Tuesday, August 4, 2015
Nina wezaje kupokea msamaha wa dhambi toka kwa Mungu?
Swali: "Nina wezaje kupokea msamaha wa dhambi toka kwa Mungu?"
Jibu: Matendo 13:38 yasema, “Basi naijulikane kwenu, ndugu zangu ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi.”
Msamaha ni nini na kwanini ninauhitaji?
Neno “samehe” linamaanisha kusafisha nia au jambo nakulifanya kutokuwa na mawaa yoyote, ku achilia, kufutilia mbali deni. Tunapo kosea mtu, huuliza msamaha wao ili tukarudishe uhusiano. Msamaha haupeanwi kwa sababu mtu anastahili kusamehewa. Hakuna anaye stahili kusamehewa. Msamaha ni ishara ya upendo, huruma na neema. Msamaha ni uamuzi wa kutoshikilia jambo ndani yako kinyume cha mtu mwengine, haijalishi amekukosea kiasi gani.
Bibilia inatuambia yakwamba sote tunahitaji msamaha toka kwa Mungu. Sote tumefanya dhambi. Mhubiri 7:20 asema, “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.” 1Yohana 1:8 asema, “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” Dhambi zote ni kitendo cha uasi kinyume chake Mungu (Zaburi 51:4). Basi kwa hivyo, tunahitaji kwa vyovyote msamaha wake Mungu. Kama dhambi zetu hazitasamehewa, tutakuwa katika adhabu ya milele tukiteseka kwa ajili ya madhara ya dhambi zetu (Mathayo 25:46;Yohana 3:36).
Msamaha-Je, ni upate vipi?
Kwa shukurani, Mungu ni mwenye upendo na huruma-mwenye ari ya kutusamehe dhambi zetu! 2Petro 3:9 asema, “Yeye hutuvumilia maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” Mungu anatamani kutusamehe, kwa hivyo alitoa kwa ajili ya msamaha wetu.
Adhabu ya haki pekee inayostahili kwa ajili ya dhambi zetu ni mauti. Sehemu ya kwanza ya kitabu cha Warumi 6:23 yasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…..” Mauti ya milele ndiyo ndiyo tuliyopokea kama mshahara wa dhambi zetu. Mungu, kwa mpango wake mahususi, alifanyika kuwa mwanadamu - Yesu Kristo (Yohana 1:1, 14). Yesu alikufa juu ya msalaba kwa kuchukua adhabu tuliyo stahili-mauti. 2Wakorintho 5:21 inatufundisha, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. “Yesu alikufa msalabani, akichukua adhabu tuliyo stahili!Kama Mungu, kifo chake Yesu kilitoa msamaha wa dhambi kwa ulimwengu mzima. 1Yohana 2:2 asema, “Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. “Yesu alifufuka katika wafu, akishuhudia ushindi juu ya dhambi na mauti (1Wakorintho 15:1-28). Mungu apewe sifa kwa kupitia kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo, Sehemu yote ya pili ya kitabu cha Warumi 6:23 ni kweli, “…bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Je, ungetaka dhambi zako zisamehewe? Je, uko na hisia za kuudhi za kila mara zinazo kuhukumu na kuonekana kuwa ngumu ku epukika?Msamaha wa dhambi zako upo ikiwa utamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako. Waefeso1:7 yasema, “katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” Yesu alitulipia deni ili tukapate kusamehewa. Unacho stahili ni kumuuliza Mungu akusamehe kupitia kwake Yesu, ukiamini yakwamba Yesu alikufa ili upate msamaha-naye atakusamehe! Yohana 3:16-17 ina habari hii ya ajab, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”
Msamaha-Je, ni jambo lililo rahisi?
Ndio, ni rahisi! Huwezi kupata msamaha toka kwa Mungu. Huwezi kulipia msamaha wako toka kwa Mungu. Unaweza ku upokea tu, kwa imani, kupitia neema na huruma za Mungu. Kama unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na kupokea msamaha toka kwa Mungu, hapa kuna ombi unalo weza kuomba. Kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haiwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutaleta msamaha wa dhambi. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea msamaha. “Mungu, najua ya kwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu na nina weak imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu/ya ajabu na kwa msamaha! Amina.”
Je umepata uzima wa milele?
Swali: "Je umepata uzima wa milele?"
Jibu: Bibilia inaonyesha njia ya wazi ya uzimani.Mwanzo ni sharti tutambue yakwamba tumetenda dhambi kinyume chake Mungu: “Kwasababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi Mungu,ambayo yanafanya tustahili adhabu.Kwa kuwa dhambi zetu ziko kinyume kabisa na Mungu aliye uzima wa milele,basi ni adhabu ya milele pekee itoshayo. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti,bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).
Hata hivyo Yesu Kristo asiyekuwa na dhambi (1 Petro 2:23), mwana wa Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Yohana 1:1,14) na akafa ili kutulipia adhabu. “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi,kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu,tulipokuwa tungali wenye dhambi” (Warumi 5:8). Yesu Kristo alikufa msalabani (Yohana 19:31-42), kwa kuchukua adhabu ambayo sisi tulistahili (2Wakorintho 5:21). Siku tatu baadaye akafufuka katika wafu (1Wakorintho 15:1-4), kudhihirisha ushindi juu ya dhambi na mauti. “kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu” (1Petro 1:3).
Kwa imani ni sharti tuungame dhambi zetu na tumrejee Kristo kwa ajili ya wokovu (Matendo 3:19). Tukiweka imani yetu kwake, kwa kuamini kifo chake msalabani kama malipo ya dhambi zetu,tutasamehewa na kuahidiwa uzima wa milele mbinguni. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). “Kwa sababu,ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10:9). Imani pekee katika kazi aliyo ikamilisha Kristo pale msalabani ndiyo njia ya kweli ya pekee ya uzimani! “Kwa maana nimeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yoyote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9).
Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako,tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haitakuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo peke yake ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumuelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu,najua yakwamba nimetenda dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Nina ziacha dhambi zangu na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu /ya ajabu na kwa msamaha - karama ya uzima wa milele! Amina!”
INJILI YA YESU KRISTO
INAMHITAJI KILA MWANADAMU.
BWANA YESU asifiwe ndugu.
Karibu tujifunze habari njema za ufalme wa MUNGU.
Injili maana yake ni habari njema za ufalme wa MUNGU.
Kama kuna kitu cha muhimu cha kuhubiri kwa wahubiri basi injili ni jambo
la kwanza.
Injili ndiyo inayohubiri wokovu.
Injili ndiyo inayohubiriwa na watu wanapata ondoleo la dhambi kama
wakimpokea BWANA YESU.
Injili ya BWANA YESU inamuhitaji kila mwanadamu, wanaoipokea injili na
kutubu na kuanza kuishi maisha sahihi ya wokovu hao wataurithi uzima wa
milele.BWANA YESU anatutaka wanadamu wote tutubu na kuiamni injili, Neno
la MUNGU ni injili na shabaha ya Neno la MUNGU ni ili wanadamu wafike
uzima wa milele, YESU anakutaka wewe ndugu uiamini injili, Marko 1:14-15
'' ......... YESU akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya
MUNGU, akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni,
na kuiamini INJILI. ''
Injili Ni Neno La MUNGU, Sehemu Nyingine Biblia Imesema Kwamba Injili Ni
Neno La Msalaba. Wokovu Wetu Unatokana Na Injili, Msingi Wa Wokovu Wetu
Umesimama Juu Ya Yale Yaliyotendeka Msalabani, Juu Ya Ukweli Na Juu Ya
Kazi Ya MUNGU. 1 Kor 15:3 '' Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo
yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa KRISTO alikufa kwa ajili ya
dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; ''
-Kama KRISTO asingelikufa msalabani basi injili isingehubiriwa, lakini
sasa BWANA wetu YESU KRISTO yuu hai, ameshinda kifo na mauti na sasa
yeye ndio sababu ya watu kuupata uzima wa milele, Hakuna Mwokozi
mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO.
Injili Ni Ujumbe Wa MUNGU, Wala Sio Maoni Ya Wakristo Tena Sio Mawazo Ya
Wafuasi Wa Kanisa Lolote. Ndugu Hubiri Injili Ya KRISTO Siku Zote Za
Maisha Yako.
Katika Biblia Kila Jambo Lazima Lithibitishwe Kwa Mashahidi Wawili Au
Watatu. Hata Wokovu Wetu Unathibitishwa Na Mashahidi Wawili NENO LA
MUNGU Na ROHO MTAKATIFU.
1: NENO Linasema Hakuna Hukumu Juu Ya Waliookoka(Warumi
8:1, Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika KRISTO
YESU. )
YESU Ndio Sababu Ya Wokovu Wetu Sisi Tunaomtii(Waebrania 5:9, naye
alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote
wanaomtii; ),
2. ROHO MTAKATIFU Anashuhudia Kwamba Sisi Tu Watoto Wa
MUNGU(Warumi 8:16-17, ROHO mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya
kuwa sisi tu watoto wa MUNGU; na kama tu watoto, basi, tu warithi;
warithi wa MUNGU, warithio pamoja na KRISTO; ......... )
-ROHO MTAKATIFU anashuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi tu watoto wa
MUNGU.
-Wasiookoka na watenda dhambi hata ROHO MTAKATIFU hayumo ndani yao
hivyo hawezi kushuhudia kwao.
-Na Ndio Maana Yeye ROHO Anakaa Ndani Yetu(Warumi 8:9, Lakini ikiwa ROHO
wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata
roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake. )
-Kama huna ROHO MTAKATIFU huwezi kuzishinda dhambi.
-Kama una ROHO MTAKATIFU na ukashindwa kumtii pia huwezi kushinda
dhambi.
-Kama huna ROHO MTAKTIFU huwezi wewe sio wa KRISTO.
-Lakini pia kuna tofauti kati ya kujazwa ROHO na kufurika ROHO. Kuna
kunena kwa lugha na pia wakati mwingine kunena kwa Lugha ni karama kama
Biblia inavyosema.
-Kuna wenye kiwango kidogo cha udhihilisho wa ROHO MTAKATIFU na kuna
wenye kiwango kikubwa.
-Kuna watu ROHO huongea nao kwa sauti kabisa, kuna watu hata akama
anaambiwa jambo lolote iwe ni kwenye simu au kwa njia ya kawaida ROHO
anamwambia ''hilo unaloambiwa ni la uongo''
-ROHO MTAKATIFU ni muhimu sana kwa kila mwenda mbinguni.
-Tamani kufikia kiwango cha juu cha udhihilisho wa ROHO MTAKATIFU.
-ROHO MTAKATIFU ni mtakatifu hivyo hakikisha unaokoka na kuwa mtakatifu.
Injili ya BWANA YESU inaambatana na uponyaji wa roho na mwili.
Ndugu, Usipoteze Uhakika Wa Wokovu Kwa Kukaa Kwenye Mafundisho Ya Kanisa
Linakataa Neno La MUNGU Na Nguvu Ya MUNGU Huku Kanisa Hilo KRISTO Kwao
Akiwa Ni Ziada Tu. Sali Kanisa Ambapo Utapata Injili Kamili, Injili
Ambayo Haijawekewa Chumvi Ya Udhehebu.
Watu Wengi Huishi Kama Wateule Wa MUNGU Lakini Hawajaokoka. Ndugu
Anayeishi Hivyo Huyo Amepungukiwa Na Utukufu Wa Ukombozi Utokao
Mbinguni. Maisha Ya Bila Kuokoka Ni Ya Kujisukuma Kwa Nguvu Zao Wenyewe.
Mteule Ni Yule Aliyepokea Asili Ya MUNGU Kwa Kuzaliwa Mara Ya Pili
Kutoka Juu. BABA Yao Wa Kiroho Yuko Mbinguni.
Hakuna anayetakiwa kuigeuza injili ya BWANA YESU, Kama yupo na alaaniwe
ndivyo Biblia inavyosema, Wagalatia 1:7-9 '' Wala si nyingine; lakini
wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya KRISTO. Lakini
ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote
isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema,
na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote
isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. ''
-Mtu akileta injili tofauti na Wokovu kupitia YESU KRISTO, huyo haijui
injili sahihi.
-Mtu akileta mafundisho yanayomkataa ROHO MTAKATIFU, huyo ni wakala wa
shetani.
-Mtu akileta mafundisho ya kwamba kuna njia nyingine ya uzima wa milele
nje na KRISTO, huyo ni baba wa uongo na ni shetani kabisa.
-Mtu akileta mafundisho yeyote yanayokataa kuokoka, huyo hajitambui na
hamjui MUNGU aliye hai.
-Mtu akihubiri kuabudu sanamu na kuabudu watu wakiwemo watakatifu, huyo,
huyo hayuko upande wa MUNGU.
=Anayeabudiwa ni MUNGU BABA(Ufunuo 19:10, 1 Nyakati 16:29) ,
=MUNGU MWANA(Mathayo 14:33, Mathayo 28:9; Luka 24:52; Yohana 9:38 )
=na MUNGU ROHO MTAKATIFU (Ayubu 33:4,Yohana 4:24) , ukimwabudu mariamu,
Musa au Eliya wewe uko upande wa sheatni hata kama una jina la Kikristo.
Ukitaka Kuwa Mkristo Mwenye Afya Njema Hakikisha Kwanza Unakula Chakula
Kizuri Ambacho Ni Neno La MUNGU. Pili Hakikisha Unakunywa Maji Mengi
Ambayo Ni Ujazo Wa ROHO MTAKATIFU. Tatu Hakikisha Unafanya Mazoezi
Ambayo Ni Kumtumikia MUNGU Na Kutenda Kazi Yake. Nne Pata Hewa Safi
Ambayo Ni Kwenda Kwenye Ibada Kanisani Kila Iitwapo Leo. Na Mwisho
Jiburudishe Kwa Kuwa Na Ushirika Na Wateule Wengine Mkishauriana Na
Kuombeana.
Mafundisho Yeyote Ya Dini Ambayo Yanakuacha Mashakani Juu Ya Wokovu Wa
Roho Yako, Hayo Hayaambatani Kabisa Na Injili Ya KRISTO. BWANA YESU
Anasema Ukimpokea Yeye Kwa Imani Maana Yake Umepita Kutoka Mautini Na
Kuingia Uzimani (Yohana 5:24, Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye
neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala
haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani) . Wokovu
Ni Muhimu Sana Kwa Kila Mwanadamu. YESU KRISTO Anaokoa, Ukiamini Leo
Unaokoka.
Neno La MUNGU Humnyamazisha Mshitaki Wetu ibilisi. Ukitaka
Kumnyamazisha shetani Tumia Neno La MUNGU Kwenye Maombi Yako Na Maisha
Yako Kwa Ujumla, Kiri Neno La MUNGU Na Hakikisha Unaishi Kama Neno
Litakavyo. BWANA YESU Anakupenda Sana.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku
nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio
kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na
utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi
kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Je, ni gani sheria hizi Nne za Kiroho?
Swali: "Je, ni gani sheria hizi Nne za Kiroho?"
Jibu: Sheria hizi Nne za kiroho ni njia za kushiriki habari njema za wokovu upatikanao kupitia imani ndani ya Yesu Kristo. Ni njia moja rahisi ya kupanga habari muhimu katika injili kwa sehemu Nne.
Ya kwanza kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Mungu anakupenda na ana mpango wa ajabu juu ya maisha yako.” Yohana 3:16 yatwambia, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 10:10 yatupa sababu ya kuja kwake Yesu, “Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” Ni kitu gani kinachotuzuia na upendo wa Mungu? Ni kitu gani kinacho tupinga kupata uzima ulio tele?
Ya pili kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Hali ya Utu wa mwanadamu inachafuliwa na dhambi na hivyo basi kutengwa na Mungu. Kwa matokeo haya basi, hatuwezi kamwe kuufahamu mpango wa ajabu alio nao Mungu juu ya maisha yetu.” Warumi 3:23 inatuhakikishia habari hii, “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Warumi 6:23 inatupatia madhara ya dhambi, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.” Mungu alituumba ili tukaweze kuwa na ushirika naye. Hata hivyo hali ya Utu/Ubinadamu ilileta dhambi katika dunia, na hivyo basi kutengwa na Mungu. Tumeharibu uhusiano pamoja naye ambao Mungu alikusudia tukaupate. Je, suluhisho ni nini?
Ya tatu kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Yesu Kristo ndiye toleo la Mungu pekee kwa ondoleo la dhambi zetu. Kupitia kwa Yesu Kristo, tunaweza kusamehewa dhambi zetu na kurudisha ushirika wa haki na Mungu.” Warumi 5:8 yasema, “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” Wakorintho 15:3-4 inatufahamisha kinachotupasa kujua na kuamini ili tupate kuokoka, “……ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko, yakuwa alizikwa; ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko….” Yesu mwenyewe akiri yakwamba yeye ndiye njia ya pekee ya wokovu katika Yohana 14:6, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Je, ninawezaje kupata kipawa hiki kikuu cha wokovu?
Ya Nne kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Ni sharti tuweke imani yetu ndani ya Yesu Kristo kama mwokozi ili tukaweze kupokea kipawa cha wokovu na kujua mpango wa ajabu wa Mungu juu ya maisha yetu. Yohana 1:12 inatuelezea hivi, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. “Matendo16:31 inazungumzia kwa ufasaha zaidi, “Mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka!” Tunaweza kuokolewa kwa neema peke yake, kwa njia ya imani pekee, ndani ya Yesu Kristo pekee (Waefeso 2:8-9).
Ukiwa unataka kumwamini Yesu Kristo kama mwokozi wako, sema maneno yafuatayo kwa Mungu. Kusema maneno haya haitakuokoa, lakini itawezekana kwa kumwamini Kristo!Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kum shukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, ninajua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha- karama ya uzima wa milele! Amina!”
Subscribe to:
Posts (Atom)