Friday, November 4, 2016

ROHO YA HEKIMA NA UFUNUO

Wapendwa wa Mungu Bwana Yesu asifiwe sana nawapenda katika Bwana. maana inapendeza sana machoni pake Mungu wetu tunapokuja kwake na kujifunza hekima yake na maarifa yake. tushirikiane katika kujikumbusha juu ya somo hili la Roho ya Hekima na Ufunuo, Karibu

Katika Waefeso 1:17 Biblia inasema ‘Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi ROHO YA HEKIMA NA YA UFUNUO KATIKA KUMJUA YEYE’. Hili moja ya maombi muhimu ambayo Mtume Paulo alifanya kwa jili ya Kanisa la Efeso. Kila nisomapo mstari huu nimekuwa nikijuliza sana ni kwa nini Mtume Paulo aliomba maombi haya kwa kanisa hili?.