Tuesday, June 30, 2015
Monday, June 22, 2015
INJILI YA NEEMA NA UTUKUFU WA MUNGU
Ni furaha yangu katika Kristo Yesu kutaka kuona mwili wa Kristo unapata chakula kila iitwapo Leo.
Najua kila mtu anajua nini maana ya "INJIRI" basi kwa yule am aye alikuwa hajui nini maana ya Injili ni hii.
Neno Injili linatokana na lugha ya Kiyunani.."euangelion" Maana yake.."HABARI NJEMA"
INJILI imegawanyika katika maeneo matatu.
1.INJILI YA MILELE
Hii uhusika na uumbaji wa Mungu.(Zaburi 18:1-6; Warumi 1:19-23)
2.INJILI YA UFALME.
Injili hii humdhihirisha Mungu kuwa mfalme na inasema juu ya ufalme wa Mungu hapa duniani.(Zaburi 26-12; Isaya 9:7; Mathayo 4:17; 10:5-6)
3.INJILI YA UTUKUFU
WA MUNGU
Injili hii hushuhudia wokovy katka Kristo kwa watu wote. "WAYAHUDI NA WAMATAIFA" Hapa Myahudi hana upendeleo wiwote mbele ya mtu wa mataifa. Injili hii hushirikusha "SIRI YA KRISTO" Waefeso 3:12-13 "....SIRI HIYO HAWAKUJULISHWA WANADAMU KATIKA VIZAZI VINGINE....YA KWAMBA MATAIFA NI WARITHI PAMOJA NASI.." Injili hii inataja kwamba kanisa ni "MWILI WA KRISTO".
Injili hii itaubiliwa mpaka wakati wa "KUNYAKULIWA KWA KANISA"
Injili ya utukufu wa Mungu itatupeleka "MBINGUNI" katika katika "UTUKUFU WA MBINGUNI" kama Kristo alivyo mbinguni sasa, ndiyo maana tunashiriki baraka za ulimwengu wa kiroho.
Injili hii ya NEEMA ilianzia tangu kukataliwa kwa Israeli mpaka matengenezo yake. (Warumi 11:25-36)
Kabla ya matengenozo haya ya Israeli kanisa (tuliookoka) litanyakuliwa , na naada na hapo mabaki ya waamini wa Israeli wataanza tena kuihubiri Injili ya Ufalme, na itakuwa katika kipindi cha dhiki kuu.
Fuatana nami katika somo lijalo linalosema
WAKATI WA KUNYAKULIWA KWA KANISA LILILO MWILI WA KRISTO.
MUNGU AKUBARIKI
Subscribe to:
Posts (Atom)