- Ni kutangaza (kutoa ushuhuda) kuhusu mambo yale ambayo uliyoyaona na kuyasikia au hata kuyaonja au kuyagusa – kuhusu Mungu. [1Yohana 1: 1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; 2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.]
- Siyo maana yake kumueleza mtu kuwa yeye ni mwenye dhambi na wewe ni mwenye haki mbele za Mungu, eti kwa sababu wewe umeokoka nayeye hajaokoka, na kwamba wewe unakwenda mbinguni; na kwa sababu yeye hajaokoka anakwenda motoni(jehanamu) hapana!
- Siyo kujisifu mbele za watu au kujivunia wokovu!
- Ni kutumika mbele za Mungu kwa ajili ya wenye dhambi(ulimwengu) ili nao walijue Neno, waamue kumuamini BWANA Yesu Kristo na waepukane na dhambi, shetani na matui; bali wapate Wokovu na uzima wa milele.
- Wapate kumjua BWANA YESU KRISTO, upendo wake, uweza wake, huruma zake, na wokovu mkuu sana wa Mungu kwa mwanadamu.
- Ni kuwashirikisha wengine habari njema yaa mema uliyoyapata kutoka kwa Mungu, ambayo Mungu anapenda nao wayapate.
Kwa nini tunashuhudia watu? Kwa nini tuwashuhudie watu?
- BWANA Yesu Kristo alitumwa kwa sababu hii ya kuhubiri ufalme wa Mungu Luka 4:43 Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa. 44 Basi, alikuwa akihubiri katika masinagogi ya Galilaya.
- Kuifikisha ujumbe wa Wokovu na upendo wa Mungu kwa wenye dhambi na wasiomjia Mungu; yaani, kuutangaza mwaka wa BWNA uliokubalika.
- Kuzivunja kazi za Ibilisi
- Kuwafungua waliofungwa na Ibilisi
- Watu wanakufa dhambini na kwenda motoni
- Utahukumiwa kwa sababu ya hao wanaopotea