtumishi, Yesu alikuwa mtumishi wa nani katika Matayo 12:18?
10. Ni nani aliyemtelekeza Yesu pale Kalvari katika Marko 15:34 na Matayo 27:46.
11. Mistari mingine inayoonesha utofauti ni Yohana 1:33; 1 Wakorintho 11:3; 15:25-28; Waefeso 1:3, 17; Waebrania 1:9
Hapa kuna baadhi ya nukuru kutoka kwa Witness Lee, aliyeanzisha kanisa la mtaa. Kanisa hili la mtaa lina vikundi vya wanafunzi viitwavyo "Wakristo katika Eneo la Kanisa." Kwa ujumla makanisa yao yanaitwa "Kanisa katika [jina la mji]" "Hivyo nafsi tatu za Utatu wa Mungu ikawa ni hatua tatu za kupokezana katika mchakato wa uchumi wa Mungu." W. Lee. Uchumi wa Mungu, Kijito Kilichohai 1968 uk.10.
"Tena, Baba, Mwana na Roho si Mungu watatu, bali hatua tatu za Mungu mmoja, kwa ajili yetu kumiliki na kufurahia" W. Lee. Kuhusu Mungu wa Utatu Kijito Kilichohai bila tarehe uk.31
"Katika mbingu ambako mwanadamu hawezi kuona, Mungu Baba, anapoelezwa miongoni mwa wanadamu, ni Mwana; na anapokuja kati ya wanadamu Yeye ni Roho. Mungu Baba alielezwa miongoni mwa wanadamu katika Mwana na Mwana akawa Roho kuja katikati ya wanadamu. Baba yuko ndani ya Mwana, na Mwana akawa Roho—hawa watatu watatu ni Mungu mmoja tu." W. Lee. Kuhusu Mungu wa Utatu Kijito Kilichohai bila tarehe uk. 8-9
Baada ya kifo na ufufuo [Mwana] akawa Roho na kuwavuvia wanafunzi W. Lee. Kuhusu Mungu wa Utatu Kijito Kilichohai bila tarehe uk.8
"...Mwana akawa Roho kwa ajili yetu tunywe kama maji ya uzima…" W. Lee. Kuhusu Mungu wa Utatu Kijito Kilichohai bila tarehe uk.8
"...Tunajua Mwana ni Bwana na kwamba Yeye ni Roho. Kwa hiyo ni lazima tuelewe wazi kuwa Kristo Bwana ni Roho pia." W. Lee. Roho wa Kristo Ajumlimshaye Wote Kijito Kilichohai 1969 uk. 4, 6, 8
"Hivyo, nafsi tatu za Utatu wa Mungu zikawa hatua tatu za kupokezana katika mchakato wa uchumi wa Mungu." W. Lee. Uchumi wa Mungu Kijito Kilichohai uk. 10
Kumbuka kwamba hoja hii imekanushwa na mistari iliyotolewa mwanzoni mwa jibu hili. Angalia pia Wakati Wenye Imani Potofu Wakiuliza uk. 130-131 kwa maelezo zaidi kwanini mafundisho ya modalism si sahihi.

S: Katika Mat 28:19, kwa kuwa modalism si sahihi, na bado Baba na Mwana wako karibu sana, na kwa kiasi gani wako karibu?
J: Japokuwa maandiko hayatoi maelezo mengi, hapa kuna mambo sita tunayoweza kuyasema.
1. Kama Yesu alivyo katika Baba, tu katika Yesu, na Yesu yumo ndani yetu.
Kuna muunganiko katika ya aina za uhusiano hizi mbili: Baba-Yesu, Yesu-nasi, Sisi-Yesu. Yohana 14:20; 17:23; 6:57
Hata hivyo, kuna zaidi juu ya Utatu wa Mungu kuliko uhusiano huu wa kimfano. Matayo 28:19; Yohana 1:1,18; Wafilipi 2:6-7; Wakolosai 1:15
Baba, Yesu, na sisi sote tunashirikiana baadhi ya mambo, kama vile uzima wa milele Yohana 16:13-15
Baba na Yesu "humiliki" vyote bila tofauti Yohana 16:15;17:10. Roho Mtakatifu hudhihirisha hili kwetu Yohana 16:14-5
Hata hivyo, Baba hana mambo mengine tunayoshirikiana na Yesu baada ya kuzaliwa kwake katika hali ya mwanadamu Waebrania 1:6-10; 2:14; 7:3
2. Kama Baba na Yesu ni mmoja, tunapaswa kuwa wamoja
Tunapaswa kuwa wamoja wenyewe kwa wenyewe kwa namna moja ama nyingine ni sawa kama Baba na Yesu Yohana 17:11,21-22
Japokuwa wao ni Mmoja kwa namna moja ama nyingine sisi hatuwezi kuwa mmoja Yohana 5:23
3. Baba huishi ndani ya Yesu
Duniani Baba aliishi ndani ya Yesu Yohana 10:38;14:10-11. Yesu alikuwa amejazwa na Roho Luka 4:1,18
Kama unamjua Yesu kwa hakika, basi unamjua Baba na umeshamwona Baba. Yohana 14:7-9
Japokuwa Baba hakuwa, kimchakato, au kugeuka kuwa Yesu. Waebrania 13:8; 1:9; Yohana 14:10,24,26; 15:1; 16:27-8,32; 17:5
4. Yesu huishi ndani ya Baba
Duniani Yesu alikuwa ndani ya Baba. Yohana 10:38; 14:11
Japokuwa [hawa wawili] ni tofuati; Yesu hakuwa mwigizaji kwa kubadili sauti. Matayo 3:16; John 8:18. Yesu alitelekezwa pale Kalvari Marko 15:34; Matayo 27:46
Hakuna ajaye kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwa Yesu Yohana 14:6; 6:45; Matendo ya Mitume 3:12
Japokuwa kama walivyo karibu duniani, Yesu alikuwa bado aende kwa Baba. Yohana 14:12; Marko 16:19; Yohana 20:11
Yesu anaitwa Baba wa milele, jina linaloashiria kuwa chanzo cha uzima wa milele. Isaya 9:6
Hata hivyo, Yesu hakuja kuwa katika mchakato, au kugeuka kuwa Baba. Waebrania 13:8; Yohana 20:17; 14:10,24,26; 15:1
5. Mungu/Baba/Kristo/Roho yumo ndani yetu
Watu humwona Mungu kupitia kwetu na ndani yetu.
Japokuwa Mungu haishi kikamilifu ndani yetu, si tofauti na nyota zinavyokuwa katika vyombo vya kuchunguzia nyota zake safari angani (telescopes). 1 Timotheo 6:16; Yeremia 23:24; Ufunuo 19:11
Baba/Yesu/Roho pia hukaa hasa/hutengeneza makao yao katika kila mwumini. Yohana 14:17,23; 17:26; Warumi 8:9-11; Wagalatia 3:6; 1 Wakorintho 6:19; 1 Yohana 4:15-16; 2 Timotheo 1:14
Hata hivyo, Mungu/Baba/Kristo/Roho hakuwa sisi, au kubadilika kuwa mwanadamu mwenye dhambi. Yakobo 1:13; Waebrania 4:15: 1 Petro 2:22; 1 Yohana 3:5
Mungu hutenda kazi na hutenda ndani yetu na kupitia kwetu Wafilipi 2:13; mifano:1 Wafilipi 15:10; Warumi 15:18-19
Watu wa Mungu, kanisa, wako pamoja mwili wa Kristo. 1 Wakorintho 6:15; 10:17; 12:27; Waefeso 4:12; Wakolosai 1:24.
Japokuwa, sisi si mwili wa Kristo kibinadamu. Wakolosai 1:22. Mungu hana mipaka kutenda kazi kupitia kwetu. Mwanzo 1; Matendo ya Mitume 9:1-6; Ufunuo
Kusaidia/kutotusaidia ni sawa kama ilivyo kwa Yesu Kristo. Matayo 25:35-45; Yohana 13:20; Matendo ya Mitume 9:4-5; 22:7-8; 26:14-15
Japokuwa, watu wanaweza kumsifu au kumkashifu Mungu moja kwa moja bila kufanya chochote kwa waumini. Warumi 1:18-32; Ufunuo 9:20-21
6. Tunaishi ndani ya Mungu/Baba/Kristo/Roho
Tumo ndani ya Yesu na Baba. 17:21; Wakolosai 2:6,12; 3:3-4; 1 Yohana 4:12,15-16; 5:20.
Ni lazima tubaki ndani ya Yesu Kristo na ndani ya upendo wake. Yohana 15:1-9; 1 Yohana 2:27
Japokuwa, hatuko pamoja na Mungu kikamilifu sasa; bado tunahitaji kwenda na kuwa pamoja na Mungu. 2 Wakorintho 5:8; 1 Wakorintho 13:12; Wafilipi 1:23
Kwasababu Yesu yu hai, tutakuwa hai. Yohana 14:19; Wakolosai 3:4; 1 Wakorintho 15:12-22
Japokuwa, huwa hatubadiliki kuwa, kimchakato, kubadilika kibailojia ama kimfumo, au kubadilika kuwa Mungu au Kristo; bali tunakuwa watauwa na wa kufanana kitabia na Kristo. Isaya 42:8; 43:10; Warumi 8:29; 1 John 3:2; Wafilipi 3:21
Tu viumbe vipya katika Kristo. 2 Wakorintho 5:17. Tuna nia ya fikra ya Kristo. 1 Wakorintho 2:16.
Japokuwa, hatubadiliki kuwa mizuka; bado tunapaswa kuwa na nia ya fikra na hulka zetu. 1 Wakorintho 6:2-6; 11:13; 13:11+14:20; Warumi 14:5-6



S: Katika Mat 28:19, je, mstari huu ulichakachuliwa wakati wa Baraza la Nikea, kwa kuwa Eusebius anaunukuru mara 18 kabla ya Nikea bila kutaja Utatu wa Mungu, na Eusebius anaunukuru tu kwa mfumo wenye kanuni katika Utatu wa Mungu kitheolojia (Trinitarian) baada ya Nikea? Victor Paul Wierwille, mwasisi wa The Way, alidai katika kitabu chake Yesu Kristo si Mungu (1981) uk.19-20.
J: Kutoka katika hali ya utulivu hoja hii ni ya hovyo kwasababu kadhaa zifuatazo. Eusebius wa Kaisaria hasa alikuwa mwanahistoria, na si mwanatheolojia hasa, hata Wierwille anakiri kuwa Eusebius anaunukuru baada Nikea.
Pili, na cha muhimu zaidi, waandishi wengi Wakristo karne nyingi kabla ya Eusebius waliunukuru mstari huu kikamilifu.
Mafundisho ya Mitume (kabla ya 125 B.K.) sura 7 uk.379 yaunukuru kama, "Baada ya kusema kwanza yote haya, batizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, katika maji yaliyo hai. [i.e. maji yanayotiririka]. Lakini kama hamtakuwa na maji yaliyo hai, batizeni katika maji mengine; na kama haitakuwa katika maji baridi, katika maji vuguvugu. Lakini kama hamtafanya hivyo, mwagieni maji mara tatu kichwani katika jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu."
Irenaeus (182-188 B.K.) aliunukuru "Nendeni na kawafundisheni mataifa yote, mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu." (Irenaeus Dhidi ya Mafundisho Potofu kitabu cha 3 sura 17.1 uk.444)
Tertullian (198-220 B.K.) kwa namna fulani analiandika wazo la mstari huu: "Yeye [Yesu] aliwaamru wale kumi na mmoja wengine, wakati wa kuondoka kwake kwenda kwa Baba, ‘kwenda kuyafundisha mataifa yote, ambao walipaswa kubatizwa katika jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu." Juu ya Maelezo Dhidi ya Walimu Potofu, sura 20 uk.252.
Tertullian anausema tofauti kidogo katika Juu ya Ubatizo sura 13 uk.676 "Mungu, Yeye [Yesu] alisema, ‘yafundisheni mataifa, mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana na Roho Mtakatifu."
Hippolytus (222-235/6 B.K.) anaunukuru kama "Nendeni ninyi na yafundisheni mataifa yote, mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu" Dhidi ya Mafundisho Potofu ya Noetus mmoja sura ya 14 uk.228
Andiko la Kitaaluma Dhidi ya Mafundisho ya Novatian (254-256 B.K.) sura 3 uk.658 "Nendeni na hubirini Injili kwa mataifa, mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Hii ina maana kuwa Utatu wa Mungu ule ule uliotenda kazi kwa njia ya mifano mbadala katika siku za Nuhu kupitia njiwa, sasa unatenda kazi katika Kanisa kiroho kupitia wafuasi."
Andiko la Kitaaluma juu ya Kubatizwa Mara ya Pili (c.250-258 B.K.) sura 7 uk.671 "Nendeni, fundisheni mataifa; wabatizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho."
Baraza la Saba la Carthage (258 B.K.) uk.567 Munnulus wa Girba alisema, "… hata hasa hasa katika Utatu wa Mungu wa ubatizo, kama Bwana wetu asemavyo, ‘Nendeni na wabatizeni mataifa, katika jina la Baba, la Mwana, na la Roho."
Baraza la Saba la Carthage (258 B.K.) uk.569 Vincentius wa Thibaris alisema, "Nendeni na wafundisheni mataifa, mkiwabatiza katika jina la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu."
Victorinus wa Pettau (-307 B.K.) anaukuru kama, "Yeye [Yesu] aliwatuma mitume, akisema: Nendeni, wafundisheni mataifa yote, mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu."
Commentary juu ya Siku za Mwisho kutoka sura ya kwanza na. 15 uk.345
Kwa hiyo kwanini basi, Wierwille anajaribu kuligubika jambo hili na kuepusha ukweli kwa uzushi mdogo mdogo kuhusiana na sehemu zipi alizonukuru Eusebius wakati tuna waandishi hawa wote kabla yake waliokuwa wazi zaidi.
Hatimaye, angalia swali kuhusu mambo mengine ambayo Wakristo wa kwanza waliyasema juu ya Utatu wa Mungu

S: Katika Mat 28:19, ni mafundisho gani mengine ya kanisa la kwanza juu ya Utatu wa Mungu?
J: Haya hapa ni baadhi yake.
Kwa Diognetus (imeandikwa c.130 B.K.)
"Kama mfalme anavyomtuma mwanaye, ambaye ni Mfalme pia, kwa hiyo anamtuma; kama Mungu (1) Alimtuma kama kwa watu alimtuma; kama Mwokozi alimtuma,…" sura 7 Nukuru (1) inasema "Mungu" hapa ikihusu mtu aliyetumwa.
Justin Martyr (mnamo 138-165 B.K.)
"kwa kuwa tunapotoa neno fulani, tunalizaa neno; bali si kwa kutenganisha, ili kulipunguza neno [ambalo hubaki lilivyo] ndani yetu, tunapolitoa; na kama vile tunavyoona vile vile kinachotokea kunapotokea moto, ambao haupunguzwi unapokuwa umewaka [kuwasha kitu kingine], lakini hubaki kama ulivyo;…Neno la hekima, ambaye ndiye Mungu mwenyewe aliyezaliwa na Baba kati ya vitu vyote, na Neno, na Hekima, na Nguvu, na Utukufu wa Mzazi, utatoa uthibitisho kwangu…"
Maongezi na Trypho sura 61. Hakika sura zote 57-63 zinajadili uungu wa Yesu.
Theofilo wa Antiokia (168-181/188 B.K.)
"Katika maana ile ile pia siku tatu zilikuwa kabla ya mianga [jua, mwezi, na nyota] ni aina za Utatu (Kiyunani triad), wa Mungu, na Neno lake, na Hekima yake." Kwa Autolycus kitabu cha 2 sura 15 uk.101.
Theofilo askofu wa Antiokia (168-181/188 B.K.)
"Kwa kuwa maandiko ya kimungu pekee yake hutufundisha kuwa Adamu alisema kuwa alikuwa ameisikia sauti. Lakini ni nini zaidi juu ya sauti hii isipokuwa ni Neno la Mungu, na Mwana ni nani pia?" Theofilo kwa Autolycus kitabu cha 2 sura 22 uk.103. Irenaeus (182-188 B.K.)
"Lakini kwamba Yeye [Yesu] yeye mwenyewe katika haki yake mwenyewe, zaidi ya mwanadamu yeyote aliyewahi kusishi, Mungu na Bwana na Mfalme wa milele, na Neno lililofanyika mwili, lililohubiriwa na manabii wote, mitume wote, na kwa Roho mwenyewe, ili lionekane kwa wote waliopokea hata sehemu kidogo ya kweli." (Irenaeus Dhidi ya Mafundisho Potofu, kitabu cha 3 sura 19.2 uk.449).
"Ujue kuwa kila mtu aidha ni tupu au amejaa. Kwa kuwa kama hana Roho Mtakatifu, hana ufahamu wa Mwuumbaji; hajampokea Yesu aliye uhai; hamjui Baba aliye mbinguni;…" (Dhidi ya Mafundisho Potofu 3:16)
"Yeye (akike) [kanisa] pia anaamini hoja hizi [za kanuni za imani] kama vile ana roho moja…Kwa kuwa makanisa yaliyopandwa Ujerumani hayaamini hivyo au kupokezana chochote kilichotofauti wala makanisa yaliyoko Hispania wala yale yaliyomo Gau wala yale yaliyoko Misri wala yale yaliyoko Libya, wala…"
Clement wa Alexandria alinena juu ya "Utatu Mtakatifu" katika The Stromata (193-202 B.K.) kitabu cha 5 sura14 uk.468.
Tertullian (198-220 B.K.)
"Kwa hiyo, Neno ni mara zote limo ndani ya Baba, kama asemavyo, ‘Mimi nimo ndani ya Baba,’ na wakati wote huwa pamoja na Mungu, kufuatana na ilivyoandikwa, ‘Na Neno lilikuwa pamoja na Mungu;’ na halikutengana na Baba kamwe, au tofauti licha ya Baba, kwasababu ‘Mimi na Baba ni mmoja.’" Dhidi ya Praxeas sura 8.
Hippolytus (170-235/6 B.K.) baada ya kunukuru Yohana 1:1
"Ikiwa, basi Neno lilikuwa pamoja na Mungu na lilikuwa Mungu ni nini kinafuata? Mtu anaweza kusema anaongelea Mungu wawili? Hakika sitaongelea juu ya Mungu wawili bali mmoja; wa Nafsi mbili hata hivyo na juu ya uchumi wa tatu (kubadilishwa kinafasi), ikiwa na maana kuwa neema ya Roho Mtakatifu. Kwa hiyo Baba hakika ni mmoja lakini wakiwa Nafsi mbili kwasababu kuna Mwana pia; na tena kuna nafsi ya tatu Roho Mtakatifu. Baba aamru, Neno hutekeleza na Mwana hudhihirisha, kupitia kwake watu humwamini Baba. Mwafaka wa uchumi hurudi nyuma kwa Mungu mmoja; kwa kuwa Mungu ni mmoja. Ni Baba aamruye na Mwana ndiye atiiye na Roho Mtakatifu ndiye atoaye ufahamu; Baba ni juu ya wote, na Mwana ni kupitia wote na Roho Mtakatifu ni katika wote. Na hatuwezi kufikiri vinginevyo juu ya Mungu mmoja, lakini kwa kuamini katika kweli, katika Baba na Mwana na Roho Mtakatifu." Dhidi ya Mafundisho Potofu ya Noetus Mmoja sura 14.
Athanasius (296-373 B.K.)
"Kuungana bila kusababisha kuchanganyikiwa, kubainika bila kutengana. Kutogawanyika bila madaraja." Mahubiri juu ya Luka 10:22
"Kwa kuwa ni msalabani pekee ambapo mtu hufa na mikono yake ikiwa imetandazwa. Ilikuwa jambo sahihi na mwafaka kwa Bwana kubeba jambo hili na kutandaza mikono yake ili kupitia mtu mmoja angewavuta watu wa zamani na wengine kutoka kwa watu wa mataifa na kuwaunganisha wote katika Yeye." Kufanyika Mwili 25:3
Basil wa Cappadocia (329-379 B.K.)
"wakati wote wanapaswa kukiri kuwa Baba ni Mungu, Mwana wa Mungu, na Roho Mtakatifu, kama walivyofundishwa na maandiko ya Mungu,…" Barua ya 7 kwa Wakaisaria (uk. 116)
Hilary (353-368 B.K.)
"Matendo ya Mungu kwa hiyo ni zaidi ya ufahamu wetu wa asili ya kibinadamu na hayaingiliani na mfumo wa fikira zetu zinazotegemea upembuzi wa mambo kwasababu ya utendaji wa milele isiyo na mwisho unaohitaji ufahamu wa kimungu kuyapima mambo mbalimbali. Kwa hiyo siyo hitimisho la upembuzi wa kibinadamu lakini uwezo ulio na kikomo wakati Mungu alifanyika mwanadamu, wakati Kisichokufa kinakufa, wakati Kilicho cha milele kinazikwa. Tena kwa upande mwingine haitegemei namna yetu ya kufikiri lakini hutegemea uwezo usio na mipaka wa Mungu kwamba hudhihirika kama Mungu kutoka kwa mwanadamu, kama asiyekufa kutoka kwa aliyekufa, na kama wa milele kutoka kwa aliyezikwa. Hivyo tumehuishwa na Mungu katika Kristo kupitia kifo chake." Utatu 1:14
"Isipokuwa mambo ni ya asili ile ile hayawezi kuwekwa kumbukumbu na heshima sawa, usawa wa heshima hauleti utengano katika wale wanaoheshimiwa. Lakini mwuujiza wa kuzaliwa hulazimu usawa wa heshima." (juu ya Yohana 5:23)
Gregory wa Nyssa (335-394 B.K.)
"Wakati tunaposema kuwa Mungu wa utatu wa Baba na wa Mwana na wa Roho Mtakatifu ni mmoja, na huku tukiwazuia watu kusema ‘kuna Mungu watatu’? Juu "Si Mungu Watatu"
Ambrose wa Milan (340-397 B.K.)
"Maneno haya, basi yameandikwa kwa ajili ya Mungu, kwa Jina ambalo heshima kuu na kweli ni ya kawaida kwa [wote wawili Baba na] Mwana." Ya Imani ya Kikristo 3:3:17.
Hitimisho
Kanisa halikuwa na watu wasioamini katika Utatu. Waliotegemea ufahamu wa kibinadamu (Gnostics), Waariani na wengine wenye imani potofu walitengwa na kanisa. Kanuni ya imani ya Mashahidi wa Yehova, Wamormon na wengineo ni ugunduzi wa imani za kisasa.
S: Kwenye Mat 28:19, je kanisa la awali liliamini nini kuhusu Utatu Mtakatifu?
J: Viongozi wafuatao wa kanisa la awali na wale wa miaka iliyofuata baraza la kanisa la Nikea walifundisha kuhusu Utatu Mtakatifu. Inafurahisha kuona kuwa machapishi ya Watchtower ya Mashahidi wa Yehova Can You Believe the Trinity? yananukuu wengi wa waandishi hawa wa kanisa la awali ili kujaribu kuonyesha kuwa hawakuamini Utatu Mtakatifu.
Kiongozi Rejea Maelezo au Imani
Ignatius: mwanafunzi wa Mtume Yohana aliyekufa mwaka 107 au 116 BK sehemu 17: Barua kwa Polycarp sura ya 3 Ephesians 7 "Yesu ni Mungu"

"Mungu aliyefanyika mwili"
Mtu asiyefahamika (karibu mwaka 130 BK) To Diognetus sura ya 7 Kristo alitumwa kama Mfalme, Mungu, Mwanadamu, na Mwokozi
Justin Martyr (karibu mwaka 138-165 BK) Dialogue with Trypho sura ya 55-56, 59, 61-64, 66, 74-78 "Anastahili kuabudiwa kama Mungu na Kristo."
Alikosea kwa kufikiria muda kabla ya kuweko kwa Kristo
Theophilus wa Antiokia (mwaka 168-181/188 BK) To Autolycus kitabu cha 2 sura ya 22 Sauti hii [kwenye bustani ya Edeni] ni kitu gani zaidi ila Neno la Mungu, ambaye pia ni Mwana wake? (Alikuwa ni mtu wa kwanza anayefahamika kutumia neno "Utatua [Mtakatifu]")
Irenaeus: mwanafunzi wa Yohana mtume (mwaka 182-188 BK) Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 19.2, uk.449 "Yesu, kwa uwezo wake mwenyewe ni . . . Mungu na Bwana . . ."
Clement wa Alexandria aliandika mwaka 193-217/220 BK Stromata kitabu cha 5 sura ya 14,
The Instructor
"Utatu Mtakatifu"
Nyimbo za kumsifu Yesu: "Bwana wa muda na mahali pote; Yesus Mwokozi wa jamii yetu ya wanadamu"
Tertullian (mwaka 198-220/240 BK) Kitabu chote kilichoitwa Against Praxeas Mwandishi wa pili anayefahamika kutumia neno "Utatu [Mtakatifu]"
Hippolytus mwanafunzi wa Irenaeus (mwaka 225-235/6 BK) Against the Heresy of One Noetus "Mwana wa Mungu ambaye, akiwa Mungu alifanyika mwanadamu." Baada ya kunukuu Yoh 1:1-3 alisema, "Kwa hiyo tunaona Neno aliyefanyika mwili, na tunamjua Baba kupitia kwake, na tunamwamini Mwana, (na) tunamwabudu Roho Mtakatifu."
Origen wa Alexandria aliandika mwaka 225-254 BK de Principis kitabu cha 1 sura ya 3.8
Origen alkuwa akibishiwa sana wakati wa uhao wake, lakini maoni yake kuhusu Utatu Mtakatifu hayakuwahi kutiliwa shaka
"nguvu ya Utatu [Mtakatifu] ni ile ile moja." Kosa la asili la kuwepo kwa nafsi kabla ya mtu kuzaliwa na wokovu wa watu wote ambao utakuja hatimaye
Novatian (mwaka 210-280 BK) Treatise on the Trinity kitabu chenye sura 32 kuhusu Utatu Mtakatifu
Athanasius (mwaka 296-373 BK) Sermon on Luke 10:22 Wana umoja lakini hachanganywi, wanatofautiana lakini hawatengani, hawagawanyiki ingawa hawana viwango
Basil wa Cappadocia (mwaka 357-379 BK) Letter 8 to the Caesareans, On the Spirit Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu, Roho Mtakatifu ni Mungu. Anayaelezea mabishano ya Arian
Gregory wa Nyssa (mwaka 335-394 BK) On Not Three Gods, Against Eunomius Asili/jinsi ya Baba na Mwana zinafanana
Hilary (mwaka 353-368 BK) Aliandika kitabu kuhusu Utatu [Mtakatifu] Ameongelea mambo mengi ya kutosha
Ambrose wa Milan (mwaka 340-397 BK) On the Christian Faith Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu kwenye Ufu 4:8 inamaanisha Utatu Mtakatifu
John Chrysostom (mwaka 392-407 BK ) Homily 3 on John 1:1 Umilele wa Neno kama nafsi; hajaumbwa
Augustine wa Hippo (mwaka 354-430 BK) Kitabu: On the Trinity Hakuafikiana na utofauti wa vyeo, viwango au madaraja
Nestorius: Baraza la kanisa lililofanyika Efeso mwaka 431 BK Alianzisha ukristo wa Kinestori (uliofundisha nafsi mbili tofauti, moja ya kibinadamu na nyingine ya kiungu, za Kristo aliyefanyika mwili) Imani yake kuwa Yesu alikuwa Mungu haikuwahi kupingwa
Cyril wa Alexandria (mwaka 431-444 BK) Mpinzani mkubwa wa Nestorius kwenye baraza la kanisa lililofanyika Efeso (Kwa bahati mbaya) alianzisha mkazo wa kuwa Mariamu ni Mama wa Mungu
Patrick wa Ireland (mwaka 389-461 BK) Hakuandika vitu vingi sana. Aliandika barua kwa Corticus. Ulinganisho unaofahamika sana wa jani la pande tatu la Utatu Mtakatifu

















S: Kwenye Mat 28:19, kwa kuwa msemo "Utatu Mtakatifu" haumo kwenye Biblia, Utatu Mtakatifu unawezaje kuwa umetokana na Biblia, na kwa ajili hiyo, wa kweli?
J: Hata maneno kama Agano Jipya au la Kale, unyakuo, umisheni, ufuasi, au uinjilisti hayapatikani kwenye Biblia. Kutoa jina kwa dhana iliyopo kwenye Biblia hakuifanyi kuwa ya kweli zaidi au kidogo. Unaziitaje nafsi Tatu ambazo zina jina moja amblo kwa hilo tunabatizwa?
Kwa Waislamu, ingawa neno "utatu" halimo kwenye Biblia, neno kuwa na umoja, tawhid halimo kwenye Qur’an pia. Kwa Warmomoni, maneno "Kuendelea kwa milele" hayamo kwenye Kitabu cha Mormoni pia.

S: Kwenye Mat 28:19, kwa nini siwezi kuuda picha ya Utatu Mtakatifu kichwani mwangu?
J: Hutakiwi kuunda picha hii. Huwezi kuunda picha ya Mungu kuwa Mwenyezi, kuwepo mahali pote, au hata wa milele, lakini madhaifu wa mwanadamu hayamzuii Mungu. Je ulitarajia kufahamu kikamilifu kila kitu kuhusu Mungu asiye na ukomo? Hata hivyo, tunaweza kufahamu mambo ambayo Mungu ameyafunua kuhusu Yeye mwenyewe.
Hakika, Utatu Mtakatifu unaweza unachanganya kwa sababu tatu.
1. Ukweli wa Mungu mara nyingi unachanganya kwa watu walio bado kuokoka.
2. Walimu wa uongo wameongeza kakarakakara. Kwa mfano, Mashahidi wa Yehova hawakubali Utatu Mtakatifu, lakini wao wenyewe mara nyingi ama wanautafsiri isivyo sahihi, au hata hawauelewi Utatu wanaoukataa. Wakati baadhi ya Wamormoni wanasema wanaukataa Utatu Mtakatifu, nimekutana na Wamormoni wengi wanaosema wanaukubali. Hata hivyo, Wamormoni nilioongea hawakujua Utatu Mtakatifu ni kitu gani. Utatu Mtakatifu ni zaidi ya nsfdi tatu kuwa kukubaliana katika upendo, roho, na makusudio.
3. Hatuwezi kuyalaumu tu madhehebu mapotofu. Wakristo wengi wa kweli hawajaamdaliwa vizuri kuweza kuuelezea Utatu Mtakatifu kwa wazi zaidi.

S: Kwenye Mat 28:19, Utatu Mtakatifu hauendani na mtazamo wangu wa sura ya Mungu.
J: Ni lazima uchague kumfuata Mungu, bila ya kujali mawazo uliyokuwa nayo kabla, au kutokufuata picha yako mwenyewe au sanamu au mungu.

S: Kwenye Mat 28:19, kama Utatu Mtakatifu ni kweli, je Yesu ni theluthi ya Mungu?
J: Hapana, tafsiri hii isiyo sahihi ya Utatu Mtakatifu ni fikara za kibinadamu, na wala si fikara nzuri sana ya kibinadamu. Kimo cha dawati si theluthi ya dawati.
Yesu ana ukamilifu wa Mungu kulingana na Kol 2:9. Kama ilivyo kichekesho kusema kuwa kwa jua linatoa mwanga haliwezi kutoa joto, kwa kuwa Yesu ni ukamilifu wa Mungu haina maana kuwa Baba na Roho hawawezi kuwa ukamilifu wa Mungu pia.

S: Kwenye Mat 28:19, je dhana ya Utatu Mtakatifu ilitokana na dini za Kibabeli na Kiashuri, ambazo zilikuwa na makundi ya miungu watatu?
J: Hapana. Yesu alipoagiza kubatiza kwa ____ la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Yesu alisema "jina", siyo "majina." Kundi la miungu watatu ni imani ya kuabudu miungu wengi ambayo ina nafsi tatu tofauti na miungu mitatu tofauti. Utatu Mtakatifu ni Mungu mmoja asiyeweza kutenganishwa na nafsi tatu tofauti.
Kwa upande mwingine, kama wangekuwa sehemu tatu za kiumbe kimoja, Kigiriki kingeweza kusema "katika jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu" lakini hakisemi hivyo. Kina "jina" kama umoja kikisisitiza umoja wao,lakini pia kina kibainishi "the" kabla ya maneno Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kusisitizia utofauti wao.

S: Kwenye Mat 28:19, kwa nini tusikatae kumwabudu baba yeyote aliyemtuma mtoto wake pekee wa kiume ili ateswe na kufa badala yake yeye mwenyewe, kama mhubiri mmoja wa Upentekosti wa Mungu mmoja alivyosema?
J: Inasikitisha endapo utakataa kumwabudu Mungu, isipokuwa kwa kufuata matakwa yako mwenyewe. Baba hakumtuma Yesu tu afe kwa hiari kwa ajili yetu, bali pia alimuuliza Ibrahimu kama atakuwa tayari kumtoa Isaka awe sadaka.

S: Kwenye Mat 28:19, je ‘Imani ya Nikea’ iliundwa kwa mara ya kwanza Nikea mwaka 325 BK?
J: Kwa kweli ilikuwa kabla ya hapo. Watu wengi hawafahamu jambo hili, lakini kwa mujibu wa Apostolic Fathers juzuu ya 7, uk.524, Imani ya Nikea ilikuwa ni marekebisho kidogo ya ‘Imani ya Yerusalem’ ilikuwepo kabla ya muda huo. Pia inafanana sana na ‘Imani ya Neocaesarea.’

S: Kwenye Mat 28:19, je kulikuwa na mambo yeyote yaliyoongezwa kwenye Imani ya Nikea?
J: Ndiyo. Ifuatayo ni Imani ya Nikea ya awali iliyoundwa mwaka 325 BK. (Tafsiri yake imetolewa kutoka kwenye Ante-Nicene Fathers juzuu ya 7, uk.524.
Imani ya Nikea ya kwanza iliyosainiwa na maaskofu 318 mwaka 325 BK
Tunamwamini Mungu mmoja, Baba Mwenyezi, Muumba wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana:
Na Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, aliyetoka kwa Baba, alitoka tu, yaani mwenye dutu moja na Baba,
Kwa Yeye vitu vyote viliumbwa, mbinguni na duniani:
Ambaye kwa ajili yetu wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu alishuka [kutoka mbinguni], na alifanyika mwili, na akawa mtu:
Aliteswa, akafufuka siku ya tatu:
Na akapaa mbinguni:
Na atakuja tena kuwahukumu walio hai na wafu.
Na Roho Mtakatifu.
[laana]
Na watu wanaosema kulikuwa na wakati ambao hakuwepo, au kuwa hakuwepo kabla ya kutoka kwa Baba, au kuwa aliumbwa bila kutumia kitu chochote; au wale wanaosema kuwa Mwana wa Mungu ni wa dutu nyingine yoyote, au kuwa anabadilika au si thabiti, - watu wa jinsi hii kanisa lililo moja tu (Katoliki) na la kimitume linawalaani.
Nyongeza iliyoidhinishwa kwenye baraza la kanisa lililofanyika Constantinople mwaka 381 BK na kuthibitishwa kwenye baraza la kanisa lilifanyika Efeso (mwaka 421 BK)
Wa mbingu na nchi.
Aliyetoka kwa Baba kabla ulimwengu wote haujakuweko.
Na Bikira Mariamu kwa Roho Mtakatifu.
Aliteswa kwa ajili yetu pia, wakati wa Pontio Pilato,
Na akazikwa.
Ameketi mkono wa kuume wa Baba,
Ambaye ufalme wake hautakuwa na mwisho.
Bwana, Mtoa uzima,
Atokaye kwa Baba;
Ambaye anaabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana;
Aliyenena kwa njia ya manabii:
[Tunaamini] kanisa moja takatifu Katoliki na la Mitume.
Tunakiri ubatizo mmoja kwa ondoleo la dhambi.
Tunatarajia ufufuo wa wafu,
Na uzima wa ulimwengu ujao. Amina.
[Laana haikuwepo]
Kwa mujibu wa Creeds of Christendom juzuu ya 1, uk.24-29, baadhi ya misemo ilikuwemo kwenye Imani ya Epiphanius na ya Cyril wa Yerusalemu mwaka 350 BK.
Mabadiliko ya pili kwenye Imani yalikuwa kuingizwa kwa maneno "na Mwana", yakisema Roho Mtakatifu alitumwa na Baba na Mwana. Mabadiliko haya yalionekana kwamara ya kwanza kwenye baraza tatu lililofanyika Toledo mwaka 589 BK. Yaliongezwa rasmi kwenye Imani na Kanisa Katoliki, na ikawa ndiyo sababu ya kutengana rasmi na kanisa la Orthodox chini ya askofu mkuu Photius mwaka 879 BK.

S: Kwenye Mat 28:19, kwa kuwa "wa" kwenye "mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza" inaongelea mataifa, na mataifa hawawezi kuzamishwa kwenye maji, je jambo hili linamaanisha kuwa msemo huu hauwezi kuwa unaongelea ubatizo wa maji?
J: Hapana. "Taifa" haliwezi kufanywa kuwa mwanafunzi pia, lakini "mataifa" inamaanisha watu wa mataifa yote. Jambo hili lilikuwa dhahiri kwa Wakristo wa awali, kwani walielewa kuwa Mat 28:19 inaongelea ubatizo wa maji. Ufuatao ni ushahidi.
Didache (karibu mwaka 125 BK) sura ya 7, uk.379 "batiza katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, kwenye maji yanayoembea. Lakini kama huna maji yanayotembea, batiza kwenye maji mengine, na kama huwezi kubatiza kwenye maji ya baridi, tumia ya moto. Lakini kama hauna yeyote kati ya hayo, mimina maji mara tatu kichwani kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu."
Tertullian (mwaka 198-220 BK) ana kazi nzima inayoitwa On Baptism. Kwenye sehemu moja, Tertullian anasema, "Lakini kwa kuwa imani imeongezeka sasa, na imekuwa imani inayomini kuzaliwa kwake, kuteswa, na kufufuka, kumekuwa ongezeko la maelezo ya sakramenti, yaani, tendo la kutia muhuri la ubatizo; mavazi, kwa namana fulani, ya imani iliyokuwa wazi hapo mwanzo, na ambayo sasa haiwezi kuwepo bila sheria yake sahihi. Kwa kuwa sheria ya ubatizo imewekwa, na kanuni imeelezewa: ‘Enendeni’, anasema, ‘mkawafundishe mataifa, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.’" On Baptism sura ya 13, uk.676.
Hippolytus askofu wa Portus (mwaka 222-235/6 BK) anasema kubatiza kwa jina la "Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Anamtaja Kornelio kwa ufupi. Against the Heresy of One Noetus sura ya14, uk.228.
Anonymous Treatise Against Novatian (mwaka 254-257 BK) sura ya 3, uk.658 inasema kubatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
Anonymous Treatise on Re-Baptism (mwaka 254-257 BK) "wabatizeni kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu."Sura ya 7, uk.671.
Cyprian wa Carthage (mwaka 246-258 BK) "Kwani baada ya kufufuka kwake, akiwa anawatuma wanafunzi wake, Bwana aliwaagiza na kuwafundisha namna wanayopaswa kubatiza, akisema, ‘Mamlaka yote imetolewa kwangu mbinguni na duniani. Basi, nendeni mkawafundishe mataifa yote, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.’ anadokeza Utatu Mtakatifu, ambao kwenye sakramenti zake mataifa walibatizwa. Je Marcion anausistiza Utatu Mtakatifu? Je, anamsema Baba yule yule, Muumba, kama sisi? Je, anamjua Mwana yule yule, Kristo aliyezaliwa na Bikira Mariamu, ambaye kama Neno aliyefanyika mwili, aliyechukua dhambi zetu, aliyeshinda mauti kwa kufa, ambaye kupitia kwake Yeye mwenyewe kwanza, alianzisha kufufuka kwa mwili, na ilionyesha kwa wanafunzi wake kuwa amefufuka kwenye mwili ule ule? Imani [ya kanisa] inatofautiana sana na Marcion, na, zaidi ya hayo, pamoja na wazushi wengine, na kwao hakuna kitu kingine ila uongo, na kufuru, na fitina, ambayo ni adui wa utakatifu na ukweli. Hivyo basi, awezaje mtu aliyebatizwa miongoni mwao kuonekana kuwa amepata utume wa dhambi, na neema ya huruma ya Mungu, kwa imani yake, wakati hana ukweli wa imani yenyewe?" Letters of Cyprian Barua ya 72 sura ya 3, uk.380-381.

S: Je kuna ushahidi gani kuwa Mtume Mathayo ndiye aliyeandika Injili ya Mathayo?
J: Kitabu chenye mlengo wa kushuku Asimov’s Guide to the Bible, uk.772 kinasema "hakuna ushahidi zaidi ya mapokeo." Hivi ni kama kusema hakuna ushahidi zaidi ya maneno ambayo Wakristo wa kwanza waliandika. Kwa kweli hatuna kanda za video zozote, lakini maandiko ndiyo ndicho kitu tunachoweza kuwa nacho."
Kanisa la awali liliafiki kwa umoja kuwa Mtume Mathayo ndiye aliyeandika Injili ya Mathayo. Kwa kweli kuna ushahidi mwingi sana wa jambo hili.
Papias (mwaka 130-150 BK) anataja majina ya vitabu vya Mathayo na Marko. Kipande cha 6 kutoka kwenye Eusebius’ Ecclesiastical History kitabu cha 3 sura ya 39.
Claudius Apollinaris (mwaka 160-180 BK) anazitaja Mathayo, Injili zote, na sheria. Ante-Nicene Fathers juzuu ya 8 sura ya 772.
Irenaeus (mwaka 182-188 BK) ananukuu Mat 1:1 akisema imeandikwa na Mathayo. Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 16.2, uk.440.
Clement wa Alexandria (mwaka 193-217/220 BK) "Na Injili ya Mathayo, orodha ya vizazi inayoanza na Ibrahimu inaendelea hadi kwa Mariamu mama wa Bwana." Stromata kitabu cha 1 sura ya 21, uk.334.
Tertullian (mwaka 198-220 BK) alisema, "Ninamaanisha Injili za Yohana na Mathayo – wakati ile ambayo Marko aliiandika inaweza kuthibitishwa kuwa ya Petro ambaye Marko alikuwa mkalimani wake. Kwani hata aina ya Injili ya Luka kwa kawaida watu wanaichukulia kuwa ni ya Paulo. Na inaweza kuwa kwamba kazi ambazo wafuasi wanaziandika ni za waalimu/viongozi wao." Tertullian Five Books Against Marcion kitabu cha 4 sura ya 5, uk.350.
Tertullian aliandika, ". . . kwamba Agano la Kiinjili limeandikwa na mitume, . . . mitume pia . . . Kwa hiyo, miongoni mwa mitume, Yohana, na Mathayo walitufundisha imani kwetu kwanza; wakati wafuasi wa mitume, Luka na Marko waliirudia baadaye." Five Books Against Marcion kitabu cha 4 sura ya 2, uk.347.
Julius Africanus (mwaka 232-245 BK) anamtaja "Mwinjilisti Mathayo" na "Luka" wakati analinganisha orodha mbili za vizazi vya Yesu kwenye barua yake iitwayo Letter to Aristides sura ya 3, uk.126.
Origen (mwaka 225-254 BK) anamtaja Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Origen Against Celsus kitabu cha 5 sura ya 56, uk.568.
Cyprian wa Carthage (mwaka 246-258 BK) anataja "Injili ya Mathayo" wakati akinukuu Mat 5:23, 24 kwenye Treatises of Cyprian - Testimonies sura ya 3, uk.533. Angalia pia The Treatises of Cyprian Tasnifu ya 12 kitabu cha tatu 1.40.
Dionysius wa Alexandria (mwaka 246-265 BK) "Ilikuwa ‘mwishoni mwa sabato’, kama Mathayo alivyosema; ilikuwa "mapema, kukiwa bado giza", kama Yohana anavyoandika: ilikuwa "mapema sana asubuhi", kama Luka anavyosema; na ilikuwa "mapema sana asubuhi, wakati jua linachomoza", kama Marko anavyotuambia. Hivyo, hakuna aliyetuonyesha muda halisi aliofufuka." Letter 5 to the bishop Basilides, uk.94.
Archelaus (mwaka 262-278 BK) "Roho kwa mwinjilisti Mathayo yu makini pia kuangaliza maneno haya ya Bwana wetu Yesu Kristo: ‘Angalieni, mtu asiwadanganye; kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; na watawapotosha wengi. Lakini mtu yeyote akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au kule; msiamini. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na mitume wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; hata kwamba, kama ingewezekana, watawadanganya hata wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya kabla. Kama wakiwaambieni, Tazama, yuko jangwani’; msiende: kama wakisema, Tazama, yupo kwenye vyumba vya siri; msiamini." Disputation with Manes sura ya 35, uk.209.
Adamantius (karibu mwaka 300 BK) "Je, utakubali endapo nitakuonyesha kutoka kwenye Injili kuwa mambo haya si uzushi" ... "Wanafunzi wa Kristo waliyaandika: Yohana na Mathayo, Marko na Luka." Dialogue on the True Faith First Sehemu "b 5", uk.41.
Victorinus wa Petau (aliyeuawa kama shahidi wa imani mwaka 304 BK) anataja Zaburi, Mathayo, Isaya, Danieli Commentary on the Creation of the World, uk.342.

S: Wakati Papias aliposema kuhusu Injili ya Mathayo, je hakuna "uhakika kuwa Papias … alikuwa anaongelea Injili tuliyonayo sasa" kama Asimov’s Guide to the Bible p.771 alivyosema?
J: Asimov alijua zaidi kuhusu kemia kuliko historia ya kanisa. Licha ya hilo, watu waliomtangulia, ambao walisema iliandikwa na Mathayo na walinukuu mistari toka kwenye Mathayo, sisi pia tunazo nukuu kutoka kwenye Injili ya Mathayo kutoka kwa waandishi wa awali wafuatao, na wote wananukuu kitabu hiki hiki tulichonacho leo, ingawa hakusema kiliandikwa na nani. Clement wa Rumi na The Epistle of Barnabas waliandika mapame kuliko Ignatius.
Clement wa Roma 97/98 BK
Waraka wa Barnabas karibu mwaka 100 BK
To Diognetus karibu mwaka 130 BK
Polycarp askofu wa Smyrna, mwanafunzi wa Yohana karibu mwaka 150 BK
Shepherd of Hermas mwaka 160 BK
Justin Martyr karibu mwaka 138-165 BK
Theophilus wa Antioki mwaka 168-181/188 BK
Athenagoras karibu mwaka 177 BK
Hivyo kama nukuu za awali zinaendana na kitabu, Wakristo wa awali walisema iliandikwa na Mathayo, na hawakuwa na kitu kingine chochote kilichoitwa Injili ya Mathayo, hakuna ushahidi tuliopewa unaotufanya tutilie shaka kitu ambacho kanisa la awali lilikijua.

S: Injili ya Mathayo iliandikwa lini?
J: Kitu ambacho tunaweza kusema ni kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa baada ya mwaka 33 BK na kuna uwezekano mkubwa sana kuwa kabla ya 70 BK. Kwanza yafuatayo ni mambo tunayoyajua, na kisha mambo ambayo wanazuoni mbalimbali wanayafikiri.
Mambo yanayojulikna kuhusiana na wakati Injili ya Mathayo ilipoandikwa
Luka: Kwenye 1 Tim 5:18, Paulo alinukuu vitabu vya Kumbukumbu la Torati (25:4) na Luka (10:7), akiviita Maandiko. Waraka wa 1 Timotheo uliandikwa mwaka 63 BK kwa mujibu wa wanazuoni wengi. (Hata hivyo, Mark White anasema kuwa 1 Timotheo iliandikwa "karibu mwaka 100-125 BK."
Hati ya kale ya Luka iliyoko Paris (p4) iliyo na sehemu ya Luka 1-6 inadhaniwa na Phil Comfort kuwa iliandikwa karibu mwaka 100 BK. Bila shaka, Injili ya Luka iliandikwa kabla ya kitabu cha Matendo ya Mitume. Maelezo zaidi kuhusiana na jambo hili yanapatikana kwenye kitabu cha Carsten P. Thiede na Mathayo d’Ancona kiitwacho, Eyewitness to Jesus: Amazing New Manuscript Evidence About the Origin of the Gospels (NY Doubleday 1996), uk.206. Hata hivyo, ingawa Thiede na d’Ancona wanachukulia muda huu wa kuandikwa kama. "si baadaye sana zaidi ya mwaka 68 BK," Philip Comfort anachukua tahadhari zaidi, anasema kuwa kitabu hiki kiliandikwa mwaka 100 BK.
Yohana: Mwanahistoria wa awali wa kanisa Eusebius wa Kaisarea anarekodi kuwa Papias, mwanafunzi wa Mtume Yohana, aliwataja Mathayo na Marko kuwa waliandika Injili zao. Alisema kuwa Mathayo aliandika Injili yake kwanza kwenye Kiebrania (Kiaramu?). Wako watu wanaofikiri kuwa usemi huu unamaanisha kuwa aliandika katika mtondo wa uandishi wa Kiebrania, ingawa wazo hili linatia shaka.
We have a fragment of the Gospel of John (the Tuna kipande cha Injili ya Yohana (hati ya John Rylands, iliyoandikwa mwaka 117-138 BK). Injili ya Yohana imekuwa ikidhaniwa kuwa ni Injili ya mwisho kuandikwa.
Wanazuoni mbalimbali wana mawazo gani?
The Expositor’s Bible Commentary juzuu ya 8, uk.20-21 inasema mwaka 66-100 BK, na "huenda miaka ya sitini ikawa miongo inayowezekana zaidi kuwa ndipo ilipoandikwa. Pia inaongeza kuwa Gundry anasema mwaka 40-100 BK, kwani anasema kuwa Injili ya Luka ilitumia Injili ya Mathayo, na vitabu vya Luka na Matendo vilikamilishwa kabla ya mwaka 63 BK.
The NIV Study Bible, uk.1439 inasema wako watu wanaosema Injili ya Mathayo iliandikwa mapema sana kama mwaka 50 BK, na wengine wanasema baada ya mwaka 70 BK.
New Geneva Study Bible, uk.1503 inasema kuwa ingawa kuwa watu wanaosema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa mapema sana kama mwaka 50 BK na mwaka 100 BK, tarehe yenye kufaa zaidi ni mwaka 64-70 BK. Kwenye uk.1558, New Geneva Study Bible inasema kuwa,"Inafikiriwa kwa ujumla kuwa Injili za Mathayo na Luka ziliandikwa karibu mwaka 80-90 BK. Pia inasema kuwa Luka na kitabu cha Matendo vinaweza kuwa vilikamilishwa karibu mwaka 62 BK, na watu wengine wanadai kuwa vitabu vyote vya Agano Jipya viliandikwa kabla ya mwaka 70 BK.
New International Bible Commentary inasema kuwa isipokuwa wakati inapochukuliwa kuwa Injili ya zamani zaidi, mara nyingi huchukuliwa kuwa iliandikwa mwaka 75-80 BK.
Believer’s Bible Commentary, uk.1202 inasema kuwa Mathayo anaweza kuwa aliandika kazi yake kwenye Kiaramu mapema sana kama mwaka 45 BK, na aliikamilisha Injili iliyomo kwenye Biblia mwaka 50-55 BK au hat baadaye. Inaongeza, "Maoni kuwa Injili hii lazima iwe imeandikwa baada ya kuangushwa kwa Yerusalemu (mwaka 70 BK) yamejengwa kwenye msingi wa kutokuamini uwezo wa Yesu wa kutabiri matukio ya baadaye kwa undani, na kanuni nyingine za kimantiki zinazopuuzia au kukana uvuvio unaofanywa na Mungu."
New International Dictionary of the Bible, uk.631 inasema kuwa hatufahamu sawasawa kabisa, lakini kuitegemea kwake Injili ya Marko na kutokukutaja kwake kuangushwa kwa Yerusalemu kunadokeza kuwa iliandikwa muda mfupi tu kabla ya mwaka 70 BK.
Kamusi yenye kushikilia fikira na viwango vya asilia na ambayo haipendi au inachukulia mabadiliko iitwayo Wycliffe Bible Dictionary, uk.1090 inasema kuwa iliandikwa kati ya mwaka 30-115 BK.
C.I. Scofield alisema Injili inaweza kuwa imeandikwa mapema sana kama mwaka 37 BK, kwa mujibu wa The Bible Knowledge Commentary New Testament, uk.16.
The Bible Knowledge Commentary: New Testament, uk.15-16 inasema kuonyesha mwaka bayana haiwezekani. Wanazuoni wachache wanasema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa baada ya mwaka 70 BK, wakiongeza kuwa kutajwa kwa "Mji Mtakatifu" kwenye Mat 4:5 na 27:53 kunamaanisha kuwa Yerusalemu ulikuwa bado haujaangushwa. Inasema kuwa muda wa karibu na mwaka 50 BK unaweza kukidhi mahitaji yote yaliyotajwa, na kushikilia maoni kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwanza.
Kitabu chenye mlengo wa kushuku kiitwacho Asimov’s Guide to the Bible, uk.771 kinasema kuwa Injili ya Mathayo huenda ilifikia hatua yake ya mwisho hatua muda mfupi tu baada ya mwaka 70 BK.
Dictionary of Jesus and the Gospels, uk.528 ni mchanganyiko wa mtazamo wenye utayari wa kupkea maoni mapya na kuachana na yale ya asilia pamoja na mtazamo wenye kushikilia maoni ya asilia (ya kanisa). Nayo pia haitoi jibu bayana la swali hili, bali inasema "kwa kuwahi sana, Injili ya Mathayo inaweza kuwa iliandikwa kati ya mwaka 75-80 BK, huku muda wa mwaka 75-85 BK ukiwa unaungwa mkono zaidi (watoa maoni wakiwa Bonnard, Grundmann, Davies na Allison).
Kitabu chenye mtazamo ulio tayari kupokea mwenendo na maoni mapya na kutilia shaka au kuacha kanuni au viwango vya asilia kiitwacho Matthew 1-7 : A Commentary, uk.93, baada ya kutoa maelezo ya kina, kinatoa hitimisho la majaribio kuwa "mtu yeyote asichukulie Injili ya Mathayo kuwa iliandikwa muda mrefu baada ya mwaka 80 BK."
Profesa mwenye kushikilia fikira na viwango vya asilia Mark White wa Chuo Kikuu cha Texas huko Austin, kwenye maelezo ya somo alisema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa karibu mwaka 80-90 BK.
Moja ya madhanio ya mtazamo ulio tayari kupokea mwenendo na maoni mapya na kutilia shaka au kuacha kanuni au viwango vya asili ni kwamba endapo Mathayo alichukua aya toka Injili ya Marko, Marko itabidi iwe inasambazwa miaka kadhaa kabla Injili ya Mathayo haijaandikwa. Dhanio la pili ni kukana kwamba Mungu angeweza kutoa utabiri wa kuangushwa kwa Yerusalemu kabla ya kungushwa kwake (Yerusalemu) mwaka 70 BK.

S: Kwenye Mathayo, tunajuaje kuwa Injili tuliyo nayo sasa imetunda kwa kuaminika mambo yaliyo andikwa mara ya kwanza?
J: Kuna sababu nzuri zisizopungua tatu.
1. Mungu ameahidi kuhifadhi Neno lake kwenye Isa 55:10-11; 59:21; 40:6-8; 1 Pet 1:24-25 na Mat 24:35.
2. Ushahidi wa kanisa la awali. Waandishi wengi walinikuu au kuongelea Injili ya Mathayo. Wafuatao ni baadhi ya waandishi wa awali zaidi.
Clement wa Roma (mwaka 97/98 BK) alinukuu Mat 6:12-15; 7:2; 15:8. Ingawa Mat 15:8 (sura ya 5, uk.9) inafanana kabisa na Mark 7:6 na Isa 29:13.
Ignatius kwenye barua zake iitwayo Letter to the Smyrnaeans 1:1 (mwaka 90-116 BK), Letter to Polycarp sura ya 2, uk.94 ananukuu Mat 10:16b.
The Didache (Mafundhisho ya Mitume Kumi na Mbili) ya mwaka 120-150 BK, sura ya 8, uk.379 inanukuu Sala ya Bwana kutoka Mat 6:5, 9-13. Kwa hakika nukuu hii inatoka Injili ya Mathayo na siyo Luka kwa mujibu wa maelezo ya 24 chini ya ukurasa.
2 Clement sura ya 3, uk.252 inanukuu Mat 10:32 kama maneno ya Yesu na pia anadokeza Mat 22:37.
2 Clement sura ya 4, uk.252 inafafanua Mat 7:21.
2 Clement sura ya 5, uk.252 inanukuu Mat 5:28 kama maneno ya Yesu.
2 Clement sura ya 9, uk.253 inafafanua Mat 12:50 kama maneno ya Yesu.
The Letter of Barnabas (mwaka 100-150 BK) sura ya 5 inanukuu Mat 20:16 (pia 22:14). The Ante-Nicene Fathers maelezo chini ya uk.139 inasema kuwa hii ni nukuu ya kwanza inayotanguliwa na kanuni "imeniandikwa."
Letter of Polycarp to the Philippians sura ya 2, uk33 (mwaka 110-155 BK.) inanukuu Mat 7:1 yote, "lakini kumbukeni maneno ambayo Bwana aliyasema kwenye mafundisho yake: ‘Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.’"
Polycarp alinuku Mat 6:13a kwenye Polycarp’s Letter to the Philippians sura ya 7, uk.34-35.
Polycarp alinukuu Mat 26:41b kwenye Polycarp’s Letter to the Philippians sura ya 7, uk.34-35.
Barua kwa Diognetus sura ya 9, uk.28 (karibu mwaka130 BK) inadokeza Mat 6:25 ikisema kuwa Mwokozi alitufundisha kutumaini . . . ili tusijisumbue kuhusu mavazi na chakula.
Barua Diognetus sura ya 8, uk.28 (karibu mwaka 130 BK) inadokeza Mat 19:17.
Papias alikuwa ni mwandishi awali aliyeongea na Petro, Yakobo, Yohana, Mathayo na wengineo (kwa mujibu wa Fragment 1). Kwenye Fragment 6 alisema kuwa Mathayo alikusanya mahubiri [ya Yesu] kwenye lugha ya Kiebrania.
Justin Martyr (karibu mwaka 138-165 BK) anategemea nukuu toka Injili za Mathayo (karibu mara 38), ambayo ni zaidi anavyotegemea kwenye Injili nyingine. Angalia Ante-Nicene Fathers juzuu ya 1, uk.591 kwa ulinganisho wa hii na nukuu za Justin za Injili nyingine. Kumbuka kuwa idadi ya nukuu za Luka zinafanana kati ya Mathayo na Luka. Ananukuu au kufafanua Mat 1:21; 3:11-12, 17; 4:9, 10; 5:20, 28, 29, 32; 3:34, 37, 44, 45, 46; 6:1, 16, 19, 20, 21, 22, 25, 26, 33 ,41; 7:15, 16, 19, 21,22; 8:11; 9:13; 10:28; 11:12-15, 27; 12:38f; 13:3, 42; 15:22-28; 16:21, 26; 17:12; 19:6, 12, 17, 26, 28; 21:13; 22:17, 19-21, 37; 23:15, 23, 24, 27; 24:11; 25:41; 26:39.
Muratorian Canon inaitaja Injili ya Mathayo (karibu mwaka 170 BK) pamoja na Injili nyingine tatu.
Shepherd of Hermas (karibu mwaka 160 BK) kitabu cha 1 sehemu ya nne sura ya 2, uk.18 inanukuu robo ya Mat 26:24 "Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa."
Shepherd of Hermas (karibu mwaka160 BK) kitabu cha 2 sura ya 6, uk.30 inadokezea Mat 10:28. "Mwogopeni yule ambaye ana nguvu zote, kuokoa na kuangamiza."
Mwasi Tatian (mwaka 177 BK) aliandika upatinifu wa Injili zote nne unaoitwa Diatessaron. Ndani mwake alitaja aya 819 za Mathayo. Hii ni 76% ya Injili yote.
Claudius Apollinaris (mwaka 160-180 BK) aliitaja Mathayo, Injili nyingine na sheria. Ante-Nicene Fathers juzuu ya 8 sura ya 772.
Apollonius wa Efeso (karibu mwaka 210 BK) alinukuu Mat 10:9 kama maneno ya Bwana kwenye Concerning Montanism sura ya 4, uk.776. Pia alinukuu Mat 12:33 kwenye Concerning Montanism sura ya 4, uk.776.
Theophilus wa Antioki (mwaka 168-181/188 BK) alinukuu Mat 5:28 kama "Sauti ya Injili" kwenye Theophilus to Autolycus kitabu cha 3 sura ya 3, uk.115.
Irenaeus (mwaka 182-188 BK) alitumia nukuu nyingi toka kwenye Injili zote nne, lakini pia alitumia Injili ya Mathayo zaidi. Alinukuu aya 223 za Mathayo ama aya nzima au sehemu zake. Irenaeus alisema Injili hii iliandikwa na Mathayo kwenye Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 16, uk.441. Ifuatayo ni orodha ya aya au ufafanuzi kwenye sura tisa za Mathayo: 1:1, 12-16, 18, 20, 23; 2:15, 16; 3:3, 7, 9-12, 16; 4:3, 7, 9, 10; 5:5, 8, 13a, 14a, 16, 18, 20-28, 33-35, 41, 44, 45; mwisho theluthi ya 5:12 na katikati theluthi ya 7:7; 6:12a,19, 24, 27; 7:1-2, 5; 8:9, 11-13; 9:2a, 6,8, 29
Irenaeus pia alidokeza Mat 2:16; 5:39; 7:15, 19, 25; 9:17 11:9; 12:18, 31; 13:25, 38, 44; 17:3, 7, 27
Bado sijathibitisha nukuu zote za Irenaeus za Injili ya Mathayo sura ya 10 na zaidi.
Clement wa Alexandria kwenye Stromata kitabu cha 1 sura ya 21, uk.334 (mwaka 193-202 BK) "Na Injili ya Mathayo, orodha ya vizazi ambayo inaanza na Ibrahimu inaendelea hadi kwa Mariamu mama wa Bwana." Alinukuu sehemu nyingi zaidi za Mathayo pia.
Tertullian (mwaka 198-220 BK) alisistizia uandishi wa Mathayo, Marko, Luka, Yohana, Ufunuo na nyingi za nyaraka za Paulo kwenye Five Books Against Marcion kitabu cha 4 sura ya 5, uk.350. Alinukuu aya nyingi za Mathayo.
Theodotus huenda alikuwa Mmontanisti.
Hippolytus (mwaka 225-235/6 BK) alinukuu Mat 7:21 na 21:31 kama maneno ya Mwokozi. Refutation of All Heresies kitabu cha 5 sura ya 3, uk.54. Alinukuu aya nyingine pia za Mathayo.
Julius Africanus (mwaka 232-245 BK) aliwataja "Mwinjilisti Mathayo" na "Luka" alipolinganisha orodha mbili za vizazi vya Yesu kwenye barua yake iliyoitwa Letter to Aristides sura ya 3, uk.126.
Origen (mwaka 225-254 BK) alinukuu kwa kiasi kikubwa sana Injili ya Mathayo, kwani alikuwa na ufafanuzi wa kitabu chote cha Mathayo. Nukuu za Origen zinahusisha Mat 24:23-27.
Novatian (mwaka 257 BK) kwenye On the Trinity sura ya 8, uk.617 alinukuu Mat 10:29-30 akisema ni maneno ya Yesu. Kwenye suray ya 12 pia alinukuu Mat 27:20 akisema ni maneno ya Yesu. Novatian alinukuu Mat 1:23 (uk.635); 5:8 (uk.639-640); 10:28a (uk.636) 10:29,30 (uk.617); 12:32b (uk.641); 16:16 (uk.637); 16:16 (uk.637); 28:20b (uk.621).
A Treatise Against Novatian ilinukuu aya nne za Mathayo: 7:2a (uk.661); 7:22, 23 (uk.659), 10:33 (uk.659), 23:12a (uk.661); huenda na aya nyingine pia.
Anonymous Treatise on Re-Baptism (karibu mwaka 250-259 BK) ilinukuu Mat 3:11b (sura ya 2, uk.668) 9:2b (sura ya 18, uk.677); 10:32 (sura ya 11, uk.673), 12:37 kama "kwenye Injili" (sura ya 13, uk.675), 16:22, 23 (sura ya 9, uk.672); 24:4, 23, 24 (sura ya 12, uk.674), 26:70 (uk.672), 28:19 (sura ya 7, uk.671).
Cyprian askofu wa Carthage (mwaka 246-258 BK) "Kwenye Injili ya Mathayo: ‘Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.’" Treatises of Cyprian Tasnifu ya 3 sura ya 28, uk542.
Cyprian askofu wa Carthage (mwaka 246-258 BK) alinukuu Mat 5:43-45, akitaja mambo ambayo Yesu aliyasema "kwenye Injili yake" kwenye Treatises of Cyprian Tasnifu ya 10 sura ya 15, uk.495.
Cyprian wa Carthage (mwaka 246-258 BK) alinukuu Mat 15:13 kama maneno ya "Bwana kwenye Injili yake" Barua ya 48:4, uk.326.
Moyses na wengine kwa Cyprian (Barua ya 25) sura ya 4, uk.303 (mwaka 250-251 BK) alinukuu Mat 10:37-38 kama maneno ya "Bwana wetu, kama kwa parapanda ya Injili yake."
Cornelio kwa Cyprian (karibu mwaka 246-256 BK) alinukuu Mat 5:8 kama "neno la kiinjili" Barua ya 45 sura ya 2, uk.323.
Firmilian wa Kaisaria kwa Cyprian (mwaka 256 BK) alinukuu Mat 16:9 kama maneno ya Yesu. (Barua ya 74 sura ya 16, uk.394).
Kwenye Baraza la Saba la Kanisa lililofanyika Carthage (mwka 258 BK) Lucius wa Castra Galbae alisema, "Kwa Bwana kwenye Injili yake alisema, ‘Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee’", uk.566.
Gregory Thaumaturgus (mwaka 240-265 BK) alinukuu sehemu ya Mat 15:11 kama maneno ya Bwana. Canonical Epistle, Canon 1, uk.18.
Dionysius wa Alexandria (mwaka 246-265 BK) "Ilikuwa ‘mwishoni mwa sabato,’ kama Mathayo alivyosema; ilikuwa "mapema, kukiwa bado giza", kama Yohana alivyoandika; ilikuwa "asubuhi sana na mapema", kama Luka alivyosema; na ilikuwa "asubuhi sana na mapema, jua lilipokuwa linachomoza", kama Marko alivyotuambia. Thus no one has shown us clearly the exact time when He rose." Letter 5 to the bishop Basilides p.94
Anatolius of Alexandria (270-280 A.D.) refers to Matthew 26:17; in ch.8, and Matthew 26:38 in ch.10.
Archelaus (mwaka 262-278 BK) "Roho kwa Mwinjilist Mathayo ni mwangalifu pia kuelezea maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo: "Angalieni mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watawadanganya wengi. Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. Kwa kuwa watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki." Disputation with Manes sura ya 35, uk.209.
Adamantius (karibu mwaka 300 BK) "Je utakubali endapo nitakuonyesha kutoka kwenye Injili kuwa siyo uongo?" . . . "Wanafunzi wa Kristo waliziandika: Yohana na Mathayo; Marko na Luka. Dialogue on the True Faith Sehemu ya Kwanza "b 5", uk.41.
Victorinus wa Petau (aliyeuawa kama shahidi wa imani mwaka 304 BK) alizitaja Zaburi, Mathayo, Isaya, Danieli Commentary on the Creation of the World, uk.342.
Peter wa Alexandria (mwaka 306, 285-311 BK) alinukuu Mat 21:6 na 6:24 kama maneno ya Bwana kwenye Canonical Epistle canon 12 uk.276-277. Pia alidokeza Mat 2:13-16 kwenye Canon 13, uk.277, na alinukuu Mat 2:22-13 kwenye Canon 13, uk.277.
Methodius (mwaka 260-312 BK) "Basi tafakari yote ya kiroho ya Maandiko imetolewa kwetu kama chumvi inayochoma ili kunufaisha, na inayosafisha, bila hii nafsi yeyote haiwezi, kwa kutumia mantiki, kuletwa kwa Mwenyezi; kwa kuwa ‘Ninyi ni chumvi ya dunia’, alisema Bwana kwa mitume." [Mat 5:13] The Banquet of the Ten Virgins kitabu cha 1 mahubiri ya 1 sura ya 1, uk.311.
Theophilus’ Martyrdom of Habib the deacon alinukuu Mat 10:39; na Mat 7:6 yote kama "Maandiko" kwenye uk.694.
Athanasius of Alexandria (karibu mwaka 318 BK) hakunukuu Mathayo kwenye Against the Heathen. Hata hivyo, kwenye Incarnation of the Word alinukuu Mat 19:4 (sura ya 2.6, uk.37), Mat 1:23 (pia Isa 7:14) (sura ya 33.3, uk.54), Mat 11:13 (sura ya 40.4, uk.57-58); Mat 26:64 (sura ya 56.4, uk.66).
Amphilochius (mwaka 289-319 BK) alinukuu Mathayo kwenye Iambi ad Seleucum
Alexander wa Alexandria (mwaka 321 BK) alinukuu Mat 11:27b kama maneno ya Mwokozi. Epistles on the Arian Heresy suray ya 5, uk.293.
Alexander wa Alexandria (mwaka 321 BK) alinukuu Mat 3:17 kama "kwenye Injili." Epistles on the Arian Heresy sura ya 8, uk.294.
Alexander wa Alexandria (mwaka 321 BK) alinukuu Mat 11:12 kama "ilisemwa na Kristo" Epistles on the Arian Heresy sura ya 12, uk.295.
Lactantius (karibu mwaka 303 hadi karibu mwaka 325 BK) alidokeza Mat 14:22-26 alipokuwa anaongea kuhusu Yesu kutembea juu ya maji. The Divine Institutes kitabu cha 4 sura ya 15, uk.116. Lactantius pia alidokeza Mat 5:44; 7:15; 18:7; na sura za 14, 19 na 21. Alinukuu Isa 7:14 kama maneno ya Isaya ambayo pia ni Mat 1:23.
Baada ya baraza la kanisa lilifanyika Nikea
Juvencus (mwaka 329 BK) aliandika ufafanuzi wa Injili zote nne.
Eusebius’ Ecclesiastical History (mwaka 323-326 BK) kitabu cha 3 sura ya 24, uk.152 ilielezea Injili nne, Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Nicene and Post-Nicene Fathers Second Series juzuu ya 1, uk.152.
Aphrahat Msiria (mwaka 337-345 BK)
Cheltenham Canon (Mommsen Catalogue) karibu mwaka 360-370 BK.
Hilary wa Poitiers (hadi mwaka 367 BK)
Athanasius (mwaka 367 BK.) aliorodhesha vitabu vya Agano Jipya kwenye Festal Letter 39, uk.552.
Ephraem Msiria (mwaka 350-378 BK)
Basil wa Cappadocia (mwaka 357-378/379 BK)
Cyril wa Yerusalemu (karibu mwaka 349-386 BK)
Synod ya Laodicea (mwaka 343-381, 363 BK)
Ambrose wa Milan (mwaka 370-390 BK)
Gregory Nazianzen (mwaka 330-391 BK)
Pacian wa Barcelona (mwaka 342-379/392 BK)
Gregory Nyssa (karibu mwaka 356-396 BK)
Didymus Kipofu (mwaka 378 BK)
Syrian Catalogue of St. Catherine’s (karibu mwaka 400 BK)
Epiphanius wa Salamis (mwaka 360-403 BK)
Rufinus (mwaka 374-406 BK)
John Chrysostom (hadi mwaka 407 BK)
Yerome (mwaka 373-420 BK)
Sozomen’s Ecclesiastical History (mwaka 370/380-425 BK)
Sulpicius/Sulpitius Severus (mwanafunzi wa Martin) mwaka 363-420 BK.
Baraza la kanisa lililofanyika Carthage (maaskofu 218), mwaka 393-419 BK.
Niceta wa Remesianus (mwaka 366-c.415 BK)
Orosius/Hosius wa Braga (dhidi ya Priscillian), mwaka 414-418 BK.
Mwasi Pelagius (karibu mwaka 390 BK)
Mwasi wa Kipelagi Theodore wa Mopsuestia (mwaka 392-423/429 BK)
Augustine wa Hippo (mwaka 388-8/28/430 BK)
John Cassian (Mpelagi nusu), mwaka 419-430 BK.
Baraza la kanisa lililofanyika Efeso na Wanestori (maaskofu 200) (Jun-Sep mwaka 431 BK)
Vincent wa Lerins (karibu mwaka 434 BK)
Socrates’ Ecclesiastical History (karibu mwaka 400-439 BK)
Nestorius’ Bazaar of Heracleides (mwaka 451/452 BK)
Euthalius wa Sulca -aliligawa karibu Agano Jipya lote kwenye sehemu mbalimbali (karibu mwaka 450 BK)
Eucharius, Instructiones (karibu mwaka 424-455 BK)
Theodoret wa Cyrus (askofu na mwana historia), mwaka 423-458 BK.
3. Hati za kale zilizoandikwa mapema zaidi tuna utofauti mdogo wa matini, lakini hakuna makosa ya kithiolojia yenye umuhimu.
p1 (=Papyrus Oxyrhynchus 2) Mat 1:1-9, 12, 14-20; (haina 2:14) (karibu mwaka 200 BK) Matini ya Kialexandria
Zifuatazo ni tarehe za kuandikwa kwa hati hii
Karne ya 3 - 1968 - The Text of the New Testament
Karne ya 3 - 1975 - Aland toleo la 3
Karne ya 3 - 1990 - Comfort, Early Manuscripts & Modern Translations of the New Testament
Karne ya 3 - 1998 - Aland toleo la 4 lililorekebishwa
Katikati ya karne ya 3, inafanana na p69 - 1999 - Comfort, The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts
Kuna jalada lenye maandishi. Ingawa O’Callaghan anadhani linaweza kuwa Mat 2:14, Philip Comfort kwenye The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts, uk.29 anasema si kwa sababu lina mwandiko tofauti na kuna nafasi ya kandoni iliyo karibu mistari mitatu isiounganika kuliko sehemu iliyobakia ya Mathayo. Matini hii inaweza kuwa ni maelezo ya kichwa kidogo au kicha chenyewe.
The Text of the New Testament (1968) uk.245 inasema hii pia inahusisha Mat 1:23, lakini vyanzo vingine havihusishi aya hii. Picha yenye sehemu ya p1 ipo kwenye The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts, uk.29.
p19 (=Papyrus Oxyrhynchus 9) Mat 10:32-11:5
Ni matini ya Kimagharibi (Western text) kwa sehemu kubwa
Karne ya nne - 1968 The Text of the New Testament
p21 (=Papyrus Oxyrhynchus 10 ) Mat 12:24-26, 31-33 (Inakubaliana na Bezae Cantabrigiensis na Sinaiticus iliyorekebishwa)
Karne ya nne - 1968 - The Text of the New Testament
p25 (=Papyrus 16388, kwa sasa imepotea. Ilikuwa Berlin kabla ya VIta Kuu ya Pili ya Dunia) Mat 18:32-34; 19:1-3, 5-7, 9-10
Mwishoni mwa karne ya 4 - 1968 - The Text of the New Testament. Matini ya Kimagharibi
p35 Mat 25:12-15, 20-23 (karne ya 3rd)
Huenda iliandikwa karne ya 4 - 1968 - The Text of the New Testament. Matini kati ya Kialexandri na Kimagharibi
p37 (=Ann Arbor 1570) Mat 26:19-52 (katikati ya karne ya 3) The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts in picha ya sehemu ya p37 kwenye uk.130. Ipo kwenye sehemu mbili na ilinunuliwa Cairo Misri mwaka 1924. Mwandiko wake unafanana na barua za Heroninos (mwaka 256 na 260 BK)
Karne ya 3 au 4 - 1969 - The Text of the New Testament.
p44b Mat 17:1-3, 6-7; 18:15-17, 19; 25:8-10 pia Yohana 9:3-4; 12:16-18 (karne ya 6 hadi 7)
The Text of the New Testament, uk.251 pia inasema ina aya 10:8-14
Karne ya 6 hadi 7 - 1968 - The Text of the New Testament
p45 Chester Beatty I (Injili zote nne na kitabu cha Matendo) (mwaka 100-150 BK) (awali ilidhaniwa kuwa iliandikwa mwishoni mwa karne ya 2 au mwanzoni mwa karne ya 3 BK) (Mat 20:24-32; 21:13-19; 25:41-26:39, sehemu za Marko, Luka, na Yohana) The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts ina picha yenye kuonyesha sehemu ya p45 kwenye uk.146. Kwenye uk.150-151 inasema kuwa nakala yake ilikuwa ni ufafanuzi, ambapo mwandishi alikuwa anajaribu kuonyesha wazo la kila msemo. A General Introduction to the Bible, uk.389 inasema hati ya awali ilikuwa karibu makaratasi 220, kati ya hayo tuna makaratasi 30. Mawili kati ya makaratasi hayo 30 ni ya Injili ya Mathayo.
Karne ya 3 - 1968 - The Text of the New Testament
Karne ya 3 - 1975 - Aland na wengine. Toleo la tatu
Karne ya 3 - 1998 - Aland na wengine. Toleo la nne lililorekebishwa
Mwishoni mwa karne ya 2 au mwanzoni mwa karne ya 3 - 1999 - The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts
p53 (= Papyrus Michigan Inv. 6652) Mat 26:29-40 na Mdo 9:33-38; barua 3 kati ya 124 kwenye 9:39; 9:40-10:1. (karibu mwaka 260 BK). The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts ina picha inayoonyesha sehemu ya p653 kwenye uk.360. Tarehe ya kuandikwa inategemea kufanana kwake na barua za Heroninos iliyoandikwa karibu mwaka 260 BK. Ni matini mchanganyiko.
Karne ya tatu - 1968 - The Text of the New Testament
p64 (Magdalen Papyrus), p67 karibu mwaka 200 BK. The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts ina picha ya sehemu ya p64 kwenye uk.32, na sehemu ya p67 kwenye uk.34. p4 (yenye sehemu kubwa ya Luka1-6), p64, nap67 ni sehemu ya hati moja ya kale. Mafunjo p64 yamehifadhi Mat 26:7, pungufu ya nusu ya maandishi ya aya ya 8; 26:10, 14-15, 22-23, 31-33 (kwenye vipande vitatu). P64 ilinunuliwa Misri mwaka 1901, lakini haikuweza kufikiwa na wanazuoni hadi mwaka 1953. P67 imehifadhi Mat 3:9,15; 5:20-22, 25-28.
Karibu mwaka 200 BK - 1968 - The Text of the New Testament. Haisemi kuwa ina aya ya 8
Mwaka 125-150 BK - 1999 - The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts. Inasema kuwa ina aya ya 8.
p70 (=Papyrus Oxyrhynchus 24) Mat 2:13-16; 2:22-3:1; 11:26-27; 12:4-5; 24:3-6,12-15. (karne ya 3) The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts ina picha inayoonyesha sehemu ya p70 kwenye uk.464. Inataja aya 11:26-27; 12:4-5 tu. Inasema kuwa ina epsilon tofauti na ya ya pekee, na mwandiko wake unaonekana kufanana na P. Medici 13 (ya Wimbo Ulio Bora) iliyoandikwa karne ya 3.
Karne ya 3 - 1968 The Text of the New Testament.
p71 (=Papyrus Oxyrhynchus 2385) ina Mat 19:10-11, 17-18 (karne ya 4)
Karne ya 4 - 1968 - The Text of the New Testament. Inakubaliana na Vaticanus
p73 ina Mat 25:43; 26:2-3 (karne ya 7). Ni matini mchanganyiko.
Tarehe ya kuandikwa haipo - 1968 - The Text of the New Testament inaitaja hii lakini haitoi tarehe yake ya kuandikwa
p77/p103 ina Mat 23:30-39 (p77); 13:55-57; 14:3-5 (katikati hadi mwisho wa karne ya 2)
p83 ina Mat 20:23-25, 30-31; 23:39; 24:1, 6 (karne ya 6)
p86 Mat 5:13-16, 22-25 (karibu mwaka 300 BK)
p101 (=Papyrus Oxyrhynchus 4401) karne ya tatu ina Mat 3:10-12; 3:16-4:3
p102 (=Papyrus Oxyrhynchus 4402) karibu mwaka 300 BK. Mat 4:11-12, 22-23
p103 (=Papyrus Oxyrhynchus 4403) ina Mat 13:55-57; 14:3-5 (karne ya 2 hadi 3)
p104 (=Papyrus Oxyrhynchus 4404) (mwanzoni hadi katikati ya karne ya pili) ina Mat 21:34-37, 43, 45?
p105 (=Papyrus Oxyrhynchus 4406) ina Mat Mat 27:62-64, 28:2-5 (karne ya 5 au 6)
p110 (=Papyrus Oxyrhynchus 4494) ina Mat 10:13-14, 25-27 (karne ya 4)
pAntinoopolis 2.54 karne ya tatu, ina Sala ya Bwana (Mat 6:10-12). Inaonekana kuwa hati hii ilikuwa Sala ya Bwana tu awali.
0171 (karibu mwaka 300 BK) ina Mat 10:17-23, 25-32
Vaticanus [B] (mwaka 325-350 BK) na Sinaiticus [Si] (mwaka 340-350 BK) zina Injili yote ya Mathayo
Alexandrinus [A] karibu mwaka 450 BK imehifadhi Mat 25:7 hadi mwishoni tu
The Washington Codex (karne ya 4t au 5) ina Injili yote ya Mathayo
Freer Gospels [W] Cambridge karne ya 5 au 6
Bohairic Coptic [Boh] karne ya 3 au 4
Sahidic Coptic [Sah] karne ya 3 au 4
Ephraemi Rescriptus [C] karne ya 5
Armenian [Arm] kuanzia karne ya 5
Georgian [Geo] kuanzia karne ya 5
Gothic mwaka 493-555 BK Ethiopic [Eth] kuanzia karibu mwaka 500 BK
Fayyumic Coptic [Fay] karne ya 4 hadi 7 Peshitta Syriac [Syr P] mwaka 400-450 BK
Chester Beatty Ms 814 mwanzoni mwa karne ya 7 ina Mat 5:28-42 kwenye Kimisri cha kale cha Kisahidi (Sahidic Coptic)
S: Je kuna hati zozote zile za kale za Mathayo zilizoandikwa mapema zaidi ambazo bado zipo leo hii?
J: Muda wa kuandikwa Magdalen Manuscript (p64 na p67) unabishiwa.
Wengi wanakubali kuwa iliandikwa kabla ya karne ya 3 BK, kwa sababu ya mtindo wake kwenye maandiko yaliko katika mafunjo, ambo haukutumiwa baada ya mwanzo wa karne ya tatu.
Mapema zaidi (karibu mwaka 50-64/65 BK). Haya ni maoni ya Carsten Thiede, mtaalamu wa mafunjo wa Kijerumani. Kuna mambo matatu yanayounga mkono maoni haya.
1) Uncial (mwandiko ambao kutokana nao herufi kubwa zilipatikana): Mafunjo ya Magdalene ilikuwa "uncial" (yenye herufi kubwa tupu) ya mafunjo, ambayo ilitumika hadi katikati ya karne ya kwanza BK.
2) Ulinganisho wa miandiko hadi kwenye matini za zilizoandikwa katikati ya karne ya kwanza zilizopatikana huko Pompey na Herculaneum
3) Kwa kukisia, Wakristo waliotaka kuhifadhi maandiko yao huenda waliaanza kutumia kodeksi mapema.
Matini ya baadaye zaidi (karne ya pili BK) ya Agano Jipya. Maoni yanayofuatwa na watu wengi zaidi siku hizi ni kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kati ya mwaka 80 na 100 BK.
Kodeksi: Inaonekana kutoka kwenye kodeksi (kitabu) na waandishi walibadilisha kutoka kutumia hati na kutumia vitabu kwenye karne ya 2.
Kwa kukisia, huenda baadhi ya ‘uncials’ kama hii ziliandikwa baadaye. Kuna wati wanaofikiri kuwa maandiko ya uncial yaliandikwa baadaye kama mwaka 85 BK. Usemi huu ni mgumu kuuelewa, kama kitabu cha Aland na wengine, The Greek New Testament, toleo la 4 lililorekebishwa linavyoonyesha, makini ya uncial yalitumika hata baadaye sana kama karne ya 9. Mack huenda alimaanisha mtindo maalumu wa uncial kwenye mafunjo.
Hitimisho: Ingawa hatujui wakati kodeksi za kwanza kabisa zilipoandikwa, hata wanazuoni wenye kushikilia fikira na viwango vya asilia wanachukulia kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa katika ya karne ya kwanza.

No comments:

Post a Comment